BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,086
Mkutano wa CCM kutumia bil. 2/-
na Martin Malera, Dodoma
Tanzania Daima
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kinatarajia kutumia zaidi ya sh bilioni 2 kama gharama za Mkutano Mkuu unaoanza leo mjini hapa.
Vyanzo vya habari vya kuaminika kutoka ndani ya CCM, vilisema kuwa fedha hizo zinajumuisha pia zilizotumika kwa ajili ya ukarabati wa Ukumbi wa Kizota, utakaotumika kwa ajili ya mkutano huo.
CCM ililazimika kuyafanyia ukarabati mkubwa majengo ya Kizota baada ya ukumbi wake maarufu wa Chimwaga kutolewa na serikali kutumika kwa ajili ya Chuo Kikuu cha Dodoma ambacho kimeanza hivi karibuni.
Kwa mujibu wa habari hizo, fedha hizo pia zinatumika kwa ajili ya kulipa posho za wajumbe zaidi ya 1,700 wa mkutano huo, kulipia gharama zao za malazi, usafiri na matumizi mengine.
Hata hivyo, kiasi hicho cha sh bilioni mbili na ushehe ni nyingi ukilinganisha na fedha ambazo kwa kawaida zimekuwa zikitumika kwa ajili ya mikutano kama hiyo siku za nyuma. Kwa mfano, Mkutano Mkuu uliopitisha jina la mgombea urais kupitia chama hicho uliofanyika Mei 2005, haukugharimu zaidi ya sh bilioni 1.5.
Kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika vya habari, fedha hizo zimetokana na ruzuku ya zaidi ya sh milioni 500 inazopata CCM, miradi mbalimbali ya chama, wafadhili na baadhi ya wanachama wenye uwezo kifedha.
"CCM inapata ruzuku ya zaidi ya sh milioni 500, ina vyanzo vingi vya mapato, ina wafadhili na hata wanachama wenye uwezo na nia ya kukichangia. Kwa hiyo ni sahihi kabisa kutumia kiasi hicho na wala watu wa habari msichukulie kuwa kiasi hicho sawa na kufuja fedha za walipa kodi. Huu ni mkutano mkubwa wa chama tawala na watu wengi wamealikwa kushuhudia," alisema mmoja wa maofisa waandamizi wa CCM ambaye aliomba asitajwe jina.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mkutano huo, Kapteni Jaka Mwambi, aliahidi kutoa gharama halisi za mkutano huo baada ya mkutano na kuongeza kuwa swali la matumizi ya fedha za mkutano huo si la siri.
Maandalizi ya mkutano huo yamekamilika, huku mji wa Dodoma ukiwa umefurika wajumbe wa mkuano huo, wengi wakiwa wamevaa nguo zenye rangi ya sare za CCM za kijani kibichi, njano na nyeusi.
Kutokana na idadi kubwa ya wajumbe na wapambe wao pamoja na kikao cha Bunge kinachoendelea mjini hapa, nyumba za kulala wageni zimefurika na imefika hatua baadhi ya wateja wa nyumba hizo kuamshwa usiku na kutakiwa kufunga virago kwa madai kuwa CCM ilishakodi nyumba zote za wageni kwa ajili ya wajumbe wake.
Tofauti na siku zilizopita, kampeni za uchaguzi huo zimeingia sura mpya mwaka huu, kwani magari ya wagombea mbalimbali yanaonekana yakiwa yamepambwa na picha zao, mabango yamebandikwa kila mahali na hata kwenye nguzo za umeme, vipeperushi vinatolewa hata kwa wapita njia wasio wajumbe wa mkutano huo.
Kampeni kubwa zimekuwa zikiendelea kwenye baa, mahoteli makubwa na hata kwenye kumbi za burudani ambako wapambe wamekuwa wakizunguka na vipeperushi vya wagombea wao.
Hata hivyo, suala kubwa linalovuta hisia za watu wengi ni nani atajaza nafasi za Makamu Mwenyekiti wa chama hicho kwa upande wa Tanzania Bara na Katibu Mkuu, ambako inasemekana kuwa Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete huenda akatangaza majina ya sekretarieti mpya baada ya ile aliyoitangaza muda mfupi baada ya kuchaguliwa kuwa mwenyekiti mwaka jana.
Majina ya John Samuel Malecela, Yusuf Makamba, Edward Lowassa, Abdulrahman Kinana na Frederick Sumaye ni baadhi ya majina ambayo yamekuwa yakitajwa na wajumbe wengi wakiwapa nafasi ya kukamata nafasi hizo za uongozi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na CCM mjini hapaa, chama hicho tawala kama ilivyo ada, kimealika mabalozi wa nchi mbalimbali nchini, marafiki na wenyeviti wa vyama vya upinzani ambao wameandaliwa ndege maalum ya kuwachukua na kuwarejesha Dar es Salaam.
Kutokana na kupanda kwa joto la uchaguzi huo, mahudhurio ya kikao cha Bunge kinachoendelea mjini hapa, yamedorora, kwani wabunge wengi ni wagombea, hivyo wako katika hatua za mwisho za kufanya kampeni.
Mkutano huo wa CCM utasimamiwa na Spika wa Bunge, Samuel Sitta, akisaidiwa na Spika wa Baraza la Wawakilishi, Pandu Ameir Kificho.
Maspika hao watasaidiwa na Mweka Hazina wa CCM, Rostam Aziz, Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM, Emmanuel Nchimbi, wote wakiwa wajumbe wa Kamati Kuu.
Kamati Kuu jana haikukaa mjini hapa, kwani tayari ilishakaa jijini Dar es Salaam, pamoja na mambo mengine, kuandaa ajenda za mkutano huo yakiwemo mabadiliko madogo ya katiba ya CCM ambayo sasa inataka kutoa nafasi za upendeleo kwa baadhi ya wazee maarufu kuwa wajumbe wa kudumu wa NEC.