Mkutano wa Kimataifa wa Wanawake na Mwamko wa Kiislamu wamaliza kazi zake, IRAN | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkutano wa Kimataifa wa Wanawake na Mwamko wa Kiislamu wamaliza kazi zake, IRAN

Discussion in 'International Forum' started by KABAVAKO, Jul 12, 2012.

 1. KABAVAKO

  KABAVAKO JF-Expert Member

  #1
  Jul 12, 2012
  Joined: Apr 5, 2011
  Messages: 209
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mkutano wa Kimataifa wa Wanawake na Mwamko wa Kiislamu ulimaliza kazi zake jana usiku mjini Tehran kwa kutoa taarifa ya mwisho ya washiriki katika mkutano huo. Taarifa hiyo imeutaja mwamko wa Kiislamu kuwa ni miongoni mwa neema na ahadi za Mwenyezi Mungu. Imesema mahudhurio makubwa ya wanawake na wanaume katika medani za kazi na jihadi ni kwa ajili ya kueneza Uislamu, kupambana na udikteta, kupinga uzayuni wa kimataifa na kupigania utukufu na uhuru wa mwanadamu.
  Taarifa hiyo imeyataja mabadiliko ya hivi karibuni kuwa yameimarisha nafasi na mchango wa mwanamke katika jamii na kuongeza kuwa hali mpya iliyojitokeza inaleta udharura wa kutumiwa vyema uwezo wa mwanamke katika nyanja za kisiasa, kijamii, kiutamaduni na kiuchumi hususan katika masuala ya kielimu, uendeshaji wa masuala mbalimbali na katika kuchukua maamuzi ya nchi za Kiislamu.
  Washiriki katika Mkutano wa Kimataifa wa Wanawake na Mwamko wa Kiislamu pia wametahadharisha kuhusu njama zinazofanywa na mabeberu za kutaka kupotosha mwamko wa Kiislamu na kusema kuwa, kama ambavyo ubeberu umefanya jitihada za kuzuia mwamko huo adhimu, daima umekuwa ukipanga mikakati ya kupotosha mapinduzi ya Kiislamu ya watu wa kaskazini mwa Afrika na Mashariki ya Kati kwa ajili ya maslahi ya mabeberu; kwa msingi huo kuna udharura wa kuwa macho zaidi mbele ya njama hizo.
  Taarifa hiyo pia imesema kuwa mapambano ya watu wa Palestina ni miongoni mwa sababu kuu za mwamko wa ulimwengu wa Kiislamu. Imesisitiza kuwa mchango wa wanawake wa Palestina hususan katika kupambana na Wazayuni umetoa ilhamu kwa wanawake wengine Waislamu duniani, kwa msingi huo njia hiyo inapaswa kudumishwa hadi Quds tukufu itakapokombolewa.
  Taarifa ya mwisho ya Mkutano wa Kimataifa wa Wanawake na Mwamko wa Kiislamu mjini Tehran imeashiria njama za nchi za Magharibi hususan Marekani za kutaka kuchafua sura ya Uislamu na kusema kuwa, hatua hizo zimeng'amuliwa na fikra za waliowengi katika ulimwengu wa Kiislamu. Wanawake walioshiriki katika mkutano wa Tehran wamelaani pia misimamo mikali na isiyokuwa na mantiki ya kuzuia shughuli za wanawake katika baadhi ya maeneo ya dunia hususan katika masuala ya kisiasa na kijamii na kusema wanawake Waislamu wanapaswa kupambana na fikra kama hizo zisizokuwa sahihi na kuwa macho mbele ya hila za Wamagharibi ambao kwa miaka mingi sasa wamekuwa wakimtumia mwanamke kama wenzo wa kutimizia matakwa yao.
  Vilevile imelaani hatua ya baadhi ya nchi za Magharibi ya kupiga marufuku vazi la hijabu la wanawake Waislamu na kusema mwanamke wa Kiislamu ataendelea kupambana na propaganda chafu za vyombo vya habari vya nchi za Magharibi zinazozuia harakati za hijabu na utakasifu wa mwanamke katika jamii na kuarifisha kigezo sahihi cha mwanamke Muislamu kwa jamii za Magharibi kwa mujibu wa mafundisho ya Uislamu.
  Ni vyema kusema hapa kuwa zaidi ya wasomi na wanaharakati 1300 wa kike Waislamu kutoka nchi 85 duniani wameshiriki katika Mkutano wa Kimataifa wa Wanawake na Mwamko wa Kiislamu mjini Tehran.
   
Loading...