Mkutano wa Jangwani Mei 26: Polisi walumbana na CHADEMA! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkutano wa Jangwani Mei 26: Polisi walumbana na CHADEMA!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by n00b, May 24, 2012.

 1. n00b

  n00b JF-Expert Member

  #1
  May 24, 2012
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 952
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 60
  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


  KURUGENZI ya Ulinzi na Usalama ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) inapenda kutoa taarifa kuwa matembezi ya wanachama wake kutoka maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam kuhudhuria mkutano mkubwa wa hadhara utakaofanyika Viwanja vya Jangwani, yako pale pale kama ilivyopangwa na kutolewa taarifa kwa Jeshi la Polisi.

  Itakumbukwa kuwa mkutano huo wa hadhara utakaofanyika Mei 26, 2012 umeshakamilisha taratibu zote, ikiwemo kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi, ambalo tayari limesharidhia kushiriki kwa kutoa ulinzi kwa mkutano huo, siku hiyo ya Jumamosi.

  Katika barua yetu ya Mei 23, 2012, kwenda kwa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, tulisema kuwa kutokana na hamasa kubwa ambayo imejitokeza kwa wanachama wetu juu ya mkutano huo mkubwa wa hadhara, katika majimbo yote ya jiji na kutokana na hali halisi ya ugumu wa maisha unaowakabili wananchi wengi unaopelekea kutomudu gharama mbalimbali za maisha zikiwemo za usafiri (nauli za mabasi) wamejipanga kufanya matembezi ya amani, ya mshikamano, kuhudhuria mkutano wa Jangwani.

  Katika mazungumzo na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam leo, tumeona dhahiri kuwa jeshi letu linajenga hoja dhanifu zaidi na kufanya kazi kwa mtindo wa kupiga ramri badala ya kufanya kazi kisasa kwa kutumia hoja yakinifu zenye mantiki, katika kutimiza jukumu lao kubwa la ulinzi na usalama wa raia na mali zao.

  Ni vigumu kwa mtu yeyote makini kuweza kukubaliana na hoja za Jeshi la Polisi kuwa hawataki wananchi watembee kwa amani kutoka maeneo mbalimbali kwenda eneo la mkutano eti tu kwa sababu kunaweza kuibuka vitendo vya ukabaji, uporaji katika matembezi hayo! Huku ni kufanya kazi kwa mtindo wa kupiga ramri!

  Kumbukumbu zinaonesha kuwa hakuna maandamano yoyote ya CHADEMA yamewahi kuwa na vurugu au vitendo vyovyote vile vya uvunjifu wa amani isipokuwa tu pale ambapo Jeshi la Polisi liliingilia kati na kusababisha vurugu, likapiga watu, likatesa watu hata kusababisha vifo kwa visingizio na hoja zisizokuwa na msingi kama hizi wanazotoa sasa, huku wakitumia lile maneno yao maarufu 'taarifa za kiintelijensia'.

  Pamoja na madai ya jeshi hilo kuwa hakuna askari wa kutosha kulinda matembezi hayo ya amani na mshikamano, kutokana na mantiki hiyo hapo juu, hatutashangaa wakipatikana askari wengi wa kuanzisha vurugu, kupiga watu, kutesa na hata kusababisha vifo, kama ambavyo imetokea katika maeneo mengine kwa kisingizio cha kuzuia maandamano.

  Imetokea hivyo Arusha, imetokea hivyo Songea (Ruvuma), imetokea hivyo Ikwiriri, Rufiji, ambako Jeshi la Polisi lenyewe limekiri wazi kabisa kuwa lilikuwa chanzo cha vurugu hata wananchi kupoteza maisha. Imetokea hivyo sehemu mbalimbali ambako polisi hudai hawana askari wa kutosha kuwalinda wananchi na mali zao, lakini wanapatikana askari wengi wakati wa kuvuruga na kupiga watu hata kusababisha vifo.

  Tunawaomba ndugu zetu wa Jeshi la Polisi watoe ushirikiano kwa wananchi. Wasifanye kazi kwa ubaguzi wa aina yoyote ile katika makundi mbalimbali ndani ya jamii wala maelekezo ya kisiasa, hasa kutoka kwa chama tawala, CCM kama ambavyo imedhihirika mara kwa mara.

  Tunapenda kusisitiza kuwa polisi wasifanye kazi kwa mtindo wa kupiga ramri na kujenga hoja dhanifu. Wanachama na wapenzi wa CHADEMA wamedhihirisha mara kadhaa, pasi na shaka yoyote kuwa wanaweza kufanya matembezi ya mshikamano bila kuathiri haki za watu wengine. Kwa amani na utulivu.

  Tutaendelea kuthibitisha hivyo Mei 26, 2012, kuelekea Jangwani na mahali pengine popote ambapo tutatumia haki ya kikatiba kufanya matembezi ya mshikamano au kuandamana katika misingi ya kutoa elimu ya uraia kwa wananchi, kudai haki, mabadiliko ya kweli katika utawala na mfumo, kudai uwajibikaji wa serikali kwa watu au katika kupiga vita ufisadi na uonevu wa watawala dhidi ya wananchi.

  Imetolewa leo Mei 24, 2012 Dar es Salaam na;

  Wilfred Muganyizi Lwakatare
  Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama-CHADEMA
   
 2. Mwakalinga Y. R

  Mwakalinga Y. R Tanzanite Member

  #2
  May 24, 2012
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 2,718
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Hii ni habari njema CDM2015
   
 3. Tumaini Makene

  Tumaini Makene Verified User

  #3
  May 24, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 2,617
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Wakati najiandaa kuondoka ofisini muda si mrefu usiku huu, Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama amenitumia nakala ya barua ya Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam iliyosainiwa na Andrew E.J. Salum-ACP, kwa niaba ya Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, ambayo sehemu yake inasema;

  "Kwa hiyo kufuatia taarifa za Kiitelijensia za Polisi tulizonazo tumebaini kuwa kitendo cha wanachama kutoka kila pembe ya Jiji kwa madhumuni ya kufanya maandamano kutaleta vurugu jambo ambalo litasababisha shughuli mbalimbali za jiji kusimama kwa sababu ya maandamano hayo.

  "Kamanda wa Polisi Kanda Maalum D'Salaam anatoa ushauri kwa dhati kwamba mfanye mkutano badala ya maandamano."

  Wakuu kwa wale ambao wako nyuma kidogo ya mjadala huu ni kwamba chama kupitia Kurugenzi ya Ulinzi na Usalama, kiliandika barua kuitaarifu polisi kuwa wanachama wengi na wapenzi wa CHADEMA wamehamasika sana kuhudhuria mkutano wa Jangwani ambao utafanyika Mei 26, 2012, Jumamosi, lakini kutokana na ukata unaosababishwa na hali ngumu ya maisha, wengine hawawezi kumudu gharama za maisha vyema, ikiwemo nauli za usafiri kwenda Jangwani.

  Hivyo wanachama kutoka maeneo ya Ukonga, Ilala, Kawe, Temeke, Ubungo, Kigamboni, Kinondoni watatembea kwa amani na mshikamano kwenda eneo la mkutano.

  Taarifa za mkutano walishazipata. Wakazipokea kwa mikono miwili. Hakukuwa na tatizo. Wakatoa ushirikiano, ikiwemo kutoa ulinzi siku hiyo. Zilipokwenda taarifa za matembezi ya wananchi kutoka maeneo mbalimbali kwenda Jangwani, oooh! Nongwa. Wakapagawa. Hatuna askari wa kutosha, ooh kutakuwa na ukabaji na uporaji, ooh kutakuwa na vurugu na ukosefu wa amani, oooh! Sababu za kudhania chungu nzima. Ndiyo hizo zinazofanana upigaji wa ramri. Tawire.

  Kinachozua mjadala hapa si mkutano. Ni wananchi kuruhusiwa kutembea kwa amani na mshikamano kwenda eneo la mkutano. Mkutano huo mkubwa wa hadhara utakaofanyika Jangwani hauna tatizo. Upo. Mbali ya kutumika kuliamusha Jiji la Dar es Salaam juu ya vuguvu la mabadiliko, mkutano huo utakuwa na madhumuni mengine kadhaa kama vile kuzindua rasmi kitaifa Kampeni ya Vuguvu la Mabadiliko, Movement for Change (M4C), kujadili mstakabali wa taifa katika mchakato wa maoni ya uandikaji wa katiba mpya.

  Tunatoa wito kwa wananchi kuhudhuria kwa wingi katika mkutano huo ambapo viongozi wakuu wa Chadema na wabunge mbalimbaliwatazungumza na wananchi wa Dsm kutoa ujumbe maalum kuhusu mabadiliko na nafasi ya D'salaam katika kuwezesha uwajibikaji nchini, katika kushughulikia changamoto za kiuchumi, kisiasa na kijamii zinazolikabili taifa.

  Aidha tofauti na CCM ambayo imeanza mchakato wa katiba mpya kwa kujifungia na kutoa misimamo ya mamlaka za chama bila hata maoni ya wanachama wake nchi nzima, CHADEMA itatumia fursa hii kuanza mchakato wa kutoa elimu ya uraia kwa umma juu ya katiba mpya na sheria ya mabadiliko ya katiba ili kuwezesha umma kumiliki mchakato, taifa lipate katiba mpya na bora badala ya katiba mbovu.  Makene
   
 4. Bado Kidogo 2015

  Bado Kidogo 2015 JF-Expert Member

  #4
  May 24, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 207
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  CCM wanapagawa bure tu, kwani hao watu hata wakija kwa usafiri wao wakati wa kurudi wakiamua kufanya maandamano itakuwaje?

