Mkutano wa tisa wa bunge la Tanzania kuanza kesho

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,409
20,758
Bungeni%20Dodoma%201.jpg

Mkutano wa Tisa wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linatarajia kuanza kesho ambapo miongoni mwa masuala ambayo yatashughulikiwa ni pamoja miswada minne ya sheria mbalimbali ikiwemo mswada wa marekebisho ya sheria ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya mwaka 2017.

Akizungumza na waandishi wa habari Katibu wa Bunge Mh Stephen Kagaigai amesema Bunge pia litajadili na kupitisha mapendekezo ya mpango wa taifa wa maendeleo unaotarajia kutekelezwa kwa mwaka 2017/2018.

Baadhi ya wabunge waliozungumza na ITV wamesema wamejipanga vyema kuisimamia serikali wakiwa kama wabunge na kujadili kwa kina hoja zitazo wasilishwa.

ITV ilifika katika Ofisi hizo za Bunge na kushuhudia maandalizi mbalimbali yakiendelea huku baadhi ya wabunge wakiwasili katika ofisi hizo za Bunge.


Chanzo: ITV
 
........Baadhi ya wabunge waliozungumza na ITV wamesema wamejipanga vyema kuisimamia serikali wakiwa kama wabunge na kujadili kwa kina hoja zitazo wasilishwa...........

Hakuna wa kujipanga, porojo tu
 
Hela zinapotea bure tu, bunge halina maana utawala huu. Kama Sizonje anapanga mwenyewe matumizi ya hela na Bunge limemezwa na mhimili wenye mizizi mirefu, la kazi gani hilo??
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom