Mkutano wa Kikatiba tu ndiyo utaandika Katiba Mpya

Nivyema Mengi akelewa ya kuwa bila ya uongozi bira hakuna maendeleo....................na URAISI ni sehemu mojawapo ya utawala ambao kama hakuna kiongozi bora kwenye nafasi hiyo basi maendeleo yatakwama.........................kwa hiyo kuujadili URAISI 2015 ni sehemu ya kuhimiza maendeleo bora.........................matatizo yote ambayo Mengi ameyataja kuanzia UFISADI ni dalili ya kukosekana kwa utashi wa kisiasa wa RAISI aliyepo madarakani na hivyo kusababisha kushamiri kwa DHULUMA hapa nchini dhidi ya raia wanyonge.................
 
Mabomu yatawala mjadala wa katiba Send to a friend Thursday, 07 April 2011 22:01

Waandishi Wetu
VIUNGA vya Bunge mjini Dodoma jana viligeuka uwanja wa mapambano baada ya askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), kutumia mabomu na risasi za moto kutawanya mamia ya wanafunzi wa vyuo vikuu waliotaka kuingia katika ukumbi wa Pius Msekwa kushiriki mjadala wa maoni wa Muswada wa Sheria ya Mapitio ya Katiba.Wakati hali hiyo ikiwa hivyo mjini Dodoma, mkutano wa aina hiyo ulifanyika jijini Dar es Salaam uliovurugika baada ya kutokea vurugu.

Mapambano yaliyotokea mjini Dodoma, kati ya wanafunzi wa vyuo vikuu na FFU yalisababisha wakazi wa maeneo ya Makole, Uhindini, Sabasaba na Mtaa wa Railway kukimbia ovyo huku baadhi yao wakifunga maduka na biashara zao kuhofia kujeruhiwa kwa risasi.Hofu hiyo ilitokana na idadi kubwa ya watu, wengi wakiwa ni wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya mjini Dodoma, kulazimisha kuingia kushiriki mjadala huo katika Ukumbi wa Msekwa wenye uwezo wa kuhimili watu 300 ambao tayari ulikuwa umeshajaa.

Katika vurugu hizo, wanafunzi hao walivunja lensi ya kamera ya Mpigapicha wa gazeti hili kwa jiwe walilokuwa wanataka kumpiga nalo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk James Msekela, wakati akizungumza nao.

Msekela aingilia kati
Vurugu hizo ambazo zililazimisha polisi kupiga risasi takribani 19 hewani, zilianzaa saa 5:00 asubuhi na kudumu kwa zaidi ya dakika 45. Hata hivyo, wakati risasi zikirindima wabunge na wadau mbalimbali walikuwa wakiendelea na mjadala huo katika ukumbi huo.

Dalili za kuwapo kwa vurugu hizo zilianza kujionyesha mapema kufuatia baadhi ya wanafunzi kuzuiliwa kuingia katika lango la ukumbi huo licha ya kufika mapema.Kuzuiliwa kwa wanafunzi hao kulisababisha baadhi ya wabunge hasa wa Chadema kulazimika kutoka nje ya ukumbi na kwenda kuwatuliza ili wasilete fujo.

"Nawashauri mtumie hekima na busara katika kuingia ndani ya ukumbi huu kwa kuwa ni haki yenu kikatiba, lakini tulieni tufanye utaratibu,"alisema Mbunge wa Kawe, Halima Mdee.Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini, naye alitumia muda mwingi kuwasihi wanafunzi kuacha kutumia nguvu, badala yake watumie hekima.

Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema, ambaye anabebeshwa zigo hilo la ghasia, naye alitoka ndani ya ukumbi huo wa Msekwa na kuwahutubia wananchi hao waliokuwa wamefunga barabara. Lema anayetajwa kuamsha umma huo kufika viunga hivyo vya Bunge, aliwaambia wanafaunzi hao kuwa ni haki yao kuchangia maoni katika muswada huo kwani unagusa mustakabali wa nchi na alipinga hatua ya muswada huo kujadiliwa na mikoa mitatu (Dodoma, Dar es Salaam na Zanzibar).

Dk Msekela alimlaumu Lema kwamba ndiye chazo cha wanafunzi kujitokeza kwa wingi.
"Matatizo haya yamesababishwa na Lema ambaye jana alikwenda katika vyuo vikuu kuwahamasisha wanafunzi wafike kujadili muswada huo," alisema Dk Msekela.Hata hivyo, Lema aliyekuwa amesimama nyuma ya Dk Msekela, alijitokeza na kukiri kufanya hivyo na kusisitiza kwamba hataacha kufanya hivyo kwa kuwa ni haki yake.

"Mimi Lema ndiye niliyekwenda UDOM kuwahamasisha waje kwa kuwa hawa ni wasomi na muswada umeandikwa kwa lugha ya Kiingereza, hivyo wananchi wa kawaida hawawezi kuujadili tusipowaleta wasomi kama hawa," alisema Lema na kusisitiza:
"Sitaacha kwenda vyuoni kwani Jumamosi (kesho) nitakwenda kufungua tawi huko."
Awali wanafunzi walikuwa wakiimba nyimbo mbalimbali za hamasa zikiwamo nyimbo za Taifa pamoja na wimbo maalumu ambao hutumiwa na wanafunzi wa Vyuo vikuu unaosema, "Kama sio juhudi zako Nyerere, mafisadi wangetoka wapi."Wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali, wanafunzi hao walisema hawatoki katika eneo hilo na wako tayari kwa lolote.

Barabara zilifungwa
Barabara ya Kati Dodoma ilifungwa na wanafunzi hao na kusababisha magari kutumia njia ya Dodoma Inn (Barabara ya kwanza) ambayo ina mzunguko mrefu.Wananchi katika maeneo ya Makole, Uhindini, Sabasaba na Mtaa wa Railway walitaharuki na kukimbia ovyo huku baadhi yao wakifunga maduka na biashara zao kuhofia mirindimo ya risasi.

Tambwe achafua
hali ya hewa Dar
Wakati Dodoma kukiwaka moto, mjadala huo ulifanyika pia katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, lakini haukuisha vizuri baada ya Mkuu wa Kitengo cha Propaganda cha CCM, Tambwe Hizza kuchafua hali ya hewa.
Hizza ambaye alikuwa ni msemaji wa 10 na wa mwisho akiwakilisha CCM , alishindwa kuendelea na mada yake baada ya washiriki wa kongamano hilo kupiga makofi ya bila mpangilio huku wakimzomea.

Akitoa hoja yake, Tambwe alianza kwa kumpongeza Rais Jakaya Kikwete kwa kile alichokiita kuonyesha nia ya kupatikana kwa Katiba mpya na kwamba kupinga muswada huo ni matokeo ya mfumo wa vyama vingi ambao unaruhusu tofauti ya mawazo.

"Tangu nchi yetu iliporuhusu mfumo wa vyama vingi tulijua kutakuwa na mawazo tofauti," alisema Hizza huku akirushiwa maneno ya kebehi na washiriki wakisema "Jadili muswada"
Lakini Hizza aliendelea kusema, "Wote tunataka Katiba mpya. Kwa mujibu wa Ibara ya 98 ya Katiba ya sasa, mabadiliko ya katiba yanaweza kuwa ni kubadilisha, kufuta au kuirekebisha ,kwa hiyo jina tu marejeo ya katiba katika muswada huu lisiwape tabu."

Washiriki walimzomea Tambwe huku wengine wakipiga makofi, lakini yeye aliendelea kuzungumza bila kujali kelele zao. Wakati washiriki wakiendelea kumzomea Tambwe, Mwenyekiti wa mdahalo huo, Mbunge wa viti Maalumu, Pindi Chana (CCM), aliwataka washiriki wa kongamano hilo kunyamaza na kumsikiliza Tambwe.

Ushauri huo Chana haukuweza kuwatuliza badala yake walizidisha kelele huku wakimzomea wakisema, "Aondoke..., aondoke, aondoke, aondoke…". Hali hiyo ilidumu kwa dakika tano, kisha Chana alitangaza kuahirisha kongamano hilo na Tambwe akarudi kuketi sehemu yake.

Uamuzi wa Tambwe kuketi ulizidi kuwasha moto kwani washiriki walianza kuzozana na nusura ngumi zipigwe, lakini askari polisi waliokuwapo katika ukumbi huo walifanikiwa kutuliza ghasia.

Vijana wazozana
Hali hiyo ilionyesha wazi kuwapo kwa makundi makubwa mawili ya Chadema na CCM, ambayo yalipingana, huku baadhi ya vijana wa chama tawala wakiwashutumu vijana wenzao wa chama pinzani, wakidai kuwa chama hicho kimewapa fedha ili wakafanye fujo.

"Chadema wamewapa fedha mje kufanya fujo, tuna ushahidi hata kijana wetu mmoja naye amepewa," alisema Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kinondoni, Emanuel Makene. Hata hivyo, kauli hiyo ilipingwa na mzee aliyejitambulisha kwa jina la Salim Nyambua Said, akisema CCM wamekosea kuleta watu wasio makini kwenye kongamano hilo,
"Chanzo cha vurugu hizi ni CCM kuleta wahuni.'' Kauli hiyo ilimsababisha kutaka kupigwa na vijana wa chama tawala kabla hajaokolewa na polisi.

Vijana wengi waliokuwapo nje ya ukumbi huo, walisisitiza kuwa hawahusiki na Chadema na kwamba wao hawakuridhishwa na maneno ya Tambwe. "Sisi hatuhusiki na Chadema, ila tumekerwa na Tambwe Hizza, badala ya kujadili muswada anaviponda vyama vya upinzani," alisema kijana mmoja ambaye hakutaka kutaja jina lake.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuvunjika kwa kongamano hilo, Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa, alisema kuna vijana wameandaliwa kufanya vurugu. "Yanayotokea hapa inaonyesha kuna vijana wameandaliwa, au hawakuandaliwa kuja kufanya fujo, mimi nawashauri kuheshimu mawazo ya watu hata kama hawayataki," alisisitiza Tendwa.

Jaji Warioba
Vurugu katika kongamano hilo zilianza kujionyesha pale aliposimama Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba, ambaye alianza kwa kumsifu Rais Kikwete kwa kuanzisha muswada huo akisema ni hatua nzuri.

"Muswada huu ni hatua ya ya kuelekea kwenye utaratibu wa kupata Katiba mpya…. Nafikiri hii ni hatua kubwa. Tunayo Sheria ya kuunda Tume ambayo Rais angeweza kuitumia, lakini kwa umuhimu wake ameunda tume ambayo atakuwa akipata ushauri, mimi sioni tatizo," alisema Jaji Warioba na kuonekana kuwakasirisha washiriki wa kongamano hilo walioanza kuguna na kupiga makofi mfululizo na kumfanya ashindwe kuendelea kuzungumza.

Hali hiyo ilimfanya Pindi Chana, kuwatuliza washiriki ili Jaji Warioba aweze kuendelea kuzungumza.
Kwa kusoma upepo, Jaji Warioba akabadilisha mwelekeo na kuanza kuukosoa muswada huo hali iliyowafanya washiriki hao kutulia kimya na kumsikiliza.

Jaji Warioba alikikosoa kifungu cha 9 (2) kinachozuia mambo kadhaa kujadiliwa, aliyaita mambo hayo kuwa ni matakatifu. "Kifungu cha 9 (2) kimeweka mambo matakatifu ambayo hayapaswi kuguswa. Haya ndiyo Katiba yenyewe, tunachotaka watu watoe maoni yao," alisema.

Kongamano hilo baada ya kufunguliwa na Waziri wa Nchi Katiba Ofisi ya Rais, Utawala Bora, Mathias Chikawe, lilikuwa na wasemaji kutoka vyama vya siasa na taasisi mbalimbali.

Viongozi wa vyama vya siasa walikuwa ni Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbrod Slaa, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa APT Maendeleo, Peter Kuga Mziray, Mwenyekiti wa NCCR- Mageuzi, James Mbatia na Katibu wake, Sam Ruhuza.

Pia walikuwapo wawakilishi wa taasisi zisizo za kiserikali kama Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kilichowakilishwa na Imelda Urio.Wengine ni Dk Modesta Opiyo kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe, Gideon Mandes kutoka vyama vya walemavu na Dk Francis Michael. Kwa ujumla, wachangiaji wote waliukosoa muswada huo na kutaka ufanyiwe marekebisho.

Imeandaliwa na Habel Chidawali na Israel Mgussi,
Dodoma, Elias Msuya, Dar
 
Comments




0 #10 mzalendomzanzibari 2011-04-08 04:26 mwandishi wa habari ajirekebishe sio mikoa mitatu na kuiweka zanzibar kama mkoa. zanzibar ni nchi ilioungana na Tanganyika kuunda Jamhuri ya muungano, acheni kupotosha kwa makusudi
Quote









0 #9 mbiligi 2011-04-08 04:10 Dr Msekela?kweli lawama alizozitoa dhidi ya Mh Lema zinaendana na elimu yake? Kuhamasisha wanafunzi kijadili katiba iliyoandikwa kwa kiingeleza ni kosa? Elimu ya Dr msekela ni ya kuchakachua.
CCM wanaleta mzaa na katiba!!! Tambwe Hiza kuwakilisha CCM? katiba si ushabiki bali ni uelewo maana itadumu kwa kipindi kirufu. CCM bora si wangewatumia wakili Ridhiwani au Mh January au Mh Nkono.
Mh Tendwa! kama kuna ushahidi watu wameandaliwa kufanya vuruga ktk mjadala wa katiba basi vyombo vya usalama vimeshindwa kazi. Hii ni hoja potofu toka kwa Mh Tendwa ambayo yaonyesha ni mbumbumbu tena hafai kabisa kwa madaraka aliyo nao
Mwenyekiti wa CCM Mr.Makene kweli CDM wanapigania Katiba, wamepata fulsa ya kuijadili kweli wanaweza kuleta vurugu? Hatudanganyiki kabisa na propaganda zako umeshindwa kazi majimbo mawili ktk wilaya yako yanamilikiwa na CDM. Leta hoja ya kuwaeleze wanaCCM wa Dar ktk mkoa wote ni kinondoni peke yake imepoteza majimbo mawili?
Quote









0 #8 Bakari 2011-04-08 04:09 CCM kila kukicha wanakuja na propaganda mfu. Watambue kuwa vijana wamechoka, wala hawahitaji kupewa FEDHA kupinga huu muswada.

