Mkutano wa kumtambulisha Mgombea Urais UKAWA-Mbeya

Watu wanapenda ushabiki na kufuata mikumbo tu na kujikomba kwa lowasa wakati yeye ni mwenyekiti wa wakora na ndiyo maana wanaomlia pesa zake wanamfuata kila mahali
 
Nadhani hili ndilo gazeti lenye kichwa cha habari kizuri kuliko magazeti yote ya leo.Gazeti linaeleza kuwa pamoja na polisi kupiga marufuku maandamano lakini wanamabadiliko waliandamana kwa wingi na kutanda barabarani kumsubiri Lowasa na UKAWA yake huko jijini Mbeya,Hivyo polisi iliishia kutoa ulinzi tu

CHANZO: Nipashe

Hata ulinzi hawakutoa tulijilinda wenyewe,maana polisi walikuwa katikati ya halaiki sasa walilindaje?nao walikuwa kwenye maandamano
 
Hawa askari wa mbeya wanafahamu kazi yao

Wanafaham haki ya kukusanyika kikatiba

Wanajiepusha na vurugu zisizo na tija wala lazima

Matokeo ya hekima zao

Wanambeya walikusanyika na kutawanyika salama

Haki yakikatiba imetimizwa kwa vitendo bila ubaguzi

Urafiki kati ya polisi na raia umeimarika maana hakuna uhasama

Imejidhihirisha 100% bila watawala kuwasukuma polisi, raia wanajiheshim na kufanya mambo kwa weled nidham na utu.

Hongera jeshi la polisi mbeya.
 
Umechanganya mambo mengi hapo, haujaeleweka vizuri unachotaka kusema ni nini. Mara ushabiki, then mkumbo, kujikomba, kuna m/kiti wa wakora, na wanaokula ela zake... Unachotaka kusema ni kipi? Tulia, tafakari, panga hoja yako vizuri ili tukuelewe. Hauna sababu ya kuandika kwa jaziba, taratibu tu ili tuelewane.

Hoja ni: Je, RPC na askari wa mbeya na wao walikula pesa kutoka kwa Eddo na ni kiasi cha bil. ngapi au ni busara tu na ukomavu wa ujuzi na maarifa ya kazi zao. Je, wanastahili pongezi kwa kuepusha vurugu na maafa kwa kutumia weledi na hekima bora au walaumiwe na kuchukuliwa hatua kwa kutokutekeleza amri halali ya kupiga marufuku maandamano??

Watu wanapenda ushabiki na kufuata mikumbo tu na kujikomba kwa lowasa wakati yeye ni mwenyekiti wa wakora na ndiyo maana wanaomlia pesa zake wanamfuata kila mahali
 
Mkuu Kyamkwikwi pole ndugu yangu. Kazi ya Polisi sio kuanzisha fujo bali kulinda wananchi na mali zao. Katika kutimiza wajibu wao hutumia akili pia. Kuzuia maandamano kwa mabomu na kusababisha watu kuumizwa dhidi ya kuyalinda yamalizike bila tafrani nini kizuri? Askari wetu pia hawataki kuwaumiza wananchi kwa kuwapiga mabomu tu bali kuwalinda na kutunza usalama wao. Kama askari waliamrishwa hivyo nao kwa utashi wao wakaona kuwa amri ingelileta madhara na shari badala ya heri, wakatumia akili na mwisho ukawa mzuri kivile, wanastahili pongezi. Mara nyingi sana askari ndo wanasababisha vurugu na tuna washukuru hawa kwa kutambua hili ambapo sasa wanalinda maandamano badala ya kuyasambaratisha kwa mabomu na risasi!!
 
Imekuwa ndo msemo wa siku hizi kutaka kutuaminisha kuwa Eddo anatumia pesa, anatumia mabillion kuwanunu watu.-

Hili la Mbeya sio jambo dogo hata, yaana marufuku ya RPC inakanyagwa kabisa mchana kweupe. Askari wanapangwa na kupewa maagizo ya kuhakikisha hakuna maandamano lakini askari wanakaidi amri ya RPC na kuamua kuyasindikiza na kuyalinda!!! Huu kama sio uasi wa kisirisiri ni kitu gani?

Amri ya RPC inawekwa pembeni na maandamano ya ujio wa UKAWA yanapewa heshima na askari, hii haikubaliki. RPC huyu ataaminika vipi mbele ya umma na jamii? RPC huyu akitwambia ametuimarishia ulinzi nani atakayemwamini kama leo amri yake inakuwa kama tope tu?? RPC, RPC, RPC??? Hii sio kabisa.

Au ndo tuseme Eddo tayari amemlambisha na huyu RPC na askari wote wa Mbeya Billion 10.

Na juzjuz tumesikia ofisa wa Tume ya uchaguzi anajisahau na kumwita Eddo mhesh. Rais... ahahahaaa!!! Cjui huyu naye alikula bil. nfapi.

Mbowe kanunuliwa, Chadema imenunuliwa, UKAWA imenunuliwa, wenyeviti wa CCM na wanachama, makatibu na viongozi wamenunuliwa, TAKUKURU imenunuliwa isimkamate huyu anayetoa rushwa..... hii ni hatari sana!! Nape amejaribu kugawa mlungula amedakwa haraka sana, kama sio kutetewa na mamlaka ya juu, saa hizi angekuwa anakalia ndoo. Kwa nini Eddo anagawa pesa kwa watu wote hawa na anaangaliwa tu utafikiri ni malaika, la hii sio hata kidogo.

Ebu wenye taarifa ni namna gani Eddo ananunua taasisi na watu woooote hawa, naomba mnijuze huyu RPC wa Mbeya na askari wake wameibuka na kitita cha Bil. ngapi hiyo jana??

KARIBU SANA

Cc: kwenu mapepe: Nape,faizafoxy, ritz, Mzee Mwanakijiji.....

Hahahahaaa, inafurahisha sana...eti na juzi kati wakati tunaandamana dar, wakasema sisi ni vibaka tunakunywa viroba, tumepora maduka kkoo... Haiwezekani eti tulihongwa pesa kutoka ara chuga kuja dar.. Mmmmmh ccm kweli mapovu yanawatoka.. #tukutane october
 
Haujakosea, uko sahii kwa sababu una tatizo la kufikiri hivyo haujaelewa. Jaribu kusoma tena kwa kumwomba jirani yako kukuelewesha halafu tupe maoni yako. Kwa sasa uko sawa sio kosa lako, jiepushe na hatari ya kutoka kuwa mikatabafeki na kuishia kuwa akilifeki...!!

​hii ndo shida ya kupiga viroba asubuhi asubuhi mnakuja na mada zilizolewa tayari
 
Acha ubwege ongea points watu wakuelewe hivi ukiambiwa toa ushahidi wa pesa hiyo utatoa!? Tuongee vitu vya msingi na kujenga na si ushabiki taka humu ndani!!!!? Cdm vema!!
 
Yeap!
Umesoma tu bila kuelewa, ungana na mikatabafeki mjadiliane mkijua maudhui ya mnachosoma njoo twendelee.....!! KARIBU!

Acha ubwege ongea points watu wakuelewe hivi ukiambiwa toa ushahidi wa pesa hiyo utatoa!? Tuongee vitu vya msingi na kujenga na si ushabiki taka humu ndani!!!!? Cdm vema!!
 
Last edited by a moderator:
Jamani acheni propaganda hivi ni pesa kiasi gani watu hawa wanaweza kupewa ni nani mwenye pesa kiasi hicho Tanzania bila ccm inawezekana kabisa.

ukiangalia haraka haraka unaeza dhani jamaa anawaponda polisi lkn ukigeza upande wa pili utagundua jamaa anafikisha ujumbe kuwa lowasa ni zaidi ya hela maana km agizo la.kisheria lunapuuzwa jua jamaa ana nguvu gani.edo ni zaidi ya hela.eddo anapendwa hata na waliopo serikalini
 
Very interesting and relaxing!!!
Tunasubiri Arusha na Mwanza,Hakika CCM(NAPE)(gazeti uhuru) Watajuta kuwaita walioandamana dar kuwa ni vibaka,Haya Mbeya nao..............,Arusha>>>>>>>>>>>>> Mwanza je!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Nguvu ya umma huwezi zuia!!
 
Back
Top Bottom