Mkutano wa Nne wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 7 Juni hadi tarehe 7 Septemba 2011 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkutano wa Nne wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 7 Juni hadi tarehe 7 Septemba 2011

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Dr-of-three-Phd, Jun 3, 2011.

 1. Dr-of-three-Phd

  Dr-of-three-Phd Senior Member

  #1
  Jun 3, 2011
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 194
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mkutano wa Nne wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unaotazamiwa kuanza tarehe 7 Juni hadi tarehe 7 Septemba 2011.


  Posho na alawansi TSh (90,000 x 90) +(7 0,000 x 90) x (239)= ()

  Aluta Continua
   
 2. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #2
  Jun 3, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,004
  Likes Received: 586
  Trophy Points: 280
  mmmmmh!!!! yaani eti mwl. analipwa kilo 3 kwa mwezi, huo sio uhuni ni nini?
   
 3. Dr-of-three-Phd

  Dr-of-three-Phd Senior Member

  #3
  Jun 3, 2011
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 194
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33

  Zembe,
  Tena Wabunge wako 360 na si 239 cheki hapo hii si elimu bure kwa wote hadi Chuo Kikuu, achilia mbali mashangingi, mikatba mibovu, EPA, KIWIRA, MISAMAHA YA KOZI, TOZO ZA MIGODI NDOGO, RICHMOND, MISHAHARA HEWA, TEN PERCENT etc etc.

  Tanzaias Lets Work Up They Have To Work For Us, Not Us fTo work For Them !!!


  Aluta Continua - Mapambano Bado Yanaendelea!
   
 4. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #4
  Jun 3, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,849
  Likes Received: 473
  Trophy Points: 180
  Gharama za posho na allowance nisawa na shs.5,184,000,000=(shs.90,000 x siku 90) +(shs.7 0,000 x siku 90) x ( wabunge360) mtajibeba wabongo
   
 5. Nico1

  Nico1 JF-Expert Member

  #5
  Jun 3, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 746
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 60
  wenyewe si wanaweza ngoja wazigawane halafu waendelee kutudanganya
  kwamba serikari haina hela
   
 6. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #6
  Jun 3, 2011
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,933
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  Kila mbunge atajikusanyia TZS 14.4m. Hii ni nje ya mshara wa kawaida! Naweza kuelewa ni kwa nini katika siku za karibuni mabasi mengi ya kwenda dodoma yana abiria wengi wasichana/wadada!
   
 7. Dr-of-three-Phd

  Dr-of-three-Phd Senior Member

  #7
  Jun 3, 2011
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 194
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kwa sasa mbunge analipwa Sh. 70,000 kwa siku kwa ajili ya kujikimu pamoja na Sh. 80,000 kama posho ya kikao kwa siku ambapo jumla analipwa Sh. 150,000 mbali na mshahara wake.

  Source: :: IPPMEDIA

  3rd June 2011
   
 8. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #8
  Jun 3, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,004
  Likes Received: 586
  Trophy Points: 280
  dawa ni kuwapopoa kwa mawe tu.
   
 9. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #9
  Jun 3, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  naomba mbunge na watu wenye acess na wabunge wajiulize swali nililoandka wenye siganture yangu.

  Japoni kizungu cha kanumba nadhani ujumbe huu uko wazi


  Itapendeza wabunge hasa wa upinzani wakinza kuonyesha mfano...... Kama wanaona mishahara yao ni sawa basi watee hata watu wa elimu afya, uhandisi mikoani na wilayani wawe na mishahara minono. Wabunge hawawezi kuleta mabadiliko ya kweli . Ni watu wanaoshughulika na elimu, biashara , kilimo afya ndo wako frontline.

  Politics will not bring change its just a catalyst for change
   
 10. Dr-of-three-Phd

  Dr-of-three-Phd Senior Member

  #10
  Jun 3, 2011
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 194
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ukitaka kuona sura halisi za wabunge wa Tanzania gusa posho zao, huo ndio msimamo wao wa miaka na miaka na jana ulijidhihirisha kufuatia ushauri wa Waziri Kivuli wa Fedha, Zitto Kabwe, wa kutaka kufutwa kwa posho za vikao kwa wabunge katika bajeti ya serikali ya mwaka 2011/2012.

