Mkutano wa CCM wazomewazomewa Serengeti

Mwl Ryoba

Member
Oct 28, 2011
55
31
leo ccm na mbunge wao kebwe wamefanya mkutano hapa serengeti ambao ni mkutano wao wa pili tangu uchaguzi uishe. viongozi wa ccm waliokuwepo ni chand-mneki,mbunge na wengine.

Mkutano huu umefanyika kwa sababu jana chadema walifanya mkutano mkubwa sana ambao ulihutubiwa na aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la serengeti mwl marwa chacha na mwkt wa vijana Wilaya ya trm chacha heche. Hoja za mwl marwa ambaye kwa sasa ni diwani wa kata ya stendi kuu ni kama ifuatavyo.

1. Madiwani wa ccm kujichukulia zabuni zote za miradi mbalimbali ikiwemo ukusanyaji wa ushuru kwenye minada na masoko pamoja na kujenga majengo na makalvati ambayo yako chini ya kiwango na tayari kuna hoja ya CAG.

2.madiwani kushiriki zoezi la uchakachuaji wa pembejeo.

3.kuna makampuni yanayokwepa kulipa vshuru wa zaidi ya 1bilioni yakisaidiwa na baadhi ya madiwani wa ccm ambao kwa sasa ni matajiri sana mfano diwani wa nata.

4.kutoza ushuru wa mbogamboga na matunda ambao uliishaondolewa waziri mkuu bungeni.

5.kutumia milioni mia mbili kila mwaka kulipanaposho
 
Mkuu embu fafanua zaidi kuhusu:
1/Kwa nini wazomewe?
2/Nini hasa walichokiongea?
3/Mahudhurio yalikuwaje?
4/Reaction yao baada ya kuzomewa?
5/Picha?
 
hawa CCM na viongozi wake katika haka kawilaya kenye asali kibao ni manyangau,mfano ni huyu cjui CHANDI MARWAambae ni mnec ndo anahusika na uchimbaji madini ndani ya hifadhi,yeye ndo aliinfluence hata wale jamaa wa TISS na OCD wa wilaya wakanasa kwenye mtego wa KIJAZI WA TANAPA,WALIVOKAMATWA MWANZONI MWA MWAKA HUU WAKICHIMBA MADINI NDANI YA HIFADHI.rejea madai ya mwenyekiti wa halmashauri na wizi wa mabillioni,kilaza CHANDE kujipa tender zote hasa za ujenzi wa barabara na makalavati,yeye ndo consultancy na ndo enginear mkuu wakati ni std seven failure,
 
Wala hawaoni taabu hao, wameshazoea kuzomewa. Mbona hata rais wao anazomewagwa?
 
Hivi kwa nini Redio za Tanzania hazisikiki kwa Upande wa Zanzibar? tangu mambo ya Uamsho yaanze husikii Redio yoyote ya Tanzania, bali Redio za kiislamu kama Radio imaan na ile ya morogoro tu. hata Tbc au R1 hamna. kuna uwezekano kwamba wamefungiwa?
 
Nyinyi walimu ndo mnachangia elimu kushuka wewe badala ya kufundisha unakalia mikutano ya ccm, au na wewe umenyimwa tenda na hao madiwani?
 
huyo diwani wa Natta Jummanne Kwiro, elimu hana lakini anaujua ufisadi balaa
 
huyu chandi si ndiye yule mwenye duka la hard ware pale mugumu namfahamu sana ametymia nafasi yake ya uhuni huo kujinifaisha
 
hawa CCM na viongozi wake katika haka kawilaya kenye asali kibao ni manyangau,mfano ni huyu cjui CHANDI MARWAambae ni mnec ndo anahusika na uchimbaji madini ndani ya hifadhi,yeye ndo aliinfluence hata wale jamaa wa TISS na OCD wa wilaya wakanasa kwenye mtego wa KIJAZI WA TANAPA,WALIVOKAMATWA MWANZONI MWA MWAKA HUU WAKICHIMBA MADINI NDANI YA HIFADHI.rejea madai ya mwenyekiti wa halmashauri na wizi wa mabillioni,kilaza CHANDE kujipa tender zote hasa za ujenzi wa barabara na makalavati,yeye ndo consultancy na ndo enginear mkuu wakati ni std seven failure,
Hivi kesi ya hawa jamaa ilimalizwa vipi?
 
Mkuu embu fafanua zaidi kuhusu:
1/Kwa nini wazomewe?
2/Nini hasa walichokiongea?
3/Mahudhurio yalikuwaje?
4/Reaction yao baada ya kuzomewa?
5/Picha?

Sure bro..jamaa aleta uzi nusunusu kama anakimbizwa bwana..daahh!!
 
kwanini wamezomewa au ilikuwaje, je unaweza kutuwekea picha za pande zote mbili? Na kusema chandi ndiye mchimbaji mkubwa serengeti na ndiye aliyeshirikiana na ocd na afisa usalama kwenda kuchimba ndani ya hifadhi unao ushahidi?
 
Mwl Ryoba sikutarajia kama wewe ni kilaza kiazi hiki. sasa hapa umeandika nini? mbona hueleweki? na huo uandishi wa habari huko chuoni unafundishaje. ewe mungu nakuomba hii thread isiwe imeletwa na yyule ayub ryoba anayefundisha.
 
Last edited by a moderator:
kwanini wamezomewa au ilikuwaje, je unaweza kutuwekea picha za pande zote mbili? Na kusema chandi ndiye mchimbaji mkubwa serengeti na ndiye aliyeshirikiana na ocd na afisa usalama kwenda kuchimba ndani ya hifadhi unao ushahidi?
Hawa waalimu hawaaminiki saana,njaa inaweza kumfanya mtu aseme uongo.Sidhani kama ana ushahidi juu ya madini mbugani.Serengeti bado haijapata mtu wa kupambana na ccm.Jamaa arudi tu akafundishe,no more.
 
Bila shaka na wewe umefundishwa na mwalimu aliyeleta aliyeleta mada hii.

Unless unaniambia unamaanisha nini kwa kusema 'hawa waalimu'
 
sikutarajia kama ryoba ni kilaza kiazi hiki. sasa hapa umeandika nini? mbona hueleweki? na huo uandishi wa habari huko chuoni unafundishaje. ewe mungu nakuomba hii thread ise imeletwa na yyule ayub ryoba anayefundisha.

Hebu nichekie huko kajiunga lini mi natumia Tecno.
 
wewe kuna ayoub rioba anaefundisha udsm na mwenye mada hii ni marwa ryoba ni x mwl tarime sec
 
Similar Discussions

3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom