Mkutano wa waandishi: Lipumba, Shelukindo, TANESCO na PPRA

Watakuja na kuhalalisha ununuzi wa mitambo; To me.. watakuwa mashujaa kama watataka serikali itaifishe mitambo hiyo.
 
Kasheshe,
Mwakyembe aliposema shirika ni la Walalahoi ana maana ni shirika na wazawa, wazalendo, wananchi na sio mgeni toka nje!..

Kifupi tuache yoteee haya nam quote 911 kwa maelezo yake machachei na mazito sana..

-TANESCO walishasema wamejitoa kwenye Dowans,
-Ngeleja alisema serikali haitanunua mitambo ya Dowans,bali wataagiza mingine ya MW 150,pia akasema ANAUFUNGA MJADALA WA DOWANS....
-Spika alisema TANESCO isije ikanunua mitambo ya Dowans,
-Thisday wameandika kuwa imeweka collateral,
-Kanuni za manunuzi ya umma haziruhusu ununuzi wa mitambo chakavu
-CHECHE imedokeza kuwa Portek haina hisa Dowans Tanzania Ltd
-TANESCO/Ngeleja wanasema hali ya maji ktk mabwawa unakozalishwa umeme.Hivyo udharura wa nchi kuingia gizani haupo.

Sasa sijui hawa wanataka kuzungumzia nini?Im confused! - MIAFRIKA NDIVYO TULIVYO!
 
Watakuja na kuhalalisha ununuzi wa mitambo; To me.. watakuwa mashujaa kama watataka serikali itaifishe mitambo hiyo.

Huu ushujaa tunaombea utokee ndio unaoepelekea mambo ya GUINEA na MALAGARASI (MADAGASCAR) ambako badala ya mlalahoi kukombolewa wanaishia kuiweka rehani nchi mikononi mwa MITANDAO YA WAUZA UNGA WA KIMATAIFA...

Demokrasia makini haiwezi kujengwa kwa kuvunja utamaduni/utawala wa SHERIA. Kama kuna nafasi ya kisheria kwa serikali kufanya hilo sawa lakini kama hakuna ni muhimu kukubali kupigwa bao kuliko kuhalalisha UBABE WA DOLA dhidi ya utamaduni wa kuheshimu mfumo wa sheria. Kama mfumo huo unatuwekea usiko basi tusisite kutumi njia rasmi zilizopo kubadili mambo hata kama itachukua muda mrefu na pia kutuongezea maumivu zaidi kwa muda...

Leo tunaweza kuwaona mashujaa kwa kupingana na utamaduni wa sheria katika kuhakikisha tunafanikiwa kupata kile ambacho kinaendana na matakwa yetu kesho watakuja haohao ama wengine wakatumia ushujaa kama huo kupingana na utamaduni wa kuheshimu sheria kufanikisha kile ambacho ni tofauti na matakwa yetu...

Ujenzi wa jamii ya kidemokrasia ni kazi isiyo na kikomo na inayohitaji umakini na uvumilivu wa hali ya juu

omarilyas
 
Taarifa:

"Tumezungumza na watu wa PPRA, TAnesco n.k tumeangalia njia mbalimbali mbadala za kuweza kuona kama tunaweza kupata umeme wa dharura kwa njia nyingine. bla bla bla

tumetambua kuwa nibora tuyanunue majenereta ya Dowans kwa sababu zifuatazo.

a. Bado ni mapya (yana umri mrefu)
b. Tayari yako nchini (hatuendi kutafuta kwingine)
c. Hakuna sheria yoyote ya manunuzi itakayokiukwa (ndiyo maana PPRA wapo hapa)
d. Dowans wako tayari kufuta kesi dhidi ya Tanesco (ndiyo maana Tanesco wako hapa)
e. Tunaamini ni kwa ajili ya maslahi ya Taifa (ndiyo maana Zitto yupo hapa)

Kwa hiyo tunaomba Watanzania watambue kuwa kununua majenereta haya ni kwa ajili ya maslahi ya taifa. Hakuna ufisadi wowote ule.

Jibu langu bado ni: HE....L.L TO THE NO!! WHY? who the f is dowans and how did they get in the country? why should a company that entered the country under false pretense be paid millions of dollars from Tanzanians taxpayers?

Kwa sababu kama wazazi wa Dowans Tanzania LImited hawakuzaliwa, Dowans haiwezi kuwepo! Otherwise, just seize and confiscate the damn turbines. Don't we have any bowls left/
 
Mzee Mwanakijiji,
Hivi huyu Zitto kaingia wazimu au kitu gani?..haya huo mkutano wao wa kesho nani analipa Posho!..
 
Mzee Mwanakijiji,
Hivi huyu Zitto kaingia wazimu au kitu gani?..haya huo mkutano wao wa kesho nani analipa Posho!..

Kipindi kile napinga wanasiasa wanaopata umaarufu kwa kupandilia migongo ya watu si unakumbuka walisema natetea mafisadi.

Sasa Mashujaa wetu na thax mvua kunani leo??
 
Mzee Mwanakijiji,
Hivi huyu Zitto kaingia wazimu au kitu gani?..haya huo mkutano wao wa kesho nani analipa Posho!..

Hakuna POSHO isipokuwa huwa wanatoa soda na biscuts na pengine lunch. fedha hutoka katika vyanzo mbalimbali vikiwemo NGOs za kimataifa na balozi mbalimbali za nchi za magharibi zinafadhili shughuli za EDITORS FORUM kwa ujumla...

omarilyas
 
Nafurahia uwepo wa Shelukindo hapo maana yeye ndiye alikuwa mpishi mkuu wa utekelezaji wa sera za ubinafsishaji zilizopelekea TANESCO kufika hapo ilipo akiwa kama Katibu Mkuu wa wizara nyeti na baadaye Mwenyekiti wa Kamati ya Mashirika ya Umma kama sikosei. Natumai wahariri watamuuliza ni alifanya kuzuia juhudi za makusudi kabisa za kumasikinisha TANESCO kama mkakati wa kuhalalisha UUZAJI wake hapo mbeleni kama ambavyo walikuwa wamepanga....

Haya yamefanyika kwa mashirika mengi ya umma na mwisho wake ni madhila makubwa kwa mtanzania na wanapotokea watu wanaotaka kubadili hali kwa kuangalia masuala haya zaidi ya siasa za UFISADI na Mashindano ya kimakundi ndani ya CCM wanatuhumiwa UFISADI. Yaleyale ya REPUBLICANS wa Marekani ambao wahubiri na walinzi wa kubwa wa sera zilizomasikinisha nchi yao halafu leo wanakuwa mabingwa wa "naming and shaming" politics dhidi ya jitihada za wengine wenye nia ya kusafisha madudu yao waliyofanya hapo nyuma.

omarilyas
 
Naona JK karejea, sijui kama hasafiri tena ndani ya wiki hii, nina wasiwasi anaweza kwenda mapumziko kwenye Mbuga za wanyama, sijui kwa kazi ipi aliyoifanya? tutashangaa sana utawala huu!!
 
Msimamo wa PPRA kuhusu ununuzi wa mitambo ya Dowans unajulikana toka 2007,
msimamo wa Zitto unajulikana,
msimamo wa Lipumba unajulikana,
msimamo wa TANESCO unajulikana na
msimamo wa serikali unajulikana - wote wako pamoja.
Msimamo wa Shelukindo unapingana na wote hao.
Msimamo wa upande gani utapeta ?
Jibu analo acting Prez wa TZ - Huyo mwingine aliyechaguliwa 2005 achaneni naye, hana lolote, yuko likizoni.
 
nashangaa sana tangu saga lianze yeye anajifanya kama ni raisi wa Malawi au nchi gani sijui....anajifanya hasikii kitu ina maana hajui linaloendelea?

......Ngoja arudi dar atatuambia ya london alipokuwa na Gordon.....

Anajua akizungumzia hilo mtataka kumhoji maswali magumu na yeye hayupo tayari kusema ukweli hivyo kukaa kimya kwake ndio suruhisho
 
edited by Mkandara...
Naogopa

Suluhisho la kuokoka na hasira za dowanz ambao wamefungua mashitaka huko Franz ni kununua mitambo na baadae kesi kufutwa la sihivyo kuna hasara ingine inakaribia ni faini tu wa kuvunja mkataba kiholela kutokana na matatizo yenu ya kukosa ulaji.
 
Wameanza kuwasili ulinzi ni mkali ,ila nimeambiwa nisionekane karibu hivyo naondoka kuelekea kusiko julikana.
 
Mwiba wewe CUF nini? maana zikiongelewa habari za Cuf au Lipumba unafurahiiiiiiii unakuja na details ile mbaya.
 
Back
Top Bottom