Mkutano wa Hali ya Siasa Nchini na maazimio yake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkutano wa Hali ya Siasa Nchini na maazimio yake

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pascal Mayalla, Oct 5, 2009.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Oct 5, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,601
  Likes Received: 18,621
  Trophy Points: 280
  Mkutano wa kutathmini hali ya Siasa hapa nchini uliandaliwa na REDET katika ukumbi wa Mkrumah Hall, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam umemalizika rasmi na haya ndio mapendekezo ya mkutano huo.

  Mkutano huo ulikuwa ufunguliwa na rais Jakaya Kikwete, lakini kutokana na hali yake (uchovu), amemtuma waziri Mkuchika kuufungua.

  Katika hotuba ya rais, kama kawaida imejaa habari njema nyingi za utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM kana kwamba hiyo ndio hali ya siasa ilivyo hapa nchini kwa sasa.

  Hata hivyo, hotuba hiyo, haikuzungumza lolote kuhusu hali ya sasa ya Pemba, wala hakuzungumzia tena prospects za muafaka, ama maendeleo yoyote ya kisiasa kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa, au maandalizi ya uchaguzi Mkuu ujao.

  Pia REDET imezindua kitabu kinachochambua kwa kina mustakabali wa Dini na Siasa za Tanzania.

  Mkutano umehudhuriwa na wanasiasa, viongozi wa dini, wanaharakati, wanabalozi wanaoziwakilisha nchini zao humu nchini, wahadhiri, wanafunzi na wananchi wa kawaida.

  Leo ninamalizia kwa kuwaletea majumuisho haya katika hii attachment.
   

  Attached Files:

  Last edited by a moderator: Oct 7, 2009
 2. MawazoMatatu

  MawazoMatatu JF-Expert Member

  #2
  Oct 5, 2009
  Joined: Sep 6, 2008
  Messages: 505
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Shukrani Ndugu Pasco! vp mambo yanaendeleaje sasa!?
   
 3. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #3
  Oct 5, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,601
  Likes Received: 18,621
  Trophy Points: 280
  Kinachoendelea sasa ni presentation ya mada ya 'Nafasi ya Taasisi za Kiraia katika Utawala Ngazi za Chini' inayowasilishwa na Bi Gema Akilimali. Itafuatiwa na pepa mbili za ' Nafasi ya Sekta Binafsi katika Utawala na Maendeleo' zitakazo wakilishwa na Prof. Samweli Mushi na ya pili Iddi Simba.

  Mchana ziliwasilishwa mada 4. moja ya 'Utawala na Maendeleo na Dr. Mohameed Bakari na mada 3 za 'Maboresho ya serikali za Mitaa' zilizowasilishwa na Prof. Athumani Liviga, Alfred Kabagire na Mhe. John Cheyo.

  Kila baada ya kundi la mada, hufuatiwa na majadiliano moto moto.
   
 4. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #4
  Oct 5, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,601
  Likes Received: 18,621
  Trophy Points: 280
  Msishangae nakaa muda mrefu sana kabla sijawaupdate, Nokia E-90 ilinifia, sasa natumia kablackbery Storm kana kichaa, mara kanagoma kabisa kupokea comand yoyote, mara kanajizima hadi kugoma kupokea charger. Kuingia mkutano wa watu na laptop naona noma nijeonekana najifanya sekretariati.

  Nitaendelea hivyo hivyo hivyo kidogo kidogo.
   
 5. M

  Mkandara Verified User

  #5
  Oct 5, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu na wewe acha kununua za machinga haaa! - Lini Nokia na Blackberry zikawana na sm card nne pamoja, ndio hayo Richmond yanakukuta sasa!
   
 6. George Kahangwa

  George Kahangwa Verified User

  #6
  Oct 5, 2009
  Joined: Oct 18, 2007
  Messages: 539
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Nitakuwa makini kusikiliza kama lolote la manufaa litatokana na mjadala huu, itakuwa ni upotevu wa wakati na rasilimali kama mjadala uataishia kuwa maneno yasiyoweza hata kuchana karatasi, ilihali nchi inazidi kulewa kwa ufisadi, uharibifu katika takribani kila sekta na uwepo wa viongozi legelege wa kisiasa.
   