  Jana baadhi ya wabunge hasa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), walipinga kwa nguvu zao zote mapendekezo ya Zitto ya kutaka posho za vikao wanazolipwa ziondolewe.

  Wa kwanza kupinga mapendekezo hayo bila hata kutafuna maneno alikuwa ni Mbunge wa Manyoni Mashariki (CCM), John Chiligati, ambaye alisema kama wabunge wa kambi ya upinzani hawataki kuzipokea fedha hizo waziache.

  Chiligati alitoa msimamo huo jana jijini Dar es Salaam, alipotakiwa kutoa maoni yake kama anaona kuna haja posho za wabunge kuondolewa kama ilivyopendekezwa na Naibu kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni, Zitto Kabwe.

  Akizungumza na NIPASHE katika viwanja vya ofisi za Bunge jijini Dar es Salaam, Chiligati ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), alisema hoja hiyo sio ya wabunge wote bali ya upinzani na hivyo kama wao wanaona hawazihitaji posho hizo wasizichukue.
  "Hii kambi ya upinzani kama haitaki hailazimishwi kupokea posho hizo za vikao wanaweza kuziacha sio lazima wazipokee," alisema.
  Naye Mbunge wa Magomeni visiwani Zanzibar, Mohammad Chomboh (CCM), alisema suala hilo halitekeleziki kwa kuwa Sh. 80,000 anayolipwa mbunge kama posho ni ndogo ikilinganishwa na hali halisi ya maisha ilivyo sasa.

  Alisema kulala nyumba ya wageni kwa siku wanapokuwa Dodoma ni Sh. 50,000 hapo bado hawajala hivyo kiasi hicho sio kikubwa kama inavyoelezwa na upinzani.

  Mbunge wa Bukoba Vijijini, Jasson Rweikiza (CCM), alisema hoja ya kutaka posho ifutwe ni mawazo ya mtu kwani waliopanga malipo ya posho hiyo nao pia wana sababu zao.

  Hata hivyo, alimtaka mbunge yeyote mwenye hoja kama hiyo, aipeleke bungeni ikajadiliwe huko, badala ya kuizungumzia nje ya Bunge.
  Mbunge wa Nzega (CCM), Dk. Hamisi Kigwangalla, alisema haungi mkono hoja ya Zitto, kwa vile imejaa unafiki na kujitafutia umaarufu.
  "Kama kweli tuna dhamira ya msingi ya kutumikia Watanzania kuna vitu vingi vilipaswa viondolewe na si posho peke yake. Kwa mfano, mashangingi yangefutwa kwa sababu yana gharama kubwa kuendesha. Lakini yanahitajika kwa wabunge kutumia kuwafikia wananchi vijijini," alisema Dk. Kigwangalla. Alisema posho za vikao, ambazo Zitto anataka zifutwe, ni ndogo kulinganisha na majukumu yanayomkabili mbunge.
  Dk. Kigwangalla alisema hata shida binafsi za wananchi, wanategemea zitatuliwe na mbunge, hivyo ni vigumu mbunge kufanya kazi bila kulipwa posho. "Vinginevyo wanataka mbunge arudi mitaani kuganga njaa. Kwa hiyo, hiyo ni kauli ya unafiki, ya wanasiasa wanaotafuta umaarufu, mimi siwezi kuiunga mkono," alisema Dk. Kigwangalla.

  Kwa sasa mbunge analipwa Sh. 70,000 kwa siku kwa ajili ya kujikimu pamoja na Sh. 80,000 kama posho ya kikao kwa siku ambapo jumla analipwa Sh. 150,000 mbali na mshahara wake.

  Kwa upande wake, mbunge wa viti maalum (CCM), Dk. Maua Daftari alipoulizwa kuhusu hoja hiyo hakuwa na jibu la kutoa.
  Badala yake mbunge huyo alibaki anaguna na kukata simu bila ya kuiunga mkono ama kuikataa hoja hiyo.

