Mkutano wa CCM Goba: Mgeni rasmi ni Nape Nnauye

Leonard Akaro

Member
Nov 1, 2010
56
13
Niko kwenye mkutano wa CCM kata ya Goba Muda huu Nape yuko anahutubia.japo nimechelewa lakini nakusudia kuwapasha.

Nape kawatambulisha wale vijana waliofukuzwa chadema. Hiace na malori nayo yanaleta watu kama kawa.

Maudhui makubwa naona wanajadili Chadema hususan Dr. Slaa, Mnyika na Mbowe haswa maisha yao binafsi. Wazee walioko jirani wanalalama. Wanahitaji yazungumzwe mambo yanayowahusu wao.

Mwampamba anadai watanzania tulikosea kumchagua Mnyika eti hada digrii. Hivi ni kweli?

Wazee walioko jirani wanakubaliana na Chadema kuwa walikuwa sahihi kuwafukuza. Hawana adabu.

Wana Goba wako na furaha, bia zinanyweka, T-Shirts, kofia na mashati zimegawanywa vya kutosha.

Waziri wa Maji ameahidi kufungua maji yaliyofungwa baada ya uchaguzi mkuu uliopita. Kwa hili limeniuma sana na hapa nilipo natamani kulia. Kumbe Goba tulipewa adhabu ya kukatiwa maji kisa jimbo la ubungo kwenda upinzani.

Niko na picha ila hapa inabidi nitafute usaidizi. Simu yenyewe ni kama ya arobaini na saba.

Barabara nazo zimezungumziwa kama kawa kuwa ziko kwenye mpango yakinifu wa kuziwezesha kuwa za lami.

Kwa mujibu wa Nnauye ni kuwa amevuna wanachama wapya wa CCM 165 wakiwamo wanachama wa Chadema.

Kwa ufupi kuna mabasi zaidi ya saba zilileta wanachama wa CCM kutoka maeneo mengine na kuletwa hapa Goba mjini. Mungu ni mkubwa angalau nimeuza crate zaidi ya arobaini za bia. CCM naomna mje tena Goba stand.
 
Niko kwenye mkutano wa CCM kata ya Goba Muda huu Nape yuko anahutubia.japo nimechelewa lakini nakusudia kuwapasha.

Nape kawatambulisha wale vijana waliofukuzwa chadema. Hiace na malori nayo yanaleta watu kama kawa.

Maudhui makubwa naona wanajadili Chadema hususan Dr. Slaa, Mnyika na Mbowe haswa maisha yao binafsi. Wazee walioko jirani wanalalama. Wanahitaji yazungumzwe mambo yanayowahusu wao.

Mwampamba anadai watanzania tulikosea kumchagua Mnyika eti hada digrii. Hivi ni kweli?

Wazee walioko jirani wanakubaliana na Chadema kuwa walikuwa sahihi kuwafukuza. Hawana adabu

Kwani Degree ndo inafanya kazi!!?? mbona kule mjengoni (Bungeni) kuna mijitu ina Mi PHd yao lakini haijawahi kutoa hoja zenye mashiko kama anazotoa Mnyika? Pia kuna miprofesa kibao ambayo hata uwezo wa kujadili mada zenye kujenga taifa hawana uwezo nazo, sie tunataka kazi, hiyo ndo inaonyesha mtu alivyoelimika na sio cheti
 
Lete habari? ususani matusi najua hoja hakuna, cheza kama jana sosoliso temeke.......... tupicha twazana za ubebaji pls.
 
Mwenyewe niko hapa mkuu wa mkoa amevalishwa tishet ya ccm anahutubia pembeni kasimaliwa na Nape....anagusia issue ya kuuana watu wanaguna
 
NAPE ALISEMA KWAMBA WANAHAMA CCM NA KUHAMIA CDM NI OIL CHAFU, ATUAMBIE HAO WALIFUKUZWA CDM NA KUHAMIA CCM WATAKUA NINI? dhahabu au kinyesi?
 
NAPE ALISEMA KWAMBA WANAHAMA CCM NA KUHAMIA CDM NI OIL CHAFU, ATUAMBIE HAO WALIFUKUZWA CDM NA KUHAMIA CCM WATAKUA NINI? dhahabu au kinyesi?

Wazee wangu wa Goba wamekasirishwa sana na vijana waliosemeshwa na wazazi wao badala ya kumwaga sera na mipango ya kutatua matatizo ya Goba wao ni kuzungumza tu mambo ya Karatu tu tuuuuu.
 
Haya wakitoa hayo maji Chadema bado itashinda. mnyika atakuja na hoja nzuri yabkuwaambia wana goba.
 
Back
Top Bottom