Kama wao iliwalazimu kuwalipa vijana ili kushiriki mikutano ya CCM, wasidhani na vyama vingine vinafanya hivyo, VIJANA WAMECHOKA!
Quote









+1 #7 elba 2011-04-08 02:43 Naomba siku nyingine CCM msimtume Tambwe hiza kuwawakilisha. Huyu mtu sio makini kabisa, Kwa jina la kitaalam waweza kumwita "BONGOLALA"
Quote









+1 #6 Michael Waso 2011-04-08 02:28 Kwenu nyie polisi na serikali ya CCM, Mwenyekiti wa mapinduzi ya China Mao Tsetung alisema: "We shall heal our wounds, collect our dead and continue fighting." Kwa hili la Katiba Mpyaa vijana wa UDOM tunarudia maneno ya Mao, tutaganga madonda yetu, tutawazika wafu wetu na kuendelea na mapambano mpaka kieleweke!
Quote









+1 #5 Michael Waso 2011-04-08 02:16 Kizazi cha karne ya 21 kimeanza kuonyesha uelewa wa haki zao. Mie namsifu Lema kwa ujasiri wake. CCM husema tusifanye siasa lakini wanayo matawi ya UVCCM hata vyuoni, sasa hi ni nini sio siasa hii? Lema anaujasiri sana, anawaamsha vijana, wasiwe kama vijana wa CCM kzi yao ju-discuss watu na siyo ideas. Oh Sumay, Oh Sitta lakini vijana wa Chadema wana-discuss ideas: Katiba mpya, Dowans, Upatikanaji wa Umeme, Kagoda, Deep Green. Mtokeo yake serikali ya CCM inawapiga mabomu. Wasomi wote wanaichukia CCm na hilo si siri! Watoto wa vigogo ndio waliobaki CCM, Januari Makamba, Vita Kawawa, Nape Nnaye, Rizwani Kikwete, n.k. Tunataka katiba mpya ili nchi hii isije ikarithishwa kwa hao wanaolinda maslahi ya familia
Quote









+3 #4 saidi 2011-04-08 02:13 kama wanadhani kwamba bado wataendelea kuwabuluza watanzania kwa vigezo vya kutokua na ufahamu nawaambia kwamba sasa si hivyo tena ule wakati umekwisha ndugu zangu, si busara kuzungumzia masuala ya hatima ya nchi kwenye kibaraza cha mjumbe wa nyumba kumi ukishirikisha wanaomzunguka mjumbe.Nionacho mimi hapa ni hawa wanaojiita waendesha nchi kutokua na taswira mpya ya watanzania kwa sasa hii ni hatari kubwa maana wanaweza toa maamuzi yatakayo gharimu amani ya nchi.
Quote









+2 #3 Miriam Awadhi 2011-04-08 02:05 Kikwete, You can fool all the people some of the time, and some of the people all the time, but you cannot fool all the people all the time. Haya aliyasema Abraham Lincoln; utawadanganya wato wote kwa wakati fulani tu lakini huwezi kuwadangaya watu wote milele
Quote









+1 #2 Abdulrahman Kisiwa 2011-04-08 01:59 Watanzani tumefikia ukingoni, madharau wanayotufanyia serikali ya CCM yametuchosa, sasa tupo radhi kuikabili dola yao head-on-collision kwa kiswahili ana kwa ana! Watatuua wachache wetu lakini tutawafikia na huo utakua mwisho wao. Katiba hii mpya inakila dalili za mapambano mazito!
Quote









+1 #1 Jerry 2011-04-08 01:52 Thanks Mwananchi! Ila mambo ya Loliondo saasa imetosha, yawekeni ukarasa wa pili. Muhmu ni katiba na mstakabali wetu watanzania. Tambwe ni muhuni na aliyosema baada ya mjadala kuiarishwa ni kwamba ni vema ulivyoairishwa ni usthibitisho wazi CCm ina nia mbaya na vuguvugu hili la kudai katiba itakayo kidhi matakwa ya watanzania wa karne y 21! Peoples Power!
Quote
 
Maoni mchakato wa Katiba vurugu tupu

Imeandikwa na Na Gloria Tesha, Dodoma; Tarehe: 7th April 2011 @ 23:59 Imesomwa na watu: 208; Jumla ya maoni: 0








UTOAJI maoni juu ya uundwaji tume ya kuendesha mchakato wa Katiba mpya nchini umeingia dosari kwa mikutano ya Dodoma na Dar es Salaam kugubikwa na vurugu.

Katika mikutano yote ya jana, polisi walilazimika kutumia nguvu za ziada kutuliza ghasia, huku
Dodoma wakitumia risasi na mabomu ya kutoa machozi kutawanya kundi la wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom).

Hata hivyo katika hali isiyo ya kawaida, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema) alikiri jana kusababisha vurugu za Dodoma katika eneo la ukumbi wa zamani wa Bunge wa Pius Msekwa mjini hapa. Mbunge huyo alikiri jana mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk
James Msekela kuhamasisha wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kwenda kwenye ukumbi huo kutoa maoni ya Katiba na kusababisha vurugu kubwa, iliyolaz-imu polisi kufyatua mabomu ya kutoa machozi na risasi nje ya jengo hilo.

Lema alitoa kauli hiyo, muda mfupi baada ya Msekela kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu vurugu hizo na kueleza kuwa zilisababishwa na baadhi ya viongozi wa kisiasa
wanaotumia vijana kuvuruga amani ya nchi na kwamba alipata taarifa ya kuwapo wanasiasa waliokwenda Udom kuhamasisha wanafunzi kuja bungeni Alhamisi.

Baada ya kauli ya Msekela iliyoambatana na kupiga marufuku wanasiasa kufanya kampeni Udom kwa kuwa ni kinyume cha sheria, Lema alijitokeza papo hapo na kukiri kuwa yeye ndiye aliyekwenda Udom na alizungumza na wanafunzi nje ya chuo kwa mujibu wa sheria na hakuwahamasisha kurusha mawe.

" Jumamosi hii nakwenda tena, ni wajibu wangu nikiwa mbunge kufanya hayo, nisingependa kutishwa kabisa, huo ni wajibu wangu mbunge kuhakikisha watu wanauelewa muswada, napenda Mkuu wa Mkoa uelewe kuwa mimi nilikwenda na nitakwenda tena kufungua tawi la chama Jumamosi hii, sheria inaniruhusu," alisema Lema ambaye baadaye aliwaambia waandishi kuwa atakwenda na Mkuu huyo akitaka kumkamata, amsubiri huko na haogopi, maana sheria anazijua.

Lema alisema alikwenda kuhamasisha wasomi waje kutoa maoni kuhusu Katiba kwa kuwa
wauza nyanya na wafanyabiashara wa magengeni, hawawezi kutoa maoni kwa sababu hawaelewi Kiingereza na masuala ya Katiba, ila wasomi.

Katika eneo la Bunge, watu waliodhaniwa kuwa wananchi, lakini asilimia kubwa kujulikana kuwa ni wanafunzi wa Udom, walizuia njia huku wakiimba nyimbo za kudai Katiba mpya kwa uhuru, lakini baadaye vurugu zilipozidi, Lema aliyekuwa ndani ya ukumbi wa maoni, alitoka nje na kuwataka watu hao watulie ili utaratibu wa kwenda uwanja wa Jamhuri zifanyike, lakini walisikika wakisema, "Lema umetusaliti."

Baadhi yao, walifika eneo la Bunge mapema asubuhi na kulazimisha kuingia ukumbini bila kupekuliwa, tena kwa idadi kubwa, huku ukumbi huo ukiwa na uwezo wa watu 540 na walipoelezwa kusubiri utaratibu wa Kamati kwenda kupokea maoni yao ukumbi wa Chimwaga (Udom), walianza kurusha mawe na kusababisha Mkuu wa Mkoa kuamuru polisi waingie
kazini.

Hali ya tafrani iliyozuka katika milango ya kuingilia eneo la Bunge kuanzia asubuhi, ilisababisha Polisi wa Kutuliza Ghasia (FFU) kutanda katika maeneo hayo, huku mchakato
wa kupokea maoni kwa wananchi walioingia ukumbini ukiwa unaendelea, lakini vurugu
zilipozidi, FFU wakiwa na gari lao waliingia kutoka nje ya uzio wa Bunge kwa kasi na kufyatua risasi walikokuwa wananchi na wanafunzi hao.

Hata hivyo, Msekela alisema uongozi wa Bunge umekubali kwenda Chimwaga saa 10 jioni Alhamisi ili kupokea maoni ya wanafunzi hao kuhusu Mchakato wa Muswada wa Uundwaji wa Tume ya kukusanya maoni ya uanzishwaji wa Katiba Mpya, lakini kinachotokea ni kutoelewa kwa wanafunzi kuwa si kupokea Muswada wa Katiba Mpya.

Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la Bunge kuhusu tukio hilo, Katibu wa
Bunge, Dk Thomas Kashililah, alisema tukio hilo ni la aibu na waliofanya fujo hawakutumia busara wala hekima, kwa kuwa uwezo wa ukumbi ni mdogo na kamati ndogo ya Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala Bora iliyopo hapa ilisharidhia kwenda Chimwaga.

"Ukumbi ni mdogo, tunapata shida, ni kwa namna gani mtu kama ana nia njema ya kutoa maoni anakuja na mawe mfukoni, maoni gani yanatolewa kwa mawe, si busara, tuliliona hilo la ukumbi na tukakubaliana awamu mbili za kupokea maoni, asubuhi mpaka saa nane na saa tisa kuendelea, tulipobaini wengi ni wanafunzi, tukasema kamati iende Chimwaga, lakini hawataki," alisema Dk. Kashililah.

Polisi walipoanza kufyatua risasi zaidi ya milio 20 ilisikika huku mabomu ya kutoa machozi
nayo yakifuatia na kusababisha wanafunzi na maelfu ya watu waliokuwa nje ya jengo la Bunge
kukimbia bila mpangilio na kusababisha kamera za wapiga picha kuharibika, watu kuanguka na
wengine kupigwa mawe. Hata hivyo, hakuna taarifa za waliojeruhiwa kiasi cha kukimbizwa hospitalini kwa kuwa Polisi ilirejesha amani baada ya tafrani hiyo.

Awali, wakizungumza kwa nyakati tofauti nje ya jengo la Bunge, wanafunzi wa Udom walisema
hawataki kwenda Chimwaga kwa kuwa wanahisi ni ujanja wa kisiasa kwani walipata matangazo
yakiwataka waje Msekwa na si Chimwaga na kama Kamati inataka waende Chimwaga, basi waambatane.

"Hakuna anayeondoka hapa, tunataka twende Jamhuri ili kila mtu aseme, kama hawataki nasi hatuondoki hapa, kama ni Chimwaga twende mguu kwa mguu," alisema Petro Karungamya, na kuungwa mkono na mwanafunzi mwenzake, Haruna Mikidadi. Kamati hiyo ndogo ya kupokea
maoni Dodoma ilikuwa chini ya Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala Bora, Angela Kairuki.

Kamati nyingine mbili ziko Dar es Salaam na Zanzibar na zitakusanya maoni kwa siku tatu, Alhamisi, Ijumaa na Jumamosi na ikibidi Jumapili. Naye Halima Mlacha anaripoti kuwa mkutano wa Dar es Salaam wa kukusanya maoni juu ya Muswada wa Uundwaji Tume ya Mapitio ya Mabadiliko ya Katiba ya nchi wa mwaka 2011, ulivurugika na kulazimika kusitishwa hadi leo kutokana na kuzuka vurugu na mapigano wakati mkutano huo ukiendelea.

Vurugu hizo zilianza baada ya Naibu Mkuu wa Kitengo cha Propaganda CCM, Tambwe Hizza, kutoa maoni kwa niaba ya chama hicho, na kujikuta akizomewa na kuitwa fisadi mara alipoanza kusifia jitihada za Serikali za kuanzisha mchakato huo wa kuunda Katiba mpya.

"Muswada huu ni jitihada za Serikali za kuwasikiliza wananchi, yatakayoongelewa yatazingatiwa, lakini pia mikutano hii ya hadhara isitumike kumnyima Rais madaraka
yake," alisema Tambwe na kabla ya kumalizia hoja yake alizomea na vurugu kuibuka.

Gazeti hili lilishuhudia ukumbi wa Karimjee ambako mkutano huo ulikuwa ukifanyika ukichafuka ghafla, kwa washiriki, wengi wao wakiwa vijana, kutishia kumtoa mbele Tambwe huku waliokuwa wakimtetea, wakiambulia kupigwa nao bila kukubali na hivyo kuzuka
mapigano.

Hata hivyo, polisi waliokuwa eneo hilo na wengine kuongezeka walidhibiti tafrani hiyo ingawa mkutano huo ulishindwa kuendelea kutokana na Tambwe kugoma kukaa chini na badala yake kuimbwa kwa kebehi.

"Aondoke, CCM ni aibu, fisadi," ndiyo maneno ya nyimbo yaliyokuwa yakisika ukumbini hapo huku baadhi ya waliohudhuria wakishindwa kuvumilia na kuvamia eneo alilosimama Tambwe hali iliyosababisha polisi kuingilia kati na mkutano huo kusitishwa.

"Kamati ilikuja hapa kukusanya maoni ya wananchi juu ya muswada huu, lakini wote ni mashahidi wa mazingira yaliyojitokeza muda mfupi, hivyo Kamati imeridhia kusitisha
mkutano huu hadi kesho (leo) ili kutengeneza mazingira mazuri ya kukusanya maoni haya," alisema Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, Gosbert Blandes.

Awali akiwasilisha maoni yake mbele ya baadhi ya wajumbe wa Kamati hiyo, Waziri Mkuu mstaafu Joseph Warioba, alisifu juhudi za Rais Jakaya Kikwete za kutengeneza muswada huo, lakini pia alishauri wananchi wapewe nafasi ya kutoa maoni juu ya masuala muhimu
yanayowahusu na kipengele kinachowabana kirekebishwe.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utawala Bora, Mathias Chikawe, alionesha kusikitishwa na vurugu zilizotokea na kusisitiza kuwa mkutano huo lengo lake ni kupokea maoni ya mwananchi yeyote yawe mabaya au mazuri na kuyafanyia kazi yatakayoonekana kuwa na tija kwa Watanzania.

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alitaja baadhi ya vifungu katika muswada huo virekebishwe likiwamo suala la kupewa madaraka makubwa Rais na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kupewa jukumu la kusimamia utaratibu wa kupigia kura Katiba hiyo.

Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alisema shinikizo na hamasa la kuundwa kwa Katiba mpya lilitoka kwa vyama vya upinzani, lakini kwa bahati mbaya muswada huo haujavitaja vyama hivyo.

James Mbatia, Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, alipendekeza muswada huo upelekwe bungeni na Ibara ya 98 ya Katiba ibadilishwe, ili kuwezesha kuundwa Baraza la Kutunga Katiba, ambalo litasimamia uteuzi wa makamishna wake na sekretarieti, kuliko
kumwachia kazi hiyo Rais pekee kama muswada unavyosema.

Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa, alisema kitendo cha baadhi ya washiriki katika mkutano huo kuanzisha vurugu ni cha kusikitisha, kwa kuwa kinawanyima wananchi wengine fursa na uhuru wa kutoa maoni yao juu ya muswada huo.

Wakati huo huo, Waziri wa Katiba na Sheria, Celina Kombani amesema mchakato wa kupokea maoni ya uundwaji wa Katiba Mpya utaigharimu Serikali zaidi ya Sh bilioni 27 kwa sasa na kiwango hicho kinaweza kubadilika kulingana na mahitaji ya mchakato.

Aidha, amelaani upotoshaji unaofanywa na baadhi ya watu hasa wanasiasa kuwa kinachofanyika Dodoma, Dar es Salaam na Zanzibar siku hizi nne ni utoaji maoni ya
wadau kuhusu Muswada wa Katiba Mpya, kitu ambacho si kweli kwa kuwa ni maoni ya Muswada wa Uundwaji wa Tume itakayopokea maoni ya wananchi.

Waziri aliwaondoa hofu wananchi na wadau wote kuhusu suala hilo kwa kusema Bunge limeongeza Jumapili pia itumike itakapobidi na kwamba Serikali itazingatia na kuyafanyia kazi maoni yaliyotolewa na wanazuoni wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDASA) na wananchi wengine kuhusu Tume hiyo kwa kuwa serikali ni sikivu wakati wote.

Kombani alisema nia ya Serikali ni kuhakikisha mwaka 2014 Katiba Mpya inapatikana na Muswada wa Uundwaji wa Tume, baada ya maoni, utafikishwa bungeni Aprili 18 ili upitishwe
na ipatikane sheria itakayowezesha Tume kuanza kazi Juni mosi.
 
Constitution talks chaos Send to a friend Friday, 08 April 2011 00:03

By The Citizen Reporters
Dodoma. Public forums on the constitutional draft Bill were yesterday marred by chaos in Dar es Salaam and Dodoma.Hundreds of people in Dodoma, the designated capital of Tanzania, mostly university students, engaged in running battles with the police.The chaos began when students from various higher learning institutions defied police orders to get away from Parliament buildings shortly before the start of a public hearing by MPs. The students started a confrontation with the police shortly after the latter denied them entry to the Bunge grounds where they had gathered from 7am.

Police officers manning the main entrance told the multitude of students that they could not allow all of them to get into Parliament buildings. This prompted an angry reaction from the crowd that started chanting patriotic songs as a way of pressing for their right to be allowed in.
Those waiting outside the Parliament buildings were people from all walks of life, including officials from civil society organisations and ordinary citizens. Their huge turnout was presumably prompted by announcements popularizing the event through the mass media a day before.

Among those who hung outside the Bunge premises from 7am to almost 11am were the executive director of the Tanzania Media Women Association (Tamwa), Ms Ananilea Nkya, and the executive director of the Legal and Human Rights Centre (LHRC), Mr Francis Kiwanga.

The students gathered in the middle of the road and announced that they would continue with a separate public hearing of people's views on the constitutional review draft bill 2011. They said this was because the one inside the Bunge premises was meant for perpetrators of graft and not ordinary Tanzanians. The Bill will be tabled in the House next week.

When the situation became tense, police began using tear-gas to disperse the students from the premises following an order by the Dodoma regional commissioner, Dr James Msekela. Police started to tear-gas the students after some of them started throwing all sorts of ‘missiles', including stones, at the armed policemen.

