Mkutano wa Sekta ya Mafuta na Gesi - Oktoba 24-26 Arusha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkutano wa Sekta ya Mafuta na Gesi - Oktoba 24-26 Arusha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Sep 20, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Sep 20, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Mkutano huu unatarajiwa kufunguliwa na Waziri wa Nishati na Madini Dr. Sospeter Muhongo. Dhamira ya mkutano huu inasema Transforming Tanzania’s mining and energy resources into wealth for Tanzanians and for future generations. Makampuni yafuatayo yametajwa kuwa yatapeleka wawakilishi wao: Oryx, Petrobras, African Barrick Gold, Uranex, Anglo Gold Ashanti na Geita Gold Mining Ltd. Waziri wa Madini wa Ethiopia Sinknesh Ejigu anatarajiwa pia kuwa mgeni katika kongamano hilo.

  Baadhi ya watu ambao wanafuatilia kwa karibio maendeleo ya sekta hii ni pamoja serikali ya Marekani na baadhi ya nchi za kiarabu. Serikali ya Marekani imekuwa ikituma wajumbe wake na wataalamu wake wa kila aina kutembelea Tanzania ili kutengeneza mazingira ambapo endapo mafuta yatagunduliwa basi na wao wasipitwe. Naibu waziri wa Nishati na Madini wa Falme za Kiarabu Bw. Khaled Ghanem Al Ghaith alipokutana na Rais Kikwete katikati ya mwaka huu aliombwa kuwa UAE isisite kuja kuwekeza kwenye sekta hii muhimu.

  Ikumbukwe katika mkutano wa mapema mwezi huu katika hoteli ya Double Tree jijini Dar wataalamu mbalimbali wa masuala ya mafuta kutoka nchi za Congo, Tanzania, Malawi, Comoro, Msumbiji, Kenya na Uganda walikutana kuzungumzia baadhi ya mambo ambayo yanahusiana na upatikanaji wa mafuta na gesi katika maeneo ya mipakani. Kwa watu wanaoweza kuona mbali ni rahisi kuona kuwa japo eneo letu limekuwa katika hali ya amani haya mafuta na gesi yanaweza kugeuka laana hasa katika maeneo ya mipakani. Mkutano huo wa Dar ulifadhiliwa (na kulipiwa) na serikali ya Marekani. Mkutano huo uliwapa nafasi ya maafisa wa Marekani kufanya "contacts" na maafisa wa wizara hizi za nishati na madini wa karibu eneo zima la Afrika ya Mashariki.

  Ikumbukwe kwamba yote haya yanafanyika wakati serikali haina sera ya kusimamia mafuta na gesi na haina mfumo mzuri wa sheria wa kuendesha sekta hii na hivyo kutuweka mahali pabaya sana hasa kama kiasi kikubwa cha mafuta kitagunduliwa nchini kama dalili zinavyoonesha.

  Sijui ni kwa kiasi gani Chama cha Demokrasia na Maendeleo kimeandaa kupeleka ujumbe huko au wataalamu wake kuweza kuchangia mawazo yao.
   
 2. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #2
  Sep 20, 2012
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,923
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Duh ngoja tuone itakuaje,manake umetoa tahadhari za msingi hasa katika upande wa sera za mafuta na gas,same thng nilisikia janakwa muh zitto na prof muhongo BBC,wakidai kuwa sera zilizopitishwa mwaka 1992 wahusika,serikali haikuwa na uelewa mzuri kwenye sector hii hivyo kuna vifungu ving vya kubadilisha. Ila MMJ hiyo tahadhari ya vita kwa sehemu za pembezoni kama mtwara bado sijailewa,au ni kama ile ya lake nyasa?
   
 3. Manyi

  Manyi JF-Expert Member

  #3
  Sep 20, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 3,256
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Hii taarifa ni nzuri sana, na kwa kweli tunahitaji CDM ipeleke mtu, na si baadae kuja na lawama baadae, hii haitasaidia!
   
 4. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #4
  Sep 20, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Kamanda Mwanakijiji, ni vyema tukaelewa kuwa washikadau wa maliasili ya nchi yetu ni wananchi wote hivyo sioni sababu ya kuwa na mkutano kuhusu madini na gesi ambao hauko wazi kwa mwananchi yeyote mwenye uwezo kuweza kuhudhulia.

  Kuna wananchi wengi wajuzi ambao hawapo kwenye kundi la hao stakeholders walioalikwa kwenye mkutano huo ambao kuwepo kwao kungeisaidia nchi; I have in mind retirees wa sector ya mafuta na madini etc. ambao hawana fursa ya kuhudhulia kongamano hilo.

  Juu ya hayo mkutano huo muhimu kufanyika huko Arusha ni strategy ya kueliminate watu ambao mchango wao ungetusaidia, na wengi wao wako Dar es salaam. Ningeshauri kuwa waziri husika angeufanya mkutano uwe open kwa wananchi wote ambao wangependa kuhudhulia na pia Dar es salaam would have been an ideal place to hold the conference if good results are anticipated!!
   
 5. bwafo

  bwafo Senior Member

  #5
  Sep 20, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 102
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Zipo taarifa kuwa kuna conference nyingine ya mambo ya gesi na mafuta iliyoandaliwa na Chuo kikuu cha Dar es Salaam ambayo itafanyika Mlimani City Hall kuanzia tarehe 18-19 October. Huenda hii ikawa fursa kwa wale waishio Dar ambao wangependa pia mapendekezo yao yasikike kwani delegate wengi ni wale walioalikwa Arusha akiwemo Prof Muhogo
   
 6. Takalani Sesame

  Takalani Sesame JF-Expert Member

  #6
  Sep 20, 2012
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Najuta kwa nini haya mafuta na gesi yamegunduliwa chini ya utawala wa CCM. Inaweza kula kwetu walahi.
   
 7. D

  Deo JF-Expert Member

  #7
  Sep 20, 2012
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 1,193
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Je kuna namna ya kuhudhuria?
   
Loading...