Mkutano wa rais na wazee 22/12/2014 : Msitegemee rais afuate mawazo yenu kuhusu ESCROW

mbeyaman

Member
Sep 28, 2013
97
28
Watanzania tunasubiri kwa hamu kusikia hotuba ya mheshimiwa rais Jakaya Kikwete atakayoitoa kesho atakapokutana na wazee. Baadhi yetu eti tunafikiria kwamba kesho mheshimiwa rais atakurupuka na kuwafukuza vigogo wanaohusishwa na kashfa ya akaunti ya ESCROW, kama tunafikiri hivyo tumepotoka.

Tanzania ni nchi inayofuata utawala wa sheria. Kuna taratibu za kuongoza nchi. Mheshimiwa rais atasimamia taratibu hizi na wala hawezi kutoa maamuzi yeye binafsi bila ya ripoti ya vyombo vya uchunguzi vinavyowachunguza vigogo na watu wanaotuhuniwa na kashfa ya ESCROW, vile vile mkumbuke pia IPTL imefungua kesi kuzuia maagizo ya bunge kuhusu wahusika wa ESCROW yasitekelezwe.

NCHI YETU INA MAMBO MENGI MUHIMU YA KUZUNGUMZIA UKIACHA SAKATA LA ESCROW, HEBU WATANZANIA TUTUMIE MUDA MWINGI KUFIKIRIA MAMBO MENGINE. TUMUACHE RAIS AFANYE KAZI YAKE, TUSILAZIMISHE AFUATE AKILI ZETU.
 
Kuna nani amemwomba kwamba tunataka afuate mawazo yetu?
Huna kielelezo na watu kama nyinyi mnaotetea ushenzi hafai kwenye jamii.
Afanye asifanye maamuzi lakni hakuna lisilo na zao. Mtu huwezi panda mahindi ukavuna mihogo.

Watz sio wajinga na subiri utaona. Ukamwambie boss wako.
 
Bunge lilitoa maazimio yake , raisi anahiari ya kuyatekeleza au kuyatupa. Watanzania tunalijua fika, tatizo lipo kwenu nyie mafisadi na majizi mnaokesha mitandaoni.
 
Hujui mhimili tuliyonayo gvmnt ys tz ndooo maana unalopoka kasome katiba ya 1977 kifungu cha 1@ na c,ukurasa wa 45
 
Rugamalila amelipa kodi lakini Rostam Azizi hakulipa Kodi baada ya kuuza hisa za Voda kwa Dola Milion 300 kisha akamugawia Mengi ili kumaliza Ugonvi wao, Tatizo lilipo ni Rais kutofanya kazi kwa Shinikizo la Mengi na Mkono ambao wanataka Mhongo ang'oke kwa gharama yeyote ile,

Huyo Mengi huwa halipi kodi hata Mkono pia huwa halipi Kodi hata wakilipa huwa hawalipi kodi Stahiki kwa kifupi si watu Saafi ndiyo maana Rais kawa makini kufanya maamuzi ya kuwafurahisha, Kumbuka hili sakata linazigusa Wizara Tatu 1-Wizara ya viwanda na biashara 2-Wizara ya fedha 3- Wizara ya Nishati iweje mengi amkomalie Mhongo peke yake?

Vitalu vya Gesi tu vimemfanya Mengi hapati Usingizi ametumia Mabilioni kuwalipa Sendeka ,Kafulila na Zito ili wamung'oe Mhongo lakini imekuwa ngumu, sasa kahamia kwenye kamati za Ufundi ambazo zipo busy mchana na Usiku. Mengi anashangaza sana yaani badala ya kuboresha Masilahi ya wafanyakazi wake ametumia Mabilioni kumng'oa Mhongo.
 
Naombea awasafishe watuhumiwa wote akiwemo yeye mwenyewe, ili liwe anguko kuu la CCM 2015. Hivi kesha pona tezi?
 
Kuna nani amemwomba kwamba tunataka afuate mawazo yetu?
Huna kielelezo na watu kama nyinyi mnaotetea ushenzi hafai kwenye jamii.
Afanye asifanye maamuzi lakni hakuna lisilo na zao. Mtu huwezi panda mahindi ukavuna mihogo.

