Mkutano wa JK na Wazee wa Darisalama: Dana Dana Inaendelea!. Sasa ni J3!.

Wanabodi,

Ule mkutano kati ya Rais Jakaya Kikwete na Wazee wa Darisalaam, uliokuwa ufanyike leo, ukaahirishwa na kutangazwa ungefanyika kesho, umeahirishwa tena, sasa kufanyika Jumatatu!.

Taarifa toka Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, iliyosomwa na TBC, imeeleza lengo la kusogezwa mbele mkutano huo, ni ili kutoa nafasi kwa Rais Kikwete, kujadiliana na wadau mbalimbali.

My Take!.
Nilipita mbele ya ukumbi Diamond, nikashuhudia masikini baadhi ya wabibi na wababu, walishajitanguliza mapema pale ukumbini, bila kujua mkutano umeahirishwa, na nadhani kulikuwa na ahadi ya kupeana japo nauli!, hivyo kujikuta hawana hili wa lile!.

Kuelezwa huelezwa kwa mdomo, lakini ahirisho ni kupitia electronic media, masikini wa watu, hawana redio wala TV, na siajabu kesho asubuhi, wengine wakadamkia Ukumbini!.

Naamini sababu kuu ya JK kutokutana na wazee hao, ni atakuwa ameisoma ile thread ya Mzee Mwanakijiji humu jukwaani na kuamua kuufuata ushauri wa JF!.

Kwa mliosoma baadhi ya sifa nzuri za JK ni "a good sense of humour", hivyo JK baada ya kusoma JF, akaamua kuwatafuta madaktari, aka wa 'charm' with a good sense of humour, kina Ulimboka wakalainika, kesho mtashuhudia wakimeza matapishi yao, kwa kutoa tamko la kuumaliza rasmi mgomo huo bila masharti yoyote!. JK atakapokutana na Wazee hiyo Jumatatu itakuwa ni kuwapatia tuu mrejesho!.

Hongera Mzee Mwanakijiji kwa kutoa angalizo muhimu!. Hongera JK kwa kumaliza kila kitu, na baada ya kina Ulimboka kuumaliza rasmi mgomo, Dr. Mponda na Dr. Nkya wajifungashie virago vyao na kujiondokea kwa amani na kwa heshima!.

Pasco.

Pasco unaongea kama unajua jambo fulani mkuu funguka usomeke JF kawaida hapa ni kufunguka kama una uhakika na unachosema
 
Wakati mgomo unaanza alikua Moshi kwa nn hakuzungumza na wazee wa moshi au Arusha anakuja kuongea na hv vigagula vya dar ambavyo havijasoma?
 
Jamani mniwie radhi kama mnaweza kuniambia ni thread ipi anayoiongelea Pasco inayohusiana na Mwanakijiji kutoa ushauri kwa Mkulu ? Mimi sikuweza kuingia jamvini maana nilikuwa safari. Nitashukuru sana
Kama wewe ni Member wa zamani na bado humjui Pasco basi nakupa pole sana. wanaomjuwa vizuri huyu ni mtu wa kupuuzwa tu!!
 
Wale wazee maskini wa watu, walitegemea kunywa japo soda leo ambazo hubahatika kuzinywa wanapokuwa wamelazwa na kuletewa na ndugu. Vi-buku tano tano vingewasaidia japo kesho kubadilisha mboga, ndo vimeyeyuka kirahisi hivyo! Kweli JK ni msanii!
Mbona imekuchukua muda mrefu namna hiyo kuamini kuwa JK ni ze komedi!!!
 
Wanabodi,

Kwa mliosoma baadhi ya sifa nzuri za JK ni "a good sense of humour", hivyo JK akaamua kuwatafuta madaktari, aka wa 'charm' with a good sense of humour, kina Ulimboka wakalainika, kesho mtashuhudia wakitoa tamko la kuumaliza rasmi mgomo huo bila masharti yoyote!. JK atakapokutana na Wazee hiyo Jumatatu itakuwa ni kuwapatia tuu mrejesho!.

Pasco.
Nimefanya mapitio ya nilichoandika jana, na kilichotokea leo!. I was right, 100%!
 
Back
Top Bottom