Mkutano wa Waislam Mnazi mmoja - Kura ya kundi inaleta maana? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkutano wa Waislam Mnazi mmoja - Kura ya kundi inaleta maana?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MC, Aug 29, 2009.

 1. M

  MC JF-Expert Member

  #1
  Aug 29, 2009
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 751
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Salim Said na Ummy Muya

  SHURA ya Maimamu Tanzania imezindua rasmi mwongozo wa pamoja kwa Waislaam kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu na uchaguzi mkuu mwakani.

  Waraka huo, ambao umetumia maneno "sidanganyiki kwa wanasiasa wasio waaminifu na kupiga kura ya kundi" unawaelezea waumini wa dini ya Kiislamu sifa za kiongozi anayefaa kuchaguliwa katika chaguzi zijazo.

  Mwongozo huo una kurasa 45 na sehemu 19 zinazoeleza taswira ya uchaguzi wa mwaka 2005, dhana ya uchaguzi, uhuru wa kutoa maoni, tumefikaje hapa tulipo, maadili, elimu, afya, kilimo, fedha na uwezeshaji, maisha bora, sheria, umoja na amani, Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, uwakilishi wa umma, hadaa za uchaguzi na dira katika uchaguzi na hitimisho.

  Akizungumza katika uzinduzi wa mwongozo huo uliohudhuriwa na mamia ya waislamu kutoka mikoa 22 ya Tanzania na kufunguliwa na amiri wa shura ya maimamu, Sheikh Mussa Kundecha, mhadhiri wa msikiti wa Idrisa, Sheikh Ally Basaleh aliwataka Waislamu kushikamana na kupiga kura kama kundi maslahi na kuwaambia wanasiasa wasio waaminifu kuwa hawadanganywi tena kwenye chaguzi.

  Katibu wa kamati kuu ya siasa ya Shura ya Maimamu, Sheikh Ponda Issa Ponda ndiye aliyezindua mwongozo huo.

  "Waislaam nchini tumedanganywa sana na wanasiasa wasio waaminifu chini ya serikali ya Chama cha Mapinduzi, lakini kuanzia sasa tunaingia katika uchaguzi na kupiga kura ya maslahi kama kundi maslahi, na hili si jambo baya," alisema Sheikh Basaleh.

  "Tumedanganywa, hatukudanganywa? Tumedanganywa, hatukudanganywa," alihoji Basaleh na kujibiwa na umati wa waumini wa madhehebu mbalimbali ya Kiislaamu kwa sauti ya pamoja wakisema: "Tumedanganywaa."

  Alisema: "Katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu na ule wa urais, wabunge na madiwani mwakani, waislamu tuseme hatudanganyiki."

  Aliwaeleza kuwa kura itakayomkomboa kila mwananchi ni kura ya maslahi pekee.

  Awali akifungua mkutano huo, Sheikh Mussa Kundecha aliiomba serikali kuufuata mwongozo huo ili kuweza kuzitawala nyoyo za wananchi na kwamba iwapo itaupuuza itawaongoza wananchi katika maafa makubwa ambayo hayajawahi kutokea nchini.

  "Mwongozo huu ni wa watu wote na Waislaam. Serikali ... ikiupuuza itawaongoza wananchi katika maafa makubwa ambayo hayajawahi kutokea nchini hata mara moja," alisema Sheikh Kundecha.

  Kwa mujibu wa Kundecha, mwongozo huo umetolewa baada ya serikali kushindwa kudhibiti makundi ya dini kutoa maoni yao binafsi, kitu ambacho alisema kinalenga kuvuruga amani, usalama na umoja wa kitaifa.

  Aliilaumu serikali kwa kushindwa kuwashirikisha Watanzania katika mambo yanayowahusu na Waislaamu katika mambo yanayowahusu.

  "Kwanza, tunakutana hapa kama Waislaam; pili kama Watanzania ili kuieleza serikali kwamba inapaswa kuwashirikisha Waislaam mapema katika mambo yanayowahusu bila ya kushinikizwa," alisema.