  Akitoa maoni yake, Ali Khamis Seif mbunge wa jimbo la Mkoani (CUF), alisema hoja ya kutaka posho ziondolewe ni nzuri lakini kwa sasa bado sio wakati wake. Alisema mbunge ana kazi nyingi za kuwasaidia wananchi hivyo ikiwa ataondolewa posho watashindwa kutatua kero mbalimbali za wananchi. Hata hivyo alisema ikiwa fedha hizo zitaondolewa kwa mbunge ziingizwe kwenye mfuko wa jimbo ili zisaidie kusukuma mbele maendeleo ya wananchi. Alitoa mfano kuwa kuna wabunge wengine wanatumia fedha hizo kuwasaidia wapiga kura wao kupata elimu pamoja na kupata matibabu kazi ambayo ingepaswa kufanywa na serikali.

  Akizungumzia hoja hiyo, mbunge wa viti maalum (CCM), Diana Chilolo, alisema Zitto ana mtazamo finyu juu ya hoja hiyo ya kutaka posho ya vikao iondolewe. Alisema fedha anayoipata mbunge sio ya kwake pekee bali inawasaidia wananchi wengine wakiwemo yatima, walemavu, wajane katika kupata mahitaji yao. Kila anapokuwa mbunge wananchi wake wanamuona kama nguzo na kimbilio lao, hivyo posho hizo zinasaidia kutatua matatizo madogo madogo kama hayo.

  Mbunge wa jimbo la Meatu (Chadema), Meshack Opulukwa, akitoa maoni yake alisema bado anatafakari hoja hiyo.
  Aliongeza kuwa hoja hiyo aliisikia jana, lakini kama Waziri Kivuli wa Kilimo, Chakula na Ushirika bado anaitafakari ili kuona kama ataiunga mkono hoja hiyo itakapopelekwa bungeni.

  Mbunge wa Muhambwe (NCCR-Mageuzi), Felix Mkosamali, aliunga mkono hoja ya Zitto ya kutaka wabunge wasiwe wanalipwa posho za vikao. Mkosamali alisema si posho tu, bali anataka pia mishahara wanayolipwa wabunge pia ipungue na kuwa chini ya ile wanayolipwa hivi sasa kwani hatua hiyo itasaidia kudhibiti mafisadi kuwania ubunge. "Hatuhitaji watu wagombee kwa ajili ya kupata posho, maana kuna watu huwa wanagombea kwa lengo la kutafuta maslahi binafsi na si kuwawakilisha Watanzania, hivyo posho ikiondolewa na mishahara ikapunguzwa waroho wa madaraka watapungua" alisema Mkosamali. Aliongeza: "Kwa hiyo, naunga mkono hoja ya kufutwa posho. Lakini mishahara ya wabunge pia ipungue, maana haiwezekani posho zipungue wakati mishahara iko palepale," alisema. Mkosamali alisema kufutwa kwa posho kwa wabunge ni hatua muhimu kwani kuna maeneo mengi ya kijamii, kama vile hospitali, fedha hizo zinaweza kupelekwa kusaidia. Alisema pia kupunguzwa kwa mishahara ya wabunge, ni muhimu kwani kutasaidia kuwafanya wanaotaka kuwania ubunge, kufanya hivyo kwa lengo la kuwawakilisha wananchi kwa dhati.

  Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila, naye pia aliunga mkono kufutwa kwa posho za vikao kwa wabunge, lakini alishauri posho hizo zibaki kwa vikao vya watumishi wasio na mishahara, kama vile wenyeviti wa vijiji. "Mtumishi yeyote alipwe posho ya vikao, ambavyo sio sehemu ya majukumu yake," alisema Kafulila. Hata hivyo, alisema malipo ya posho za vikao, yasiishie tu kufutwa kwa wabunge, bali yafutwe serikalini na kwenye mahakama pia. "Hatupaswi kulipwa kwa kukaa. Pesa nyingi inavuja. Mfumo wa sitting allowance (posho za vikao) must end (ikomeshwe)," alisema Kafulila. Alisema pia posho nyingine zote zinapaswa kutozwa kodi na suala hilo liwe ni utaratibu na sera kwa mihimili yote ya dola; Bunge, Serikali na Mahakama.

