Mkutano wa waandishi: Lipumba, Shelukindo, TANESCO na PPRA

Invisible

Robot
Feb 11, 2006
9,075
7,878
Wanatarajiwa kukutana na jukwaa la wahariri kesho katika Hoteli ya Kilamanjaro (Kempinski).

Kitakachoongelewa tutajitahidi kukileta kama kilivyo.

Tutarajie nini?
 
Last edited by a moderator:
Mr dowans aka Zitto mwaka huu atajua watz sio lelemamama tena...

.......mbona naona kuna kutapa tapa kwenye sakata hili?

......jana kajibu Dr mwakyembe...kesho hao tena na bado A nae atakuja kujibu......

.......hivi JK mbona hazungumzii hii issue???
 
Ikiwa Lipumba yupo basi kuna muelekeo wa kufundishwa watu na sio mtu ,naona Mchumi wa kutegemewa duniani ameamua kuwaweka sawa mafisadi wajanja lazima atatoka na mahesabu ya kutegemewa ila watakaopoteza masilahi hawatakosa la kusema ,huyu jamaa namwaminia kabisa maana nilimuona akitoa mada kule ulaya mizungu yote inaandika notes kama haina akili vizuri ,na hawakuwa la kuuliza isipokuwa kumpongeza.
 
Hata mimi nimejiuliza hilo swali....na saa ingine huonekana kama vile tuna ma co-presidents!!
nashangaa sana tangu saga lianze yeye anajifanya kama ni raisi wa Malawi au nchi gani sijui....anajifanya hasikii kitu ina maana hajui linaloendelea?

......Ngoja arudi dar atatuambia ya london alipokuwa na Gordon.....
 
-TANESCO walishasema wamejitoa kwenye Dowans,
-Ngeleja alisema serikali haitanunua mitambo ya Dowans,bali wataagiza mingine ya MW 150,pia akasema ANAUFUNGA MJADALA WA DOWANS....
-Spika alisema TANESCO isije ikanunua mitambo ya Dowans,
-Thisday wameandika kuwa imeweka collateral,
-Kanuni za manunuzi ya umma haziruhusu ununuzi wa mitambo chakavu
-CHECHE imedokeza kuwa Portek haina hisa Dowans Tanzania Ltd
-TANESCO/Ngeleja wanasema hali ya maji ktk mabwawa unakozalishwa umeme.Hivyo udharura wa nchi kuingia gizani haupo.

Sasa sijui hawa wanataka kuzungumzia nini?Im confused!
 
JK hawezi kuongelea hilo kwa sababu anajua watu watammalizia hapo, hapo ni pagumu atasimama upande upi? je atasimama kwa watu wanaosema ni busara kununua mitambo ya dowans ambayo ina utata mkubwa, ili mwakani watu wampige chini? au atasema kwamba mitambo haifai kununuliwa ambayo ni mali ya jamaa zake ambao walimweka madarakani, akifanya hivyo je hawa jamaa watakubaliana na hilo la kuangamizwa na mfuasi wao JK?. Kazi ipo jamaa amezibwa mdomo, maana jamaa nao wanaweza kumpoteza kabisa kwenye ulingo wa siasa. Tunasubiri kitakacho jiri kesho. asante mkuu kwa information
 
Of course, it doesn't make sense rais kuliongelea hilo jambo kwa wakati ambao hata haija-be-escallated kwa PPRA.

Jamani Mwakyembe ameongea yote nikamwelewa... lakini kuna moja sipendi kulisikia sana... watu wakikosea mambo yao ya kibiashara wana kawaida ya kututumia sisi wananchi kama ngao...

Ati mtu anasema kampuni ni la walala hoi kwa masilahi ya Taifa... well mimi nafahamu biashara yoyote ni kwa ajili ya kupata faida...

Mwakyembe alinikumbusha wakati mengi alipozidiwa kete na african media wale wa DTV kwenye world cup ya 1998... jamaa akasema ati anafanya kwa maslahi ya wananchi... ..nikasema du.... haya mzee... kwa sababu sisi wadanganyika tunakubali kila kitu!
 
Ikiwa Lipumba yupo basi kuna muelekeo wa kufundishwa watu na sio mtu ,naona Mchumi wa kutegemewa duniani ameamua kuwaweka sawa mafisadi wajanja lazima atatoka na mahesabu ya kutegemewa ila watakaopoteza masilahi hawatakosa la kusema ,huyu jamaa namwaminia kabisa maana nilimuona akitoa mada kule ulaya mizungu yote inaandika notes kama haina akili vizuri ,na hawakuwa la kuuliza isipokuwa kumpongeza.

Heheheeeeeeeeeeeeeee Lipumba anafundisha kesho jamani, kweli maji ya kifuu ni bahari ya chungu na sisimizi

Haya waandike minotsi hiyo tuone dhana ya mkono mtupu.... yaani asilimia 1 ya watz wataunga mkono
 
Of course, it doesn't make sense rais kuliongelea hilo jambo kwa wakati ambao hata haija-be-escallated kwa PPRA.

Jamani Mwakyembe ameongea yote nikamwelewa... lakini kuna moja sipendi kulisikia sana... watu wakikosea mambo yao ya kibiashara wana kawaida ya kututumia sisi wananchi kama ngao...
Ati mtu anasema kampuni ni la walala hoi kwa masilahi ya Taifa... well mimi nafahamu biashara yoyote ni kwa ajili ya kupata faida...

Mwakyembe alinikumbusha wakati mengi alipozidiwa kete na african media wale wa DTV kwenye world cup ya 1998... jamaa akasema ati anafanya kwa maslahi ya wananchi... ..nikasema du.... haya mzee... kwa sababu sisi wadanganyika tunakubali kila kitu!

Kasheshe.. katika mjadala huu wote usifanye kosa kama la Zitto.. never count politics out of this. Kwa sababu at the end of the day.. wanachezea hoja mbele ya wananchi.
 
Hata mimi nimejiuliza hilo swali....na saa ingine huonekana kama vile tuna ma co-presidents!!

Kaka sasa kama RAIS atakuwa anaingilia kila kitu hivi ASASI zingine kama bunge, baraza la mawaziri, mahakama, vyombo vya habari, watendaji nk si zitaendelea kudumaa. Hii style ya JK kukaa kimya na kuacha wahusika kama Mawaziri, Wabunge, Vyama vya upinzani, Watendaji, Wataalamu, Waandishi, Wanaharakati, Mafisadi na wengineo kushughulika na masuala motomoto kama haya inaweza kuonekana kama ni uoga lakini ukweli ni kuwa inasaidia sana kukuwa kwa ASASI zetu za utawala na pia mfumo wetu wa demokrasia.

Ukweli ni kuwa huyu JK zaidi ya RAIS yeyote tuliyewahi kuwa naye amefanikiwa sana katika kusaidia kukua kwa asasi zingine za utawala ama kwa kutaka au kwa kulazimika kufanya hivyo...

omarilyas
 
Mwakyembe alinikumbusha wakati mengi alipozidiwa kete na african media wale wa DTV kwenye world cup ya 1998... jamaa akasema ati anafanya kwa maslahi ya wananchi... ..nikasema du.... haya mzee... kwa sababu sisi wadanganyika tunakubali kila kitu!

Hili ndilo nililokua nalifikiria jana nzima. Na zaidi matumizi ya neno "wazawa" na "wazalendo". Typical MENGI strategy akiwa anajitahidi kulazimisha ushindi pale anapokamatwa kubaya....

omarilyas
 
Tatizo ni kuwa hawa jamaa wana agenda nyingine kabisa!! Issue ni JK na "nasaba" zake, si utendaji wake!! Wasome vizuri utawaelewa siku moja......kaaazi kweli!!!

Kaka sio wote wenye agenda hiyo. Wapo wengi tu ambao wanaamini kuwa style ya JK ni mbaya kwani wangependa RAIS wa aina ya NYERERE na wanashindwa kutambua athari za kuwa na rais wa aina hiyo katika enzi za DEMOKRASIA ya ushindani/kiliberali...

omarilyas
 
-TANESCO walishasema wamejitoa kwenye Dowans,
-Ngeleja alisema serikali haitanunua mitambo ya Dowans,bali wataagiza mingine ya MW 150,pia akasema ANAUFUNGA MJADALA WA DOWANS....
-Spika alisema TANESCO isije ikanunua mitambo ya Dowans,
-Thisday wameandika kuwa imeweka collateral,
-Kanuni za manunuzi ya umma haziruhusu ununuzi wa mitambo chakavu
-CHECHE imedokeza kuwa Portek haina hisa Dowans Tanzania Ltd
-TANESCO/Ngeleja wanasema hali ya maji ktk mabwawa unakozalishwa umeme.Hivyo udharura wa nchi kuingia gizani haupo.

Sasa sijui hawa wanataka kuzungumzia nini?Im confused!

NDIO demokrasia hiyo kaka. Kuzungumza na kuzungumza na kuzungumza zaidi. Hata kama mitambo haitanunuliwa lakini mimi na wewe tunaelimika zaidi na zaidi kuhusu siasa na hali ya uongozi wa nchi yetu. Na hii ni muhimu katika kuwezesha kukuwa kwa utamaduni wa demokrasia katika jamii kama yetu.
omarilyas
 
Ikiwa Lipumba yupo basi kuna muelekeo wa kufundishwa watu na sio mtu ,naona Mchumi wa kutegemewa duniani ameamua kuwaweka sawa mafisadi wajanja lazima atatoka na mahesabu ya kutegemewa ila watakaopoteza masilahi hawatakosa la kusema ,huyu jamaa namwaminia kabisa maana nilimuona akitoa mada kule ulaya mizungu yote inaandika notes kama haina akili vizuri ,na hawakuwa la kuuliza isipokuwa kumpongeza.

Kumbuka kuwa Lipumba aliunga mkono ununuzi wa mitambo hii chakavu. Sasa sijui kama amejirudi au ndo ataendelea kuwapalilia njia Dowans wauze mitambo yao.
 
Back
Top Bottom