Mkutano wa Godbless Lema - Kahama, Shinyanga 28 April, 2015

ka-picha tafadhali.

Ndg wana JF na watanzania kwa ujumla, leo kutakuwa na mkutano mkubwa sana wa hadhara wa Chadema hapa kahama maeneo ya CDT. Mbunge wa Arusha mjini kamanda mpambanaji Godbless Lema atakuwepo kuwajaza ujasiri watu wa huku. Pia ataambatana na m/kt wa Bavicha taifa kamanda Patrobass K.Paschal.

Kama ilivyoada ya JF iliyojaa wawakilishi kila kona ,itakuwa nawe moja kwa moja toka eneo la mkutano.
Ungana nami Sir. E.J.Buyamba, m/kt wa vijana jimbo la Msalala mkoani Shinyanga nikiwa na makamanda wengine kibao ktk kuhakikisha hakiharibiki kitu.
Karibuni sana!!.
 
mkuu na wasiwasi hako kajimkutano kao kamedoda. wanaona aibu kutupia japo kapicha. chezea sumu ya zitto weye. yaelekea lema alifikiri anafanya mkutano kule kwa machalii arusha!

ALIANZA MNYIKA , KAFUATA MBOWE ; KAENDA MH LEMA

KABAKI MH IBRAHIMU LIPUMBA;

SOMO HALIJAELEWEKA; WATU MKOA WAOTE NI ACT-WAZALENDO


huu muziki ndo unawatia wenge si tupo Dar; Tuankuja baada ya ya operation fyeka msitu , sasa ni operation andaa palizi
attachment.php
 
  • Thanks
Reactions: R.B
Sasa inabidi nikubaliane na kauli ya Mzee Tupatupa wa Lumumba "CHADEMA ACHENI SIFA"

Maana hii nchi inaongozwa kwa mfumo wa vyama vingi, na kama Chadema watakuwawanafanya siasa kila mahali hapa nchini na kuchukuwa watu wote, Je! hii si sifa na ni dhuluma kabisa maana vyama vingine vimeshindwa kufanya siasa kwasababu siasa ni watu na watu wote wamechukuliwa na Chadema.

cc Mzeetupatupa wa lumumba njoo huku tuiseme Chadema ili iache sifa.
 
Linaweka habari halafu halitoi mrejesho hata ka-picha tu hakuna! Majitu mengine sijui yakoje!!
 
Ndg wana Jf, taarifa zilizotangazwa hapa na katibu wa wilaya ni kuwa kamanda Lema kapata ajali wakati anakuja kahama. Kwa hiyo amekwama kuja leo.
 
habari za ubunge wasahau kabisa

walidhani tutahaibika mungu ni mwema; tunamaombi ya wabunge majimbo yote

1.wazalendo
2.wanaoomba nafasi ya ukimbizi ;baaada ya kutoswa na vyama vyao ccm, chadema, lakini tutawapokea kama wanakubali falsafa za mwalimu julius kambarage nyerere
3. Wapenzi wa damu wa zitto na wananchama wa act
4. Wapiganaji wa ufisadi na demokrasia ktk vyama
 
Wamesema jembe lema hatakuwapo kwani wakati anatoka mwanza amepata ajari kwenye gari alilokuwemo limepasuka tairi la mbele na kuingia mtaroni amepelekwa bugando.
watu wametawanyika na mkutano umefungwa.
pole kamanda lema
 
Linaweka habari halafu halitoi mrejesho hata ka-picha tu hakuna! Majitu mengine sijui yakoje!!

Mkuu nimesema pc yangu imegoma kurusha picha. Kama unaweza(hii ni kwa yeyote) ni pm namba yako ya whatsaps nikutumie ili uzipost hali ilivyokuwa.
 
zitto hawezi kupata ubunge nchi hii , hakuna mahali hawajui kuhusu usaliti wake , hicho ndio usichokijua .

mawazo yako wewe na bavicha;
uliza uambiwe watu wanapiga simu ; vijana graduate wapinga ufisadi
umebaki wewe na mbowe wenu kung'ang'ania madaraka kama nkurunzinza ahalfu unasema nkurunzinza kaa miaka 10; mbowe kakaaa miongo mingapi? Miaka 10 na ngapi?

Shame to young generetaion ; underating other young leader like zitto
 
mtahangaika sana lakini ukweli unabaki palepale kuwa ACT imewashika sehemu nyeti. mmebaki kulalama tu humu. kama huo ubunge huwa mnatoa nyinyi mko sahihi lakini kama kila mmoja anashiriki mtashangaa hiyo october. tukutane oktoba.

bwt mbona hamna hata kapicha? au kumedoda?

Habari za ubunge wasahau kabisa

kwanza muulize wamepata wanachama wangapi ?

Najiuliza kila siku hivi act ndio mdudu gani huyo?
 
picha ziMETUMWA makao makuu
wanaedit kwa adobephoto shop WATU 110 WALIOUDHULIA ; ilikuweka za uchaguzi wa 2010 ; zitto alipokuwa kwenye kampeni za kunadi dr slaa

soon 'watazieka baada ya kuongeza umati wa watu;
Mdogo wangu yupo buzwagi ananiambia Zitto kashafua hali ya hewa.

Nsikia Mbowe alikimbia kaenda vijiji vya itilima na Bukoba amabapo zitto hakufika.

soon CHADEMA WIIL DIE
 
Mkuu ni pm basi wasap namba yako nikurushie picha ili uzibandike hapa. Hawa vitukuu wa ccm wanaweza chonga sana ili hali wanajua kabisa mtu huwezi jisingizia ajali kwa sababu isiyo ya msingi kama hii.

Sasa hayo ya picha mkuu tuyaache tufuatilie afya ya kamanda wetu! Nani sasa anatupatia maendeleo ya afya yake? MUNGU AMSIMAMIE APONE HARAKA!
 
Back
Top Bottom