Mkutano wa Jangwani Mei 26: Polisi walumbana na CHADEMA!

CDM wakikubali kuzuiwa wamekwisha!! Wawalazmishe polisi kutoa ulinzi..

Mkuu unanipa wasiwasi unaposema walazimishe! How? Wote tuliona yaliyotutokea Arusha. Bado tupo na walemavu ambao hawawezi kushiriki tena ujenzi wa taifa. Ni wanachama wenzetu wa cdm lakini hawawezi kufika kwenye mikutano yetu! Najua inaumiza sana lakini tutafute namna nyingine ya kufanya na sio kuandamana! Hapa naona wanatafuta sababu ya kuvuruga tukio zima. Bila kujipanga na kuweka tahadhari, tutajikuta tunapiga stori za vurugu, majeruhi na maumivu badala ya mafanikio!
Pia kuna mikutano imeandaliwa huko kusini. Wakiweza kusambaratisha kesho, hata hiyo mingine haitakuwa na mafanikio maana itawatia hofu wananchi na ccm watajaza propaganda hapo kuongeza hofu hiyo. Au wataikataza/kupiga marufuku kwa kisingizio cha vurugu tukarudishwa nyuma!
Nakuelewa unalenga nini na faida zake na natumaini utanielewa pia.
 
Maandamano hayaepukiki!!
Kwa mfano, mkutano ukiisha watu wataishaje uwanjani bila kuandamana(kutembea wengi kwa pamoja)!
Hata wakati wa kuhudhuria mkutano, natarajia watu watakuwa wanakuja kwa makundi makubwa!!
Mambo mengine ni utumwa wa fikra! Ukiruhusu mkutano, umeruhusu maandamano!!
 
Tuache ushabiki na tufuate taratibu, kilichoombwa ni mkutano na kibali kimetolewa sasa suala la maandamano linatoka wapi? wakati kila mtu natoka nyumbani kwake?

Jamani tubadilike!!! why maandamano si kila mmmoja anatoka kwake kwenda kwenye Mkutano sasa maandamano yanatoka wapi? Please wakati tunakubali mabadiliko tusiache hisisa zitutawale.

Wanzania wote wasio magamba na magamba twendeni tukasikie wawakilishi wetu wametuandalia kauli ipi ya matumaini. Maandamano ya nini sasa.
Usibwabwa je tu, polisi watanzania ukitembea kwa miguu unaambiwa unaandamana (kwa wanachadema tu) sasa unategemea nini kwenye mkutano wakesho watu wote watapata magari.....
 
Jeshi la police kutoa kauli hiyo sishangai kwani ni taasisi iliojaa watu wenye upeo mdogo sana wa kufikiri na kusoma alama za nyakati.

CDM wafanye mkutano kwa amani .Hizi ni mbinu za kuzuia wanamapinduzi wasiendelee na harakati za kuikomboa tz dhidi ya utawala mbovu wa CCM.
 
Hivi kuna shida gani wakajikusanya na kuelekea jangwani pamoja?

Watu hawana viwembe,visu,mapanga,mikuki,mishale,mashoka hata chelewa ya kumtobolea mtu jicho watu hawana.

Sasa kunaubaya gani mtu akija na mama,dada,kaka au hata ndugu na majirani pamoja? Je jeshi la polisi linajipanga kuzuia raia watz wasifunguliwe kifikra?

Hawataki watz waondolew stress(msongo wa mawazo)?

Nafikiri wakizuia maandamano(ya amani na si ya shari) watakuwa wanakiuka katiba ya bongoland.
 
CDM wakikubali kuzuiwa wamekwisha!! Wawalazmishe polisi kutoa ulinzi..

Huu ndio ufataani wako nnaousema mimi mara kwa mara. Sasa wewe Kamanda wa Polisi ameshasema wasifanye maandamano, wewe unataka wakafanye maandamo kinyume na maagizo ya Kamanda wa Polisi?

Njoo wewe uwalazimishe Polisi kama unaweza, mbona umejichimbia tu?

Njoo wewe uingie barabarani ufanye maandamano, mbona unawachombeza wenzako tu? Watu kama wewe huwezi kuwakuta hata siku moja kwenye maandamano, umekaa mafichoni huku unawachombeza wenzako. Mbona hatukuoni kuwaambia CCK wafanye maandamano?
 
Hata wewe unasupport vurugu?

Hivi wewe kila maandamano ni vurugu na hasa yapofanywa na Chadema....chadema imeprove kuwa ikifanya maandamano yake hata kama itakuwa na zaidi ya watu 20,000 na kusiwepo na polisi wala sungu sungu huwa hakutokei na vurugu yoyote, Kova analake jambo...
 
