Mkutano wa JK na Wazee wa Darisalama: Dana Dana Inaendelea!. Sasa ni J3!.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,467
113,581
Wanabodi,

Ule mkutano kati ya Rais Jakaya Kikwete na Wazee wa Darisalaam, uliokuwa ufanyike leo, ukaahirishwa na kutangazwa ungefanyika kesho, umeahirishwa tena, sasa kufanyika Jumatatu!.

Taarifa toka Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, iliyosomwa na TBC, imeeleza lengo la kusogezwa mbele mkutano huo, ni ili kutoa nafasi kwa Rais Kikwete, kujadiliana na wadau mbalimbali.

My Take!.
Nilipita mbele ya ukumbi Diamond, nikashuhudia masikini baadhi ya wabibi na wababu, walishajitanguliza mapema pale ukumbini, bila kujua mkutano umeahirishwa, na nadhani kulikuwa na ahadi ya kupeana japo nauli!, hivyo kujikuta hawana hili wa lile!.

Kuelezwa huelezwa kwa mdomo, lakini ahirisho ni kupitia electronic media, masikini wa watu, hawana redio wala TV, na siajabu kesho asubuhi, wengine wakadamkia Ukumbini!.

Naamini sababu kuu ya JK kutokutana na wazee hao, ni atakuwa ameisoma ile thread ya Mzee Mwanakijiji humu jukwaani na kuamua kuufuata ushauri wa JF!.

Kwa mliosoma baadhi ya sifa nzuri za JK ni "a good sense of humour", hivyo JK baada ya kusoma JF, akaamua kuwatafuta madaktari, aka wa 'charm' with a good sense of humour, kina Ulimboka wakalainika, kesho mtashuhudia wakimeza matapishi yao, kwa kutoa tamko la kuumaliza rasmi mgomo huo bila masharti yoyote!. JK atakapokutana na Wazee hiyo Jumatatu itakuwa ni kuwapatia tuu mrejesho!.

Hongera Mzee Mwanakijiji kwa kutoa angalizo muhimu!. Hongera JK kwa kumaliza kila kitu, na baada ya kina Ulimboka kuumaliza rasmi mgomo, Dr. Mponda na Dr. Nkya wajifungashie virago vyao na kujiondokea kwa amani na kwa heshima!.

Pasco.
 
Wanabodi,

Ule mkutano kati ya Rais Jakaya Kikwete na Wazee wa Darisalaam, uliokuwa ufanyike leo, ukaahirishwa na kutangazwa ungefanyika kesho, umeahirishwa tena, sasa kufanyika Jumatatu!.

Ili Rais apate muda wa kujadiliana na wadau wa suala atakaloliongelea!
 
Wanabodi,

Ule mkutano kati ya Rais Jakaya Kikwete na Wazee wa Darisalaam, uliokuwa ufanyike leo, ukaahirishwa na kutangazwa ungefanyika kesho, umeahirishwa tena, sasa kufanyika Jumatatu!.

Hata asikutane nao haina maana yeyote zaidi ya kuvujisha KODI YA WANAINCHI tu!

Hakuna jipya kwa jk ila tuna hasara naye kubwa ktk Nchi!
 
Wanabodi,

Ule mkutano kati ya Rais Jakaya Kikwete na Wazee wa Darisalaam, uliokuwa ufanyike leo, ukaahirishwa na kutangazwa ungefanyika kesho, umeahirishwa tena, sasa kufanyika Jumatatu!.

...na nimesikia radioni jioni hii mmoja wa wawakilishi wa madaktari amekaririwa akisema mgomo utaendelea hadi hapo JK atakapotoa hotuba kwa hao wazee ndipo mstakabali utakapojulikana.....hii ni itategemea tija (au lack of it) itakayoletwa na hotuba hiyo!
 
Nadhani mazungumzo na Drs yamekuwa magumu kama ya CDM. inawezekana yataendelea weekend nzima.
Pasco wa JF mshauri Salva au Premi watoe japo muhtasari wa yaliyozungumzwa leo
 
Hivi wazee wa Dar ni nani hao ktk nchi hii huru?
Je wanamchango gani ktk kutatua mgogoro wa mgomo wa madaktari?
Je wanauwezo wa kuchukua nafasi ya madakatari ya kutibu raia kwa ndumba zao?
Je hawa si wale wazee wa CCM wenye masilahi ya pekee na CCM?

Hoja:
-Mambo wazee katika nchi hii yamepitwa na wakati.
-Wazee wa TZ hasa walipo CCM wamekuwa chazo cha mateso kwa raia kwa kupenda kung'ang'ania madaraka,kutowajibika.
-Wazee ndo chanzo cha mgomo wa madaktari.
-Katika ulimwengu wa leo wa sayansi na teknolojia ni upuuzi kutegemea kutatua matatizo kwa kutegemea fikra kuu kuu na zilizochakaa za wazee.
-Fikra za kuwaamini wazee ni fikra mgando ambazo zimepitwa na wakati.