  Waache uoga, ingekuwa CCM ndiyo yenyewe inapaswa kufanya hivyo basi wangechekelea na kujigamba kama wanavyojiita magamba!!!!
   
 5. F

  FJM JF-Expert Member

  #5
  May 24, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Jeshi la Polisi hawaoni aibu kutumia neno 'intelligensia? What intellegensia? Huu ni uchovu.
  Kwanza nani anahitaji ulinzi wa hawa polisi? Wakae nyumbani waone kama hata mende atakanyagwa.
   
 6. K

  Kiumbo JF-Expert Member

  #6
  May 24, 2012
  Joined: Feb 4, 2012
  Messages: 561
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  tunashukuru kwa wapenda maendeleo wote. Daima mbele.
   
 7. s

  sweke34 JF-Expert Member

  #7
  May 24, 2012
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 2,533
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  hapa inabidi kukomaa tu na huo mkutano maana naona endapo cdm watafanya hayo matembezi ya amani kuna mazingira fulani yanaandaliwa na polisi ili huo mkutano usifanyike kabisa...!
   
 8. Bado Kidogo 2015

  Bado Kidogo 2015 JF-Expert Member

  #8
  May 24, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 207
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Halafu maandamano haya yanafanaa kabisa na yale ya Arusha. CCM hofu yao ilikuwa ni M4C iishie huko huko kaskazini, kuona imetinga jijini kihoro juu kama mume anayesubiri mkewe aliye labour ajifungue.
   
 9. z

  zamlock JF-Expert Member

  #9
  May 24, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  mimi nilifanya vyema kununua skafu yangu arusha nitaitinga shingino nakwenda kuwasikiliza viongozi wangu
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  May 24, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Na CDM wakiback down wamekwisha; wawalazimishe polisi kufanya kazi yao - kutoa ulinzi.
   
 11. E

  Elizabeth Dominic Platinum Member

  #11
  May 24, 2012
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 4,547
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Aisee! Sa miye nsiye na nauli nitafanza nini? Hakuna mjadala njia yetu wengi ya kufika ni kutembea....ni crime nayo?
   
 12. m

  mpigilie JF-Expert Member

  #12
  May 24, 2012
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 306
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Bila polisi hata mchanga utakanyagwa kwa amani
   
 13. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #13
  May 25, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,606
  Trophy Points: 280
  Ninaisubiri kwa hamu sana hiyo jumamosi ifike tuone mwamko wa wapenda mabadiliko jijini Dar,kazi itakuwa si ndogo kabisa,Magamba wana kazi sana na uchaguzi ujao wajipange hasa la sivyo ijiandae kuwa chama cha upinzani!!
   
 14. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #14
  May 25, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,445
  Likes Received: 19,813
  Trophy Points: 280
  nyie mnadhani polisi na ccm yao wanapata raha kutokana na hii mikutano?
   
 15. Boniface Evarist

  Boniface Evarist JF-Expert Member

  #15
  May 25, 2012
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 1,100
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Gob bless tanzanians, God bless Chadema.
   
 16. chitalula

  chitalula JF-Expert Member

  #16
  May 25, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,307
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  me nasubiri tamko tu la chadema maandamano yanaanzia wapi maana nshachoka na kauli za hawa polisi
   
 17. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #17
  May 25, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  ha!,ha!,ha!.....vijana wa mwema wanapagawa weeee!!msihofu bwana raha ya maandamano ni kushiriki na raha ya ngoma nikuingia kucheza hivyobasi njooni polisi wote mvue magwanda ya polis mvae haya ya chadema ambayo yana AC,....teh,teh,teh sipati picha jinsi ambayo wako wanafanya mazoezi kwa ajili yetu.peopleeeeees.......powerrr
   
 18. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #18
  May 25, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,583
  Trophy Points: 280
  Si unawajua polisi wa magamba Mkuu!? Wanaweza kufanya kila hila kuzuia mkutano huu kwa niaba ya magamba.
   
 19. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #19
  May 25, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Inaumiza sana kwa kweli. Wakati sumatra inaitisha mkutano wa wadau juu ya kupandisha nauli za daladala, wananchi hawana nauli ya kwenda kwenye mkutano wa siasa. Sijui tutasukumwa hadi kwenye kona hadi ukuta uanguke?
  I'm really hurt! Aibu kwa chama tawala, kinachoangalia 'habari za kiintelijinsia'
   
 20. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #20
  May 25, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,953
  Likes Received: 1,277
  Trophy Points: 280
  kitaeleweka tu
   
Loading...