The students shouted down Dr Msekela telling him that the public hearing should be held at Jamhuri Stadium where it could have accommodated many Tanzanians and not MPs alone. The Arusha Urban Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ticket, Mr Godbless Lema, who was in favour of the students, tried to cool them down.

After the police had dispersed the students, Dr Msekela told an impromptu press conference that a decision was made to hold another public hearing at the Chimwaga conference hall on the outskirts of Dodoma municipality. Without mentioning names, Dr Msekela accused politicians who he said had instigated the students to become riotous.

At this point, Mr Lema told the RC that he went to the University of Dodoma to ask the students to participate in the hearing, but did not tell them to engage in a violent behaviour. The Clerk of the National Assembly, Dr Thomas Kashililah, also called another press conference at which he blamed the students for breaching parliamentary rules and regulations.He said parliament premises were under strict security and all people, including journalists and MPs, have to undergo special inspections before being allowed to enter its halls and rooms.

Some of the songs they chanted included the popular "Kama Siyo Nguvu Zake Nyerere Uhuru Tungepata Wapi?" Others sang Tanzania, Tanzania Nakupenda while the rest sang the national anthem.
The group later quietly started parallel discussions of some sections of the draft bill which they said were riddled with massive irregularities.

They likened the public hearing inside the Bunge premises to a kitchen party where entry was specifically for people with "exclusive" rights."We insist that the debate on the constitutional review process is the right of all Tanzanians. We will not retreat or relinquish the fight for it until the process that respects public opinion for a new constitution is put in place," said the students in unison.

They said there was room for authorities to arrange for the public hearing at spacious venues like the Jamhuri Stadium and not the Pius Msekwa Hall. The Dodoma regional police commander, Mr Zelothe Steven, said nobody was arrested in connection with the chaos.

In Dar es Salaam, another constitutional public hearing was temporarily suspended yesterday when a crowd of university students disagreed with Mr Tambwe Hiza who was representing Chama Cha Mapinduzi.It all started when Mr Hiza differed with those who challenged presidential powers in the bill, saying: "You cannot just decide to infringe upon the president's powers through such a forum, and the bill is right but….."

The crowd did not give him time to continue and persistently clapped their hands for more than ten minutes. This forced the chairman, Mr Pindi Chana, to intervene and calm down the audience. But the trend continued as Mr Tambwe attempted to proceed. Finally the whole meeting became uncontrollable, forcing the chairperson to postpone the debate.

Earlier yesterday, members of the public rejected the Constitutional Review Bill 2011, saying it contained a lot of shortcomings. They contended that it would jeopardise the conception of a new constitution.Reported by Polycarp Machira in Dar, Joas Kaijage, Daniel Msangya and Mkinga Mkinga in Dodoma
Speaking during the public debate held at the Karimjee Hall, some members of the public felt that the bill needed serious changes for it to serve the intended purpose.

Common issues that arose include restriction of public members from discussing the presidency, the Union government and the government of Zanzibar as outlined in section two of the bill.They argued that these were some of the pertinent issues that needed to be clearly debated on to ensure mutual understanding is reached.

Former Prime Minister Joseph Warioba, who praised the government for the goodwill to establish a new constitution, faulted the ‘sanctity' of the three issues that would dilute the whole process.
The retired Judge said: "Matters of presidency, both the Union and government of Zanzibar which is classified as untouchable, are in real sense the real constitution. How can you refrain from discussing them?"

He said people may have various opinions on what kind of government they want; whether to have one government instead of the current situation, among other things, which they should be freely allowed to discuss.

He also noted that the campaign for or against the draft constitution, once that stage is reached, ought to be public responsibility unlike the bill which states that it remains the work of the commission to carry out such campaigns.
But the Civic United Front (CUF) chairman, Prof Ibrahim Lipumba, expressed lack of trust in the National Electoral Commission in carrying out the referendum as indicated in the bill. He said there should be serious reforms that would see the formation of an independent electoral commission if it is to oversee the referendum.

Dr Modesta Opiyo of the Mzumber University‘s Law department, pointed out that the bill does not clearly point out how the public will get a feedback once the report has been compiled.

She said this is because the bill states that the commission will submit the report to the president.
She observed that the provision that allows the president to compose the terms of reference was not in order as he could misuse the opportunity to compile what suits him/her.
 
Warioba: Wananchi wasizibwe midomo


*Ni katika mjadala wa Muswada wa Katiba mpya
*Ataka kila kitu kijadiliwe kupata kwa uwazi
*CCT yasema rais amepora madaraka ya wananchi


Na Tumaini Makene

PAMOJA na kuzuka kwa zogo kubwa lililosababisha mkutano wa utoaji maoni ya Muswada wa
Sheria ya Marekebisho ya Katiba kuvunjika, muswada huo umeendelea kukosolewa kwa kiasi kikubwa, huku serikali ikiambiwa isizibe watu midomo, kuhoji au kuzungumza baadhi ya masuala 'kwani hayo yanayozuiliwa kuhojiwa ndiyo katiba yenyewe'.

Imeelezwa kuwa itakuwa si sahihi kuwazuia Watanzania kuhoji baadhi ya masuala ya msingi hata kama tayari yapo katika katiba ya sasa, kwani ni bora yakajadiliwa kwa kina ili yajulikane kama yanakidhi mahitaji ya watu kujitawala au la.

Hayo yalisemwa jana Dar es Salaam na mmoja wa viongozi waandamizi wastaafu nchini, Jaji Joseph Warioba, wakati akitoa maoni yake katika kuboresha muswada wa sheria ya marekebisho ya katiba, akisisitiza kuwa masuala yaliyoko sehemu ya 3, kifungu cha 9(2), yajadiliwe bila zuio lolote.

Kifungu hicho cha muswada, kinataja mambo 8 ambayo ni marufuku watu kuyahoji au kuyazungumzia wakati tume ya kukusanya maoni ya watu juu ya katiba mpya itakapokuwa ikitekeleza majukumu yake.

Masuala hayo yanayoitwa kuwa ya 'heshima na utukufu', hivyo hayapaswi kuguswa kwa maslahi ya taifa, yameainishwa katika muswada kama ifuatavyo; Kuwepo kwa Muungano wa Tanzania na Zanzibar, kuwepo kwa mihimili mitatu ya dola (bunge, serikali na mahakama), nafasi ya urais, mshikamano wa kitaifa na amani ya nchi.

Mengine ni; kuwepo kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, kuwepo kwa mfumo wa uchaguzi wa kidemokrasia, haki za binadamu, dhana ya utu wa mtu, usawa mbele ya sheria na mfumo unaoweka utaratibu wa kufuata sheria, dhana ya Serikali ya Tanzania kutokuwa na dini na uhuru wa mahakama.

"Haya mambo yanayoitwa matakatifu na hivyo hayaguswi ndiyo katiba yenyewe, ndiyo mambo ya muhimu katika katiba huwezi kuyaondoa watu wasiyazungumze...lazima watu wayazungumze hata kama tayari yako katika katiba ya sasa. Msiwazuie watu kusema, kama ni muungano tuwaruhusu waseme.

"Watu wasikilizwe, wengine hawafurahishwi na muundo wa muungano ulivyo sasa, wengine watataka serikali moja, wengine serikali tatu, kama wakiweza kuwashawishi watu wengi wasikilizeni, hata kama watasema hatutaki kuwa na rais waache waseme, wanataka kuzungumzia Serikali ya Mapinduzi waacheni, huu ni wakati wa masuala haya kujadiliwa, maana ndiyo yanayozungumzwa sana sasa, ndiyo katiba haya.

Jaji Warioba ambaye mbali ya kuwahi kuwa jaji wa mahakama kuu pia aliwahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais, alisema kuwa kifungu hicho kifanyiwe marekebisho kisiwazuie Watanzania kujadili mwafaka wa kitaifa juu ya mstakabali wa taifa lao.

Jaji Warioba pia alionekana kushangazwa na vyama vya siasa na asasi zingine za kiraia kuzuiwa kuelimisha wananchi kwa kufanya kampeni wakati wa upigaji kura ya maoni ya 'ndiyo' au 'hapana' ili kupitisha sheria ya kuanza kutumika katiba mpya, badala yake shughuli hiyo kusimamiwa na tume ya uchaguzi.

Huku akionya Watanzania kuacha ushabiki katika suala la utungaji wa katiba mpya, Jaji Warioba alisema "sasa mimi najiuliza hii tume itakwenda kufanya kampeni juu ya nini, tume iliyohusika katika mchakato wa katiba kweli inaweza kwenda kuwaambia wananchi wapige kura ya ndiyo au hapana. Waachwe watu wafanye kampeni.

"Kama ni vyama vya siasa au watu waacheni wapige kampeni. Lakini natoa angalizo hili si jambo la ushabiki, huu ni mwafaka wa kitaifa. Tusifanye ushabiki, tutafute mantiki," alisema Jaji Warioba, huku akishangiliwa baada ya mwanzoni kuonja zomea zomea, alipoonekana akisifia baadhi ya vipengele katika muswada huo.

"Pia hapa imeelezwa kuwa baada ya bunge la katiba kupitisha rasmu ya katiba, rais atatia saini, sasa kwa kawaida bunge la katiba likishapitisha kitu hakuna tena assent ya rais. Halafu baada ya rais kutia saini mnataka iende kwa wananchi, sasa sheria inapitishwa halafu inakwenda kwa wananchi, je, wakiikataa itakuwaje."

Jaji Warioba alishauri kuchaguliwa kwa njia mojawapo kati ya bunge la katiba au mkutano jumuiko la kitaifa la katiba, huku pia akitoa angalizo juu ya kura ya maoni kuangalia namna ya kuratibu kura za pande mbili za muungano.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambaye alikuwa mchangiaji wa tatu baada ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na Wanataaluma wa Chuo Kikuu Mzumbe, alisema kuwa ni vyema serikali ikaweka wazi juu ya jina la muswada huo, kwani wananchi wanazungumzia utungwaji wa katiba mpya, si marekebisho ya katiba.

Alisema kuwa ni vyema muswada huo ukabeba dhana sahihi kwa ajili ya mabadiliko ya katiba kwani kinyume chake, kitasababisha hata vifungu vya muswada huo kuwa vibovu, huku akitoa angalizo kuwa si sahihi muswada huo kutoa mamlaka makubwa kwa rais, kwani mamlaka ya kuongoza nchi yanapaswa kutoka kwa wananchi.

Alisema kuwa katiba inazaa taasisi zote, ikiwemo ya urais, hivyo Watanzania wanapaswa kuzungumzia masuala yote, bila kuzuiwa, huku akitaka baadhi ya maneno yaliyomo katika muswada huo yafafanuliwe vizuri ili yasitumike kuminya haki za Watanzania katika tafsiri zake.

"Hiki kifungu cha 9(2) kinachosema mambo yasiyogusika, si kwamba Watanzania hawataki muungano, anayesema kuwa hataki muungano huyo ana matatizo yake, lakini Watanzania wanachotaka ni kuzungumzia aina gani ya muungano, wanahoji madaraka ya Tanganyika yako wapi, maana kumekuwa hakuna clarity katika suala la muungano.

"Si kwamba hawataki rais awepo, wanahitaji kujadili urais wa namna gani, maana hapa kuna suala limechakachuliwa, tumechukua mfumo wa Marekani na Uingereza, sasa wanataka kujua tuko upande upi, tusianze kuweka limit (vizuizi) katika kujadili katiba, maana hapa tunatengeneza nchi yetu si nchi ya mtu mmoja.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, alisema kuwa kama mchakato wa uandikaji wa katiba mpya utaanza vibaya, nchi inaweza kuingia katika matatizo makubwa ya kisiasa, hivyo ni vyema mchakato huo ukapata uhalali wa kisiasa kutoka kwa wananchi, badala ya mamlaka makubwa kuachiwa rais.

Akisisitiza suala la matumizi ya lugha ya Kiswahili na jina la muswada huo kubadilishwa, kutoka kusomeka marekebisho ya katiba, bali uandikwe Muswada wa Utungaji wa Katiba mpya, Prof. Lipumba alisema kuwa wananchi hawana imani na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kusimamia mchakato wa kura ya maoni kwani inaweza kuzichakachua.

"Karibu kila kitu kinatokana na rais hapa, mapendekezo yatokane na wananchi, si rais. Tukianza hivyo itakuwa mwanzo mbovu, ili mchakato huu upate uhalali ni bora utokane na wananchi, msimpatie rais mzigo mkubwa kiasi kwamba mambo yakiharibika aonekane yeye ndiyo kaharibu. Katika kura ya maoni hatuna imani kabisa na tume ya uchaguzi.

"Hatuna imani nayo kabisa maana tume hii mwaka jana katika uchaguzi mkuu ilituchakachua kweli kweli, sasa hawa hawa tena wanapewa kazi ya kusimamia kura za maoni, matokeo yatakuwa tayari yanajulikana, tunataka tume inayoaminiwa na watu. Kuwepo na nia thabiti, maana tukianza vibaya tutaingia katika matatizo makubwa ya kisiasa," alisema Prof. Lipumba.

Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, Bw. James Mbatia alisema kuwa muswada huo haujatungwa kwa nia njema, akitaka umma upatiwe nafasi kubwa ya kuamua namna ya kujitawala, si mamlaka hayo kuwekwa mikononi mwa rais kwa kuamua mchakato mzima utakavyokwenda, huku naye akisisitiza suala la jina la muswada huo libadilishwe, usomeke kuwa ni 'katiba mpya'.

"Hatutaki damu imwagike lakini serikali inaweza kuchochea vurugu, hatutaki katiba ya CCM, tunataka katiba ya wananchi, rais hapa anapewa madaraka yote. Pia lazima tuwe makini hapa maana tuna complex state maana tuna Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tofauti na nchi kama Kenya ambao wana simple state, maana ni Jamhuri ya Kenya," alisema Bw. Mbatia.

Zamu hiyo ya wawakilishi wa makundi mbalimbali iliendelea mpaka kufikia kwa Chama cha APP- Maendeleo na Chama cha Walemavu nchini, ambaye alitaka kundi hilo kuzingatiwa na kupewa umuhimu mkubwa unaostahili katika mchakato mzima mpaka kupatikana kwa katiba mpya, akitoa angalizo kuwa kwa sasa muswada umewaweka pembeni na kuwasahau.

Ilipofika zamu ya mwakilishi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Naibu Mkuu wa Kitengo cha Propaganda, Bw. Tambwe Hizza, ambaye mara muda mfupi baada ya kuwasilisha hoja yake, yalianza kusikika makofi yasiyokoma yakipigwa na baadhi ya wahudhuriaji, ikiwa ni dalili ya kuzomea, huku yeye akipuuza kwa kusema "Mwenyekiti hayo tulishayazoea, yaache."

Katika hoja yake ambayo ilikuwa ikikatishwa mara kwa mara kutokana na zomea zomea hiyo, hatimaye ilizua mtafaruku wa kambi mbili zinazopingana na kusababisha mkutano huo kuahirishwa kwa muda, Bw. Hizza alisema kuwa iwapo mchakato wa katiba mpya hautafuata sheria zilizopo na katiba iliyopo, nchi haitapata katiba mpya, badala yake itaambulia vurugu.

Alisema kuwa si sahihi wananchi kutaka kumnyang'anya rais mamlaka yake katika mkutano kama huo wa utoaji maoni ya muswada, kwani mamlaka aliyonayo yamewekwa kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi, akisema kuwa ibara ya 98 ya katiba ya sasa, inaruhusu katiba kubadilishwa au kufutwa kabisa.

Zomea zomea, zilizoanza kwa makofi yasiyo na mwisho, hatimaye kupigwa miguu chini na kibwagizo cha 'atokeeee atoke, aondokeeee aondoke, ilizidi na kumlazimisha Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, Bi. Pindi Chana kuahirisha mkutano kwa ajili ya chakula, kisha uanze baadaye.

Hata hivyo aliporudi baada ya kusimama kwa mkutano huo takribani saa mbili, Bi. Chana alisema haiwezekani kuendelea, bali mkutano huo wa kuchukua maoni utaendelea leo kwa watoaji kuwasilisha kwa maandishi na wengine wataruhusiwa kuzungumza.

Mbunge wa Singida Mashariki, Bw. Tundu Lissu alisema kuwa zomea zomea hiyo ni suala la aibu, kwani kila mtu anayo haki ya kutoa maoni yake na wengine wanapaswa kusikiliza hata kama hawataki au hawaungi mkono maoni hayo. Aliongeza kuwa hali hiyo ikiendelea muswada utapitishwa bungeni bila wananchi kutumia fursa hiyo ya kuujadili na kuuboresha.