 7. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #7
  Oct 5, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,601
  Likes Received: 18,621
  Trophy Points: 280
  .
  Mzee Mkandara, E-90 na Storm mchina bado mchina hajagusa ila pia lazima tufike mahali tukubali Mchina ni mkombozi fulani hivi, suti 35,000/= nokia 50,000/= blakiberi 90,000/=!.
   
 8. Domenia

  Domenia JF-Expert Member

  #8
  Oct 5, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 462
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  ha mme kosa kazi za kuafanya...manafanya tasimini zenu wenyewe...hakuna kitu...Ratiba kama hizi zinamfanya Raisi achoke...Tasmini gani- mimi mwananchi wakawaida ina nisaidiaje....

  acheni upumbavu...
   
 9. M

  Mkandara Verified User

  #9
  Oct 5, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Sawa mkombozi kwa mwezi mmoja kwa mwaka utanunua simu 4 sawa na moja original itakuchukua miaka 10. Kaka unakumbuka mshindi? zilikuwa original zote na hadi leo kuna watu kibao Bongo wanazo na zinafanya kazi tena makini ile mbaya..wee endelea kumtajirisha Mchina tu, ukombozi wa kijamaa ndio hivyo tena kila siku ni ukombozi wa jana.

  Ebu turushie kinachoendelea haswa maswala muhimu yaliyozungumziwa tutapenda kuchangia mada hizi..Na pengine wambie waingie na warushe moja kwa moja ktk twitter, tutafuatilia.
   
 10. Domenia

  Domenia JF-Expert Member

  #10
  Oct 5, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 462
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ujinga wa wajinga
   
 11. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #11
  Oct 5, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,601
  Likes Received: 18,621
  Trophy Points: 280
  Mjadala wa mada ya 'Nafasi ya Taasisi za Kiraia katika Utawala Ngazi za Chini' iliyowasilishwa na Bi Gema Akilimali na mada mbili za ' Nafasi ya Sekta Binafsi katika Utawala na Maendeleo' zilizowakilishwa na Prof. Samweli Mushi na ya pili Iddi Simba ndio zinazungumzwa.

  Mada ya Iddi Simba na sera zake za Uzawa imeibua mjadala mzito haswa baada ya kueleza kuwa Watanzania ni watazamaji tuu ndani ya game la uwekezaji. Main players ni wageni na ndio wanaokomba faida yote.

  Prof. Mushi amesema serikali yote ni ya mafisadi na yote inanuka rushwa, ila pia sekta binafsi inayoshamiri, ni walezi wazuri wa hiyo rushwa ya serikali kwa sababu watoaji ni sekta binafsi, wapokeaji ni serikali.

  Sasa hivi Ramadhani Madabida ndio anachangia, amejitambulisha kama mjasiliamali mmiliki wa kiwanda cha madawa na mjumbe wa NEC wa CCM. Kwanza anaitetea serikali kuwa sio kweli serikali yote ni ya mafisadi yote inanuka rushwa. Amekiri kuna maofisa wa serikali wamejihusisha na ufisadi na rushwa at individual level.

  Sasa Iddi Simba anahitimisha hoja zake
   
 12. Domenia

  Domenia JF-Expert Member

  #12
  Oct 5, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 462
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ok....labda lakini no proper system
   
 13. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #13
  Oct 5, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,601
  Likes Received: 18,621
  Trophy Points: 280
  Simba anaunguruma kuhusu udumavu wa akili za Watanzania akiitaka REDET ifanya utafiti kuhusu kwanini Watanzania tumedumaa kiakili katika maendeleo ya uchumi.

