Mkutano wa Jangwani Mei 26: Polisi walumbana na CHADEMA!

kumbe bado Polisi wanahizo propaganda? makamanda wa Alshabab wameuliwa juzi juzi
 
Ni kupitia chanel ten habari,anasema cdm wameomba mkutano na si matembezi.anasema polisi watadil na mtu individual atakaetembea na mguu kuelekea jangwani.IVI DAR WOTE WANA MAGARI?
 
Tuache ushabiki na tufuate taratibu, kilichoombwa ni mkutano na kibali kimetolewa sasa suala la maandamano linatoka wapi? wakati kila mtu natoka nyumbani kwake?

Jamani tubadilike!!! why maandamano si kila mmmoja anatoka kwake kwenda kwenye Mkutano sasa maandamano yanatoka wapi? Please wakati tunakubali mabadiliko tusiache hisisa zitutawale.

Wanzania wote wasio magamba na magamba twendeni tukasikie wawakilishi wetu wametuandalia kauli ipi ya matumaini. Maandamano ya nini sasa.
 
No publicity is bad publicity. Kadri police wanavyozidi kupiga makelele ya kuzuia haya maandamano ndivyo ujumbe unawafikia watu wengi kwamba kesho Jangwani kuna 'shughuli'

NB: Hakuna haja ya kusubiri katiba mpya, wabunge wa CHADEMA waanzishe harakati za kutunga muswada utakao badilisha utaratibu wa ajira kwenye sehemu muhimi kama polisi, usalama na mahakama. Watu wahojiwe na wasiwe chini ya ofisi ya rais kama ilivyo sasa. Ni lazima tuwe na polisi huru, TISS huru, na mahakama huru.
Tofauti na hapo tusahau amani na utulivu.
 
Kamanda Kova amezuia maandamano ya aina yeyote kufanyika kesho kwa mkoa wa Dar,sababu ni zile zile za uvunjifu wa amani.
Ameruhusu mkutano tu nakusema watashughulikjia mtu mmoja mmoja atakae kiuka agizo hilo.
Source.Channel ten

vuvuzela la magamba hilo.nilijua tu lazima abwabwaje.
ni ufinyu wa kufikiri kila wakati mtu ufikiri vurugu tu km wewe si mtu wa vurugu pia.
kama hamjui
kova alikuaga kibaka.ndio maana anawaza,analala na kuota vurugu tu.
 
Kamanda Kova amezuia maandamano ya aina yeyote kufanyika kesho kwa mkoa wa Dar,sababu ni zile zile za uvunjifu wa amani.
Ameruhusu mkutano tu nakusema watashughulikjia mtu mmoja mmoja atakae kiuka agizo hilo.
Source.Channel ten

yeye ndo source ya vurugu. Whats a big deal kuwaacha watu wanaotembea kwa amani toka majumbani mwao kuelekea kaatka mkutano. Yote kwa yote na kwa namna yoyote maandamano yatazuiliwa lakini uwanja utajaa sana. Kitu ambacho nadhani kamanda kova na askari wake watakachozuia ni 'maandamano ya kurejea majumbani' hata kama wao watakuwa kwa idadi kubwa kiasi gani
 
Nimefurai aliposema mutu mmoja akiandamana atakiona, hivi atajuaje kwamba nipo kwe maandamano ya peke yangu.!labda angesema atakaekutwa na bango barabarani ndio ata dili nae.!
 
Nimefurai aliposema mutu mmoja akiandamana atakiona, hivi atajuaje kwamba nipo kwe maandamano ya peke yangu.!labda angesema atakaekutwa na bango barabarani ndio ata dili nae.!

swadakta hili ndilo la muhimu!
 
Ironically incredible news."Vyama vya msimu...""CHADEMA wako kaskazini tu..."CHADEMA hawawezi kuja pwani... Pwani ni ngome ya CCM...."So why all these force and heavy hand in dealing with CDM?
 
  • Thanks
Reactions: FJM
CDM wakikubali kuzuiwa wamekwisha!! Wawalazmishe polisi kutoa ulinzi..

Tena utakuwa ndiyo mwanzo wa mwisho wa M4C. Watu hawawezi kufika Jangwani kwa parachutes, ni lazima watembee kwa makundi kuelekea jangwani. Polisi naona wanataka kuvunja amani kwa kuanzisha vurugu.

CDM you have upper hand maeneo yote mliyofanya maandamano na mikutano yamekuwa na amani mpaka pale polisi wanapoanzisha vurugu. Nchimbi aangalie katika kuchanganya siasa na utendaji wizara itamshinda muda si mrefu.
 
Kamanda Kova amezuia maandamano ya aina yeyote kufanyika kesho kwa mkoa wa Dar,sababu ni zile zile za uvunjifu wa amani.
Ameruhusu mkutano tu nakusema watashughulikjia mtu mmoja mmoja atakae kiuka agizo hilo.
Source.Channel ten


nafikiri sasa Dar Es Salaam ina kamannda wa polisi kilaza kuliko wakati wowote huko nyuma.
 
Maandamano ni haki ya kila raia wa nchi hii ili mradi havunji sheria.
 
MMM

si lazima kuandamana, sauti za Jangwani tu zatosha kuamsha waliolala

Mkuu kinachopiganiwa hapa si maandamano ila Polisi kukiamulia chama halali cha siasa chenye haki zote za kuendesha shughuli za siasa nini cha kufanya, hiyo si kazi ya polisi. Kazi yao ni kulinda maandamano na kumchukulia hatua mtu yeyote anayevunja sheria wakati wa maandamano. Wakitaka kuvunja maandamano kwa nguvu basi watakuwa wanaibadili Dar polepole into Arusha. Kitendo hiki cha polisi kinaisaidia CDM zaidi kama kilivyoisaidia CDM Arusha.
 
Duh hapa kuna shida. Sijui kama waliomba kibali cha kuandamana. Lakini inaweza kutokea kwamba watu walikuwa wanakunywa kahawa pale fire na baada ya hapo wakainuka wakiwa katika kikundi cha watu kama kumi hivi na kuamua kwenda mkutanoni jangwani kwa miguu; haya nayo ni maandamano? Watu wakiwa wanatoka buguruni wakashuka pale mapipa bila kujuana lakini wote labda 20 wakaamua kutembea kwa amani kwenda jangwani haya nayo ni maandamano? Basi itabidi CDM waandae ma fuso. Wakiwa kwenye mafuso wamejazana si itakuwa kuvunja sheria za barabarani? Kizungumkuti.
 
Ni wakti muafaka polisi hasa vijana ndan ya jeshi la polisi kubadilisha hawa wazee. Kova anaogopa kuambiwa...mzee umekosea! Mkiwa wadogo,baba yako anaweza akakwambia lolote ata liwe baya wewe ni kutekeleza.ukifkisha miaka 18,baba anaanza kushauliana na wanawe na watoto mnakuwa part of any decision withn ur family.kova ajue kuwa watoto wake si wa miaka 5 bali ni wa miaka 18 hadi wengne wana mnvi.vyama vya ushindani si watoto tena bali ni watu wazima anaopashwa akae nao ili wapange kwa pamoja.kama hoja ni kuwa hakuna maandamano,je kama watu wataamua kuandamana na kwa wingi polisi wa kuwazuia atawatoa wapi?akili za kuamlishwa achanganye na zake!
 
Back
Top Bottom