Mkutano wa Magufuli na Mwinyi ni habari, je mkutano wa Magufuli na Lukuvi nayo ni habari?

Ileje

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,759
12,175
Jana Mkurugenzi wa mawasiliano wa Ikulu Bw. Msigwa aliutaarifu umma kuwa Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi alikutana na Rais John Pombe Magufuli Ikulu Dar es Salaam na kufanya naye mazungumzo. Habari hii iliwafariji wananchi wengi kwa sababu wanaona kuna mshikamano mkubwa baina ya viongozi wastaafu na wa sasa! Na kwamba wanashauriana kuhusu mustakabali wa Taifa ili chombo kisije kwenda mrama!

Lakini wengi tulishangaa Msigwa kututaarifu kuwa Rais Magufuli pia alikutana na Bw. Lukuvi, waziri wa ardhi.

Maswali:
1. Je Mhe. Rais hana mazoea ya kukutana na mawaziri wake hadi Msigwa aone mkutano wa Magufuli na Lukuvi nayo ni habari ya kutuarifu?

2. Je utendaji wa mawaziri wetu uko vipi au ndiyo sababu kila waziri anatoa matamko kila kukicha?

3. Kama uhusiano baina ya Rais na mawaziri uko mbali kiasi hiki je uhusiano baina ya Rais na watendaji wengine wa serikali kama wakuu wa mikoa na wilaya uko vipi?
 
Lazima kuna tatizo kubwa sana.
Hata mimi hilo limenishangaza sana.
Rais na baraza lake la mawaziri ni timu moja, wanaweza kukutana wakati wowote mahali popote ili kupanga na kujadili mipango ya serikali bila mtu yoyote kujua au kujulishwa. Ni kama Mume na Mke ndani ya Nyumba.

Sasa nimeshaangaa kusikia Waziri anaomba Special Appointment kwenda ikulu kuonana na rais na tukio hilo kuwa ni News.

Kikao cha Rais na waziri wake mmoja pale ikulu nayo ni News?
 
Aidha msigwa na waandishi wetu wanapwaya au ni dhahiri umma na baraza zima la mawaziri ni waoga mno kwa boss wao na kwamba kumwona ni kama kutokewa na malaika au mtume fulani! Kama tunadhani tutafika basi hatujui urefu wa safari yetu na nguvu ya chombo tunachotumia.
 
Ajabu ni kwamba baada ya mkutano huo Lukuvi hakutokea mbele ya kamera za waandishi wa habari kuwa waliteta nini? Mkutano huo ungekuwa habari kama Lukuvu angepeleka barua yake ya kujiuzulu wadhifa wake kwa maelezo kuwa kazi imemshinda!!
 
Nchi hii imefikia patamu sana kama vile tamthilia ya Isidingo ndo Linc kamuua Catlego aaaf tunaambiwa itaendelea wiki ijayo unataman uende ITV ukaombe mwendelezo
 
Jana Mkurugenzi wa mawasiliano wa Ikulu Bw. Msigwa aliutaarifu umma kuwa Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi alikutana na Rais John Pombe Magufuli Ikulu Dar es Salaam na kufanya naye mazungumzo. Habari hii iliwafariji wananchi wengi kwa sababu wanaona kuna mshikamano mkubwa baina ya viongozi wastaafu na wa sasa! Na kwamba wanashauriana kuhusu mustakabali wa Taifa ili chombo kisije kwenda mrama!

Lakini wengi tulishangaa Msigwa kututaarifu kuwa Rais Magufuli pia alikutana na Bw. Lukuvi, waziri wa ardhi.

Maswali:
1. Je Mhe. Rais hana mazoea ya kukutana na mawaziri wake hadi Msigwa aone mkutano wa Magufuli na Lukuvi nayo ni habari ya kutuarifu?