CCT yaonya rais kupora madaraka ya wananchi

Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) imeonya serikali kuwa kitendo cha rais kuteua tume kukusanya maoni ya katiba mpya ni kuwapokonya wananchi haki zao kwamba lengo la kazi hiyo haitafikiwa.

Pia imesema serikali isithubutu kuharakisha suala hilo kulenga Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 na kuongeza kuwa iwapo watanzania hawatapata muda wa kutosha kutoa maoni yao kwa uhuru itakuwa haijakidhi matakwa ya watanzania.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kusainiwa na Makamu wa kwanza wa Mwenyekiti wa CCT, Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana, Dkt. Valentino Mokiwa, jumuiya hiyo imesema mwenye mamlaka ya kuteua tume hiyo ni bunge kwa niaba ya wananchi na si rais ambaye ni mwenyekiti wa chama tawala.

"Ipo hatari ya kukasimu mamlaka haya kwa Mheshimiwa Rais ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Tawala kuteua Tume ya kusimamia mchakato huu ikiwemo sekretarieti yake.

"Ni sharti wananchi wenyewe wawezeshwe kutoa maoni yao moja kwa moja au kwa njia ya wawakilishi wa makundi yote ya kijamii, alisema Askofu Mokiwa katika taarifa hiyo na kuongeza.

"Utaratibu huu unamfanya Rais awe wa mwanzo na mwisho (Alpha na Omega) na kuondoa ushiriki wazi wa wananchi katika kusimamia na kuamua mstakabali wa nchi yao. Ni vyema mamlaka haya yakakasimiwa na wawakilishi wa wananchi kupitia bunge na vyama vya siasa," alisema Askofu Mokiwa katika taarifa hiyo.

Alisema Watanzania wanahitaji katiba mpya ili kukidhi matakwa yao ambayo hayajawai kufikiwa na marekebisho yaliyokuwa yakifanyika katika katiba ya sasa, chini ya mfumo huo bila kuleta faida.

Katika barua hiyo iliyoelekezwa kwa Waziri wa Katiba na Sheria Bi. Celina Kombani yeye kichwa cha habari, tahadhari kutoka CCT juu ya muswada wa mapendekezo ya kutungwa kwa sheria ya mabadiliko ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2011, CCT iliikumbusha serikali kuwa wananchi ndio wenye maamuzi ya mwisho juu ya nchi yao na si rais.

"Tunakuomba utumie weledi na hekima yako kuhakikisha kwamba rai yetu inapewa nafasi na umuhimu katika jambo hili, ili kuleta umoja, usawa, amani na utangamano pamoja na maendeleo ya nchi yetu yatakayotokana na katiba iliyoandaliwa na wananchi wenyewe," alisema.

CCT ilisema katiba ijayo inatarajiwa kukidhi haja ya kizazi cha leo, kesho na kijacho na si kama marekebisho yaliyopita ambayo hayakukidhi haja ya Watanzania.

"Muswada unafifisha na kudhoofisha ari na matarajio yao, mabadiliko yamekuwa yakifanyika kila mara lakini bado lengo la kupata katiba mpya halijakidhiwa," alisema Askofu Dkt. Mokiwa.



6 Maoni:

blank.gif

Anonymous said... Tafadhali kumbukeni kuwa wananchi ndio wanamuweka hata rais madarakani, kwa hiyo ndio wenye nchi, budi washirikishwe kikamilifu katika suala hili. Hayo mambo matukufu yatabakiza utukufu wake ikiwa wananchi wanaridhia iwe hivyo na si kulazimishwa iwe hivyo. Kumbukeni leo ni CCM kesho anaweza kuwa mwingine, hivyo katiba isitungwe kwa kukidhi haja ya chama au kundi fulani kwani ni ya wote. Hakuna ajuaye kesho na kesho kutwa. Ikitungwa vibaya itaumiza waliopo na wajao.
April 8, 2011 12:02 AM
blank.gif

Anonymous said... huu ndo mwanzo wa uharibifu wa amani,na serikali ndo inataka kuharibu, wangefanya research ktk nchi zilizowahi kutokuwa na amani. wataona mazingira tuliyonayo kwa sasa yalichangia kiasi kikubwa ktk uvunjifu wa amani.
April 8, 2011 1:21 AM
blank.gif

Anonymous said... Hatuhitaji Marekebisho ya Katibu maana Katiba hii ya Kizazi cha Nyerere Kilichopita. unahitaji KATIBA MPYA. Itakayoendana na mahitaji ya Kizazi hiki. Tafadhali serikali msitutungia katiba kama hadithi za kibibi kizee. Tunahitaji Katiba Mpya. Tambwe acha propaganda za kipuzi laana ya Mungu itakushukia.
April 8, 2011 1:54 AM
blank.gif

Anonymous said... Wapendwa Wana wa Tanzania wenzangu, nina maswali machache tu kuhusu swala la Katiba mpya. Pamoja na kukubali kwangu ya kwamba Katiba mpya ni muhimu kwa sasa ninaogopa ya kwamba mambo yanaweza kwenda bila uhakika. Hapa nina maswali machache kwa wachangiaji wa hoja hii: 1. Je nikwamba Watanzania hawajapewa nafasi ya kutoa mawazo yao hadi sasa? Mbona naona kuna mijadala mbalimbali inayofanyika nchini? Baba Mpendwa Askofu Mokiwa na CCT je ni kweli ya kwamba Rais wa nchi yetu hawakilishi Watanzania wote kwa uteuzi wa Tume hii. Iwapo sisi ndio tuliompa utumishi huu je kuna ubaya gani iwapo yeye atatenda jambo kwa niaba yetu? Nina hakika ya kwamba yeye hutamka kwa niaba ya wote na bila shaka kabla ya kutamka huwa amepata mawazo na mahusia toka kwa watu mbali mbali wakiwemo viongozi. Ombi langu ni hili; Rais wetu asaidiwe na wote, ili atoapo jambo lisiwe lake; na kama atafanya kinyume chake hivyo basi alaumiwe na kukosolewa.
April 8, 2011 4:37 AM
blank.gif

Anonymous said... Ninacho ona hivi sasai kwamba viongozi wa chama tawala wameshalewa madaraka na wanataka kuwaburuza watu.Wananchi wanatakiwa vilele kutowa maoni yao.kwa sababu wao ndio wako mitaani kila siku na kuona mambo yanavyo kwenda.Itakuwa sio haki kabisa ya kusema ya kuwa raisi ndio atoe kauli ya mwisho ya katiba iwe vipi.Haya ndio mambo yanayotokea leo hii huko Tunisia,Egypt na kwingineko,Kama kweli ccm imedhamiria kuondoa machafuko nchini basi haina budi kusikiliza wananchi wake badala ya kiongozi moja kusimama na kusema hiyo haiwezekani na hayo ni mawazo ya watu kumi.Je watu hao ni akina nani?,Labda angeulizwa alafu afafanue hiyo kauli yake.Hivi kweli tunaviongozi ambao wanawezakukaa chini na kujiuliza kama wanachofanya kiko sawa au hakikosawa?
April 8, 2011 12:43 PM
blank.gif

Digumile Mulungu said... Mtoa maoni wa nne kutoka juu nashukuru kwa maoni yako yakistaarabu sana. Swali ulilomuuliza askofu Mokiwa linaweza kujibiwa na yeyote siyo lazoma Mokiwa mwenyewe. Naomba nikujibu kama ifuatavyo:-
1. Ni kweli kuwa watanzania bado hawajapewa nafasi ya kutoa maoni kuhusu katiba mpya maana ndio sasa muswada wa mchakato wa katiba unatarajiwa kupelekwa bungeni. Muswada huu unahusu ni jinsi gani watu watatoa maoni yao katika tume ya kukusanya maoni ya katiba. Muswada huu una mapungufu mengi kwani unataja kuwa ni marekebisho ya katiba na siyo utungwaji katiba mpya. Pia muswada umeweka limit katika mambo ya msingi ambayo ndio katiba yenyewe yasizungumziwe katika katiba hiyo inayotarajiwa kurekebishwa au kuandikwa upya.
2. Katika suala la katiba rais kamwe hawezi kuwa mwakilishi wa wananchi. Hapa hata bunge ambalo wajumbe wake ni wawakilishi wa wananchi nalo halina nafasi ya kuwatungia wananchi katiba. Hii inatokana na ukweli kuwa katiba ni mkataba wa wananchi jinsi wanavyotaka nchi yao itawaliwe namna gani, anayewatawala afanye nini na siyo rais awatungie watu katiba. Rais, serikali na wabunge na mamlaka ya mihimili mingine yapo kwa mujibu wa katiba iliyotungwa na wananchi. Katiba yetu ya sasa ilitungwa na wakoloni na wananchi sasa baada ya kujitawala miaka 50 na kupata weledi wa kutosha sasa tunataka kujitungia katiba yetu inayoendana na Tanzania ya sasa na si vinginevyo.
3. Kwa kuweka limit baadhi ya mambo kama madaraka ya Rais, Muungano, Masuala ya uchaguzi, na mengineyo kuwa ni matakatifu yasizungumziwe ni ishara tosha kuwa serikali haina nia njema ya kutunga katiba mpya bali inatekeleza wajibu tu. Hii ni wazi kuwa maneno ya akina Kombani na Werema sasa yamejidhihirisha kuwa hawataki katiba mpya. Hii inaweza kusababisha amani kunjika na tukiwaruhusu wapumbavu kama akina Tambwe basi tutaweka rehani nchi yetu na amani itatoweka na hapa wa kulaumu atakuwa ni serikali.
4. Kwa maoni yangu ni kwa Rais kwa kuwa ni mwenyekiti wa Chama cha sisa na kwa kuzingatia kuwa alichaguliwa kwa kura nyingi lakini wapo wananchi zaidi ya milioni 2 ambao walimktaa, haistahili apewe madaraka ya kuunda tume ya maoni ya mchakato wa katiba kwa vile ataendesha mambo hayo kwa kuzingatia ushauri na kanuni za chama chake hivyo hatawatendea haki wadau wengine wa vyama vya siasa. Pili tume ambayo ataunda kwa kushirikiana na Rais wa Zanzibar ni lazima ataipa hadidu za rejea kuwa wafanye yale ambayo atataka kama ilivyo tume ya uchaguzi ya sasa ambayo huagizwa ni lazima Rais wa CCM ashinde. Tatu, mambo yaliyokatazwa yasizungumziwe ndio hasa katiba yenyewe. Kwa mfano hamtaki watu wazungumzie muungano wala madara ya Rais kuna nini hapa? Wananchi tunataka katiba ambayo tutampa Rais majukumu ya kufanya akiwa ikulu, siyo kwenda kutalii ughaibuni wala kuteua vidosho na mamis kuwa wakuu wa wilaya au mikoa. Rais apangiwe ni namna gani atawapata watumishi wake amam wa serikali. si katiba ya sasa inayomruhusu Rais kuteua hata shemeji zake kushika madara makubwa ya kitaalamu wakati hawana uwezi wala taluma. Tunataka katiba itakayomuwajibisha Rais akizembea kwa mambo ya msingi kama ya Richmond, dowans, n.k
5. Watanzania tuache ushabiki wa akina Werema na Kombani na wengine wanaofanana na hao maana ni wapumbavu hawa waliolewa madaraka haya ya muda. Rais kama ameamua kweli kwa moyo mkunjufu kuandika katiba mpya basi aruhusu mjadala wa uhuru kusiwe na vikwazo kama wanavyoleta sasa.
Mwisho nawaonya kuwa CCM na serikali wsipoangalia watangamiza nchi hii kwa suala hili la katiba. Naona walidandia hoja za wapinzani za kuandika katiba mpya bila kufanyia utafiti wa kutosha. Katiaka hili la katiba jikazeni kama wanaume ili watanzania waandike katiba yao hata kama haitawapendelea nyie mtatafuta mbinu ingine ya kujiimarisha zaidi bila ya kutegemea katiba hii ya sasa ambayo inawanufaisha kwa asilimia mia. Huu ni wakati wa CCM kutahiriwa bila ganzi acheni kulia maana nje ya boma la kutahiria kuna wanawake watawasikia mkilia kitu ambacho kwa mwanaume ni aibu. Nia aibu kubwa chama dola kama hiki kuchakachua hata muswada wa katiba.
April 8, 2011 1:50 PM
 
UDOM watawanywa kwa mabomu bungeni


Na Edmund Mihale, Dodoma

ASKARI wa Kikosi cha Kuzia Fujo (FFU) jana, walilazimika kutumia mabomu ya machozi na risasi kuwatawanya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma na
wanaharakati wengine baada ya kufunga barabara kuu ya kutoka Morogoro ili kulishinikiza waruhusiwe kuingia kwenye eneo la kushiriki mjadala Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba.

Wakizungumza katika lango kuu la Ofisi za Bunge majini Dodoma jana kwa nyakati tofauti wanafunzi hao walisema kuwa ni jambo la kushangaza kwa ofisi hiyo kuwaalika wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya City na kukiacha chuo hicho bila ya kuwa na uwakilishi.

"Muswada huo umeandikwa kwa lugha ya Kiingereza wamealika wanafunzi wa Shule ya Sekondari City ambao hawajui Kiingereza shule yenye matokeo mabovu kila mwaka, huku ni kuwachezea wananchi, alisema mmoja wa wanafunzi hao.

Mmoja ya wanafunzi hao ambaye alijitambulisha kwa jina la moja la Denis, alisema iwapo wabunge watapitisha muswada huo wako radhi kuingia mtaani kupinga tume hiyo kwa kuwa haiwezekani kufanya majadiliano katika mikoa mitatu ya Zanzibar, Dar es Salaam na Dodoma, ilihali kuna mikoa mingi inatakiwa kuwasilisha maoni yake.

"Hawa wabunge wakipitisha mambo hayo tutashtaki kwa wananchi na kisha tunahamia mtaani tunafanya kama ilivyo Tunisia, Libya na Misri lazima kieleweke," alisema mmoja wa wanafunzi hao kwa kipaza sauti.Alisema kuwa muswada uliowasilishwa bungeni na serikali chini ya hati ya dharura haukidhi mahitaji ya Watanzania.

"Watanzania wa leo sio wa juzi au jana, hatutaki kijitabu chenye maandishi kinachoitwa katiba bali makubaliano ya utaratibu wa jinsi ya kuendesha maisha yetu katika nchi hii kwa kujadiliana kila kitu jambo linalohusu kwa manufaa ya wote, kwa haki na usawa ulioandikwa katika kitabu kitakachokuwa na kumbukumbu ya makubaliano.

"Kwa matiki hii rasmu ya serikali inaonesha kuzidisha matatizo badala ya kuyapunguza kwa kuwa inaonesha kuwepo kwa kikundi cha watu wachache wanaotugilibu na kujitengenezea katiba ya kujilinda wao na mambo yao kwa manufaa yao. Tena wanaonesha kuwa wananufaika kwa sisi kupata shida, kwa kuwa ukisoma utagundua katika yale matatizo yetu makubwa hawataki tujadili kwa pamoja na kuyatatua," alisema.

Hata hivyo, hotuba hizo zilikatishwa baada ya kujitokeza kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. James Msekela ambaye alijikuta katika wakati mgumu kwa kuzomewa na wanafunzi hao.

"Mtoe huyo mtoe huyo mtoe huyo alitupiga mabomu, hatumtaki anaongea pumba, pumba, pumbaaaa pumbaaaa," walisikika wanafunzi hao wakisema kwa jaziba.

Dkt. Msekela alishindwa kutuliza fujo hizo hadi alipojitokeza Mbunge wa Arusha mjini, Bw. Godbless Lema ambaye alipokewa kwa shangwe na vigelegele, 'jembee, jembee, jembee zilisikika sauti za wanafunzi hao.

Baada ya kuwashusha munkari, Bw. Lema aliwataka wanafunzi hao kuacha jazba, lakini aliulaumu utaratibu uliowekwa na bunge kwa kuwa haukuwatendea haki wananchi wanaoishi katika Mkoa wa Dodoma na migine kwa kutumia ukumbi mdogo wakati wakijua kuwa wananchi wana shauku ya kutoa maoni yao kwenye muswada huo.

"Nimewaita wanafunzi wa chuo kikuu ili kuja kujadili muswada huu kwa kuwa umeandikwa kwa lugha ya Kiingereza, hivi muuza mchicha, bagia anaweza kujadili muswada huu? Kuna watu wangapi wanapenda kuja hapa kujadili mustakabali nchi yao, hamuwezi kuita watu 300 ambao ni sawa na idadi ya wabunge wote," alisema Bw. Bw. Lema.

Alisema kuwa bora ofisi hiyo ikatafuta sehemu nyingine kubwa itakayoshirikisha watu wengi kujadili muswaada huo na kutoa maoni yao kwa uhuru kuliko kufanya katika chumba kidogo na kuwanyima haki watu wengine.

Mazungumzo hayo yalikatishwa na vurugu za wanafunzi hao waliotaka majadiliano hao yafanyike katika Uwanja wa Jamhuri, jambo lilopingwa na Dkt. Msekela ambaye alitaka kufanyika katika ukumbi wa Chimwaga.

Wanafunzi hao walipiga kelele kushinikiza kufanyika katika uwanja huo huku wakirusha mawe na kumzomea ndipo, Dkt. Msekela alipoamru Jeshi la Polisi kuwatanya, jambo lilozua kizazaaa katika mitaa mbalimbali ya mji wa Dodoma.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya vurugu hizo, Dkt. Msekela alisema kuwa ameamua kufanya hivyo kutokana na kushindwa kuelewana na wanafunzi hao, huku akimrushia lawama, Bw. Lema kuwa ndiye chanzo cha vurugu hizo.

"Ninatoa onyo kwa wanasiasa wanaojihusisha na siasa katika Chuo Kikuu cha Dodoma nimeambiwa kuwa jana kuna mwanasiasa mmoja alikwenda kule kuwahamasisha wanafunzi hawa," alisema Dkt Msekela.

Baada ya kusikia hivyo, Bw. Lema, alisema kuwa hakuna haja kuuma maneno, bali yeye ndiye aliyekwenda katika chuo hicho na kuzungumza na wanachama chama chake na atarudi tena Jumamosi.

"Mie ndiyo nilikwenda huko na kuzungumza na wanachama wangu na Jumamosi nitakwenda tena, njoo tutakutana tusitishane, si muda wa kutishana. Nimekwenda nikafanya siasa nje ya maeneo ya chuo sasa tatizo langu nini," alisema Bw. Lema. Baada ya kauli hiyo, Dkt. Msekela alionekana kunywea.



9 Maoni:

blank.gif

Anonymous said... Ya.mimi sishangai kuona hali hii ya wasomi kuzuiwa kwani watanzania mmesahau ni serikali hii hii iliyowanyima wanachuo haki ya kupiga kura kwa kudai anayetaka apande gari aende alipojiandikishia...mi nadhani mfumo wa wanasiasa wa kiafrika kuhofia wasomi ndio huo unatufikisha hapo.Udom tuakilisheni nyie mlio karibu na mjengoni...Mungu wabariki wote wenye mawazo mema na TZ
April 7, 2011 11:53 PM
blank.gif

Anonymous said... by grace;
kama uchangiaji wa mawzo ya katibani huru na wazi, kwa nini wanavyuo wanazuiwa? kila mmoja anatakiwa kuchangia bila kutumia uwakilishi uliobuniwa kwa makusudi ili kuharibu taswira halisi iliyokusudiwa.
kwa mustakabali huo, wanaozuia wana vyuo wasiingie inaonesha walikuwa na watu maalum waliowaandaa ili kuwakilisha kilichoandaliwa, na kuna habari ambazo wapo wa2 maalum waliochomekwa ili kuwakilisha majumuisho yasiyo na lengo halisi.maandalio hayo ya kundi dogo,baada ya habari kuvuja na kugundulika, ndiyo yamesababisha wanavyuo kutotulia na wao kuhitaji nafasi. hivyo ndivyo ilivyo, tusidanganyane.
April 8, 2011 1:02 AM
blank.gif

Anonymous said... Kwa kweli nchi hii viongozi wa chama tawala wanataka kuleta vurugu.Kwani wanahofu nini uundwaji wa katiba mpya. Ninachofahamu ni kuwa katiba ya nchi ndiyo sheria mama ya kila kitu.Hawa watu wasitengeneze hati ya dharula kutaka kutufisha ambako siko wabunge wa chama tawala naomba mjadiliane kwa kuangalia maslahi ya wananchi waliowatuma kuwakilsha katika bunge mjue mkifanya haya mambo kwa ushabiki wa chama mkaye mkijua 2015 hata kwa katiba hiyo mbovu hamtapita labda mchakachue sana.kitu ambacho kitakuwa ni kigumu watu watalinda masanduku ya kura.Chondechonde wabunge wa chama tawala jadilini huu mswada kwa manaufaa ya watanzania na si vinginevyo.
April 8, 2011 1:36 AM
blank.gif

Anonymous said... Kwa vile kumbi zilizoandaliwa ni ndogo kulingana na jumla ya watu wanaotaka kushiriki na umuhimu wa kazi yenyewe, basi mijadala ifanyike katika maeneo mengi na wawakilishi wachaguliwe kati yao ili kuwakilisha maoni yao. Mchango wa wasomi, wafanyakazi, na idara nyingi ni muhimu, hivyo kuwepo na vituo mabali mbali vya kukusanya maoni na baadye yawekwe pamoja na tume huru. Huwezi kuweka mijadala ya namna hii katika sehemu wazi na kwenye watu wengi kwani muda utatuminka mwingi na mawazo yanapishana. Kwa mfano, Walimu wa vyou vikuu wangejipanga pamoja na wanafunzi wao wajadili mswada na wachague wawakilishi wa maoni katika tume huru. Sioni sababu ya watu kuvamia ukumbi. Wabunge tumieni busara kupanga namna ya kuongoza mijadala. Mbona ktk kujadili mishahara yenu hatusikii fujo?
April 8, 2011 5:58 AM
blank.gif

Anonymous said... wasomi gani uchwara chuo hakina hata hadhi za kimataifa?vitanda dabodeka utafikiri sekondari du mue na aibu tatizo vyuo vya kuongea vimezidi hapo bongo mbona muhimbili hao wanasiasa hawaendi?nani ataacha kusoma akamsikilize mwana siasa?hatuwasikii hata maprofesa wa kweli ambao wote wapo muhimbili kujihusisha na vyama?lkn hao maprofesa wa kozi za kuongea ndio wenyewe kila kitu wanajua wenyewe nchi hiyo umasikini utaisha kweli? ama kweli inasikitisha maana kwa sisi tulio ughaibuni tunaona maprofesa wanavyo fanya kazi zao za kitaaluma sio siasa wana tunga vitabu na ndio vinavyotumika mashuleni lkn sio kwetu vitabu hakuna mpaka tupewe msaada maprofesa tunao wanafanya kazi gani?
April 8, 2011 9:32 AM
blank.gif

Anonymous said... Viongozi wa ccm wote ni mbumbumbu. Yaani mnashindwa kusoma alama za nyakati.. nawasikitikiea sana. Mnatafuta mchawi wa vurugu za kujadili katiba na mnadhani kuwa mchawi ni chadema au mbunge G. lema. Huu uhuru na haki wa kila mtanzania kutoa maoni yake umetoka wapi? Mswaada wenyewe umeandikwa kwa kiingereza kwa makusudi ili kuwaondoa kwenye majadiliano asilimia kubwa ya Watanzania ambao mnajua hawajui klugha hiyo. majadiliana yanafanyika katika kumbi ambazo hazimudu idadi kubwa ya watu. Huu uhuru wa watanzania wengi kujadili mswada huu utafanyika vichakani au kwenye vilabu vya pombe ikiwa hakuna mazingira mazuri ya kuchangia mswada huu. Tunaomba usituletee kichefuchefu.
gazeti lako siku zote linabezi kutetea CCM tu ambao sasa wanataka kuchakachua mswada wa katiba mpya. Na ndiyo maana akina Prince Bagenda, Tambwe Hizza .. na mzee warioba walizomewa hovyo! Someni alama za nyakati.. watanzania wamechoka na uchakachuaji wenu! Mnakwenda kwenye mijadala wa mswada wa hamsemila maana ila mnamjadili rais ambaye ameonyesha wazi nia ya kuchakachua kupatikana kwa katiba...bohhh! Msizomewe!!
April 8, 2011 12:05 PM
blank.gif

Anonymous said... wewe uliyechangia maoni muda 9.32 ndiye uchwara! nchi ambayo hata baada ya miaka 50 ya uhuru haina umeme na maji unataka iwe na vyuo vyenye vitanda vya vioo! Nchi itaendeleakuw maskini kam wasomi hawatajihusisha na siasa.Na si kweli vitabu havitungwi, tatizo hata vile vichache vianvyotungwa havipati sapoti ya serikali.DAWA YA MATATIZO YETU SI KUWAACHIA WATU MBUMBUMBU WAENDELEE KUTUONGOZA BALI NI KILA MMOJA (HASA WASOMI)N KUJIHUSISHA NA SIASA KWANI HATA DAKTARI, PROFESA WA MUHIMBILI UFANISI WAKE UNAATHIRIWA NA SERA ZA WANASIASA
April 8, 2011 1:04 PM
blank.gif

Anonymous said... Mswada huu utakuwa na maaana kama watu wote watachangia kwa naman ambalimbali. Vitolewe vipeperushi mbalimbali vya kudondoa vipengere kimojakimoja visambazwe, machapisho pia kwenye magazeti juu ya mswada huo yawekwe, watu wasome na watoe mawazo yao, vipindi vya redio na television virushwe kueleza mambo muhimu kwenye mswada ili kila mtanzania aelewe. Zaidi uwekwe kwa lugha ya taifa, mbona kampeni na mabango ya uchaguzi mkuu yaliandikwa kiswahili? hili la mswada liweje kiingereza ambapo wengi hawajui?
April 8, 2011 6:34 PM
blank.gif

Anonymous said... CCM na serekali yake msiwafanye watanzania wajinga kuwaendesha mtakavyo. Muda umefika mkubali utawala wazi na haki vinatakiwa si kudanganya watu. Mswada huu ufike kwa wote hadi vijijini, kama mlivyoweza kufikisha kampeni za uchaguzi mkuu. Kufanya manvyofanya mnachochoa vurugu na kuhatarisha amani. Sasa siyo CHADEMA tena wanaochochea vurugu ni ccm na serekali yake. Mswada huu usiwe wa kundi dogo la watu hiyo siyo Demokrasia.Tafadhari wapeni watanzania haki yao ya kutoa maoni na kunda katiba mpya. Msifanye siri maana hata ile katiba ya zamani watu wengi hawaijui maana haipatikani kwa urahisi. Hizi ni mbinu za kutawala maana mtu kama hajui katiba ambayo ndo sheria mama atadai vipi haki yake? Watanzania wamekuwa wanaburuzwa miaka mingi na hawajui wadai haki vipi kwa vile hata katiba haiwaijui tokana na kuwa ni kitu cha wachache. Utaratibu au mfumo huu usiendelezwe katika msikabali mzima wa mswada. Mambo yawekwe wazi na huru na watu wafaffanuliwe nchi nzima, siyo ilivyowekwa sasa hivi kujadiliwa kumbi za Dom na Dar ni kuwakosea haki watanzania. Kama Kikwete ulivyotumia lugha ya kumuonya Magufuli asitumie "ubabe", basi ccm na serekali msitumie ubabe kuwalazimisha watanzania maamuzi ya wachache kujadili mswada. Wapeni watanzania fursa kuchangia mswada.
April 8, 2011 6:54 PM
 
Spika akemea wanaogeuza Muswada mtaji

Imeandikwa na Na Gloria Tesha, Dodoma; Tarehe: 8th April 2011 @ 23:59 Imesomwa na watu: 19; Jumla ya maoni: 0








SIKU moja baada ya Polisi kutumia mabomu na risasi za moto kutawanya wanafunzi nje ya ukumbi wa Bunge, Spika Anne Makinda, amewacharukia wabunge wanaotumia Muswada wa Mabadiliko ya Katiba kama mtaji wa kisiasa.

Amekemea wanasiasa wanaotumia fursa hiyo kupotosha wananchi hasa wanafunzi, kuacha mara moja tabia hiyo, kwa kuwa inahatarisha amani na usalama wa nchi. Aidha, amewaonya wanafunzi na wananchi wanaozomea watoa maoni nao kuacha kufanya hivyo katika mazingira ya Bunge, kwa kuwa kanuni za taasisi hiyo haziruhusu jambo hilo.

Hata hivyo, Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, alimtaka Spika kuwaonya kwanza wabunge wa CCM kwa kile alichodai kuwa huzomea wapinzani bungeni. Spika alionya Ijuma bungeni, mara baada ya kipindi cha maswali na majibu katika taarifa yake kwa Bunge, kuhusu vurugu zilizotokea Dar es Salaam na Dodoma Alhamisi wakati wa kukusanya maoni ya wananchi kuhusu Muswada huo.

Kwa masikitiko, Spika alisema matukio hayo ni ya kulaaniwa kwa kuwa inasemekana wapo baadhi ya wanasiasa wanautumia vibaya Muswada huo kwa manufaa binafsi.

"Kama kweli kitendo hicho cha wanasiasa kutumia Muswada kama mtaji kinafanyika, hakileti picha nzuri na hakifai na kinapaswa kukemewa na kuachwa mara moja, kwani kinahatarisha amani na usalama wa nchi yetu," aling'aka Spika.

Alisema madai ya wanafunzi waliokuwa nje ya Bunge mjini hapa, kuwa Kamati ya Bunge ilikuwa na njama kuchagua watu maalumu kutoa maoni si ya kweli, kwa kuwa baadhi ya wananchi na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) waliokubali kupekuliwa langoni na kuingia ukumbini, walitoa maoni yao kwa uhuru.

Alisema utaratibu wa kupokea maoni ya wananchi baada ya Muswada kusomwa bungeni kwa mara ya kwanza, kabla ya kusomwa mara ya pili ni nia njema ya kushirikisha umma katika mchakato na kuonya kuwa upokeaji maoni unaoendelea si mdahalo, hivyo busara, kanuni na sheria zifuatwe.

Spika akinukuu Ibara ya 18 ya Katiba inayompa uhuru mwananchi kutoa maoni, alisema uhuru huo ni lazima uheshimu na kuzingatia haki na madaraka ya Bunge kama ilivyofafanuliwa katika Ibara ya 100 (1) ya Katiba, Kanuni ya Bunge na Sheria ya Kinga, Haki na Madaraka ya Bunge, Sura ya 296 ya Sheria za Tanzania, ambazo zimeweka utaratibu maalumu wa kuendesha mikutano ya Bunge na kamati zake.

"Kutokana na umuhimu huo, kila mtu anapaswa kuheshimu mawazo ya mwenzake, kuzomea hakuundi Katiba bali kunabomoa, Watanzania tumekuzwa kwa kushirikiana, kusikilizana, nimeweka kamati katika makundi hayo kwa makusudi, tena nimewajaza wanasheria humo, ili hata wakilala wapi kwa siku ngapi ni haki yao, mradi mambo yaende, hivyo wabunge na wananchi, tufuate utaratibu," alisema Spika na kushangiliwa.

Akifafanua mchakato wa suala hilo, alisema, "baada ya Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala Bora kukutana Dodoma Aprili 5, iliweka utaratibu wa kukusanya maoni ya wadau kutokana na uzito wa Muswada huo na iliamua kuwashirikisha wadau kwa mujibu wa Kanuni za Bunge, Kanuni ya 114 (9) na 84 (5) na kutoa taarifa kupitia vyombo vya habari na barua," alisema Spika na kuongeza:

"Ili kupata michango mingi, Kamati ilijigawa katika kamati ndogo tatu kwenda Zanzibar, Dar es Salaam na Dodoma, hapa wananchi wengi walijitokeza wakiwamo wanafunzi wa UDOM, Chuo cha Mipango, St John na Chuo cha Mkwawa Iringa na idadi ilikadiriwa kufika zaidi ya 1,000 wakati uwezo wa ukumbi wa Pius Msekwa ni watu 500."

Katika taarifa hiyo aliyokuwa akiisoma huku akishangiliwa na Wabunge, Spika alisema jitihada za kuwataka wananchi hao hasa wanafunzi kuingia kwa awamu baada ya kuonekana ukumbi ni mdogo ziligonga mwamba baada ya wao kushinikiza kuwa wanataka waingie wote tena bila kukaguliwa langoni, kinyume cha utaratibu wa kuingia eneo la Bunge.

