Mkutano wa uwekezaji kufanyika Mpanda; RAIS Jakaya Kikwete anatarajiwa kufungua mkutano huo

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,779
Monday, 26 September 2011 20:51
jkikwete.jpg
Rais Jakaya Mrisho Kikwete​
Aziza Masoud

RAIS Jakaya Kikwete anatarajiwa kufungua mkutano wa uwekezaji kwa Kanda ya Ziwa Tanganyika unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao.

Mkutano huo wa siku nne utafanyika Oktoba 17 katika Mji wa Mpanda utahusisha Mikoa ya Rukwa, Katavi na Kigoma utaanza rasmi Oktoba 15 mpaka 18 mwaka huu ambao utaambatana na maonyesho ya vivutio mbalimbali vilivyopo katika ukanda huo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Stella Manyanya alisema kuwa lengo la mkutano huo ni kuonyesha vivutio vilivyopo katika ukanda huo pamoja na mafanikio yaliyopatikana kwa wale walioanza kuwekeza.

“Watu watapata fursa ya kutembelea mabanda ya maonyesho katika eneo la mkutano yenye lengo la kuonyesha vivutio mbalimbali vilivyopo katika ukanda huu na mafanikio yaliyopatikana kwa wale walioanza kuwekeza,” alisema Manyanya.

Alisema kuwa sababu ya kufanya mkutano kwa ushirikiano wa mikoa hiyo mitatu ni kufanana kwa mazingira ya kijiografia ya mikoa hiyo katika sekta nyingi.

Pia mikoa yote mitatu ipo pembezoni huku ikipakana na Ziwa Tanganyika na nchi za Zambia, Kongo, Rwanda na Burundi pamoja na kufanana kwa mila na desturi zao.

Manyanya pia aliwataka wananchi kuwa wazalendo na kuwekeza katika mkoa huo kutokana na kuwa na vivutio vingi na kuacha fikra za nchi kuwekezwa na watu kutoka nje ya nchi.

 

jogi

JF-Expert Member
Sep 25, 2010
25,581
25,244
Mnatengeneza mgogoro wa taifa letu dhidi ya wawekezaji. Kwa tafsiri ya moja kwa moja wanatengeneza uhalali wa kutumia vifungu vya sheria kuwashirikisha wananchi kuridhia mikataba ambayo tafsi yake ni kuuza kipande cha nchi ya tanganyika. Wanarukwa kama mko tayari kutawaliwa, tunawaambia huo ni uhaini!!!!! Narudia uhaini, uhaini, haiwezekani mmu itamke mkiwa na mgogoro juu ya ardhi yenu na mwekezaji mwenye mamlaka ya kuwaamua ni kaka yake na mwekezaji. Uhaini... Some one stop this madness.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom