Mkutano wa jana wa CCM, mtoa hoja mmoja muamuzi mmoja

Joyce joyce

Senior Member
May 23, 2020
111
1,000
Yani Jana nimefuatilia mkutano wa CCM jana, kiukweli nimegundua kuwa vikao vyote vya CCM vya sasa vimekosa mvuto Kabisaaa, hiii ni kutokana na namna vinavyoendeshwa, haihitaji akili kugundua kuwa Mwenyekiti ndie muamuzi wa kila kitu na wajumbe wanaenda tu kwa kutimiza takwa la kuitwa Kamati, mfano Mwenyekiti alileta hoja ya kusamehewa Kinana. Ukiangalia alivyoileta inaonesha kuwa hata alipofukuzwa atakuwa aliileta yeye maaana alianza kwa nini ameileta kisha akauliza wajumbe mnakubali wajumbe? Wachache wakasema ndio akaaanza kumuongelea Saana Kinana, namna alivyokuwa anamuongelea watoto wa mjini tunasema ni kinafiki wakati inaonesha ndio yeye aliemfukuza.

Pili alipoulizwa issue ya wapinzani kupewa nafasi na kuwaacha wanaCCM watiifu yeye hakulitaka lijadiliwe wala kutaka litolewe maoni, matokeo yake alionesha wazi kuwa Jambo hilo linasimamiwa na yeye yaani yeye ndie aliesema kuwa wapewe wapinzani, Mwenyekiti alionesha dhahiri kuwa Jambo hilo haliwezi kubadilishwa na kidogo akasirike.

Hii inaonesha kuwa maaamuzi yoooote Yanayohusu CCM anayo mtu mmoja tu sio kamati wala wajumbe, hii imerudisha CCM nyuma Sana, CCM ilikuwa na mfumo mzuri sana na inaonesha kuwa kwa sasa ili uwe Mbunge wa CCM itakulazimu uwe na ukaribu wa hali ya Juu na mtu mmoja tu Mwenyekiti, hii tabia alikuwa nayo Mbowe ila sasa kwa sasa anaonekana ni afadhali kuliko huyu Mwenyekiti.
 

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
1,465
2,000
Magufuli ni kama ameshazijua akili za wale wajumbe, anajua chochote atakachosema lazima watakubali, japo hufanya hivyo kama kutoa wazo, lakini binafsi anajua hakuna wakumpinga, na kama aina za wajumbe ndio wale waliojaa mipasho mpaka wanaume, wacha awaendeshe tu anavyotaka.
 

pakaywatek

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
3,804
2,000
Ndiyo umegundua leo! Wewe huoni yupo kwenye kikao cha CCM na jeshi limevalishwa sare ya chama? Magufuli karoga hadi akili za wanaCCM zimesinyaa yule mzee aliyeuliza swala la upinzani huenda alijiapiza kuwa lazima akaulize kwanini wanaCCM wamesinyaa hivyo.
 

Lord denning

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
1,771
2,000
Mwaka huu ndo mtaona subottage halisi ya wana CCM halisi dhidi ya Chama Chao.

Mwaka huu ndo mtaona wana CCM wanasuport upinzani mchana kweupe huku wakipinga ubabe wa viongozi wao.
Ndo mana nasisitiza hakuna mwaka ambao ni rahisi katika kuiondoa CCM madarakani kama mwaka huu.

Upinzani unahitaji kuhamasisha nguvu ya umma tu katika kupiga kura, kulinda uhesabuji wa kura na kulinda utangazaji wa matokeo.
 

Lord denning

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
1,771
2,000
Magufuli ni kama ameshazijua akili za wale wajumbe, anajua chochote atakachosema lazima watakubali, japo hufanya hivyo kama kutoa wazo, lakini binafsi anajua hakuna wakumpinga, na kama aina za wajumbe ndio wale waliojaa mipasho mpaka wanaume, wacha awaendeshe tu anavyotaka.
Matokeo atakayoyapata magufuli na wenzake kutoka huko field mwaka huu ndo atajua kuwa hajui na ubabe sio dili
 

Pohamba

JF-Expert Member
Jun 2, 2015
22,699
2,000
Gwajima na Mbowe walipochukua ngawira za Masai ili agombee Urais alishirikisha vikao vya chama kubariki au kujadili?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom