Mkutano wa Rais wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan na Vijana, Uwanja wa Nyamagana Mwanza

vvm

JF-Expert Member
Jul 18, 2014
6,284
10,287
Huu ni uzi huru (sio rasmi)

Kumulika Ziara ya Rais wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan mkoani Mwanza ambapo ataongea na vijana wa Kanda ya ziwa kwa niaba ya vijana watanzania yote.

Huu ni muendelezo wa Rais Samia kukutana na kuongea na Makundi Mbali mbali katika jamii.

Ikumbukwa kwamba vijana ndio kundi la maamuzi na inakadiriwa asilimia 60 ya watanzania ni vijana.

Moja ya Agenda kubwa inayotegemewa kujadiliwa ni ujumuishaji wa vijana katika uchumi ikiwemo ajira, fursa za biashara na kilimo, bila kusahau vijana na siasa jinsi gani vijana wanahusishwa katika maamuzi ya nchi na siasa kwa ujumla.

Vijana ndio taifa la leo na kesho.

Viongozi na Wasanii mbali mbali watakuwepo akiwemo Rayvany,Zuchu, Kala Jeremaya, Peter Msechu, TOT Band, Eliza Band. . nk

Tujumuike pamoja katika mkutano huu moja kwa moja kutoka uwanja wa Nyamagana Mwanza

Na mwisho nitaweka uchambuzi wangu binafsi hapa.

View attachment 1819104
IMG_20210615_081036.jpg
 
Fursa za kijana ziko kwenye dhamira yake, ajue anachokitaka na vipi atakipata haijalishi level ya elimu, hakuna mafanikio ya kweli bila kuwa na lengo na kuhakikisha unajinyima mpaka ulifikie.

Pia hakuna lengo la muda mrefu linalofikiwa bila kupoteza au kuacha sehemu ya mazoea yako ili upate kiasi cha ku-save upate kutimiza malengo yako.

Rais anachofanya leo ni kutengeneza njia, lakini wakuipita njia hiyo ili imfikishe anapopataka ni kijana mwenyewe.
 
exactly
 
  • Thanks
Reactions: vvm

Umesema vyema
 
Hivi mikusanyiko kama hiyo ina ulazima kweli ikiwa kweli mnaamini corona ipo? Au mnategemea barakoa?
 
Fursa za kijana ziko kwenye dhamira yake, ajue anachokitaka na vipi atakipata haijalishi level ya elimu, hakuna mafanikio ya kweli bila kuwa na lengo na kuhakikisha unajinyima mpaka ulifikie.

Pia hakuna lengo la muda mrefu linalofikiwa bila kupoteza au kuacha sehemu ya mazoea yako ili upate kiasi cha ku-save upate kutimiza malengo yako.

Rais anachofanya leo ni kutengeneza njia, lakini wakuipita njia hiyo ili imfikishe anapopataka ni kijana mwenyewe.
malengo binafsi ndo yatakayomuondoa kijana kwenye utegemezi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom