Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,443
- 113,452
Wanabodi,
Leo nimepata tena fursa ya kuendelea na zile makala zangu za kwa Maslahi ya Taifa, leo natoa angalizo kuhusu kuchangamkia fursa za Mkutano wa SADC na Maonyesho ya SADC, kwanza kwa vile maonyesho haya ya SADC, yamegongana na maonyesho ya Nane Nane ambayo kitaifa yanafanyika mkoani Simiyu, ombi langu la kwanza ni tusiache mbachao kwa msala upitao, Maonyesho ya Nane Nane ni mbachao, Maonyesho ya SADC ni msala upitao, uhamasishaji wa maonyesho ya SADC, pia uende sambamba na uhamasishaji maonyesho ya Nane Nane, maana kwa sisi huku Nyakabindi Simiyu, zaidi ya kuzinduliwa na Makamo wa rais Mhe. Samia Suluhu, nimewaona mawaziri wawili tuu, na manaibu wawili, inamaana wengine wote ni SADC?.
Hoja yangu kuu katika bandiko hili ni kwanza kutoa pongezi kwa kazi kubwa na kazi nzuri inayofanywa kuhamasisha mkutano huu wa SADC ambao umerudi tena kufanyika nchini Tanzania baada ya miaka 16. Kiukweli uhamasishaji ni mkubwa, na Watanzania tumehamasika, na kila kada kujipanga kuchangamkia fursa za mkutano huu, kitu muhimu kuliko hata kuchangamkia fursa ni sisi Watanzania na Tanzania yetu kama nchi, inachangamkia vipi fursa za soko la SADC lenye watu milioni 450?.
Pia naomba kutoa angalizo muhimu kwa viongozi wetu, kuhusu conference tourism katika kuwapatia wafanyabiashara fursa za mkutano huu, naombeni sana msiwape too much expectations wengine wakakopa kwa kutegemea zitarudi, hili ninilishuhudia kwenye mkutano wa Sullivan, ulikuwa ni mkutano wa fursa, wakazi wa Arusha wakajitoa kwelikweli, mwisho wa siku kuna wafanyabiashara waliishia kulia na kujuta, haswa kwa kuzingatia hii mikutano ya ngozi nyeusi ni tofauti na mikutano ya ngozi nyeupe, targets ya ngozi nyeusi ni save, save save, wakati ngozi nyeupe ni spend spend spend. Sikubahatika kupata mrejesho wowote ni fursa zipi za Sullivan, Tanzania tulifanikiwa kuzipata.
Mimi nilipata bahati ya kuwemo kwenye kundi la waandishi wa habari wa Tanzania, waliopelekwa nchini Marekani kuelimishwa kuhusu fursa za soko la AGOA. Shirika la misaada la watu wa Marekani USAID wakagharimia viongozi wa wizara ya Viwanda na Biashara, viongozi wa BET (sasa Tantrade), na viongozi wa vyama vya vya wafabiashara mtambuka chini ya TCCIA, CTI na kundi kubwa la wafanyabiashara zaidi ya 100, kwenda nchini Marekani kuonyeshwa bidhaa zinazotakiwa ili kuchangamkia fursa za soko la AGOA.
Kule tulionyeshwa soko la Marekani linataka bidhaa gani, zenye ubora gani, viwango gani, ufungashaji gani na taratibu za kufuata, soko hilo ni kubwa na linahitaji bidhaa nyingi za kila aina zaidi ya 1000 kutoka Tanzania zikiwemo bidhaa za kiutamaduni, vinyago, mapambo, maua.
Wamarekani wakafanya hivyo hivyo kwa Kenya, Uganda, Ghana, Rwanda na Burundi na nchi mbalimbali.
Kilichofuatia ziara hiyo, wafanyabishara wa Tanzania, wakahamasika sana, na waliporejea tuu nyumbani Tanzania, orders zikaanza kumiminika. Kuna kikundi cha akinamama wasuka mikeka ya majani, wakapewa order ya kupeleka 40ft contena la mikeka hiyo inayosukwa akinamama wa vijijini mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara.
Wakinamama wale na kikundi chao, walitembea na hiyo order wakitafuta mtaji wa kuitekeleza hadi ika expire. Ukishindwa ku deliver order ndani ya siku 90, order ina expire, sasa inakuwa wazi kwa kila mwenye uwezo, yaani an open order.