Watz sio wajinga na subiri utaona. Ukamwambie boss wako.

Lini Bunge watajadiili haya na kutoa Maazimio 1- Rostam kuuza hisa za Vida kwa dola milion 300 hakulipa Kodi lakini alimugawia Mengi mamilioni Wakamaliza Ugonvi wao, Mengi alikopa NBC kisha akapoteza Ushahidi na akalikwepa Deni, Mengi si mlipaji Kodi mzuri amejaa Madhambi Mengi Kama lilivyo jina lake,

Bunge wajadili hizo pesa alizopewa Sendeka ili apige Mayowe Bungeni zimekatwa Kodi? Dowans iliuzwa kwa Dola M 120 kama lilivyo deni la IPTL je? Dowans waliilipa Kodi? Serikali ilitoa fidia ya dola milion 100 je? Zilikatwa Kodi? Wakiletwa FBI hapa Tz wawachunguze kwa kiina Mengi na Mkono lazima wataelekea jela kwani si watu Saafi, Nchi Hii hakuna aliye Msaafi kiasi cha kumnyooshea mwenzake kidole.
 
Naombea awasafishe watuhumiwa wote akiwemo yeye mwenyewe, ili liwe anguko kuu la CCM 2015. Hivi kesha pona tezi?

Mimi simsafishi Mtu bali nahoji iweje Rais afanye kazi kwa Shinikizo la Mengi ambaye yupo kwa Masilahi binafsi ya Vitalu vya Gesi huku akiwa amesheheni Madhambi kibao Lakini yupo busy kuwanyooshea wenzake vidole.
 
Bunge lilitoa maazimio yake , raisi anahiari ya kuyatekeleza au kuyatupa. Watanzania tunalijua fika, tatizo lipo kwenu nyie mafisadi na majizi mnaokesha mitandaoni.

Mwizi ni baba yako Mengi ambaye Anawaibia wafanyakazi wake kwa kuwalipa mishahara mibovu Huku akitumia Mabilioni kwenye Ligi za kuwang'oa wapinzani wake kibiashara, Mengi halipi Kodi Mengi kama lilivyo jina lake ana Madhambi Mengi sana hapaswi kumnyooshea mtu Kidole kwani yeye ni Mwizi number one.
 
Bila ya swala la escrow kupatiwa ufumbuzi Watanzania tusubiri maumivu.BRN tutaisikia redioni tu.
 
minyoo

Ndiyo maana mimi siku zote nawaambia mengi ni mwizi kama wezi wengine mzee ni fisadi wa hali ya juu hafai kabisa.
 
Last edited by a moderator:
Lini Bunge watajadiili haya na kutoa Maazimio 1- Rostam kuuza hisa za Vida kwa dola milion 300 hakulipa Kodi lakini alimugawia Mengi mamilioni Wakamaliza Ugonvi wao, Mengi alikopa NBC kisha akapoteza Ushahidi na akalikwepa Deni, Mengi si mlipaji Kodi mzuri amejaa Madhambi Mengi Kama lilivyo jina lake, Bunge wajadili hizo pesa alizopewa Sendeka ili apige Mayowe Bungeni zimekatwa Kodi? Dowans iliuzwa kwa Dola M 120 kama lilivyo deni la IPTL je? Dowans waliilipa Kodi? Serikali ilitoa fidia ya dola milion 100 je? Zilikatwa Kodi? Wakiletwa FBI hapa Tz wawachunguze kwa kiina Mengi na Mkono lazima wataelekea jela kwani si watu Saafi, Nchi Hii hakuna aliye Msaafi kiasi cha kumnyooshea mwenzake kidole.

Mauzo makubwa namna hiyo yalifanyikaje kimya kimya bila vyombo vinavyohusika na kodi kuhusika? Pesa zilipita mkono kwa mkono au ndio yale ya viroba vya stanbic? na kuhusu Mengi kukopa na kisha kupoteza ushahidi, aliwezaje kupoteza ushahidi ina maana benki iliyomkopesha haikuwa na ushahidi kuwa imemkopesha? Naona hizi ni porojo tu au kama si porojo basi TRA na hiyo benki wanahusika moja kwa moja.