  Mjumbe wa kamati kuu ya siasa ya shura ya maimamu, Sheikh Mohammed Issa alisema Tanzania ina makabila 120 na watu zaidi ya milioni 40 hivyo serikali inapaswa kujenga umoja katika makabila hayo badala ya kuendeleza ubaguzi mtu, dini na ukabila.

  "Ukifanya ubaguzi wa aina yoyote unatengeneza bomu na dhambi kubwa isiyofutika. Kwa Tanzania, Waislaam ndio waliobeba uhuru na ukombozi wa nchi hii," alisema Issa.

  "Waislaam hawapaswi kukubali kudhulumiwa hata kidogo na serikali haipaswi kufanya ubaguzi wa aina yoyote kwa sababu sote tunaipenda nchi yetu, sote tuna haki ya nchi yetu na sote ni muhimu na hakuna aliye muhimu zaidi kuliko mwingine."

  Alisema wazee wa kiislaam walisimama katika viwanja vya Mnazi Mmoja miaka 50 iliyopita kupambana na dhulma, uonevu na kudai ukombozi wa Tanzania na kwamba na wao wamekutana hapo kufanya kama kile kilichofanywa na wazee hao.

  "Tutachagua kiongozi mwenye imani ambaye atakuwa muadilifu na hatutakubali kubabaishwa na suti ya mtu yeyote. Sisi kuingia katika uchaguzi kama kundi maslahi si dhambi," alisema Issa.

  Pia alimshukia Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Philip Marmo kwa kuwaonya Waislaam kutoa mwongozo huo wakati alishindwa kufanya hivyo kwa waraka wa Kanisa Katoliki uliotolewa miezi kadhaa iliyopita.

  "Hii yote ni kwa sababu serikali haina mdomo mbele ya kanisa na hata Kingunge ambaye alionya waraka huo amezidiwa nguvu na kufunga mdomo kwa kusema 'No Comments' alipoulizwa na vyombo vya habari juzi,"alisema.

  Baada ya hotuba hizo, mwongozo huo ulianza kuuzwa kwa Sh2,000 kwa nakala na watu walijipanga kwenye misululu wakisubiri kununua waraka huo.  Mawazo yangu,
  Kama kuna kitu kitawachanganya waislaam wenyewe na kufanya wasielewane wakati fulani ni kura ya kundi, hata kama maelezo yao ni mazuri kiasi gani, kwenye kura ya kundi wamekurupuka na ndio maana BAKWATA imewatosa

  Nimeamini Katoriki wako very smart na approach zao ukiwalinganisha na hawa ndugu zetu!!
   
 2. M

  Malila JF-Expert Member

  #2
  Aug 29, 2009
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Je unaweza kutuwekea hapa waraka/mwongozo huo ili kila mmoja wetu asome neno kwa neno?
   
 3. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #3
  Aug 29, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mkuu Catholics are not only smart kwenye kuandika na hata kujibu hoja .Wao hakuna kura maslahi wala nini ni kupiga kura kwa mtu ambaye wanaamini si fisadi na anaweza ku deliever awe muislam ama mpagani .They are after changes na kuikoa nyoyo za watu na kuwaacha mafisadi wakaitumikie Dunia nyingine .

  Wekeni waraka tuuzamie
   
 4. M

  MC JF-Expert Member

  #4
  Aug 29, 2009
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 751
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Niko mbali na TZ, ila kuna mtu ana hard copy, nimemshawishi atafute soft copy!!!

  Najua wana JF mbalimbali wanashughulikia pia hili, yeyote atakaye pata mapema atuwekee, tuusome weekend hii.
   
 5. c

  chach JF-Expert Member

  #5
  Aug 29, 2009
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 433
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 60
  Hivi hawa waislam hawawezi kujenga hoja bila kutaja au kutoa reference kwa wakatoliki au wakristo?
   
 6. c

  chuli Member

  #6
  Aug 29, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 5
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  MIMI NAONA HAWAJAKOSEA,
  Walichofanya nikuonyesha kwamba hawapingi ufisadi bali wanapinga kanisa.
   
