Elections 2010 Mkutano wa Kikwete Kigamboni wakosa shamrashamra

1:17 "Nikasema jamani, mswahili uongo, hachoki". Kikwete bonge la simpleton.

Rais mzima anawatukana watu wake hivi hivi, halafu hapo hapo anawaomba kura.

Anavyosema "Mswahili uongo hachoki" ina maana yeye naye yumo katika waswahili hao? Au yeye mzungu ?

Hivi nchi yetu ikoje ?
 
Na Miswahili tulivyo, tar 31 Oct 2010 tutampa kura ha ha ha
 
Hii nayo itabidi wajanja waitengenezee T-Shirt. Rais hawezi kuwatukana watu wake matusi rejareja kama hivi.
 
Attachments

  • Kikwete4.jpg
    Kikwete4.jpg
    14.9 KB · Views: 213
1:17 "Nikasema jamani, mswahili uongo, hachoki". Kikwete bonge la simpleton.

Rais mzima anawatukana watu wake hivi hivi, halafu hapo hapo anawaomba kura.

Anavyosema "Mswahili uongo hachoki" ina maana yeye naye yumo katika waswahili hao? Au yeye mzungu ?

Hivi nchi yetu ikoje ?

bila ya maneno ya aina hiyo unafikiri atapata kura vipi?

hapo anazungumza lugha ambayo ni rahisi kueleweka na wananchi na ambayo pia wananchi wanataka kuisikia.

mgombea anaezungumza 'nambari' tu na maneno magumu ya kitaaluma hapati kura Tanzania
 
Ili usiwatukane wananchi si lazima kuongea nambari wala kitaaluma. Angeweza kusema kuna watu wazushi sana, sasa yeye kaenda kuwa brand waswahili wote kwamba uongo ni tabia yao.

Halafu yupo katika kampeni za kuomba kura hapo, na watu watampa kura zao. Hatuthamini kauli, ndiyo maana anaona hata akitupa ahadi ambazo hazitekelezeki poa tu, si anaweza hata kututukana bila consequences, itakuwa ahadi tu ? Tena mtu mwenyewe huu ndio uchaguzi wake wa mwisho.
 
1:17 "Nikasema jamani, mswahili uongo, hachoki". Kikwete bonge la simpleton.

Rais mzima anawatukana watu wake hivi hivi, halafu hapo hapo anawaomba kura.

Anavyosema "Mswahili uongo hachoki" ina maana yeye naye yumo katika waswahili hao? Au yeye mzungu ?

Hivi nchi yetu ikoje ?
Ahadi kafikisha ngapi mpaka saa hizi?
 
Halafu yupo katika kampeni za kuomba kura hapo, na watu watampa kura zao. Hatuthamini kauli, ndiyo maana anaona hata akitupa ahadi ambazo hazitekelezeki poa tu, si anaweza hata kututukana bila consequences, itakuwa ahadi tu ? Tena mtu mwenyewe huu ndio uchaguzi wake wa mwisho.

mind set za kitanzania wewe achana nazo...

kikwete hajali kutukana wananchi kwa sababu anajua fika kuwa haina athari yoyote kwa kura atakazopata, na wananchi hata hawajijui hasa kama wametukwana. wanaona "waswahili kwa uongo!" ni maneno aliyeelekezewa huyo alosema uongo tu na wao halijawahusu.

mimi siwashangai hao wananchi wa chini kutoelewa tusi ukizingatia kuwa mgombea ubunge wa chama cha upinzani (ambae anatakwa kuwa makini zaidi ya ccm) alimpongeza na kumshukuru mtu alomtukana yeye na jinsia yake nzima ya wanawake kuwa ina infiriority complex na dhaifu.

raia bado sana kujielewa tanzania
 
Nimependa aliposema "JAMANI MIMI SIYO DIWANI...MSIITAFUTE ELIMU KWANGU... wakuu mezani walitazamana wakaangalia pembeni ndhani kimoyomoyo wakasema mwenyekiti na Rais Tunaye.. Yaani isu ya Ardhi kama kigamboni anasema ni ya DIWANI?
 
Kisa ni wakazi wa Kigamboni kuambiwa mpango mji unataka kubomoa nyumba zao.
Fuatilia kwenye video hii

http://www.youtube.com/v/UaviGdsJJN...&feature=player_embedded&fs=1"></param><param

Amekwepa hoja ya msingi na kurusha kwa mzigo kwa Diwani kwamba ndiye ana maelezo, sasa diwani aliyekuwepo kaenda kugombea ubunge, huyu mpya hajui chochote. Hapo kwa kweli naona wananchi wameliwa.

JK anasema atasaidia kuhakikisha haki inatendeka, wale watu wa Kipawa serikali hii hii ya JK haikuwatendea haki, je, wa Kigamboni watatendewa haki? Sana sana wakigoma, watapelekewa FFU na kuvunjiwa nyumba zao, maana sheria ya Ardhi iko wazi, kwamba ardhi ni mali ya serikali na wakati wowote serikali inaweza kubadilisha matumizi ya ardhi hiyo na ndio maana akina Chiligati huwa wanafika mahali wanatumia nguvu tu bila kuelewesha wananchi, maana wanajua mwisho wa siku whether mwananchi anataka au hataki, ataondoshwa tu.
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom