(Mkutano wa FOCAC wa Dakar) Fursa Mpya za Ushirikiano kati ya China na Afrika (1): afya, uchumi wa kidigitali na maendeleo ya kijani

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
1128113735_16382045757441n.jpg
Mkutano wa 8 wa mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC ulifanyika tarehe 29 na 30 mjini Dakar, Senegal. Rais Xi Jinping wa China hapa Beijing amehudhuria ufunguzi wa mkutano huo kwa njia ya video na kutoa hotuba akisema, China na Afrika zimetoa mfano wa kuigwa katika kujenga uhusiano wa kimataifa wa aina mpya, na anaamini kuwa mkutano wa Dakar utahimiza ujenzi wa hali ya juu wa jumuiya yenye hatma ya pamoja kati ya China na Afrika.


Katika miaka 21 iliyopita, FOCAC imefungua ukurasa mpya wa ushirikiano wa kunufaishana kati ya China na Afrika na kukuza uhusiano kati ya pande hizo uendelee kufikia kwenye kiwango kipya. Kutokana na athari mbaya za janga la COVID-19, mabadiliko ya hali ya dunia yanazidi kuwa mengi. Ili kujenga jumuiya yenye hatma ya pamoja kati ya China na Afrika katika zama mpya, rais Xi Jinping amesisitiza kuwa pande hizo mbili zinapaswa kushirikiana kupambana na virusi vya Corona, kuimarisha ushirikiano wa kivitendo katika sekta mbalimbali ukiwemo uchumi wa kidigitali, kuhimiza maendeleo ya kijani pamoja na kulinda usawa na haki. Zikiwa sekta kuu zilizotajwa na rais Xi, “afya, uchumi wa kidigitali na maendeleo ya kijani” vinatarajiwa kuwa fursa mpya za ushirikiano kati ya China na Afrika katika siku za baadaye.

China na Afrika kujenga jumuiya ya afya na matibabu yenye hatma ya pamoja


1638239970491.png

Chanjo ya China dhidi ya COVID-19 yawasili Zimbabwe na kupokelewa na rais wa nchi hiyo


Miaka ya hivi karibuni, ushirikiano wa afya na matibabu kati ya China na Afrika umeendelezwa kwa kasi baada ya kutajwa kwenye “mipango 10 ya ushirikiano” na “mapendekezo makuu manane ya utekelezaji” kwenye utaratibu wa FOCAC. Janga la COVID-19 lililofika ghafla limekuwa mtihani mkubwa kwa binadamu, lakini pia limeonesha umuhimu wa wazo la kujenga jumuiya ya afya na matibabu yenye hatma ya pamoja kati ya China na Afrika. Rais Xi Jinping wa China alipohutubia ufunguzi wa mkutano wa nane wa mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika uliofanyika mjini Dakar, Senegal alisema, China na Afrika zinatakiwa kupambana na virusi vya Corona kwa pamoja, kuhakikisha upatikanaji na bei nafuu ya chanjo barani Afrika na kuziba “pengo la kinga mwili”.


Mapema mwaka 2020, wakati China ilipokumbwa ghafla na virusi vya Corona, ilipokea salamu na uungaji mkono kutoka nchi zaidi ya 50 za Afrika, na hata kuna nchi zenye taabu za kiuchumi zilitoa msaada wa fedha kwa China. “Akufaaye wakati wa dhiki ndiye rafiki wa kweli”, wakati Afrika ilipokumbwa na janga hilo, mara moja China ilianza operesheni kubwa ya msaada wa dharura unaozifikia nchi 53 za Afrika na Umoja wa Afrika, kwa kutoa vifaa tiba na fedha, pamoja na kupeleka wataalam wa afya.