Baada ya siku 90 kupita kwa Tanzania kushindwa kudeliver, makampuni ya jirani zetu Kenya, walikuja nchini, wakaenda Pwani, Lindi na Mtwara wakawalipa wale wamama na kuinunua mikeka yote kwa bei ya karibu na bure na kuisafirisha hadi Nairobi, wakaipakia kwenye makontena na kuifikisha sokoni Marekani, mikeka yenye certificate of origin ya Tanzania, lakini imeingizwa sokoni na Wakenya, huku sisi Watanzania tumelala. Hivi ndivyo inavyofanyika kwa vinyago vyetu, madini yetu, mazao yetu.
Huu ni mfano mmoja tuu wa jinsi sisi Watanzania tunashindwa kuchangamkia fursa za masoko, hadi AGOA ya awamu ya kwanza ya kipindi cha miaka 10 kimepita, Tanzania tumeshindwa kabisa kutumia kikamilifu fursa hizo, huku jirani zetu wakijivinjari kwa kuzinunua bidhaa zetu na wao ndio wanazifikisha sokoni. Sasa AGOA imeongeza miaka 10 mingine, na bado sisi Tanzania kama nchi, bado hatujaweza kuchangamkia fursa za soko la AGOA.
Hali ni hivyo hivyo kwa soko la Afrika Mashariki, Tanzania ndio nchi inayoongoza kwa fursa za kila kitu, ndio nchi inayoongoza kwa utajiri wa kila kitu, kuanzia vivutio vya utalii, maliasili, madini, vyanzo vya maji, ardhi ya kutosha kwa kilimo, udongo wenye rutuba, na sasa tuna gesi asili na soon tutagundua mafuta.
Tanzania tunapakana na nchi 8, kati ya hizo, nchi 6 ni land locked, zisizo na bahari, hivyo sekta tuu ya usafiri na usafirishaji ingeweza kututoa kimasomaso toka kwenye lindi hili la umasikini uliotopea, lakini sivyo. Kufuatia Tanzania kuwa na bandari ya Dar es Salaam, Kariakoo ilikuwa kitovu cha biashara ya bidhaa kwa nchi za Uganda, Rwanda, Burundi, Zambia, Malawi na DRC, lakini sasa, mzingo unashukia bandari ya Dar, unasafirishwa kwenda Uganda, halafu wafanyabishara wa nchi hizo sasa wananunulia Uganda. Hivyo Tanzania tuna kila sababu ya kuwa ni nchi tajiri sana kwa kuchangamkia tuu fursa, lakini hali sii hivyo, bado tunaendelea na umasikini tulionao, ukijiuliza kwanini Tanzania ni masikini, huwezi kupata jibu sahihi.
Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliwahi kusema “umasikini mkubwa zaidi na umasikini mbaya zaidi ni umasikini wa fikra”, fikra ni kama kauli, huumba, ukijifikiria kuwa wewe ni masikini, ni kweli unakuwa masikini kweli, ndio maana msimamo wa Rais Magufuli na kauli yake kuwa Tanzania sio masikini bali ni nchi tajiri na tunakwenda kuwa a donor country , inapaswa kuungwa mkono na watu wote wenye mapenzi mema na nchi yetu Tanzania yetu, tuache kabisa kujiita masikini tukajikuta tunajiumbia umasikini, tuanze kujiita Tanzania ni nchi tajiri ili kujiumbia utajiri.
Nikiangalia kiwango cha uhamashaji mkutano huu na nguvu inayotumika kuuhamashisha mkutano huu, tukiitumia katika kuhamashisha kuchangamkia soko la SADC, uhamasishaji huo utakuwa na manufaa ya muda mrefu zaidi baada ya mkutano kumalizika.
Kinachofanya jirani zetu Wakenya, watushinde kwenye kuchangamkia fursa ni serikali yao kuingiza mkono wake kusaidia, hivyo sasa serikali awamu ya tano imeishaonyesha njia, kwanza kwa rais Magufuli kukaa na wafanyabiashara na kusikiliza kero zao ikiwemo kuchukua hatua za papo kwa papo. Bila mkono wa serikali katika kuweka mazingira wezeshi, wafanyabiashara wenyewe tuu kama wafanyabiashara, hatutaweza kuliteka soko la SADC lenye watu milioni 450, kama hili soko tuu la Africa Mashariki, Tanzania bado!, kwa sasa wanunuzi wakubwa wa mazao yetu ni jirani zetu na sio sisi.
Nawatakia maonyesho mema ya SADC na pia Nane Nane njema.
Paskali