Alisema haikuwa sawa kwa wanafunzi kituo cha Dodoma waliokuwa na mabango, wakipiga kelele na kutoa lugha chafu kutaka mkutano ndani usitishwe ili waende uwanja wa Jamhuri kutoa maoni na kukataa ombi la Kamati na Bunge la kwenda Chimwaga jioni ya juzi na kisha kuanza kurusha mawe bungeni, hali iliyosababisha Polisi kuwatawanya kwa mabomu na risasi.
Kwa mujibu wa Spika mchakato katika kituo cha Zanzibar ulianza jana na katika vituo vyote utakamilika Jumapili.

Mbowe akizungumza na waandishi baada ya Spika kutoa taarifa hiyo na kuahirisha Bunge hadi Jumatatu, alisema haungi mkono fujo zilizofanywa na wanafunzi na pia anaulaumu uongozi wa Bunge kuandaa ukumbi mdogo wakati walialika wananchi bila idadi.

"Siungi mkono vurugu na kweli walikosea wale vijana jana (juzi) lakini si wao wa kulaumiwa, Bunge ndilo la kulaumiwa, walialika watu wote bila idadi na wanafunzi ni wananchi, Spika hakupaswa kutoa lawama yoyote kwa wanasiasa, ni kweli, sisi Chadema tulienda UDOM na tulizunguka vyuo vyote nchini, suala la Katiba si la wachache ni la umma wote," alisema Mbowe.

Mbowe alimtaka Spika aulize walichokwenda kufanya Chadema UDOM kabla ya kulaumu huku akisisitiza kuwa ni haki ya kikatiba kufanya walichokifanya na hasa ikizingatiwa kuwa, matangazo ya Bunge yalihamasisha watu waje na kinyume chake alimtaka Spika aeleze idadi ikiendelea katika siku zijazo ni nini cha kufanya badala ya kulaumu wanasiasa.

Juzi baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk James Nsekela kulaani kitendo hicho na kupiga marufuku siasa ndani ya UDOM, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema aliibuka na kueleza kuwa yeye ndiye aliyekwenda UDOM kuhamasisha wanafunzi kuja kutoa maoni na si kufanya fujo na alijigamba pia kuwa ataendelea kufanya hivyo nje ya vyuo na anayetaka amkamate, kwani anazijua sheria.
 
Chadema kuandamana nchi nzima

Imeandikwa na Basil Msongo, Dodoma; Tarehe: 8th April 2011 @ 23:58 Imesomwa na watu: 48; Jumla ya maoni: 0








VIONGOZI wote wakuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wakiwemo wabunge, Aprili 16 wataungana na wafuasi wa chama hicho kuandamana nchi nzima kukusanya maoni ya wananchi kuhusu namna bora ya kuendelea na mchakato wa mabadiliko ya Katiba ya Tanzania.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, amewaeleza waandishi wa habari nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma, kuwa, wafuasi wa chama hicho wataandamana katika makao makuu ya mikoa kama Serikali itaendelea kuharakisha mchakato wa mabadiliko ya Katiba.

"Tuna haraka gani jamani?"amehoji Mbowe na kubainisha kwamba, wabunge wote wa Chadema watatawanyika nchi nzima kufanikisha maandamano hayo.

Amesema, Chadema wanakwenda kwa wananchi ili waseme wanataka muundo gani wa sheria ya mabadiliko hayo ya Katiba ya nchi.

"Sio mikutano ya Chadema, sisi tunajitolea kupata maoni ya wananchi" Amesema Mbowe baada ya kipindi cha maswali na majibu na akaongeza kuwa siku hiyo pia kutakuwa na mikutano ya hadhara katika mikoa yote Tanzania.

Kwa mujibu wa Mbowe, Chadema watatoa taarifa polisi kwa kuwa hawahitaji kuomba kibali cha kuandamana na akasema, "Na tutaiomba Serikali itulinde"
Amesema, Serikali ikiacha kuharakisha mchakato huo, Chadema hawataandamana Aprili 16, ila wanaweza kufanya hivyo kuipongeza.

Amesema, wamekuwa wakidai mabadiliko ya Katiba ya nchi kwa takribani miaka 20, hivyo kuwezi kuibadilisha kwa wiki moja.

Kiongozi huyo wa Kambi ya Upinzani bungeni, amesema , kati ya sasa hadi Bunge la Juni kuwe na utaratibu wa kupata mawazo ya wananchi, hivyo hakuna umuhimu wa kuharakisha mchakato huo wa mabadiliko ya Katiba.

Mbowe amesema, Serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiendelea kushinikiza mchakato uendelea kama ilivyo sasa, na kuupitisha muswada kwa namna ulivyo, Chadema watafanya kazi za siasa nje ya Bunge.

"Hii ni mood ya taifa mzee lazima uelewe" amesema Mbowe na kuitaka CCM isome alama za nyakati na akadai kuwa, nchi ipo kwenye mashaka hivi sasa.
Mbowe amesema, Chadema wanawawakilisha wananchi, na wana hoja za msingi, zikikataliwa Bungeni watarudi kwa wananchi ili waamue.

Amesema kuna mapungufu mengi katika muswada wa mabadiliko ya Katiba, lakini Serikali inapaswa kutambua kuwa Katiba si mali yake, si mali ya Rais , si mali ya CCM, ni mali ya Watanzania.

Mbowe amesema, unahitajika muda wa kutosha ili mchakato huo uwe na manufaa kwa kuwa Serikali ina mawazo yake, vyama vya siasa vina mapendekezo yao, na wananchi wana mtazamo wao kuhusu muundo mzuri wa Katiba yao.

Kwa mujibu wa Mbowe, Chadema watashiriki katika hatua zote za mchakato wa mabadiliko ya Katiba, lakini pia itaendelea kuwaelemisha wananchi kuhusu haki zao za msingi.

Amesema, Chadema wanadai haki za msingi, Serikali isizuie uhuru wa mawazo, na pia viongozi wajifunze kukosolewa na wawaheshimu wananchi wa vyama vyote.
 
Mazingira haya ndani ya CCM yanathibitisha ya kuwa umuhimu wa kuwa na mgombea binafsi ambaye hata wale waliodhaminiwa na vyama kama wakifukuzwa huko bado waendelee kuwa wabunge kupitia nafasi ya mgombea binafsi.......chama sicho kilichowachagua bali ni raia hivyo kumnyang'anya mbunge kadi ya uanachama kama kigezo cha kumnyang'anya ubunge ni kuchakachua demokrasia na CCM ni magwiji kwenye hilo.......................

Viongozi CCM Mbarali waonywa


Na Esther Macha, Mbarali

SAKATA la Mbunge wa Mbarali (CCM), Bw. Dickison Kilufi kufanyiwa njama za kutaka kunyang'anywa kadi ya uanachama limeingia katika sura mpya baada ya Chama cha

Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mbeya kuwaonya viongozi wa ngazi ya wilaya wasithubutu kufanya hivyo kwa sababu hawana uwezo wala mamlaka ya kufanya hivyo.

Akizunguma na gazeti hili jana, Katibu wa CCM mkoa wa Mbeya, Bi. Verena Shumbusho alisema viongozi wa chama hicho ngazi ya wilaya hawana madaraka kumnyang'anya kadi mbunge, hivyo kama kweli wanafanya njama hizo wanajidanganya.


Mbunge wa jimbo hilo anafanyiwa njama hizo hizo kutokana na kuwa na msimamo tofauti na viongozi wa chama na serikali ya wilaya na mkoa kuhusu mgogoro unaoendelea kufukuta kati ya wananchi wa wilaya ya Mbarali wanaomlalamikia mwekezaji wa shamba la mpunga la Mbarali Estate kuwanyanyasa.


Wakizungumzia hali hiyo, baadhi ya wananchi walisema hatua hiyo ni ya hatari kwa kuwa waliomuweka mbunge huyo madarakani ni wananchi kwa kumchangia fedha ya kuchukulia fomu ili kuwa mwakilishi wao.


Walisema msimamo wa mbunge kufuatilia haki na maslahi ya wananchi wa wilaya hiyo kunamfanya aonekane yupo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), na hali hiyo inatokana na mwekezaji wa shamba la mpunga la Mbarali Estate kuwa na mgogolo na wananchi wa Wilaya hiyo.


"Sisi ndiyo tuliompa ridhaa Bw. Kilufi kuwa mbunge, na maamuzi hayo yanayoshinikizwa na kundi la watu kwa maslahi yao binafsi yataigharimu serikali, kwani na sisi hatutakubali sauti yetu ikazimwa, tumempeleka bungeni akawe mwakilishi wetu," alisema Lusekelo Mwilongo.


Bi. Lucy Msemwa alisema mbunge huyo ni maskini na hali ndiyo inayomfanya awatetee wanyonge, huku wananchi wakiamini kuwa ni msaada wao mkubwa, na hali hiyo baadhi ya watu wanataka kumtumia kwa maslahi yao jambo ambalo mbunge amekuwa akilipinga na wao kumuona hawafai na kufikia hatua ambayo itajenga historia.

 
PHP:
Mbunge wa jimbo hilo anafanyiwa njama hizo hizo  kutokana na kuwa na  msimamo tofauti na viongozi wa chama na serikali ya  wilaya na mkoa  kuhusu mgogoro unaoendelea kufukuta kati ya wananchi wa  wilaya ya  Mbarali wanaomlalamikia mwekezaji wa shamba la mpunga la  Mbarali Estate  kuwanyanyasa. 

Wakizungumzia hali hiyo, baadhi ya wananchi walisema hatua hiyo ni ya   hatari kwa kuwa  waliomuweka mbunge huyo madarakani ni wananchi kwa   kumchangia fedha ya kuchukulia fomu ili kuwa mwakilishi wao.

Do we need another proof?????????????????
 
Saturday Apr 09, 2011
04_11_au07u8.jpg
CHADEMA legislator (Singida East), Mr Tundu Lisu (centre in suit), addresses the media outside Karimjee Hall in Dar es Salaam on Friday where public opinion over the new Constitution Bill was held. (Photo by Yusuf Badi).
 
Saturday April 09, 2011 Local News
Speaker clarifies on anti-riot police use of force





From CHRISTOPHER MAJALIWA IN DODOMA, 8th April 2011 @ 12:16, Total Comments: 0, Hits: 244

The speaker of the National Assembly, Ms Anne Makinda has explained the grounds for anti-riot police move to use force in dispersing hundreds of students who demanded to take part at the public hearing session for the Constitution Review Bill of 2011 in Dodoma, saying the unruly group was causing disarray and disobeyed the order.

Ms Makinda said the venue for the occasion was Msekwa Hall which can only accommodate 500 people while people who attended were more than 1,000 and mostly were students from University of Dodoma, St John University, Institute of Rural Development Planning and Mkwawa University College of Education (MUCE).

"Considering security reasons and limited space of the venue, we could not accommodate them all, therefore, we advised them to send their representatives to participate in the discussion.

The students rebuffed and started rioting as they wanted to enter the parliament buildings uninspected," said Ms Makinda adding that even MPs are inspected.

She said such disobedience led to unrest in Dodoma township resulting in intricate passage of Dodoma-Morogoro road hence the police had to disperse them.

She fingered at some politicians saying it was out of their personal interest are lobbying students in higher learning institutions to behave in a disorderly manner, something which is against the law.
 
Saturday April 09, 2011 Local News
Zanzibar rejects union constitutional draft bill





From ALI YUSSUF in Zanzibar, 8th April 2011 @ 12:00, Total Comments: 0, Hits: 182

A PUBLIC forum on the union constitutional draft Bill was on Friday rejected by majority Zanzibaris including senior ministers pushing for a fresh start because "legal procedures concerning union bills have not been followed as par the current Zanzibar and union constitutions."

Participants including ministers and other executives, leaders from political parties, and ordinary civilians gathered at the Salama Hall, Bwawani Hotel in the Stone Town to give their views on the constitution, but many said:

"The bill has been rushed, and the required procedures on issues concerning bills to be applied in Zanzibar have been violated."

Zanzibar's Attorney General (AG) Mr Othman Masoud told the forum, "Our intention is not to undermine the process, but it is obvious, legal procedures have been violated. We ask for our suggestion to be considered."

The Minister of Constitution and Legal affairs, Mr Abubakari Khamis Bakari, said that it was unacceptable, not considering Zanzibar interest in the draft bill and also not involving Zanzibar.

According to lawyers in Zanzibar, both Zanzibar and union constitutions say that any bill that is intended to be extended to Zanzibar, should get the consent of the Zanzibar House of Representatives. It emerged at the forum that Zanzibar authorities and members of the House were not consulted prior to preparation of the Bill."

Mr Hamza Hassan Juma (CCM- Kwamtipura) complained against the use of English, while the majority Zanzibaris could not understand the foreign language.

Mr Salum Bimani, CUF party's director for information, threatened that should Zanzibar's interests be ignored, he would mobilize Zanzibaris to reject the proposed constitution at the time of referendum.

Mr Mansour Yussuf Himid, Zanzibar Minister of Agriculture and Natural Resources, said: "This is the right time to press for our (Zanzibar) interest.

We may not have other time. Let us join forces with one voice to make sure Zanzibar's interests including resolving problems in the Union are considered in the new constitution."

Prior to the forum chaired by Ms Samia Suluhu Hassan, the State Minister (Union affairs), Mr Samuel Sitta made a presentation on the Union Constitution draft bill, emphasizing that the bill was a process to write the bill. "It is not yet the constitution bill."
 
PHP:
A  PUBLIC forum on the union constitutional draft Bill was on Friday   rejected by majority Zanzibaris including senior ministers pushing for a   fresh start because "legal procedures concerning union bills have not   been followed as par the current Zanzibar and union constitutions."   

Participants including ministers and other executives, leaders from   political parties, and ordinary civilians gathered at the Salama Hall,   Bwawani Hotel in the Stone Town to give their views on the constitution,   but many said:  

"The bill has been rushed, and the required procedures on issues   concerning bills to be applied in Zanzibar have been violated."

Kila mahali kilio ni kuwa huu muswada hakuna ushirikishwaji..............................how shameful for JK and his mercenaries..................
 
Bunge halina uwezo kutunga Katiba mpya Send to a friend Saturday, 09 April 2011 08:39

Salma Said, Zanzibar
MWANASHERIA Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Othman Masoud amesema Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania halina uwezo wa kutunga Katiba mpya, bali kuifanyia marekebisho iliyopo."Bunge la Jamhuri halina uwezo wa kutunga Sheria ya Katiba hili ni jambo la msingi sidhani Zanzibar na watu wake kama watakubali kuvunja Katiba," alisema.

Masoud alisema hayo jana akitoa mchango wake katika mjadala wa maoni ya Muswada wa Sheria wa Mapitio ya Katiba unaoendeshwa na Kamati ya Bunge, Sheria na Katiba ya Bunge la Muungano
uliofanyika katika Hoteli ya Bwawani mjini hapa.

Alisema msingi wa hoja yake unatokana na Kifungu cha 98(1)(b) cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano kinachoeleza. Kifungu hicho kinasema: "Muswada wa Sheria kwa ajili ya kubadilisha masharti yoyote ya Katiba hii au masharti yoyote ya Sheria yoyote yanayohusika na jambo lolote kati ya mambo yaliyotajwa katika Orodha ya Pili kwenye Nyongeza ya Pili iliyoko mwishoni wa Katiba hii, utapitishwa tu iwapo utaungwa mkono kwa kura za Wabunge ambao idadi yao haipungui theluthi mbili ya Wabunge wote kutoka Tanzania Bara na theluthi mbili ya Wabunge wote kutoka Tanzania Zanzibar."

Orodha hiyo ya pili kwenye nyongeza ya pili iliyoko mwishoni wa Katiba inaeleza mambo ambayo mabadiliko yake yanahitaji kuungwa mkono na theluthi mbili ya wabunge wote kutoka Tanzania bara na theluthi mbili ya wabunge wote kutoka Tanzania visiwani moja likiwa mambo ya muungano ambalo suala la Katiba ni mojawapo.

Alisema Bunge lililopo sasa haliwezi kutunga Katiba mpya, bali kazi yake ni kurekebisha hivyo linatakiwa liwepo Bunge jingine ambalo litakuwa maalumu kwa ajili ya kutunga Katiba.

Akiwasilisha madhumuni na sababu za muswada huo, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta alisema umependekeza kutungwa kwa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya nchi ya mwaka 2011 na unakusudia kuanzishwa kuweka masharti ya uanzishaji wa tume pamoja na sekretari kwa madhumuni ya kuendesha na kusimamia mchakato wa mabadiliko ya hayo.

Mchakato wa mabadiliko ya Katiba pamoja na mambo mengine, utaangalia chimbuko na uhusiano wa katiba iliyopo kwa kuzingatia uhuru wa wananchi na mfumo wa siasa.

Alisema pindi muswada huo utakapopitishwa na kuwa sheria, utakuwa na utaratibu wa kisheria utakaomwezesha Rais kuunda tume ya kukusanya maoni kuhusu katiba na kuunda Bunge la Katiba kwa madhumuni ya kutunga Katiba mpya.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Jimbo la Kwamtipura, Hamza Hassan Juma amesema muswada wa marekebisho ya Katiba ya Muungano una upungufu mwingi ukiwemo kutoshirikishwa kwa Serikali ya Zanzibar ambayo alisema haikushirikishwa kikamilifu ili kutoa maoni yake na wala haukupelekwa katika Baraza la Wawakilishi kupata maoni ya Baraza, hivyo haukustahiki kupelekwa Bungeni kujadiliwa kwani umekosa ridhaa za pande mbili.

"Muswada huo ni vyema kurudi serikalini na ukafanyiwe marekebisho na badala yake upelekwe katika Baraza la Wawakilshi ili upate ridhaa ya nchi mbili zilizoungana," alisema Hamza.

Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Dk. Omar Dadi Shajak alisema kwa kuwa utaratibu haukufuatwa basi muswada huo haufai."Taratibu hazikufuatwa na misingi ya kujadili kama Jamhuri ya Muungano mchakato wa muswada huu haukubaliki kwani utaratibu haukufuatwa," alisema Shajak.

Alisema mu8swada huo uko upande mmoja na umepitishiwa bungeni bila kuzingatia pande mbili zilizounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jambo ambalo haliwezi kuachiwa kupita hivyo hivyo kwani kufanya hivyo ni kuidharau Zanzibar ambayo ni mshirika kamili katika Muungano huo.

"Muswada huu wote urejeshwe bungeni na utengenezwe tena kama kwa kuweka usawa au vyinginevyo, lakini kwa hivi haukubaliki kabisa," alisema Shajak.

Shajak alisema katika Bunge, jambo linalohusu Katiba ya Zanzibar na suala lolote lile la Muungano ni vyema kutumika usawa wa wajumbe Zanzibar na Bara na siyo kuamuliwa tu na wajumbe kutoka upande wa Tanzania bara peke yao.Mjumbe kutoka CCM, Ali Mwinyi Msuko aliwataka wanasheria wa Zanzibar kukutana na wenzao wa Tanzania bara kuupitia upya muswada huo akisema hakuna sababu ya kuuharakisha kuufikisha bungeni.

Waziri wa Kilimo, Mansour Yusuf Himid alisema muswada huo una lengo la kuwadanganya Wazanzibari na hakuna jambo jingine."Nashukuru siku hii ya leo, Kamati ya Bunge imekuja kutudanganya Wazanzibari na siku ya leo nina huzuni kubwa sana kama Mtanzania, kama Mzanzibari, naona kiini macho tu tunafanyiwa kama Baraza la Wawakilishi hawajashirikishwa, basi hakuna haja ya kukubali hilo," alisema kuongeza:

"Lazima tushirikishwe ipasavyo. Tumeungana kwa hiari. Hii ni Jamhuri ya pande mbili tumekwenda kwa hiari, tutarudi kwa hiari, tutabaki kwa hiari. Kama Wazanzibari hawajashirikishwa kupitia kura ya maoni na kufanyiwa kiini macho hicho, basi wasikubali kudanganywa," alisema huku akiungwa mkono na wananchi wengine walioshiriki mjadala huo.

Mansoor ambaye pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki (CCM), alisema binafsi anaupinga muswada huo huku akisema hiyo ni nafasi pekee ya kuhakikisha muungano unafanyiwa marekebisho na kwamba hiyo ni fursa ya pekee kwa wananchi wa Zanzibar kupinga kwani hawataipata tena iwapo muswada huo utapita.

"Hii ndiyo fursa yetu ya mwisho Wazanzibari, nikwamabie tukicheza hapa ndiyo basi hatutakiona kitu chochote ndiyo basi tena," alisisitiza.Mwandishi wa habari mwandamizi wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), Ally Saleh alisema muswada huo haukugusia Katiba ya Zanzibar jambo alillotafsiri kama dharau juu ya makubaliano ya Muungano.

"Kura ya maoni ni kitu gani? Je, Wazanzibari wakisema hawataki athari yake itakuwa nini? Tusifikiri Wazanzibari watapinga Katiba je, athari zake zitakuwa ni nini? Kusema tume isipelekwe mahakamani huko ni kuizuia demokrasia," alisema.
 
Chadema kusambaza wabunge nchi nzima kupinga muswada wa Katiba Send to a friend Saturday, 09 April 2011 09:10

Midraji Ibrahim, Dodoma
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema Jumamosi ijayo kitafanya maandamano nchi nzima kupinga muswada wa sheria wa mabadiliko ya Katiba unaoendelea kujadiliwa.

Akizungumza kwenye Viwanja vya Bunge jana, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema wabunge wote wa chama hicho watatawanywa nchi nzima kushiriki maandamano hayo.

Mbowe alisema lengo kubwa la maandamano hayo ni kupinga muswada huo kupelekwa haraka haraka na pia kukipa chama hicho fursa ya kupata maoni ya wananchi wengi zaidi.

"Jumamosi wiki ijayo tunaandamana nchi nzima, wabunge wote wa Chadema watatawanyika nchi nzima, lengo ni kupata maoni ya wananchi wengi," alisema Mbowe.

Alipinga hoja ya Serikali kwamba muswada huo usipopitishwa hivi sasa, hautakuwa na nafasi kwa sababu Bunge la Juni linahusika na Bajeti. Alisema miswada mingi imeshapitishwa kwa hati ya dharura.

"Tunataka maoni ya wananchi wengi yakusanywe ili yazingatiwe, muswada uletwe bungeni Juni. Suala la kwamba Bunge la Juni ni la bajeti ni sawa, lakini mwaka jana uliletwa muswada wa Gharama za Uchaguzi kwa hati ya dharura ukapita," alisema.

Mbowe alisema Chadema kitaendelea kupinga muswada huo kusukumwa haraka haraka na kuwakosesha wananchi fursa ya kuchangia na kwamba, iwapo makosa yatafanyika na kupitishwa hivi sasa, yatakuwa ni majuto makubwa siku zijazo.

Kuhusu vijana wanaozomea kuhusishwa na Chadema, Mbowe alisema kuzomea ni kuonyesha hisia na kwamba muda wa ubabe kwa CCM umekwisha."Waacheni wazomee, waacheni washangilie kama unawakataza kuzomea, wakataze na kushangilia. Mbona CCM wakishangiliwa hawakatai, sisi tunazomewa sana lakini tunaamini wanaonyesha hisia zao," alisema na kuongeza:

"Kuna wanaozomea kama wabunge wa CCM humu ndani? (Bungeni), tunapoonyesha hisia zetu, hisia za wananchi kwa kutoka ndani ya ukumbi mnaona na kusikia jinsi wanavyotuzomea."

Mbowe alisema kuzomewa kunawafundisha wanasiasa kusoma alama za nyakati na kwamba tuhuma za kila mara kwa chama hicho ni hofu ya watawala.Alisema suala la Katiba halitakiwi kubebwa na kuonekana kama ni mali ya kundi, chama au watu fulani, bali kushirikisha wananchi wote, huku akitahadharisha kuwa iwapo wataacha muswada huo kupita na upungufu huo, yatakuwa majuto makubwa siku zijazo.

Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, alidai muswada wa sheria unaopingwa na wadau takriban asilimia 90, hauwezi kusimamiwa kupita kwa nguvu ya dola.Kuhusu chama hicho kutuhumiwa kuhusika na vurugu, Mbowe alisema hizo ni propaganda kwa chama chochote cha siasa, lakini Chadema itaendelea kuhamasisha wananchi kudai haki zao.

Spika atoa tamko
Spika wa Bunge, Anne Makinda amesema Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala inasikiliza maoni ya wadau kwa lengo la kuboresha muswada huo na kusisitiza kwamba huo si mdahalo.

"Hivyo busara lazima zitumike. Ibara ya 18 ya Katiba inatoa haki ya uhuru wa mawazo. Kwa kutambua haki ya kikatiba ndiyo maana Bunge limetoa fursa ya kushirikisha wananchi katika masuala muhimu yanayoihusu jamii," alisema Makinda.

Hata hivyo, alisema hiyo haina budi kuzingatia haki na madaraka ya Bunge na kwamba kuheshimu mawazo ya mtu mwingine hata kama hukubaliani nayo lazima izingatiwe, tabia ya kuzomeana haikubaliki.

Kuhusu wadau waliojitokeza kushiriki na kufyatuliwa mabomu ya machozi na risasi za moto, Makinda alisema inasemekana wapo baadhi ya wanasiasa wanautumia muswada wa mabadiliko ya Katiba kama mtaji wa kisiasa, kuwapotosha wananchi hususan wanafunzi.

"Kama kweli kitendo hicho kinafanyika, hakileti picha nzuri na hakifai. Kinapaswa kukemewa na kuachwa mara moja kwa kuwa inahatarisha amani na usalama wa nchi yetu," alisema Makinda.

Aliongeza katika mjadala wa Dodoma, dosari zilizojitokeza zimeonekana dhahiri kwa kuwa wadau wengi walioshiriki walitoa michango yao ya kina baada ya kupewa fursa ya kutosha, wakiwamo wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma. Tofauti na mawazo yaliyokuwa yakitolewa na baadhi ya wanafunzi waliokuwa nje ya geti la Bunge kuwa Kamati ya Bunge au Bunge lilikuwa na njama za kuchagua watu maalumu kushiriki kwenye mkutano huo wa kamati.

Alisema wanafunzi hao walikata ushauri waliopewa mwanzo, huku wakiimba na kupiga kelele wakitaka kuingia wote ukumbini bila kukaguliwa, hali ambayo ilitishia usalama wa viongozi na wananchi maeneo ya Bunge.
 
Watu 10 mbaroni kwa vurugu za K'nondoni Send to a friend Saturday, 09 April 2011 09:09

Pamela Chilongola na Alphey Athanas
POLISI katika Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, wanawashikilia watu 10 kwa tuhuma za kuhusika na vurugu za kugombea ardhi, zilizotokea juzi katika Mtaa wa Mivumoni, Kata ya Wazo Hilll, jijini Dar es Salaam.

Watu wawili walikufa na wengine nane kujeruhi, katika vurugu hizo.Wanaoshikiliwa ni pamoja na mtoto wa mtu anayedaiwa kuwa mmiliki wa ardhi inayogombaniwa, anayetuhumiwa kuwa ni kiini cha vurugu hizo.

Juzi asubuhi zaidi ya watu 100 wakiwa katika magari aina ya Coaster, walivamia mtaa huo na kuanza kubomoa nyumba za watu kwa madai kuwa wameagizwa na kampuni ya udalali.Akizungumzia tukio hilo jana, Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Charles Kenyela, alisema mtoto wa mtu anayedaiwa kumiliki eneo hilo, anatuhumiwa kuwapeleka watu 160, ili kuvunja nyumba za wananchi.

Kwa mujibu wa kamanda huyo waliouawa katika tukio hilo wametambuliwa kuwa ni, Godfrey Samweli mkazi wa Makumbusho na Hatibu au Dabo Difa.Alisema waliojeruhiwa na kulazwa katika Hospitali ya Mwananyamala ni Meleki Mwangoti (53), Said Mugabe (25), Salum Kimaya (54),Peter Mfolo (23), Jafet Mtenganga (27) na Bakari AthumaniI (38).

Wengine ni Wilbord Ezekiel (33) na Amiri Abdala (40) ambaye hali yake si nzuri na amehamishiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Katika hatua nyingine Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana alisema Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Mvumoni, naye anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuwapa ruhusa wananchi kuwatimua wavamizi kwa madai kuwa polisi walishindwa kusaidia.Aliwataka wananchi wa eneo hilo waache vitendo vya kujichukulia sheria mkononi na badala yake wafuate taratibu za kisheria.
 