2. Je utendaji wa mawaziri wetu uko vipi au ndiyo sababu kila waziri anatoa matamko kila kukicha?

3. Kama uhusiano baina ya Rais na mawaziri uko mbali kiasi hiki je uhusiano baina ya Rais na watendaji wengine wa serikali kama wakuu wa mikoa na wilaya uko vipi?
Msisahau kwamba kuna sekretarieti mpya ya chama inasukwa, na ndugu Lukuvi ni mzoefu katika chama.
 
Hili la Waziri Lukuvi kwenda Ikulu baada ya Mzee Mwinyi itakuwa kukamilisha ule mkakati wa kumfanya
S.G. wa CCM baada ya kuiondoa Sekretarieti iliyopo..
 
Mambo hayo wangeyafanya pale Lumumba!
 
Mzee Mwinyi itakuwa kadhulumiwa ardhi yake si bure. Kaona huku chini wanamzungusha kagonga Ikulu.

Lukuvi kaitwa mbio mbio amalize tatizo.

Zingine zote ni porojo tu.
Sijawahi kusikia Mzee Mwinyi kuwa na tatizo la ardhi!
 
Mzee Mwinyi itakuwa kadhulumiwa ardhi yake si bure. Kaona huku chini wanamzungusha kagonga Ikulu.

Lukuvi kaitwa mbio mbio amalize tatizo.

Zingine zote ni porojo tu

Hii taarifa sahihi toka jikoni!!! Vijana wa wizara ya ardhi kweli hawataingia peponi kama alivyowachulia Makonda!!! Hawamuogopi hata RAIS mstaafu je sisi makabwela si ndio wanatuua kabisa!!
 
msigwa na zile taarifa zake ananukuu mambo meengi,mpaka zinafika kurasa tano.

kazoea tv,anaongea,halafu anamuweka na chanzo,halafu anajumuisha
 
Jana Mkurugenzi wa mawasiliano wa Ikulu Bw. Msigwa aliutaarifu umma kuwa Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi alikutana na Rais John Pombe Magufuli Ikulu Dar es Salaam na kufanya naye mazungumzo. Habari hii iliwafariji wananchi wengi kwa sababu wanaona kuna mshikamano mkubwa baina ya viongozi wastaafu na wa sasa! Na kwamba wanashauriana kuhusu mustakabali wa Taifa ili chombo kisije kwenda mrama!

Lakini wengi tulishangaa Msigwa kututaarifu kuwa Rais Magufuli pia alikutana na Bw. Lukuvi, waziri wa ardhi.

Maswali:
1. Je Mhe. Rais hana mazoea ya kukutana na mawaziri wake hadi Msigwa aone mkutano wa Magufuli na Lukuvi nayo ni habari ya kutuarifu?

2. Je utendaji wa mawaziri wetu uko vipi au ndiyo sababu kila waziri anatoa matamko kila kukicha?

3. Kama uhusiano baina ya Rais na mawaziri uko mbali kiasi hiki je uhusiano baina ya Rais na watendaji wengine wa serikali kama wakuu wa mikoa na wilaya uko vipi?
Pamoja na kuwa ni muhimu kutoa habari jinsi ilivyo.Ni muhimu pia kujua Rais anaweza akitaka kuonana na Waziri wake wakati wowote INAPOBIDI na ukweli hiyo si habari ya ku disseminate/kugawa kama habari mhimu.

Pia Waziri yeyote ni LAZIMA aombe appointment kutoka ofisi ya Ikulu na kuambiwa ni siku ipi ana nafasi. UNLESS ni jambo la dharura!
La sivyo itakuwa si Ikulu tena bali ni kama nyumba ya Babu.

Waziri hawezi tu kwenda kama vile aenda nyumbani kwake. . Hiyo ndo protokali ilivyo.
Kwa Grson Msigwa ni vizuri upande mwingine
Kukumbuka "SPIRAL of SILENCE theory"
in Mass communication.
Itakusadia.
Otherwise so far so good!!
 
Kwa namna Msigwa alivyoitoa habari hii ni kama vile Lukuvi ni waziri wa nchi nyingine amekwenda ikulu ku- pay courtesy call!!
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom