Mkutano wa Marais wastaafu barani Afrika - South Afrika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkutano wa Marais wastaafu barani Afrika - South Afrika

Discussion in 'Jamii Photos' started by Candid Scope, May 25, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  May 25, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  Hii ndio safu ya Marais wastaafu Afrika waliohudhuria mkutano wao Afrika Kusini ukiongozwa na Balozi wa zamani nchini Tanzania Bwana Charles. Mwinyi, Mkapa na Karume kutoka Tanzania, Thabo Mbeki wa South Afrika, Obasanjo wa Nigeria, Banda wa Zambia, Pedro wa Cape Verde, Soglo wa Bernin. Baada ya kuhudumia vipindi vyao katika nchi zao sasa wameamua kuwa watume wa maendeleo barani afrika.
   
 2. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #2
  May 25, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  Mzee Mkapa na mwenzake Soglo wa Bernin wakipiga michapo ya hapa na pale ili mradi kujikumbushia enzi zao wawapo kwenye vikao kama marais.
   
 3. a

  arigold JF-Expert Member

  #3
  May 25, 2012
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 594
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 60
 4. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #4
  May 25, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  Mzee mkapa mambo yalivyokolea pale ukumbini kasahau karabasha lake, lakini Mzee Mwinyi na kinana mstaafu Karume wangali makini wamebana makarabasha yao huku wakitafakari yaliyojilia ndani ya kikao chao.
   
 5. mpayukaji

  mpayukaji JF-Expert Member

  #5
  May 25, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Karume hakupaswa kuhudhuria mkutano kwa vile hajawai kuwa head of state zaidi ya rais wa baraza la mapinduzi ambalo si nchi. Kesho utasikia Sanago naye anahudhuria.
   
 6. N

  Njele JF-Expert Member

  #6
  May 25, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 275
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwani Tanzania ilikuwa lazima kuwakilishwa na wote hao? Mbona Nigeria wanao wengi tu lakini walimtuma mwakilishi mmoja. Afrika kusini yenyewe mzee Madiba licha ya uzee hata kwenda kuwataka khali tu haikufanyika.
   
 7. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #7
  May 25, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  hivi zanzibar ni nchi?
   
 8. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #8
  May 25, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Hahaha, kwani we bongo kama huijui? Kuna kitu posho huko ndo wanachochangamnkia.
   
 9. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #9
  May 25, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  kwa afrika kusini tanzania is very special. hivyo exceptions kama hizo are to be expected!
   
 10. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #10
  May 25, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Huyu Mkapa juzi ameingia Mahakamani Tanzania akiwa mkakamavu vila fimbo, inamaana alikatazwa na mahakama siingie na fimbo asije akampiga hakimu? Huko Afrika kusini anaonekana mchofu kulika alivyoonekana majuzi mahakamani.
   
 11. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #11
  May 25, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Hata kama ni hivo lakini hii ya nusu ya wahudhuriaji toka nchi moja imekaaje?
   
 12. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #12
  May 25, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kweli viongozi wetu ulimbukeni umewazidi
   
 13. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #13
  May 25, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kuna mdau alituchekesha hapa kwa kutuambia samansi ya mahakama ilimpa ukakamavu.
   
 14. z

  ziwapohazipo Member

  #14
  May 25, 2012
  Joined: Jan 29, 2012
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Poleni nduguzanguni mpayukaji unapayuka kama ID ilivyo na kigogo maskini hujijui hata kigogo cha mti gani wewe umo Zanzibar ni nchi kamili
   
 15. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #15
  May 25, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Wangepanga tu kupeana zamu nani ahudhurie safari hii, lakini nusu ya wawakilishi bara zima ni kutoka Tanzania, mie binafsi ningeona aibu.
   
 16. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #16
  May 25, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Naelewa kwamba Zanzibar ni state ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ni sawa na kusema nchini marekani gavana wa state fulani ni rais mstaafu wa Taifa la Marekani.
   
 17. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #17
  May 25, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  ni awkward!
   
 18. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #18
  May 25, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Hata mie ningeona aibu katika hili, lakini wenzetu wanaona sawa tu nusu ya wajumbe toka nchi moja.
   
 19. Ngangasyonga

  Ngangasyonga JF-Expert Member

  #19
  May 25, 2012
  Joined: Sep 13, 2010
  Messages: 456
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapo ndio utaona kasoro za muungano, Karume kaiwakilisha nchi gani na Mkapa na Mwinyi nchi gani. Tunataka Tanganyika yetu! huu muungano wa kiini macho!
   
 20. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #20
  May 26, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Wabongo bana bila aibu ni kufuatana kama kumbikumbi, hata wakijaa chumba kizima peke yao ugenini kwao ni sawa tu.
   
Loading...