 7. c

  chuli Member

  #7
  Aug 29, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 5
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Unauliza majibu?
   
 8. m

  mdini Member

  #8
  Aug 29, 2009
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unajua waislamu kutokana na historia yao ya kulipua na mabomu na shari za hapa na pale wanadhani hakuna wakristu tulio beyong ya hapo walipofika wao.

  Shime wakristu wenzangu huu ndio muda wa kusimama imara kuliko nyakati zote, MUNGU wa Israel lazima atapigana upande wetu.

  Lolote liwe, kama ni mapigano na yaje tuu, tutapigana tuu, watakaobaki watafaidi matunda ya ushujaa wetu.
   
 9. Ngida1

  Ngida1 JF-Expert Member

  #9
  Aug 29, 2009
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 554
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  "MUNGU wa Israel lazima atapigana upande wetu".
  Mungu wetu kwani yupo wapi hata tukachukue huyo wa Israel??????
   
 10. m

  mdini Member

  #10
  Aug 29, 2009
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mungu wako ni shetani hatufai
   
 11. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #11
  Aug 29, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Vijana mjue kwamba hapa forum kuna wazee pia tuko na sisi huwa huna ungana na hoja yenye nguvu na si nguvu ya kuweka hoja .Maongezi yenu haya nadhani hapa si mahala pake .
   
 12. J

  Jews4ever Member

  #12
  Aug 29, 2009
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 74
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mahala pake wapi babu?
  Nadhani wewe ndiye umepotea,hapa siyo mahala pako.
   
 13. M

  Magezi JF-Expert Member

  #13
  Aug 29, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  ninyi mnao kashfiana mnapoteza muda tu wala hata huyo shetani hawasikii
   
 14. d

  dullymo Senior Member

  #14
  Aug 29, 2009
  Joined: Aug 21, 2009
  Messages: 107
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  bro, waisilamu lazima watoe reference kwa wakatoloki kwa sababu wao ndio waliotoa waraka.in case ungekuwa wewe mwenzetu je ungetoa reference kwa mabaniani au kwa wapagani? lazima watatoa reference kwa wakatoliki kwa sababu ndio walioanzisha na hata kama likija kutokeas kundi lingine la dini nalo likatoa waraka wake basi litarefer kwa waisilamu na wakristo na itaendelea kuwa hivyo. nafikiri umenipata
   
 15. Z

  Zhule JF-Expert Member

  #15
  Aug 29, 2009
  Joined: May 22, 2008
  Messages: 354
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [quote

  "Waislaam nchini tumedanganywa sana na wanasiasa wasio waaminifu chini ya serikali ya Chama cha Mapinduzi, lakini kuanzia sasa tunaingia katika uchaguzi na kupiga kura ya maslahi kama kundi maslahi, na hili si jambo baya," alisema Sheikh Basaleh.

  "Waislaam hawapaswi kukubali kudhulumiwa hata kidogo na serikali haipaswi kufanya ubaguzi wa aina yoyote kwa sababu sote tunaipenda nchi yetu, sote tuna haki ya nchi yetu na sote ni muhimu na hakuna aliye muhimu zaidi kuliko mwingine."
  "Tutachagua kiongozi mwenye imani ambaye atakuwa muadilifu na hatutakubali kubabaishwa na suti ya mtu yeyote. Sisi kuingia katika uchaguzi kama kundi maslahi si dhambi," alisema Issa.
  "Hii yote ni kwa sababu serikali haina mdomo mbele ya kanisa huo.[/quote]

  Anyway ni mambo mazito.
  Lakini ili la kupiga kura kama kundi maslahi inamaana mtatanguliza maslahi ya waislamu na kusahau Tanzania? katiba ya jamuhuri ya muungano mmeipa nafasi au la? Kama yes Ok. Kupiga kura kama kundi kufanya kazi ni vigumu. Mungesema maslahi ya nchi (watanzania) Ni raisi kueleweka.Maisha ni ya mmoja,mmoja na sheria haitawabagua.
  "Waislaam hawapaswi kukubali kudhulumiwa hata kidogo na serikali haipaswi kufanya ubaguzi"
  Angalia list ya kamati kuu ya CCM,NEC ya CCM, wabunge, wakuu wa mikoa, wilaya, mawaziri, majaji, makatibu wakuu, makamanda, rais,makamu wa rais, mwenyekiti wa CCM, katibu mkuu wa CCM je idadi ya waisilamu ni haba kweli?Hapa sijui hoja ya kudanganywa iko wapi au kudhulumiwa iko wapi.
  Tutachagua kiongozi mwenye imani " Hii list kubwa ya waisilamu waliopo madarakani hawana imani? Labda wanamaana serikali iwe na dini?.Na hao wasiowaslamu wamewafikiria? wanajua idadai yao? Nadhani hapa kuna mapungufu.
  Hii yote ni kwa sababu serikali haina mdomo mbele ya kanisa.
  Inamaana kama kanisa isingetoa muongozo wao, udanganyifu, dhuluma mnayofanyiwa na serikali isiyekuwa tatizo?
  Nadhani mungejenga hoja zaidi kwenye matatitizo yanayowakabili watanzania mungeeleweka na kuungwa mkono Zaidi kuliko Dini.Naamini jamii kubwa ya wasomi wa Tanzania makazini, vyuoni, secondari za serikali, vijiji, mashuleni matatatizo yao yanafanana si dhani kuna wenye unafuu kwa sababu ni wakristo. Mishahara posho,kazi zao ni moja. Hili la waislamu (akiwemo raisi na makamu) ni wa daraja la Pili sidhani kama mnaweza kueleweka kwa hili.
   
 16. M

  Magezi JF-Expert Member

  #16
  Aug 29, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Ni nani asiyejua waislamu siku zote kila walipo ni kulia tu, tunaonewa tunaonewa. Cha ajabu ni nchi kama Pakistani, karibu nchi yote ni waislamu lakini wao kwa wao bado tu wanachinjana sasa sijui pale pakistani anayewaonea ni mkristu au ni nani?

  ninyi chinjaneni tu sisi tutakuwa tunawaangalia kupitia dirisha alilotupa Bwana yesu.
   
 17. S

  Shamu JF-Expert Member

  #17
  Aug 29, 2009
  Joined: Dec 29, 2008
  Messages: 511
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0


  Una maana ya wako smart na vitendo vyao vya Crusaders. Wanataka kila mtu awe mkatoliki. Soma historia ujue Wakatoliki walivyokuwa wanaua wasio Wakatoliki. Walikuwa wanua hata Wakristo wenzao ambao siyo Wakatoliki.
   
 18. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #18
  Aug 29, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Shamu bwana
  Unakuwa kama si mwelewa ?
  Ni kweli Wakatoliki waliua sana wale ambao hawakuutaka Ukatoliki .Maisha ya mwanadamu ni historia na Ukatoliki sasa kwa yale ya zamani ni historia wakaja na misingi imara .Nakuwa sikuelewi ukisema wakatoliki wanataka kila mmoja awe mkatoliki sijui kama unaweza kunipa mfano.Ila nina kijua ni kwamba waaslimu wanaota muda wote kudhani wataweza kuubadilisha ulimwengu kuwa wa kiislam .Wakatoliki baada ya mauaji waliona ni ujinga mtupu na ndiyo maana leo wanakuja na issues ambazo si rahisi kuzielewa kwa kuwa mna mawazo potofu muda wote .Yes they are smart na endeleeni kulia lia sisi tunapeta .

  jadilini waraka wa ndugu zetu waislam tuone kama una akili kama ule wa wakatoliki ndiyo issue pekee .
   
 19. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #19
  Aug 29, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Waislam ni tatizo sana hapa duniani.
   
 20. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #20
  Aug 29, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Ni mwongozo mzuri kabisa ya kupiga kura kama Muislamu na si Mtanzania,ukweli wamepiga kura kama Watz na hakuna wanalopata zaidi ya marungu ,na hapa ndipo CCM itakapoumbuka ikumbukwe tu asilimia 75 ya waTz ni waislamu.
   
Loading...