Ccm na polisi chanzo cha vurugu,. Chadema hawanaga vurugu mpaka uwavuruge,. Nchi yetu wote hi kwanini polisi mtunyanyase wakati mnaubiri demokrasi kila sku
 
Huu ndio ufataani wako nnaousema mimi mara kwa mara. Sasa wewe Kamanda wa Polisi ameshasema wasifanye maandamano, wewe unataka wakafanye maandamo kinyume na maagizo ya Kamanda wa Polisi?

Njoo wewe uwalazimishe Polisi kama unaweza, mbona umejichimbia tu?

Njoo wewe uingie barabarani ufanye maandamano, mbona unawachombeza wenzako tu? Watu kama wewe huwezi kuwakuta hata siku moja kwenye maandamano, umekaa mafichoni huku unawachombeza wenzako. Mbona hatukuoni kuwaambia CCK wafanye maandamano?
Hivi kazi ya Polisi nikusema fanyeni maandano au msifanye..!?
 
Jeshi la polis limepiga marufuka wapenzi wa chadema kufanya matembezi wakati wanaelekea kwenye mkutano wao wa jangwani kesho.

Chanel ten.

Upuuzi mtupu watu wasitembee kwa vipi? mi nafikiri cha msingi ni kuwaachia barabara zao tutatembea pembezoni mwa barabara na njia za kitaa kwa makundi sasa kama wataleta u polisiccm watakuwa wameazimia kusababisha uvunjifu wa amani
 
Mkuu unanipa wasiwasi unaposema walazimishe! How? Wote tuliona yaliyotutokea Arusha. Bado tupo na walemavu ambao hawawezi kushiriki tena ujenzi wa taifa. Ni wanachama wenzetu wa cdm lakini hawawezi kufika kwenye mikutano yetu! Najua inaumiza sana lakini tutafute namna nyingine ya kufanya na sio kuandamana! Hapa naona wanatafuta sababu ya kuvuruga tukio zima. Bila kujipanga na kuweka tahadhari, tutajikuta tunapiga stori za vurugu, majeruhi na maumivu badala ya mafanikio!
Pia kuna mikutano imeandaliwa huko kusini. Wakiweza kusambaratisha kesho, hata hiyo mingine haitakuwa na mafanikio maana itawatia hofu wananchi na ccm watajaza propaganda hapo kuongeza hofu hiyo. Au wataikataza/kupiga marufuku kwa kisingizio cha vurugu tukarudishwa nyuma!
Nakuelewa unalenga nini na faida zake na natumaini utanielewa pia.

Mkuu nakuunga mkono.Viongozi wa CDM waachane na hii habari ya maandamano.Polisi wanatumiwa na CCM ili kuvuruga mkutano wote wa kesho na pia iwe kisingizio cha kuvuruga mikutano ya kusini.Wakati mwingine viongozi wa CDM watumie hekima na busara ili kulinda maslahi yetu wanachama.Hii kuanza kusumbuana na hawa polisi vibaraka wa Magamba kwanza itasababisha wananchi kuingia hofu na kuogopa kuja mkutano.Pia wataanza kukamata viongozi wetu na kuwafungulia mashtaka hali itakayosababisha viongozi wetu kupoteza tena muda wa kwenda mahakamani kitu ambacho polisi na CCM yao watachekelea.Tutashindwa kupata mafanikio tunayotarajia na hii itatupa hasara Sisi huku Magamba wakishangilia.Mbona uzinduzi wa Dr Slaa mwaka juzi hakukuwa na maandamano lakini nchi ilitikisika.Hapa ndipo busara ya viongozi wetu inapaswa kuonekana.Imebaki miaka 3 tu CCM kuondoka madarakani na haya yote yatakuwa historia.
 
Jeshi la polis limepiga marufuka wapenzi wa chadema kufanya matembezi wakati wanaelekea kwenye mkutano wao wa jangwani kesho.

Chanel ten.

some tym ukiwa polisi inawezekana na akili inapungua kwenye folder ya akili,,,,,,nimecheka naposoma hii thread,,,,inamaana watapaaa,au anataka asikike na kuonekana kwamba ameongea,,,,,najiuliza watakaoenda wataendaje?????
 
Kuanzia mwaka Nov/2015 CCM ni chama cha upinzani wana bahati katiba itakuwa imebadilishwa tungeitumia hii kuwanyosha....
 
some tym ukiwa polisi inawezekana na akili inapungua kwenye folder ya akili,,,,,,nimecheka naposoma hii thread,,,,inamaana watapaaa,au anataka asikike na kuonekana kwamba ameongea,,,,,najiuliza watakaoenda wataendaje?????
Anataka wakodi malori kama CCM inavyofanya...
 
Back
Top Bottom