  Mbunge wa Kilwa Kaskazini (CCM), Murtaza Mangungu, aliunga mkono si kufutwa tu kwa posho za vikao kwa wabunge, bali hata mishahara nayo pia ifutwe akisema kazi ya ubunge haitakiwi malipo. "Mimi maoni yangu ni kwamba, kwa kazi ya ubunge, wabunge hawapaswi kabisa kulipwa hata mshahara, ikifanyika hivyo itawafanya watu kujikita zaidi katika kuwatumikia wananchi," alisema Mangungu.

  Kwa upande wake, mbunge wa Mpanda mjini (Chadema), Said Arf aliunga mkono hoja hiyo ya Zitto na kusema kuwa umefika wakati wabunge kuwajali wananchi wenzao kwa kukubali kuachia posho zao ili ziweze kuwasaidia. Aliwataka viongozi kupunguza anasa ili fedha hizo zisaidie watu wenye mahitaji ya lazima ikiwemo kuwapatia maendeleo. Alisema mfumo unaotumiwa na Bunge wa kusema "ndiyoooo au hapanaaa" katika kupitisha hoja mbalimbali haufai kwa kuwa huo ni mfumo wa kijima. Aliongeza kuwa hoja hiyo ya kutaka posho hizo ziondolewe inaweza kukwamishwa kwa kutumia mfumo huo wa upigaji kura kwa kusema ndiyo au hapana.

  Juzi Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema) na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, alisema haoni sababu mbunge kuendelea kulipwa posho nono kwa ajili ya kuhudhuria vikao kwa kuwa hiyo ni sehemu ya kazi yao ya kila siku. Alisema anataka sheria ya Bunge inayotoa mwanya kwa wabunge kulipwa posho hizo ibadilishwe haraka ili kiasi hicho cha fedha kitumike kwa ajili ya kuwasaidia Watanzania wengine wenye matatizo. Zitto alisema ingawa suala hilo ni gumu, lakini ataliwasilisha katika mkutano wa Bunge la bajeti wakati atakapowasilisha bajeti yake kama Waziri Kivuli wa Fedha na Uchumi. Alisema ana imani wabunge wenzake watakubali pendekezo hilo na kumuunga mkono kubadilisha sheria hiyo ili posho hizo zisiwe zinatolewa.

  Katika Bunge lililopita aliyekuwa Mbunge wa Karatu, Dk. Willibroad Slaa (Chadema), aliwahi kutoa wazo kama hilo pamoja na kupendekeza mshahara wa wabunge upunguzwe kwa kuwa ni mkubwa, lakini wabunge wenzake walipinga hoja hiyo kwa nguvu zote.
  Dk. Slaa alishindwa kupitisha hoja yake katika Bunge lililopita baada ya wenzake kukataa kumuunga mkono huku baadhi yao wakitoa kauli za kumkejeli na kumuona kama mtu aliyekuwa akitafuta umaarufu wa kisiasa. Kiutaratibu wabunge wote hulipwa posho ya vikao ya Sh. 80,000 kwa siku, na posho ya kujikimu kwa kuwa nje makazi ya Sh. 70,000 hivyo kwa siku moja tu wabunge hulipwa wastani wa Sh. 150,000 siku za kazi, wakati mwishoni mwa wiki hulipwa Sh. 70,000, kwa maana hiyo kati ya wabunge wote waliopo ambao ni 350 kama posho hizo zitaondolewa serikali itaokoa kiasi cha Sh. milioni 52.5 kwa siku.

