Mkutano wa CCM Jangwani: Usafiri Upo (Mabasi na Fuso)

Kashaijabutege

JF-Expert Member
Oct 20, 2010
2,696
740
Imefahamika kuwa kila matawi mawili ya CCM katika Jiji la Dar es salaam yatapatiwa basi moja, iwapo wangepeleka ombi lao kabla ya leo (Ijumaa) saa 7. Ili kufanikisha mkakati huo wa kutoa usafiri, makada wenye mabasi na malori wametakiwa kujitolea magari yao, ukiwa kama mchango wao kwa Chama. Aidha, viongozi wote wa mashina, vitongoji, mitaa, kata, wilaya na mkoa, kwa tiketi ya CCM wametakiwa kuhudhuria bila kukosa; labda kwa udhuru usioweza kuzuilika. Mitaa mingine wajumbe na wakereketwa wameombwa kuchangia walau shilingi elfu moja kwa ajili ya kukodi magari ya kuwapeleka na kuwarudisha mikutanoni.

Matawi yamehamasishwa kuandaa mabango yenye ujumbe wa kukiponda chama cha CHADEMA na vyama vya upinzani kwa ujumla.

Source: Rafiki yangu ambaye ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa (lakini anaipenda sana CHADEMA)
 
Uzuri wa kanga manyoya yake, Uzuri wa CCM ufisadi wake ..... CCM OYEEEE

Source: Bango, mwenge, Dar es salaam, Tanzania
 
Ni kweli maana jana jioni wajumbe wa nyumba kumi KATA YA MAKUBURI walikutana kupewa maelekezo ya kuwatafuta watu wa kwenda jangwani kwenye mkutano huo. Ninapokaa external walikutana Mabibo/Makuburi S/M magari wameambiwa watafute ya gharama ndogo yale yaendayo MAKOKA ili watu wa maeneo hayo watumie usafiri huo, lakini kuna tetesi kuwa walishapelekwa kwenye mikutano ya Jangwani kwa magari wakati wa kurudi wakaambiwa wajitegemee.
 
Mama mwenye nyumba wangu ni balozi wa ccm , asubuhi nimetoka tu nje nikamkuta getini akaniuliza kesho una shughuli gani nilijua nia yake nikamwambia niko busy sana si unajua kesho ni siku yangu ya kupumzika, nikamuacha hapo nje anashangaa.
 
Ndugu zangi maswali madogo: -
1. Lengo la mkutano nini nini?
2. Je utarushwa live ili nasi wa mbali tuone?
Nashukuru.
 
Kuna bango wameweka kwenye mataa Mwenge " uzuri wa kanga manyoya na uzuri wa CCM ni sera zake"
 
Imefahamika kuwa kila matawi mawili ya CCM katika Jiji la Dar es salaam yatapatiwa basi moja, iwapo wangepeleka ombi lao kabla ya leo (Ijumaa) saa 7. Ili kufanikisha mkakati huo wa kutoa usafiri, makada wenye mabasi na malori wametakiwa kujitolea magari yao, ukiwa kama mchango wao kwa Chama. Aidha, viongozi wote wa mashina, vitongoji, mitaa, kata, wilaya na mkoa, kwa tiketi ya CCM wametakiwa kuhudhuria bila kukosa; labda kwa udhuru usioweza kuzuilika. Mitaa mingine wajumbe na wakereketwa wameombwa kuchangia walau shilingi elfu moja kwa ajili ya kukodi magari ya kuwapeleka na kuwarudisha mikutanoni.

Matawi yamehamasishwa kuandaa mabango yenye ujumbe wa kukiponda chama cha CHADEMA na vyama vya upinzani kwa ujumla.

Source: Rafiki yangu ambaye ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa (lakini anaipenda sana CHADEMA)

attachment.php
 
Matawi yamehamasishwa kuandaa mabango yenye ujumbe wa kukiponda chama cha CHADEMA na vyama vya upinzani kwa ujumla. Source: [COLOR=#FF0000 said:
Rafiki yangu ambaye ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa (lakini anaipenda sana CHADEMA[/COLOR])

nimependa hapo kwa red
 
Wali utakuwepo? Bila ubweche hatuji maana mapenzi yetu kwenye hiki chama ni kwa ajili ya kupata madili tu ila mioyo yetu iko chadema
 
Ndugu zangi maswali madogo: -
1. Lengo la mkutano nini nini?
2. Je utarushwa live ili nasi wa mbali tuone?
Nashukuru.

Uko live TBC,STAR TV,ITV.CLOUDS TV

1.- lengo ni kujibu mapigo ya CDM
2. Kubadilisha jina la CDM square to CCM square
3. Kuelezea malengo na mahitaji katika katiba mpya
4. Kuongelea vurugu za Zanzibar(UAMSHO)
5. Kuelezea ujenzi wa bara bara(Mradi wa DART)
6. Kukaribisha wale wanaovua gamba vua gwanda vaa uzalendo
7. uchaguzi ndani ya chama.
 
Jibu

1. Kujipima nguvu kwa CHADEMA.
2. Bila shaka.

Ni aibu ya karne hii kwa chama kinachoshika dola kuweweseka majukwaani ilhali shule hazina madeski, maisha yanazidi kuwa magumu, waalim wamekata tamaa na nchi inadidimia kiuchumi. Au ccm ikienda Jangwani matatizo ya nchi hii yatapungua? Kweli sera mbovu huzaa mawazo finyu! Haya ccm, nendeni Jangwani mkamalizie waliyoacha CDM
CCM! AIBUUU!
 
Uko live TBC,STAR TV,ITV.CLOUDS TV

1.- lengo ni kujibu mapigo ya CDM
2. Kubadilisha jina la CDM square to CCM square
3. Kuelezea malengo na mahitaji katika katiba mpya
4. Kuongelea vurugu za Zanzibar(UAMSHO)
5. Kuelezea ujenzi wa bara bara(Mradi wa DART)
6. Kukaribisha wale wanaovua gamba vua gwanda vaa uzalendo
7. uchaguzi ndani ya chama.

mfumuko wa bei,mishahara duni kwa wafakazi wa umma,ufisadi,ufukara,manyanyaso na mauji kwa raia wasio na hatia,na upumbavu mwingine mlio wafanyia watanganyika,acheni kuiga chadema wenzenu wana hoja za mvuto na zina kubalika,wezi wa kubwa nyie
 
Back
Top Bottom