#COVID19 Mkutano wa hadhara na Mpira wa hadhara kipi ni hatari kwa maambukizi ya Covid 19?

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
7,354
2,000
Tanzania ni yetu sote hebu tuutangulize utanzania na Mungu mbele.

Tunapofikiria kuzuia maambukizi ya Covid 19 kwa kuzuia mikutano ya kisiasa tufikirie pia kuzuia maambukizi kwenye viwanja vya mpira wa miguu kwakuwa watu ni walewale.

TFF kupeleka mechi ya Simba na Yanga Kigoma kwenye uwanja mdogo sana maana yake kusiwepo na distancing Kati ya watazamaji. Hakuna shabiki wa Simba na Yanga anayeweza kushangilia na barakoa mdomoni. Watu wataanza kuingia uwanjani masaa mengi kabla ya mechi, hivyo hakuna atakaeweza kunywa maji na kula uwanjani bila kutoa barakoa yake mdomoni.

Kama kwenye mpira wanaruhusiwa bila shaka hata kwenye mkutano wa siasa inaswihi pia. Shida ni nini?
 

michosho

JF-Expert Member
Mar 17, 2012
545
500
Pale dar mbona mpira ulichezwa na Hakuna shida?

Acha watu waendelee na maisha yao bana.

Atakayejiona afya Yake hairuhusu, abaki ndani na akachanje!
 

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
9,308
2,000
Hii nchi ina mambo ya kijinga sana! Kuna umuhimu wa kuhamia Burundi haraka iwezekanavyo.
 

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
7,354
2,000
Tena mkutano wa ndani ni hatari kuliko mpira wa miguu
Nchi hii tutairarua wenyewe kwa itikadi za win-lose na uhatimiliki. Tangu tulipokubaliana kujenga shule nyingi za msingi, secondary, vyuo na vyuo vikuu vingi nchini maana yake ndio tumekubaliana pia kupunguza iadadi ya wajinga na kuongeza idadi ya watu werevu na wajuaji nchini. Tusifanye mazoea sisi sio tofauti na wengine duniani.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom