Ileje
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 8,797
- 12,239
Jana Mkurugenzi wa mawasiliano wa Ikulu Bw. Msigwa aliutaarifu umma kuwa Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi alikutana na Rais John Pombe Magufuli Ikulu Dar es Salaam na kufanya naye mazungumzo. Habari hii iliwafariji wananchi wengi kwa sababu wanaona kuna mshikamano mkubwa baina ya viongozi wastaafu na wa sasa! Na kwamba wanashauriana kuhusu mustakabali wa Taifa ili chombo kisije kwenda mrama!
Lakini wengi tulishangaa Msigwa kututaarifu kuwa Rais Magufuli pia alikutana na Bw. Lukuvi, waziri wa ardhi.
Maswali:
1. Je Mhe. Rais hana mazoea ya kukutana na mawaziri wake hadi Msigwa aone mkutano wa Magufuli na Lukuvi nayo ni habari ya kutuarifu?
2. Je utendaji wa mawaziri wetu uko vipi au ndiyo sababu kila waziri anatoa matamko kila kukicha?
3. Kama uhusiano baina ya Rais na mawaziri uko mbali kiasi hiki je uhusiano baina ya Rais na watendaji wengine wa serikali kama wakuu wa mikoa na wilaya uko vipi?