Vurugu mjadala Katiba
• Mchangiaji mmoja ang'olewa meno Dar

na Mwandishi wetu, Dodoma


amka2.gif
MJADALA wa wazi wa Muswada wa Marejeo ya Katiba unaotarajiwa kuwasilishwa katika kikao cha Bunge kinachoendelea jijini Dodoma ulikumbwa na dhoruba ukiwa unaingia siku ya pili jana.
Jijini Dar es Salaam, mjadala huo uliingia dosari baada ya ukumbi wa Karimjee unakofanyika kuvamiwa na kundi kubwa la watoto waliokuwa wakipiga kelele za kuzomea wachangiaji waliokuwa wakitoa hoja zenye mwelekeo wa kuhoji na kupinga mwenendo wa marejeo ya katiba.
Hali hiyo ya kuzomea ambayo ilianza tangu mjadala huo ulipoanza juzi, ilihitimishwa na tukio la mmoja wa wachangiaji kuvamiwa, kupigwa na kujeruhiwa na kundi kubwa la vijana waliojitokeza katika mjadala huo.
Vurugu hizo zilisababisha Mbunge wa Singida Mashariki na mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria, Tundu Lissu (CHADEMA), kususia ushiriki wake katika mjadala huo kwa kile alichokieleza kuwa kuwapo kwa dalili za wazi za kuvurugwa.
Wakati hayo yakitokea jijini Dar es Salaam katika kituo cha Dodoma vurugu hizo zilisababisha Spika wa Bunge, Anne Makinda, kutoa kauli nzito ya karipio akielekeza lawama kwa wabunge wa chama kimoja cha siasa kuwa kiini cha tafrani hiyo.
Ingawa hakutaja chama gani wala wabunge aliodai kuhusika kuchochea vurugu za wanachuo wa Chuo Kikuu Dodoma (UDOM), ni wazi Makinda alikuwa akikilenga Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema alikiri kuwa alikwenda UDOM kuwashawishi kujitokeza kwenye mdahalo huo, lakini hakuwaambia wafanye vurugu.
Akitoa taarifa yake kwa wabunge, Spika Makinda alisema kuna baadhi ya wanasiasa wanaotumia muswada wa mabadiliko ya Katiba kama mtaji wao kisiasa kwa kuwapotosha wananchi hasa wanafunzi.
"Kama kweli kitendo hicho kinafanyika, hakileti picha nzuri na hakifai na kinapaswa kukemewa na kuachwa mara moja, kwani kinahatarisha amani na usalama wa nchi," alisema.
Alisema katika kituo cha Dodoma, wadau wengi walijitokeza zikiwemo asasi zisizo za kiserikali, watu binafsi, wataalamu na wanafunzi kutoka vyuo vikuu, ikiwemo UDOM.
Kwa mujibu wa Makinda, kwa kuzingatia ukumbi wa Msekwa ambao unachukua takriban watu 500, ofisi ya Bunge iliweka utaratibu maalumu wa kuwasikiliza kulingana na idadi yao.
"Kwanza kwa kuzingatia taratibu za ulinzi na usalama za kibunge na uwezo wa ukumbi, wadau walishauriwa waingie kwa kutuma wawakilishi wao, pili, waliweka mlango maalumu wa kusajiliwa na kukaguliwa, UDOM walikataa ushauri huo, huku wakiimba na kupiga kelele wakitaka waingie wote, tena bila kukaguliwa.
"Katika kuendelea kusikiliza kilio chao, uongozi wa Bunge, Mkoa wa Dodoma, waliwashauri wanachuo hao waingie kwa awamu. Baadhi yao walitii na kufuata utaratibu na kuruhusiwa kuingia.
"Hata hivyo waliokuwa nje ya geti, hawakukubaliana na utaratibu huo na walilazimisha kamati iahirishe kikao na kuhamia Uwanja wa Jamhuri, huku wakiimba nyimbo na kuonyesha mabango na kutoa lugha chafu na kuendelea kuleta fujo," alisema Spika Makinda.
Alisema kutokana na hali hiyo iliyoashiria uvunjifu wa amani, polisi walilazimika kuwatawanya kwa mabomu.
Akitoa taarifa ya kituo cha Dar es Salaam, Spika Makinda alisema maelfu ya wadau walijitokeza wakiwamo viongozi wa siasa, viongozi wastaafu, wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali na wengine.
Hata hivyo, alisema mjadala huo ulivunjika baada ya kufunguliwa kutokana na kujitokeza hali ya kurushiana maneno makali miongoni mwa wadau wakati mjadala wa Zanzibar ulipangwa kufanyika jana.
Akijibu tuhuma za Spika dhidi ya CHADEMA, Mwenyekiti wa chama hicho na Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe, alisema tuhuma hizo hazina msingi kwani vurugu zilizotokea zimesababishwa na uzembe wa Ofisi ya Bunge katika kupanga mjadala huo.
Alikiri baadhi ya wabunge na viongozi wa chama chake wamekuwa wakihamasisha wananchi waende kwenye mijadala hiyo kuisaidia serikali ambayo alisema hadi sasa imeshindwa kuwahamasisha wananchi kujitokeza kwenye mijadala hiyo.
Alisema ofisi ya Bunge ilifanya uzembe kwani ilipaswa kujua uwezo wa Ukumbi wa Pius Msekwa kuwa na nafasi ya kuchukua watu 300.
"Matangazo yanatolewa kwenye vituo vya televisheni na radio kwamba wananchi waende. Sisi tunawahamasisha wananchi na wanachama wetu kwamba waende kutoa maoni yao, wala hatuwaambii kufika na kufanya fujo, tatizo liko wapi?" alihoji Mbowe.
Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, alisema Jumamosi ijayo CHADEMA kwa kutumia wabunge wake, itafanya maandamano makubwa na mikutano ya kukusanya maoni ya wananchi na kuyawasilisha bungeni ili kupata fursa ya kuchangia mjadala huo.
"Tumepanga kufanya maandamano nchi nzima Jumamosi ijayo, tutakusanya maoni ya wananchi na kuyaleta bungeni. Tunataka kuwashirikisha Watanzania wengi baada ya kubaini kuwa serikali imeshindwa kuwahamasisha wananchi kujitokeza kutoa maoni yao.
Hata hivyo, alipendekeza kuwa muswada huo ambao alisema una kasoro nyingi, ungeachwa kwa sasa ili kuwapa fursa wananchi kuusoma na kutoa maoni yao kuliko uharaka unaofanywa na serikali kwa sasa.
Jijini Dar es Salaam
VURUGU zilitawala katika mjadala wa Katiba na kusababisha kijana, Fakihi Mwakisu, kung'olewa meno baada ya kukosoa muswada wa marejeo ya Katiba kwa kusema ufanyiwe marekebisho yote kwa kufuata vifungu.
Tukio hilo lilitokea jana majira ya saa 7:00 mchana kwa Fakihi kung'olewa meno na kundi ambalo lilidhaniwa kutumwa na upande fulani katika mjadala huo.
Fakihi alivunjwa meno baada ya kutoka nje ya ukumbi na kufuatwa na vijana ambao walianza kummwagia matusi, hali ambayo ilimfanya kuondoka na kuacha mjadala ukiendelea.
Hata hivyo, kuondoka kwake hakukumukoa, kwani muda mfupi aliona kundi kubwa la vijana likimfuata ambalo lilimvamia na kuanza kumpiga na kusababisha kung'oka meno yake pamoja na kuchanika mdomo.
Akizungumza baada ya tukio hilo, Mwakisu alisema hakujua kuwa mjadala huo ungeweza kusababisha kupoteza meno yake na kupata maumivu makali.
Alisema alichokuwa akifahamu mjadala huo ni kwa ajili ya wananchi wote bila kujali itikadi za vyama, lakini kumeonekana kuna makundi ambayo hayataki kukosolewa kwa muswada wa katiba.
"Siamini kama mjadala huu ungeweza kupelekea kung'olewa meno yangu, hii ni historia mpya kwangu. Sitasahau milele, watu wa CCM wameletwa kwa ajili ya vurugu," alisema Mwakisu huku akibubujikwa damu mdomoni.
Tundu Lissu
Mjumbe wa Kamati ya Katiba na Sheria na Mbunge wa Singida Kaskazini, Tundu Lissu, alijikuta akilazimika kususia mjadala huo jijini Dar es Salaam kwa kudai kuwa hauna faida kwa Watanzania katika kupata haki ya kuwa na katiba mpya.
Akizungumza na waandishi wa habari nje ya Ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Salam, Lissu alisema uamuzi wake umetokana na kuwapo na vurugu zinazotokana na baadhi ya watu kuletwa kwa ajili ya kufanya vurugu, ili kuharibu mjadala wa katiba.
Lissu alisema mjadala wa Katiba unahitaji umakini na si kujadili kwa haraka kwa ajili ya kumnufaisha mtu kwa kuwa na katiba mbaya.
Mjumbe huyo alikerwa na utitiri wa watoto waliofurika katika ukumbi na kuwafanya watu wazima wengi wenye uwezo wa kuchangia kukosa nafasi ya kuingia ukumbini.
Alisema makada wa CCM wamepeleka watu kwa kutumia malori kwa ajili ya kuharibu mfumo wa kupata katiba mpya, ili waendelee kutawala.
"Hawa watoto wameletwa ili kuharibu utaratibu uliopo hali ambayo utaipa meza kuwasilisha kwa kusema tumepata maoni hali ambayo kutapelekea katiba mpya yenye viraka zaidi kuliko iliyopo," alisema Lissu.
Alisema utaratibu wa kuharakisha katiba mpya hutaweza kufanikiwa kutokana na muda uliwekwa kuwa mchache, hivyo wananchi wengi watashindwa kufikiwa.
Lissu alisema utaratibu wa kujadili katiba utanyima wananchi kupata haki kutokana na vituo vya kujadili kuwa vichache ambavyo vitasababisha kuwa na katiba viraka.
Alisema kuweka vituo vitatu vya Dodoma Dar es Salaam na Zanzibar ni kunyima Watanzania wengine fursa wasiweze kuchangia katika katiba mpya.
"Mimi sikubaliani na utaratibu uliowekwa katika kujadili katiba mpya, ambao utasababisha kurudishwa katiba iliyopo kwa ajili ya masilahi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)," alisema Lissu.
Taarifa hii imeandaliwa na Martin Malera (Dodoma), Chalila Kibuda na Mariana Mathias (Dar).
 
Vurugu mjadala Katiba
• Mchangiaji mmoja ang’olewa meno Dar

na Mwandishi wetu, Dodoma


amka2.gif
MJADALA wa wazi wa Muswada wa Marejeo ya Katiba unaotarajiwa kuwasilishwa katika kikao cha Bunge kinachoendelea jijini Dodoma ulikumbwa na dhoruba ukiwa unaingia siku ya pili jana.
Jijini Dar es Salaam, mjadala huo uliingia dosari baada ya ukumbi wa Karimjee unakofanyika kuvamiwa na kundi kubwa la watoto waliokuwa wakipiga kelele za kuzomea wachangiaji waliokuwa wakitoa hoja zenye mwelekeo wa kuhoji na kupinga mwenendo wa marejeo ya katiba.
Hali hiyo ya kuzomea ambayo ilianza tangu mjadala huo ulipoanza juzi, ilihitimishwa na tukio la mmoja wa wachangiaji kuvamiwa, kupigwa na kujeruhiwa na kundi kubwa la vijana waliojitokeza katika mjadala huo.
Vurugu hizo zilisababisha Mbunge wa Singida Mashariki na mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria, Tundu Lissu (CHADEMA), kususia ushiriki wake katika mjadala huo kwa kile alichokieleza kuwa kuwapo kwa dalili za wazi za kuvurugwa.
Wakati hayo yakitokea jijini Dar es Salaam katika kituo cha Dodoma vurugu hizo zilisababisha Spika wa Bunge, Anne Makinda, kutoa kauli nzito ya karipio akielekeza lawama kwa wabunge wa chama kimoja cha siasa kuwa kiini cha tafrani hiyo.
Ingawa hakutaja chama gani wala wabunge aliodai kuhusika kuchochea vurugu za wanachuo wa Chuo Kikuu Dodoma (UDOM), ni wazi Makinda alikuwa akikilenga Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema alikiri kuwa alikwenda UDOM kuwashawishi kujitokeza kwenye mdahalo huo, lakini hakuwaambia wafanye vurugu.
Akitoa taarifa yake kwa wabunge, Spika Makinda alisema kuna baadhi ya wanasiasa wanaotumia muswada wa mabadiliko ya Katiba kama mtaji wao kisiasa kwa kuwapotosha wananchi hasa wanafunzi.
“Kama kweli kitendo hicho kinafanyika, hakileti picha nzuri na hakifai na kinapaswa kukemewa na kuachwa mara moja, kwani kinahatarisha amani na usalama wa nchi,” alisema.
Alisema katika kituo cha Dodoma, wadau wengi walijitokeza zikiwemo asasi zisizo za kiserikali, watu binafsi, wataalamu na wanafunzi kutoka vyuo vikuu, ikiwemo UDOM.
Kwa mujibu wa Makinda, kwa kuzingatia ukumbi wa Msekwa ambao unachukua takriban watu 500, ofisi ya Bunge iliweka utaratibu maalumu wa kuwasikiliza kulingana na idadi yao.
“Kwanza kwa kuzingatia taratibu za ulinzi na usalama za kibunge na uwezo wa ukumbi, wadau walishauriwa waingie kwa kutuma wawakilishi wao, pili, waliweka mlango maalumu wa kusajiliwa na kukaguliwa, UDOM walikataa ushauri huo, huku wakiimba na kupiga kelele wakitaka waingie wote, tena bila kukaguliwa.
“Katika kuendelea kusikiliza kilio chao, uongozi wa Bunge, Mkoa wa Dodoma, waliwashauri wanachuo hao waingie kwa awamu. Baadhi yao walitii na kufuata utaratibu na kuruhusiwa kuingia.
“Hata hivyo waliokuwa nje ya geti, hawakukubaliana na utaratibu huo na walilazimisha kamati iahirishe kikao na kuhamia Uwanja wa Jamhuri, huku wakiimba nyimbo na kuonyesha mabango na kutoa lugha chafu na kuendelea kuleta fujo,” alisema Spika Makinda.
Alisema kutokana na hali hiyo iliyoashiria uvunjifu wa amani, polisi walilazimika kuwatawanya kwa mabomu.
Akitoa taarifa ya kituo cha Dar es Salaam, Spika Makinda alisema maelfu ya wadau walijitokeza wakiwamo viongozi wa siasa, viongozi wastaafu, wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali na wengine.
Hata hivyo, alisema mjadala huo ulivunjika baada ya kufunguliwa kutokana na kujitokeza hali ya kurushiana maneno makali miongoni mwa wadau wakati mjadala wa Zanzibar ulipangwa kufanyika jana.
Akijibu tuhuma za Spika dhidi ya CHADEMA, Mwenyekiti wa chama hicho na Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe, alisema tuhuma hizo hazina msingi kwani vurugu zilizotokea zimesababishwa na uzembe wa Ofisi ya Bunge katika kupanga mjadala huo.
Alikiri baadhi ya wabunge na viongozi wa chama chake wamekuwa wakihamasisha wananchi waende kwenye mijadala hiyo kuisaidia serikali ambayo alisema hadi sasa imeshindwa kuwahamasisha wananchi kujitokeza kwenye mijadala hiyo.
Alisema ofisi ya Bunge ilifanya uzembe kwani ilipaswa kujua uwezo wa Ukumbi wa Pius Msekwa kuwa na nafasi ya kuchukua watu 300.
“Matangazo yanatolewa kwenye vituo vya televisheni na radio kwamba wananchi waende. Sisi tunawahamasisha wananchi na wanachama wetu kwamba waende kutoa maoni yao, wala hatuwaambii kufika na kufanya fujo, tatizo liko wapi?” alihoji Mbowe.
Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, alisema Jumamosi ijayo CHADEMA kwa kutumia wabunge wake, itafanya maandamano makubwa na mikutano ya kukusanya maoni ya wananchi na kuyawasilisha bungeni ili kupata fursa ya kuchangia mjadala huo.
“Tumepanga kufanya maandamano nchi nzima Jumamosi ijayo, tutakusanya maoni ya wananchi na kuyaleta bungeni. Tunataka kuwashirikisha Watanzania wengi baada ya kubaini kuwa serikali imeshindwa kuwahamasisha wananchi kujitokeza kutoa maoni yao.
Hata hivyo, alipendekeza kuwa muswada huo ambao alisema una kasoro nyingi, ungeachwa kwa sasa ili kuwapa fursa wananchi kuusoma na kutoa maoni yao kuliko uharaka unaofanywa na serikali kwa sasa.
Jijini Dar es Salaam
VURUGU zilitawala katika mjadala wa Katiba na kusababisha kijana, Fakihi Mwakisu, kung’olewa meno baada ya kukosoa muswada wa marejeo ya Katiba kwa kusema ufanyiwe marekebisho yote kwa kufuata vifungu.
Tukio hilo lilitokea jana majira ya saa 7:00 mchana kwa Fakihi kung’olewa meno na kundi ambalo lilidhaniwa kutumwa na upande fulani katika mjadala huo.
Fakihi alivunjwa meno baada ya kutoka nje ya ukumbi na kufuatwa na vijana ambao walianza kummwagia matusi, hali ambayo ilimfanya kuondoka na kuacha mjadala ukiendelea.
Hata hivyo, kuondoka kwake hakukumukoa, kwani muda mfupi aliona kundi kubwa la vijana likimfuata ambalo lilimvamia na kuanza kumpiga na kusababisha kung’oka meno yake pamoja na kuchanika mdomo.
Akizungumza baada ya tukio hilo, Mwakisu alisema hakujua kuwa mjadala huo ungeweza kusababisha kupoteza meno yake na kupata maumivu makali.
Alisema alichokuwa akifahamu mjadala huo ni kwa ajili ya wananchi wote bila kujali itikadi za vyama, lakini kumeonekana kuna makundi ambayo hayataki kukosolewa kwa muswada wa katiba.
“Siamini kama mjadala huu ungeweza kupelekea kung’olewa meno yangu, hii ni historia mpya kwangu. Sitasahau milele, watu wa CCM wameletwa kwa ajili ya vurugu,” alisema Mwakisu huku akibubujikwa damu mdomoni.
Tundu Lissu
Mjumbe wa Kamati ya Katiba na Sheria na Mbunge wa Singida Kaskazini, Tundu Lissu, alijikuta akilazimika kususia mjadala huo jijini Dar es Salaam kwa kudai kuwa hauna faida kwa Watanzania katika kupata haki ya kuwa na katiba mpya.
Akizungumza na waandishi wa habari nje ya Ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Salam, Lissu alisema uamuzi wake umetokana na kuwapo na vurugu zinazotokana na baadhi ya watu kuletwa kwa ajili ya kufanya vurugu, ili kuharibu mjadala wa katiba.
Lissu alisema mjadala wa Katiba unahitaji umakini na si kujadili kwa haraka kwa ajili ya kumnufaisha mtu kwa kuwa na katiba mbaya.
Mjumbe huyo alikerwa na utitiri wa watoto waliofurika katika ukumbi na kuwafanya watu wazima wengi wenye uwezo wa kuchangia kukosa nafasi ya kuingia ukumbini.
Alisema makada wa CCM wamepeleka watu kwa kutumia malori kwa ajili ya kuharibu mfumo wa kupata katiba mpya, ili waendelee kutawala.
“Hawa watoto wameletwa ili kuharibu utaratibu uliopo hali ambayo utaipa meza kuwasilisha kwa kusema tumepata maoni hali ambayo kutapelekea katiba mpya yenye viraka zaidi kuliko iliyopo,” alisema Lissu.
Alisema utaratibu wa kuharakisha katiba mpya hutaweza kufanikiwa kutokana na muda uliwekwa kuwa mchache, hivyo wananchi wengi watashindwa kufikiwa.
Lissu alisema utaratibu wa kujadili katiba utanyima wananchi kupata haki kutokana na vituo vya kujadili kuwa vichache ambavyo vitasababisha kuwa na katiba viraka.
Alisema kuweka vituo vitatu vya Dodoma Dar es Salaam na Zanzibar ni kunyima Watanzania wengine fursa wasiweze kuchangia katika katiba mpya.
“Mimi sikubaliani na utaratibu uliowekwa katika kujadili katiba mpya, ambao utasababisha kurudishwa katiba iliyopo kwa ajili ya masilahi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),” alisema Lissu.
Taarifa hii imeandaliwa na Martin Malera (Dodoma), Chalila Kibuda na Mariana Mathias (Dar).
 
Back
Top Bottom