Joyce joyce
JF-Expert Member
- May 23, 2020
- 457
- 1,973
Yani Jana nimefuatilia mkutano wa CCM jana, kiukweli nimegundua kuwa vikao vyote vya CCM vya sasa vimekosa mvuto Kabisaaa, hiii ni kutokana na namna vinavyoendeshwa, haihitaji akili kugundua kuwa Mwenyekiti ndie muamuzi wa kila kitu na wajumbe wanaenda tu kwa kutimiza takwa la kuitwa Kamati, mfano Mwenyekiti alileta hoja ya kusamehewa Kinana. Ukiangalia alivyoileta inaonesha kuwa hata alipofukuzwa atakuwa aliileta yeye maaana alianza kwa nini ameileta kisha akauliza wajumbe mnakubali wajumbe? Wachache wakasema ndio akaaanza kumuongelea Saana Kinana, namna alivyokuwa anamuongelea watoto wa mjini tunasema ni kinafiki wakati inaonesha ndio yeye aliemfukuza.
Pili alipoulizwa issue ya wapinzani kupewa nafasi na kuwaacha wanaCCM watiifu yeye hakulitaka lijadiliwe wala kutaka litolewe maoni, matokeo yake alionesha wazi kuwa Jambo hilo linasimamiwa na yeye yaani yeye ndie aliesema kuwa wapewe wapinzani, Mwenyekiti alionesha dhahiri kuwa Jambo hilo haliwezi kubadilishwa na kidogo akasirike.
Hii inaonesha kuwa maaamuzi yoooote Yanayohusu CCM anayo mtu mmoja tu sio kamati wala wajumbe, hii imerudisha CCM nyuma Sana, CCM ilikuwa na mfumo mzuri sana na inaonesha kuwa kwa sasa ili uwe Mbunge wa CCM itakulazimu uwe na ukaribu wa hali ya Juu na mtu mmoja tu Mwenyekiti, hii tabia alikuwa nayo Mbowe ila sasa kwa sasa anaonekana ni afadhali kuliko huyu Mwenyekiti.