Mkutano wa injili wa mwakasege;arusha kulipuka tar 28jan-5feb 2010

Mungu akupe moyo uhudhurie maana utapata mengi ila jitahidi uhudhurie hata siku moja tuu...be blessed
 
Mimi niliiona mkutano wa Arusha kwa luninga nikiwa Morogoro kupitia Star TV siku ya Ijumaa na Jumamosi. Bahati mbaya sauti haikutoka vizuri na haswa Jumamosi sauti haikusikika kabisa. Watu wengine niliongea nao wakiwa Dar walisema walikuwa wanasikia vizuri, sasa sijui kwa nini Morogoro sikuweza kupata sauti. Niliporudi Dar Jumapili tarehe 7 ndio ilikuwa siku ya mwisho, nilimsikia vizuri sana kupitia Star TV. Ujumbe mmoja wapo muhimu nilioupata ni kwamba kufanya dhambi huondoa uwepo wa Mwenyezi Mungu, hivyo tujitahidi kufanya maombi ya toba ili kuongeza uwepo wa utukufu wa BWANA.
 
Nilibahatika kumwona live kupitia star TV siku ya Jumamosi kulikuwepo na udhihirisho wa nguvu za Mungu usio wa kawaida.Mungu ambariki mtumishi wake huyu.
 
Back
Top Bottom