  Mkutano wa Bunge la Bajeti unatarajiwa kuanza Juni 7, mwaka huu hadi Agosti 15, mwaka huu, kwa maana hiyo kutakuwa na siku za kazi 48 ambazo zitaigharimu serikali Sh. bilioni 2.52 kama posho ya vikao kwa wabunge. Kiasi hicho kikiongozewa Sh. milioni 490 za posho ya kujikimu ya mwishoni mwa wiki ambazo ni kwa siku 20, serikali itakuwa inaokoa jumla Sh. bilioni 3.01 ambazo ni posho za wabunge bila mshahara. Kiasi hicho kinaweza kuelekezwa kutunisha bajeti ya elimu, barabara au afya, ambako kuna upungufu mkubwa wa fedha.
  Mshahara wa mbunge kwa sasa ni Sh. milioni 2.5, kiasi hicho kikichanganywa na posho ya mafuta, kuendesha ofisi mapato yake ya ubunge yanafika kiasi cha Sh. milioni 7.19.

  Serikali inatarajia kutumia Sh. trilioni 12.8 kwa mwaka wa fedha wa 2011/2012, kati ya hizo Sh. trilioni 8.8 ni kwa matumizi ya kawaida, yaani posho na mishahara na ulaji mwingine, wakati fungu la maendeleo ni Sh. trilioni nne tu. Utaratibu wa kupitisha bajeti ya ulaji umekuwa ni utamaduni wa taifa hili, kwani hata mwaka huu wa fedha unaomalizika serikali ilipitisha bajeti ya Sh. trilioni 11.6, kati yake Sh. trilioni 7.7 zilikuwa kwa fungu la kawaida na Sh. trilioni 3.8 kwa ajili ya maendeleo.

  CHANZO: NIPASHE 3rd June 2011

  Aluta Continua !
   
 11. A

  Abunuas JF-Expert Member

  #11
  Jun 3, 2011
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 8,730
  Likes Received: 420
  Trophy Points: 180
  Tanzania kwa wabunge ni bwerere.
   
 12. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #12
  Jun 3, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Halafu serikali inadai haina pesa za kuongeza mishahara!
   
 13. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #13
  Jun 3, 2011
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Kila mtu anakimbilia kuwa mwanasiasa kwasababu siasa inalipa nchi hii; wanahonga milloni 30 wakati wa mchakato wa kuusaka ubunge halafu kila mmoja anakuja pata milliono 90 anapoingia bungeni!! The return on investment 90/30*100=300% Only a fool will not invest in such a lucrative venture!! Ndio maana watu wameanza kuuana kwa sababu ya kitega uchumi hiki.
   
 14. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #14
  Jun 3, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Wa nchi za Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi wanalipwaje ? fanya uchambuzi acha siasa na kulaza bongo !
   
 15. Dr-of-three-Phd

  Dr-of-three-Phd Senior Member

  #15
  Jun 3, 2011
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 194
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Umeona ehh, wanatudanganya eti madawa hakuna vitanda hakuna eti madwati hakuna kumbbe wanakula na matumbo yao!
   
 16. Dr-of-three-Phd

  Dr-of-three-Phd Senior Member

  #16
  Jun 3, 2011
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 194
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wewe GuniusBrain, brain yako hovyo, wewe nyumbani kwako unapanga ule nini ukiangalia jirani yako amekula nini, acha ulimbukeni wa kishabiki, watu wanaongea mantiki wewe unaleta utani. p*(&%^$#*f(&.

  Aluta Contunua !
   
 17. Dr-of-three-Phd

  Dr-of-three-Phd Senior Member

  #17
  Jun 3, 2011
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 194
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33

  Ndiyo maana waua, wanfanya kila kitu ili waishi milele kwenye siasa mbovu za maji taka ili wapate kra za kula.
   
 18. Wanitakiani

  Wanitakiani JF-Expert Member

  #18
  Jun 3, 2011
  Joined: Apr 18, 2008
  Messages: 644
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwakweli hata mie nadhani nitagombea 2015 kwa mataji huo!
   
 19. n

  nyuki dume JF-Expert Member

  #19
  Jun 3, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 438
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Tshs 150,000.00 kwa siku mimi ambaye ni mtumishi wa serikali kima chini Tshs 135,000.00 kwa mwezi,kodi,nauli ya daladala chakula,mavazi, nisemeje , wao 150,000.00 kwa siku hazitoshi,Na bado watapata posho kama atahudhuria kwenye kikao cha kamati
   
Loading...