Mkutano wa chadema reading, wanachama wengi wa ccm kurudisha kadi

Chilisosi

JF-Expert Member
Oct 19, 2008
3,051
747
[h=3]CHADEMA KUWASHA MOTO KATIKA MJI WA READING SIKU YA TAREHE 26/08/2012[/h]



LONDON
Ili kufikia malengo yetu ya kuzunguka kwenye Miji mbalimbali ya UK kuhamasisha Watanzania waishio uk kujiunga na Chadema, kueneza kampeni ya m4c na kufungua matawi mengine, Tawi la Chadema London linapenda kuwatangazia Watanzania wote waishio katika Mji wa Reading na maeneo ya jirani kuwa kutakuwa na mkutano mkubwa wa M4C UK utakao fanyika Tarehe 26/08/2012 siku ya Bank holiday.

Dhumuni la mkutano huo ni kuwahamasisha Watanzania waishio UK kujiunga na chama, kushiriki katika harakati za mabadiliko, kusajili wanachama wapya, kuchagua wawakilishi wa muda kutoka mji wa Reading pamoja na kuanzisha mfuko wa kufa na kuzikana kwa manufaa ya watanzania wote.

Tumekusudia kuanzisha Mfuko wa kufa na kuzikana kwa sababu mpaka hivi sasa Mtanzania akifariki akiwa UK hakuna taasisi wala ofisi yoyote inayotoa msaada. Jukumu ambalo kwa muda mrefu Serikali yetu kupitia ubalozi umelipuuzia na kushindwa kulisimamia na kulishughulikia.

Mfuko huu utasaidia katika kumsafirisha Marahemu na Mfiwa pamoja na kusaidia kushughulikia matatizo na usumbufu utakaojitokeza baada ya mtu kufariki dunia na kusaidia matatizo mbalimbali yakiwemo majanga ya dharura.


Pia katika mkutano huo wanachama mbalimbali wa CCM walio na uchungu na nchi yetu na wanaopenda maendeleo na mabadiliko ya kweli watapewa nafasi ya kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo kama sehemu moja wapo ya kampeni yetu ya Kuvua Gamba na Kuvaa Gwanda ukiwa Ughaibuni.


Mkutano utafanyika siku ya Tarehe 26/08/2012, Kuanzia saa saba mchana mpaka saa kumi na mbii jioni.

Risc Reading International Solidarity Centre,
35-39 London Street,
Reading, RG1 4PS



Watanzania wote, marafiki na wadau mbali mbali wa maendeleo na mabadiliko ya kweli mnakaribishwa sana.
Huu ndio wakati wa mabadiliko, kusimama na kusema tumechoka!

KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NA;

MWENYEKITI: Chris Lukosi 07903828119,


KATIBU MWENEZI: Chris Chagula 07405889880
au
Tutumie email kupitia chademauk@gmail.com

HATULALI MPAKA KIELEWEKE!!!!!!!!!!!

Peooooople's Power

 
Hivi na hao wa UK wanapigia kura wapi, kurudi bongo yenyewe ni tabu,si unajua tena visa za magumashi. Mimi naona CCM na CDM wanapoteza wakati tu na hao jamaa. Kwanza hata mchango wao ni michuma ilio zidi miaka 10. Ushuru wake ni mkubwa kuliko uzima wa gari.
 
Chilisosi naweza kupata friji za mitumba na vijiko huko uingereza nipe bei zake kwa jumla.
 
Huku TZ tunajiandaa kuingia Magogoni 2015. Vilevile tunapanga kuweka mifumo bora ya Sheria 2016 kabla ya kuwatia mbaroni Kikwete, Chenge, Rostam, Mkapa, Karamagi, Mkullo, Ritz, Rejao na Mafisadi Wengine Wote.
Chilisosi naweza kupata friji za mitumba na vijiko huko uingereza nipe bei zake kwa jumla.
 
Mpaka wajibebe miccm
mwaka huu.....

peoplesssssss....... power

V
SENGEREMA
 
Safii, safi sana. Mwaka huu mpaka Nape atuongezee posho vijana wake wa Lumumba, maana harakati za M4C zinapiga kotekote.
 
Safii, safi sana. Mwaka huu mpaka Nape atuongezee posho vijana wake wa Lumumba, maana harakati za M4C zinapiga kotekote.
Nimepata habari ambazo bado hazijathibitishwa kuwa Ritz na NAPE wameamua kuja kuhudhuria huu mkutano na watarudisha kadi zao za CCM
 
Nimepata habari ambazo bado hazijathibitishwa kuwa Ritz na NAPE wameamua kuja kuhudhuria huu mkutano na watarudisha kadi zao za CCM

aibu sana kwa chama chetu. gamba kubwa ndani ya ccm ni NAPE. huyu mtu ndiye anayekivuruga chama chetu
 
Chilisosi naweza kupata friji za mitumba na vijiko huko uingereza nipe bei zake kwa jumla.
RITZ ,mmebanwa na MBEKO hamna pa kupumulia wala pa kukimbilia.na bado mtaongea kila lugha
 
Nimepata habari ambazo bado hazijathibitishwa kuwa Ritz na NAPE wameamua kuja kuhudhuria huu mkutano na watarudisha kadi zao za CCM
hiyo post ilikuwepo humu naona imepotezwa na wazee wa mabwepande
 
Nasikia Ni kwelli nape anawatafuta waandaaji wa mkutano ili akaribishwe
 
Back
Top Bottom