Kizuri ni kwamba katika kumtetea huyo mzee wenu Ruge na profesa wenu Muhongo, mnaanika maovu zaidi ya CCM. Sisi kwetu tunataka pesa za umma zirudi, iwe kachukua Rostam, Mengi, Ruge, Kikwete au gamba jingine lolote. Mwisho wa siku, CCM mtayaona matokeo ya uchafu wenu kwenye chaguzi zinazofuata.
 
Mwizi ni baba yako Mengi ambaye Anawaibia wafanyakazi wake kwa kuwalipa mishahara mibovu Huku akitumia Mabilioni kwenye Ligi za kuwang'oa wapinzani wake kibiashara, Mengi halipi Kodi Mengi kama lilivyo jina lake ana Madhambi Mengi sana hapaswi kumnyooshea mtu Kidole kwani yeye ni Mwizi number one.

Ujira wa kazi ni makubaliano kati ya mwajiri na mwajiriwa. Kama wao wameridhika huna sababu ya kulalamika wewe. Kama hawajaridhika, ninaamini wanajua taratibu za kudai nyongeza ya mishahara na ninahisi hata chama cha wafanyakazi kitakuwa na tawi mahali pale kwa hiyo wanaweza kukitumia.

Otherwise, ambao wameshindwa kabisa tumeona wakiondoka kwenda kufanya kazi mahali pengine. Kama yeye ndiye mlipaji mbovu kuliko wote, kwa nini watu wasikatae kwenda kufanya kazi kwake na hivyo IPP Media ife? Kuna ambaye anafanya kazi kwa shurutii pale? Naamini ni hiari. Kama hukubaliani, unatafuta kazi nyingine mahali penngine. Period.
 
Mimi simsafishi Mtu bali nahoji iweje Rais afanye kazi kwa Shinikizo la Mengi ambaye yupo kwa Masilahi binafsi ya Vitalu vya Gesi huku akiwa amesheheni Madhambi kibao Lakini yupo busy kuwanyooshea wenzake vidole.

Heee! Mi nilikuwa sijui kuwa kumbe Mengi ni mkubwa kiasi hiki hadi atoe maazimio kwa Rais na Rais akose usingizi kujaribuu kuyatekeleza. Nilidhani Rais alitakiwa kufanyia kazi mapendekezo ya Bunge la JMT kufuatia ripoti ya kamati ya bunge ya PAC.

Hii ya kudai ni mashinikizo ya Mengi naona ni chuki yako tu dhidi ya Mengi, na kwa kuwa sijui wapi mligongana, binafsi sitaki kuingilia, mtamalizana huko huko. Ila kama unataka kutuamimisha kuwa Mengi kaliteka bunge la JMT, basi huyu mzee atakuwa na nguvu za ajabu pia.
 
Kuna nani amemwomba kwamba tunataka afuate mawazo yetu?
Huna kielelezo na watu kama nyinyi mnaotetea ushenzi hafai kwenye jamii.
Afanye asifanye maamuzi lakni hakuna lisilo na zao. Mtu huwezi panda mahindi ukavuna mihogo.

Watz sio wajinga na subiri utaona. Ukamwambie boss wako.

Kama kifo kingekuwa na rushwa basi ningetoa Nyerere arudi tukae nae mwaka tu basi unatosha.
 
Heee! Mi nilikuwa sijui kuwa kumbe Mengi ni mkubwa kiasi hiki hadi atoe maazimio kwa Rais na Rais akose usingizi kujaribuu kuyatekeleza. Nilidhani Rais alitakiwa kufanyia kazi mapendekezo ya Bunge la JMT kufuatia ripoti ya kamati ya bunge ya PAC. Hii ya kudai ni mashinikizo ya Mengi naona ni chuki yako tu dhidi ya Mengi, na kwa kuwa sijui wapi mligongana, binafsi sitaki kuingilia, mtamalizana huko huko. Ila kama unataka kutuamimisha kuwa Mengi kaliteka bunge la JMT, basi huyu mzee atakuwa na nguvu za ajabu pia.

Duuuu hata mimi nimestaajabu ya Musa wazungu kweli huwa wanatushangaaa kwa mengi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom