Mkutano wa mashauriano kati ya serikali, wafanyabiashara na wawekezaji mkoa wa Shinyanga

Avriel

JF-Expert Member
Jun 25, 2017
4,947
5,342
Mkutano unaendelea ndani ya ukumbi Wa NSSF mkoani Shinyanga, mgeni rasmi ndugu Angela Jasmin Kairuki.

Mkutano umewahusisha viongozi Wa SERIKALI ngazi ya mkoa na wilaya zote tatu za mkoa Wa Shinyanga yaani Kahama, Shinyanga na Kishapu pamoja na asasi na taasisi mbalimbali zikiwemo za dini, wawekezaji mkoa mzima, wafanyabiashara ngazi zote.

Mkutano umefunguliwa na mkuu Wa mkoa anatoa fursa mbalimbali zilizomo mkoa Wa Shinyanga, maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya kilimo, viwanda na uwekezaji mwingine.

Changamoto mbalimbali zilizopo mkoani na wilaya zake zimekuwa address kwa mgeni rasmi
Rasmi mkoa umetambuliwa kuwa ni mkoa wa almasi na dhahabu

Manaibu Waziri wengine walioshiriki mkutano huu ni pamoja na:
1. Mwita Waitara
2. Ashatu Kijaji
3. Angelina Mabula
4. Stanslaus Nyongo
5. Stella Manyanya
6. Ulega
7. Kanyaso
8. Masauni
9. Musa Sima
Mkuu Wa mkoa wa Kigoma pia ndugu Maganga ameshiriki.
Mnakaribishwa Shinyanga mkoa Wa dhahabu na almasi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
bila shaka taasisi za kifedha zitakuwepo. hizi fursa zipo miaka yote, labda mikutano kama hii iwe na lengo la kubainisha vikwazo mbali mbali na kuvipatia ufumbuzi. Kwa sababu Shinyanga inajulikana kwa almasi tangu sijabalehe na sasa nina watoto wanasoma

Avriel

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Wa mkoa Wa kigoma ameongea anasema kigoma sio mwisho Wa reli Bali mwanzo Wa reli maana yeye daily anaiona treni inaanzia safari kigoma kuelelea Dar.

Amesimama mwenyekiti Wa ccm mkoa Wa Shinyanga aliposema ccm oyee ukumbi ukanyamaza ikabidi aombe watu waikubali ccm maana ilani inatekelezwa ya ccm.
Mimi nawakilisha Sauti ya Umma nimenyimwa kisemeo hapa ....


Barick Gold wametambuliwa kama wafadhili wakuu Wa mkutano pamoja na bank za Crdb, NBC, NMB, TCCIA,

MAJADILIANO YANAANZA ......
wafanyabiashara na wawekezaji wamepewa nafasi kutoa changamoto na kero zao ambapo TCCIA kwa niaba ya wanachama wake wanatoa changamoto zao.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeipenda sponsor number 1 Barrick...
Baniani mbaya kiatu yake dawa....

Twiga Gold Mining company imeshiriki??

Everyday is Saturday..................... :cool:
 
Msururu Wa kodi na tozo kwa taasisi mbalimbali za SERIKALI umezungumzwa pia kama ni kikwazo endelevu kwa wafanyabiashara hivyo SERIKALI imezidi kushauriwa kupunguza hizi tozo ziwekwe eneo moja mfanyabiashara mwekezaji azilipie Mara moja na si mzunguko .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom