Mkutano wa mbunge Dr.T.Kamani CCM wasusiwa na Wananchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkutano wa mbunge Dr.T.Kamani CCM wasusiwa na Wananchi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nngu007, May 1, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  May 1, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  Na John Maduhu,Mwanza

  MAANDAMANO yaliyoandaliwa na Mbunge wa jimbo la Buseta, Dk. Titus Kamani Mlengeya kumpongeza kwa ajili ya kuchaguliwa kuwa mwakilishi wa wabunge wa Jamhuri ya Muungano katika Bunge la Jumuia ya Maendeleo ya Nchi za Kusini(SADC),yameingia dosari baada ya wananchi kuyasusia huku wakimzomea.

  Dk. Kamani aliwasili Jijini Mwanza jana asubuhi na kuanza safari ya kwenda jimboni kwake Busega Wilayani Magu, ambapo alipanga kuwepo na maandamano kuanzia Magu mjini hadi eneo la Nyashimo.

  Baadhi ya Makatibu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)na Wenyeviti wa Kata waliozungumza na MTANZANIA Jumapili, walisema waliweka msimamo wa kutokuhudhuria mikutano ya mbunge huyo kutokana na kupoteza mvuto na kushiindwa kujali wananchi wake.

  Akizungumza na MTANZANIA Jumapili kwa nyakati tofauti, viongozi hao, walisema walikutana jana katika kikao na kuamua kuwa hawawezi kusafirisha wananchi kwenda kwenye mkutano wa Dk. Kamani umbali wa kilomita zaidi ya 100 bila kujua gharama hizo zitalipwa na nani.

  “Hapa nilipo niko Nassa nyumbani wananchi wamemzomea Mbunge alipopita katika msafara wa magari matatu, akielekea katika eneo la Nyashimo,wananchi waliposikia gari la matangazo, walianza kuzomea “,alisema kiongozi mmoja wa kata kwa sharti la kutotajwa jina lake.

  MTANZANIA Jumapili ilimtafuta Dk. Kamani kwa njia ya simu kwa ajili ya kuzungumzia suala la wananchi kugomea maandamano na mkutano wake, hakupokea simu yake ya kiganjani licha ya kuita mara nyingi
   
 2. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #2
  May 1, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  nguvu wa umma sasa watu wanaelewa soma
  mpaka hawa watawala watakapo soma ramani na
  wengine kujitoa wenyewe kabla ya muda wa kuumbuka kuwadia
   
Loading...