Mkutano wa IMF ndani ya Dar es Salaam | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkutano wa IMF ndani ya Dar es Salaam

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by KiuyaJibu, Mar 9, 2009.

 1. KiuyaJibu

  KiuyaJibu JF-Expert Member

  #1
  Mar 9, 2009
  Joined: Aug 29, 2007
  Messages: 769
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  Mkutano wa International Monetary Fund(IMF) yaani shirika la fedha duniani unafanyika jiji Dar es salaam,Tanzania kesho tarehe 10.03.2009 ambapo utawashirikisha mawaziri wa fedha na magavana wa benki kuu za Afrika.

  Wakati mkutano huo unafanyika,taarifa zilizopatikana zinaonyesha kwamba Policy Support Instruments zilizomo ndani ya IMF ndiyo hizo hizo zilizomo katika mpango/programme ya MKUKUTA ndani ya serikali ya Tanzania na mpango huo ambao uko katika utekelezaji wake;binafsi na baadhi ya watu wameanza kuutilia mashaka baada ya kugundulika sera zimehamishwa kama zilivyo katika makablasha ya IMF. Wakati serikali(TZ) inadai kwamba hiyo ni sera ya nchi!

  Mojawapo ya udhaifu huo ni kudai uchumi wa Tanzania umeendelea kukua kwa asilimia saba(7%) tokea mwaka 2000;wakati hali halisi ya maisha ya Watanzania haiendani na ukuaji wa uchumi wenyewe.Takwimu zinaonyesha kwa kipindi chote hicho maskini wameongezeka kutoka million 11-12 hivi sasa.Na shutuma zinaonyesha kwamba yote hiyo ni kutokana na serikali kukubaliana na kupangiwa utekelezaji wa masuala ya kiuchumi na IMF; kwa upande mwingine inawezekana pia viongozi wetu wanaogopa kusema ukweli wa hali halisi na matatizo tuliyonayo katika nchi yetu.Hii inamaanisha kuna upotoshwaji wa taarifa,ukizingatia IMF yenyewe haifanyi kazi ndani ya serikali husika wao ni wageni lakini kama tukisimama katika ukweli kwa pande zote mbili inaonyesha kutakuwa na hali nzuri tofauti na ilivyo sasa.

  Au kuifukuza IMF isishiriki katika kutupangia mambo ya kufanya na kuyatekeleza kama ilivyofanya nchi ya Zambia,ambayo sasa imepata ahueni baada ya kulikacha shirika hili la kimataifa.

  Hebu semeni wenyewe tunafaidika vipi kama kuna nchi zinalikacha shirika hili halafu sisi bado tunalikumbatia na umaskini unaongezeka ukilinganisha na hizo nchi nyingine!?
   
  Last edited by a moderator: Mar 9, 2009
 2. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #2
  Mar 9, 2009
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,037
  Trophy Points: 280
  Mkuu ni IMF na si IFM
   
 3. M

  MiratKad JF-Expert Member

  #3
  Mar 9, 2009
  Joined: May 2, 2008
  Messages: 294
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakuu mlio Dar, tuelezeni kitakachojiri kwenye hiyo conference. Waziri wetu si atakuwepo, ataleta taarifa gani?
   
 4. Binti Maringo

  Binti Maringo JF-Expert Member

  #4
  Mar 9, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 2,805
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  hahahahaha....kazi kweli kweli!
   
 5. M

  Mwan mpambanaji JF-Expert Member

  #5
  Mar 9, 2009
  Joined: Apr 3, 2008
  Messages: 468
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Hii IMF ni mufilisi ndo wanaotumamaskinisha na hawana nia ya kweli ya maendeleo ya nchi za dunia ya tatu,so solution ni kuachana nao kabisa.Hawana tija kwetu.Daima nasisitiza maendeleo ya kweli yataletwa na sisi watz kwa kila mmoja kuwajibika kwa nafasi aliyoko,na si sera za IMF,BW,wa nchi za nje,tuanze kujiamini sasa na kuwa na sera zetu zinazotokana na utamaduni wetu,vipaumbele vyetu,na asili yetu na si vinginevyo.INAWEZEKANA TIMIZA WAJIBU WAKO
   
 6. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #6
  Mar 9, 2009
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  KiuyaJibu!
  International Monetary Fund (IMF)

  Institute of Finance Management (IFM)
   
 7. R

  Raphsam Member

  #7
  Mar 9, 2009
  Joined: Sep 11, 2008
  Messages: 31
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Kama mambo ni hayo yabidi tuwe makini zisije tolewa taarifa za uongo kuhusu kukua kwa uchumi wa nchi yetu pendwa Tanzania
   
 8. Companero

  Companero Platinum Member

  #8
  Mar 9, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Makala hii inaelezea mantiki ya hizo Policy Support Instruments (PSI): UDADISI: Rethinking in Action: Because the IMF says so?
   
 9. Sabode

  Sabode Senior Member

  #9
  Mar 10, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 159
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Heshima kwa wana JF wote
  Jamani ukuaji wa uchumi mimi naupimia mfukoni kwangu pia. Pamoja na nyimbo zote kwanza global kraisisi naona ina madhala moja kwa moja kwangu halafu nashangaa wakubwa wanabishana na hilo, huo ukuaji wa uchumi siufeel kabisa naona kila kukicha mambo yanazidi kuwa magumu. Anyway acha nisubiri single mpya kutoka conference hii.
   