  Pia anamjibu Mpesya kuwa waliopigania uhuru wa nchi hii ni watu walala hoi, wasomi hawakuruhusiwa kujiunga kwenye siasa. Baada ya uhuru, wengi wa viongozi waliopata ulaji baada ya uhuru hawakuwa wasomi, unategemea nini kwa kiongozi Lumpen ploretariat kuongoza na kusimamia maendeleo yaliyokuwepo.

  Concetration ya Mwalimu ilikuwa ni kujenga umoja wa kitaifa na sio kuleta maendeleo.

  Simba anasema udumavu wa akili ndio adui yetu mkuu, wanasiasa ni wajinga wajinga tuu, wasomi wenye akili wanaogopa siasa.

  Simba anaomba radhi kwa Watanzania wote kuwa sheria mbaya ya madini ilipitishwa akiwa bungeni, anaomba radhi kwa hilo. Bunge linaletewa sheria za kiingereza, huku bunge limegubikwa na wabunge vihiyo ambao hawawezi kuzitafsiri sheria hizo.

  Kitendo cha Iddi Simba kuomba radhi kumepokewa kwa makofi ukumbi mzima.
   
 14. Domenia

  Domenia JF-Expert Member

  #14
  Oct 5, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 462
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  na wao wenyewe wane dumaa..
  What da hell are You waiting for...
   
 15. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #15
  Oct 5, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,601
  Likes Received: 18,621
  Trophy Points: 280
  Simba amesema kitenda cha kuingiza ubinafsishaji ilikuwa ni kubadili sera toka ujamaa mpaka ubebari kulikochukua dakika 45 tuu, ujamaa dead, ubepari juu, likabakia jina tuu la Ujamaa kwenye katiba.

  Ubinafsishaji ulimnufaisha nani, kulikuwa hakuna sekta binafsi imara ya wazawa wenye uwezo na uzoefu, matokeo yake ndio haya, karibu viwanda vyote vilivyobinafsishwa kwa wazawa ni ama muflish ama kwishnei
   
 16. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #16
  Oct 5, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,601
  Likes Received: 18,621
  Trophy Points: 280
  Prof. Mushi anajibu hoja na kukiri kuwa wasomi wamelikosea sana taifa hili kwa kutojadili kwa kina suala zima la ubinafsishaji. kunahitajika kufanya mabadiliko makubwa kabisa katika sera zote ili kutoka hapa tulipo, tuweze kusonga mbele.
   
 17. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #17
  Oct 5, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,601
  Likes Received: 18,621
  Trophy Points: 280
  Bi Gema Akilimali, anaigema akili mali yake kwa kiishambulia CCM kuwa haikubali jambo lolote zuri toka kwa wapinzani.
  Pia amewakandia wapinzani kuwa hawana sera, kazi ni kupiga makelele tuu. Amesifu taasisi za kiraia kuibua mijadala mbalimbali.

  Prof Bana anahitimisha mjadala wa siku ya leo.
   
 18. M

  Mkandara Verified User

  #18
  Oct 6, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Shukran sana mkuu wangu lakini pamoja na yote haya - What happened in Vegas!.......
  Kwa wasomi wetu maelezo mengi na kunyoosheana vidole wakati wao ndio wanatakiwa kuwa mstari wa mbele ktk harakati za mageuzi.
  Baada ya mkutano huu, hawa wote hatutawasikia tena hadi baada ya uchaguzi mwakani wakiponda tena matokeo.
   
 19. K

  Koba JF-Expert Member

  #19
  Oct 6, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  Sina hamu na hao so called wasomi wa mlimani,niliwashangaa sana wakati wa ile mikutano yao kuhusu dual citizen majority walikuwa wanapinga(sio vibaya) lakini kwa sababu walizokuwa wanatoa nilibaki mdomo wazi,wengi wa wasomi wetu ni big disappointment!
   
 20. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #20
  Oct 6, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Sasa kama hawawezi kusema hali ya pemba na kutoa Tamko huko wanafanya nini Mkutano, Mambo kama Katiba mpya, Tume huru ya uchaguzi na mambo ya kuwa fair election ni jambo nzuri kabisa la kuongelea kwenye mkutano wetu
   
Loading...