Mkutano wa kibiashara kati ya China Council for the Promotion of International Trade (CCPIT- Shenzhen) na EPZA

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,802
11,961
Mkutano wa kibiashara kati ya China Council for the Promotion of International Trade (CCPIT- Shenzhen) na Mamlaka ya Maeneo ya Uzalishaji wa Mauzo ya Nje (EPZA)

Dar es Salaam, 09 September 2021.
Katika siku za hivi karibuni Serikali ya awamu ya sita imekuwa ikiweka nguvu kubwa kuvitia uwekezaji na takwimu zinaonyesha kuwa jitihada hizo zimezaa matunda kwa kuwa na idadi kubwa ya wawekezaji kutoka nje walioonyesha nia ya kuwekeza hapa nchini.

Wakati juhudi hizo zikiendelea hivi karibuni kampuni ya Vipawa Management Group (VMG) ilifanikisha mkutano wa kibiashara wa aina yake kati ya wawekezaji wa China Council for the Promotion of International Trade Shenzhen (CCPIT) na Mamlaka ya Maeneo ya Uzalishaji wa Mauzo ya Nje (EPZA).

Mkutano huo ulilenga kuchangiza biashara na mahusiano ya kibisahara kati ya China na Tanzania. Watu wa China walitaka kupata uelewa wa kina na kuimarisha urafiki katika ya mataifa haya mawili katika muktadha wa kisheria na sera za serikali.
Katika mkutano huo uliofanyika Agosti 31, 2021 jijini Dar es Salaam China Council for the Promotion of International Trade Shenzhen (CCPIT Shenzhen) walikuwa wanashauku ya kujua fursa zilizopo katika sekta ya kilimo, madini, utalii biashara na viwanda na namna gani Serikali ya Tanzania inaunga mkono uwekezaji.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maeneo ya Uzalishaji wa Mauzo ya Nje ( EPZA) Bw. John Mnali alishiriki mkutano huo wa kibiashara uliofanyika kwa njia ya mtandao ambapo aliwapatia wawekezaji hao maeleze ya mambo yote waliyotaka kujua sambamba na kuwafafanulia juu ya fursa zilizopo.

Kabla ya kuzitaja na kuzifungua fursa zilizopo katika maeneo husika Mnali alieleza kuwa kwa hapa nchini mwekezaji ana milango mitatu ya kuanzisha uwekezaji wake akiitaja kuwa ni;Mamlaka ya Maeneo ya Uzalishaji wa Mauzo ya Nje (EPZA) ambayo inahusisha uwekezaji wa viwanda zinavyozalisha bidhaa za kuuza nje, Kituo Cha Uwekezaji- (TIC), Zanzibar Investment Promotion Authority (ZPA), ambayo inasimamia uwekezaji Tanzania-Zanzibar.

Bw. Mnali alieleza kuwa kwa upande wa EPZA mwekezaji mwenyewe anaweza kwa kutumia leseni ya maeneo ya uzalishaji kwa mauzo ya nje- EPZ, aambapo mwekezaji anatakiwa kuuza nje ya nchi asilimia kuanzia 80 ya kile anachokizalisha.

Kuhusu fursa zilizopo nchini katika sekta ya kilimo, Bw. Mnali alisema “Kwa sasa mwelekeo wa Serikali ni kupata wawekezaji wa kuongeza thamani katika mazao mbalimbali ya kilimo na sio kuuza nje ya nchi yakiwa ghafi, pia alieleza kua Kuna fursa kubwa ya kuzalisha mafuta ya kupikia kutoka katika mazao yetu”. Kwakua soko la mafuta ya kula bado ni kuwa ndani na nje ya nchi, na Tanzania inazalisha kwa wingi mazao kama; ufuta, alizeti, na michikichi ambayo ni malighafi ya kuzalishia mafuta ya kula.

Mbali na ukamuaji wa mafuta, Bw.Mnali alieleza kuwa kuna fursa ya kilimo cha maparachichi ambayo yanahitajika kwa wingi katika maeneo mbalimbali Duniani, sanjari na mazao mengine ya bustanini (horticulture).

Alisema kuongeza thamani sio tu kwenye mazao ya kilimo bali kila sekta ya uzalishaji ikiwa ni pamoja na madini kwa kuyaongezea thamani hapa nchini na sio kuyauza yakiwa ghafi “Tunahitaji vitu kama uchenjuaji, ili kuchenjua na kuyaongezea thamani madini yetu”.

Katika sekta ya madini ambayo huchangia sehemu kubwa ya uchumi wa Tanzania. Bw. Mnali aliongeza pia kuna fursa zingine za biashara zilizo wazi kama fursa ya kujenga hoteli za hadhi tofauti tofauti pamoja na miundombinu ya burudani na ukarimu kwa watalii.

Katika biashara na viwanda Bw.Mnali alisema kuna mengi ya kufanya katika viwanda kwakuwa bidhaa nyingi za viwandani Tanzania zinazinunua kutoka nje ya nchi hususani vyakula, dawa na vifaa tiba.

Alisema kwa sasa Tanzania inatumia fedha nyingi kununua bidhaa hizo nje ya nchi akitolea mfano wa dawa na vifaa tiba akisema soko lake hapa nchini ni kubwa pia aliongezea kwa kusema, taasisi ya kununua na kusambaza dawa (MSD), imepewa idhini ya kusambaza dawa katika nchi za SADC, hivyo mwekezaji yeyote katika eneo hilo atakuwa na uhakika wa soko la bidhaa zake.

Mbali na fursa hizo Bw. Mnali alisema, katika sekta ndogo ya mbao na bidhaa za mbao fursa ni kubwa kutokana na uwepo wa misitu ya asili na miti ya kupandwa, lakini pia kuna fursa ya uvuvi katika maziwa na eneo la bahari na fursa zote hizo ziko wazi kwa wawekezaji.

Vilevile Bw.Mnali alisema kuna fursa ya kuzalisha bidhaa za kielektroniki hapa nchini pamoja na uunganishaji wa magari, mashine na mitambo mbalimbali ambayo inahitaji katika soko la ndani na nje.

Baada ya kusikia fursa hizo CCPIT Shenzhen, ilieleza kufurahishwa na uwepo wa fursa hizo na motisha ambazo nchi inatoa kwa wawekezaji; hivyo wakaahidi kua wawekezaji kutoka China watakuja siku zijazo, hata hivyo walisema Tanzania inafahamika nchini China kwa uwepo wa mlima mrefu barani Afrika (Kilimanjaro), Visiwa vya Zanzibar na fukwe nzuri.

6M5-1.jpg
 
Back
Top Bottom