Kwenye mkutano maalum wa wakuu wa mshikamano wa kupambana na janga la COVID-19 kati ya China na Afrika uliofanyika mwezi Juni mwaka jana, rais Xi Jinping wa China alipendekeza kujenga “jumuiya ya afya na matibabu kati ya China na Afrika”. Pendekezo hilo sio tu limeonesha urafiki wa jadi kati ya pande hizo, bali pia litainua ubora wa ushirikiano wa afya na matibabu kati yao. Katika mwaka zaidi ya mmoja uliopita, China imesaidia nchi za Afrika kupambana na COVID-19 na pia kujitahidi kuziwezesha zitimize usawa wa afya katika siku za baadaye.


Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Ofisi ya uratibu wa Masuala ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa OCHA, mwaka 2020, asilimia 74 ya ufadhili wa China ulio wa utaratibu wa pande nyingi wa kupambana na ugonjwa huo ulielekezwa kwenye nchi moja moja, kati yao asilimia 93.72 ikienda katika nchi za Afrika. China imejitahidi kutekeleza ahadi yake ya kufanya chanjo kuwa bidhaa ya umma, na kutangulia kutoa msaada wa chanjo kwa nchi za Afrika, na hadi sasa imetoa chanjo milioni 200 kwa Afrika. Kwenye mkutano wa Dakar wa FOCAC, rais Xi Jinping ameahidi kuwa ili kusaidia Umoja wa Afrika kutimiza lengo la asilimia 60 ya watu wa Afrika kuchanjwa ifikapo mwishoni mwa mwakani, China itatoa dozi nyingine bilioni 1 kwa Afrika, na kati ya hizo milioni 600 zitatolewa bure, na nyingine milioni 4 zitatolewa kupitia uzalishaji wa Pamoja kati ya kampuni za China na nchi za Afrika. Hivi sasa Algeria, Misri na Morocco zinajitahidi kuzalisha chanjo ya China. Pamoja na chanjo zinazozalishwa ndani ya China zinazowasili Afrika, China inaweza kujenga “kinga imara ya chanjo” kwa watu wa Afrika.



Wahenga wanasema “Ni bora ufundishwe kuvua samaki kuliko kugaiwa samaki. Rais Xi Jinping pia amesema China itasaidia nchi za Afrika kutekeleza miradi 10 ya matibabu na afya, na kutuma wahudumu wa matibabu na wataalam wa afya Afrika wapatao 1,500. Tarehe 26, mwezi huu, ujenzi wa sehemu ya kwanza ya mradi wa makao makuu mapya ya Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa cha Afrika (Africa CDC) ulikamilika, na kabla ya hapo, hospitali ya mama na watoto ya Senegal na jengo la magonjwa ya kuambukiza la hospitali ya taifa ya Mauritius lililojengwa kwa msaada wa China pia lilikabidhiwa. Imefahamika kuwa baada ya mradi mzima wa Africa CDC kukamilika, kitakuwa ni kituo cha kwanza cha kudhibitii magonjwa chenye ofisi na vifaa vya kisasa na mazingira bora ya kufanya utafiti.



Kusaidia nchi za Afrika kujenga mfumo bora wa afya ya umma unaoweza kukabiliana na dharura kunalingana na Ajenda ya 2030 ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa inayotaja “kuhakikisha maisha ya afya na kuleta ustawi wa watu wa rika zote” na Ajenda ya 2063 ya Umoja wa Afrika kuhusu lengo la kutokomeza magonjwa ya kitropiki, kudhibiti magonjwa ya kuambukiza na kuongeza muda wa maisha ya watu, kwa hivyo hii itakuwa sekta muhimu ya ushirikiano kati ya China na Afrika. Janga la ugonjwa limethibitisha kuwa China na Afrika siku zote zinashirikiana katika sekta ya afya na matibabu. Inatarajiwa kuwa pande hizo zitatumia mkutano wa nane wa mawaziri wa FOCAC kama mwanzo mpya na kuchangia juhudi zaidi katika ujenzi wa jumuiya ya afya na matibabu kati ya China na Afrika.

1638239861516.png
 
Back
Top Bottom