 10. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #10
  Mar 10, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Mkuu achana na taarifa zinazotolewa na Bretton Wood institutions, angalia hali toka Ben Mkapa alipochukua nchi kutoka kwa Mzee Mwiny na hali iliyopo sasa utaona tofauti kubwa. Nchi yetu sasa hivi inapesa sana, sio serikali maskini tena kama ilivyokuwa kama alivyoichukua mzee Mwinyi kutoka kwa JKN au kama alivyoichukua Ben Mkapa kutoka kwa Mzee Mwinyi, labda tatizo kidogo uchumi umedorora kwenye utawala wa JK, lakini still bado tuko kwenye hali nzuri.
  Tatizo kubwa ni kwamba tumeshindwa kuzitumia vizuri fedha na kuzifikisha mifukoni au kwenye meza za watanzania wanaofanya kazi kufanya tuwe na hizo fedha. Mafisadi wanatuvuruga sana na wanatukwamisha sana. IMF ni wezi tu hawana jipya, watakuja na sera zao za kuwanufaisha wao, sisi wenyewe tunatakiwa kuwa na akili ya ku-deal nao. Kama sasa hivi ukiangalia hata waziri wa fedha hatuna(aliyepo ni ineffective), kwa hiyo utaona kuwa IMF wana easy ride na Tanzania.
   
 11. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #11
  Mar 10, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135

  Subiri usikie atakachokiongea, naweza kusema before hand kitakuwa pumba tu.
   
 12. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #12
  Mar 10, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Tatizo haliko IMF wala world Bank, wao kwa kawaida hushauri serikali na jukumu la serikali husika kukubali ushauri wao au kama wanauona haufai kukataa. Mwalimu Nyerere aliwahi kutofautuana na hizi multilateral institutions; lakini hivi sasa tatizo liko kwa viongozi wetu wa nchi kwa vile ni "VILAZA" wanakubali kila kitu wanachoambiwa na wageni na hawathamini ushauri wa nyumbani!! Tulifika mahali mpaka nchi yetu ilikuwa inamhusudu mtu YEBO YEBO kama George Walker Bush; haya yalikuwa matusi makubwa kwa watanzania tuliokuwa na heshima yetu huko nyuma na hili la kuwaua maalbino ndio limemaliza kabisa heshima yetu duniani!!
   
 13. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #13
  Mar 11, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Umenfurahisha comment yako juu ya waziri wetu wapesa ''Kama sasa hivi ukiangalia hata waziri wa fedha hatuna(aliyepo ni ineffective)'' Ha ha haaaaaaaaaaaaaaa, mkuu JK sialiwaambia uwaziri hausomewi? hivyo mchezo wa ana ana anado unatosha kuchagua mawaziri
   
 14. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #14
  Mar 11, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mkuu acha munkari, nikweli katika dunia tunasema ''there is no free lunch'' lakini mchango wa IMF unahitajika sana si katika nchi masikini bali hata katika nchi zilizoendelea. Hivyo kusema tuachane nao kabisa hiyo siosahihi mkuu wangu.
   
 15. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #15
  Mar 11, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mkubwa mbona unatuchanganya, mara tulikuwa tunamhusudu YEBO YEBO Bush, mara mauwaji ya albino, mara heshima yetu duniani imepungua. Sijakupata unachotaka kuzungumza hapa kuu samahani lakini kwa hilo
   
 16. KiuyaJibu

  KiuyaJibu JF-Expert Member

  #16
  Mar 11, 2009
  Joined: Aug 29, 2007
  Messages: 769
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  Samahani sana Wana-JF wote ni nilikosea(typing error)ukweli ni IMF=International Monetary Fund.
  Hence,save the correction as provided herein.
   
 17. The Farmer

  The Farmer JF-Expert Member

  #17
  Mar 11, 2009
  Joined: Jan 7, 2009
  Messages: 1,581
  Likes Received: 433
  Trophy Points: 180
  Bado tuna safari ndefu sana ya kupambana na huu umasikini, viongozi wetu wengi ni MAFISADI.
   
 18. B

  Bunsen Burner Member

  #18
  Mar 11, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 95
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Guys , tulifutiwa madeni and guess what, our people todate didnt even get any relief on reducing poverty but we only ended up getting these "Generation & Isidingo dramas" of EPAS and etc....!!!
  IMF will not help us unless we kick our corruption scandals and b serious on changing our country into real actions of positive development for everyone to play his/her part get rid of bad apples!!
   
 19. A

  Audax JF-Expert Member

  #19
  Mar 11, 2009
  Joined: Mar 4, 2009
  Messages: 444
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Thats write, we dont have to count on "msamaha wa madeni tu" Na misaaada tunayopata inaishia wapi jamani? Hivi hela aliyotupatai bush hizo barabara watajenga lini? Maana kila cku tunashuhudia sahii tuu,hamna changes,jamani ufisadi ni mbya.Mimi binafsi naumia saana na umaskini wa nchi yetu. Tembalea nchi watu,utalia machozi,barabara ilijengwa ina miaka zadi ya 60 na ipo mpaka leo na ipo imara,sisi ukikaribia uchaguzi wanamwaga changarawe ili wagombea wasipate shida, lkn c wananchi waishio maeneo hayo. Uchaguzi ukiisha wananchi wanaugua magojwa mbalimbali kutokana na vumbi la barabara.Viongozi wa Tz usanii mtaacha lini?
   
Loading...