Take note: Wa TZ tuache kufikiri kiujima kwa kutegemea umri mkubwa ndo unatatua matatizo.Wazee waliaminika ktk kipindi cha zama za mawe, siyo leo.
 
Nadhani mazungumzo na Drs yamekuwa magumu kama ya CDM. inawezekana yataendelea weekend nzima. Pasco wa JF mshauri Salva au Premi watoe japo muhtasari wa yaliyozungumzwa leo
Mkuu Bitabo, kama ni kweli, fungua thread yangu ya Mapungufu ya JK, uone ushauri niliowapa hao wasaidizi wa JK!. Wale wanaodhania mimi ni mshabiki wa CCM, watafute thread yangu ya "CCM Imechokwa", wanaodhania mimi mshabiki wa Chadema, watafute thread yangu ya "Chadema Haijajipanga". Mimi sina chama, sijikombi kwa yoyote, I just speak out my mind!.
 
Hivi wazee wa Dar ni nani hao ktk nchi hii huru?
Je wanamchango gani ktk kutatua mgogoro wa mgomo wa madaktari?
Je wanauwezo wa kuchukua nafasi ya madakatari ya kutibu raia kwa ndumba zao?
Je hawa si wale wazee wa CCM wenye masilahi ya pekee na CCM?

Hoja:
-Mambo wazee katika nchi hii yamepitwa na wakati.
-Wazee wa TZ hasa walipo CCM wamekuwa chazo cha mateso kwa raia kwa kupenda kung'ang'ania madaraka,kutowajibika.
-Wazee ndo chanzo cha mgomo wa madaktari.
-Katika ulimwengu wa leo wa sayansi na teknolojia ni upuuzi kutegemea kutatua matatizo kwa kutegemea fikra kuu kuu na zilizochakaa za wazee.
-Fikra za kuwaamini wazee ni fikra mgando ambazo zimepitwa na wakati.

Take note: Wa TZ tuache kufikiri kiujima kwa kutegemea umri mkubwa ndo unatatua matatizo.Wazee waliaminika ktk kipindi cha zama za mawe, siyo leo.
Moma2k, ukubwa dawa!, hawa ni Wazee wa Busara!. Thamani yao ni hekima zao!
 
...na nimesikia radioni jioni hii mmoja wa wawakilishi wa madaktari amekaririwa akisema mgomo utaendelea hadi hapo JK atakapotoa hotuba kwa hao wazee ndipo mstakabali utakapojulikana.....hii ni itategemea tija (au lack of it) itakayoletwa na hotuba hiyo!

Mbona kwa mujibu wa TBC1 mgomo umeisha?!! au nina kiwi ya macho?
 
Wale wazee maskini wa watu, walitegemea kunywa japo soda leo ambazo hubahatika kuzinywa wanapokuwa wamelazwa na kuletewa na ndugu. Vi-buku tano tano vingewasaidia japo kesho kubadilisha mboga, ndo vimeyeyuka kirahisi hivyo! Kweli JK ni msanii!
 
Wazee wa Dar ndio waliokuwa wanampa nauli, sabuni , baskeli ya kwenda pugu na kurudi na kila kitu alicho achieve Nyerere ni jitihada na dedication ya hao wazee wa daslaam wakisaidiwa na kina Chifu Kunambi. In case kama hufahamu mchango wa hao wazee.
 
naona baada ya chamoto watakiona umekuja tena na kulainishwa kuacha mgomo bila masharti yeyote...unazungumzia sharti la nkya na mponda kuondoka au ?
 
Da, afadhari. Ninaamini asilimia mia JK lazima kuna kitu angebofoa tu......!
Na hakuna, walichokwepa washauri wake ni kumnusuru na aibu ya aina ya mbayuwayu!
 
Wazee wa Dar ndio waliokuwa wanampa nauli, sabuni , baskeli ya kwenda pugu na kurudi na kila kitu alicho achieve Nyerere ni jitihada na dedication ya hao wazee wa daslaam wakisaidiwa na kina Chifu Kunambi. In case kama hufahamu mchango wa hao wazee.

Maundumula,

..ni wazee wa miaka hiyo ya 50 na 60.

..mwenyekiti wa wazee wa Dsm sasa hivi ni Brig.Gen.Hashim Mbita[rtd].

..tena huyu kwa asili ni wa kutokea Tabora.

..Brig.Gen.Mbita ni mdogo sana kiumri ukimlinganisha na Mwalimu au wazee waliomkarimu miaka hiyo.
 
Back
Top Bottom