Mkutano wa ACT - Wazalendo kuhusu Mgombea Urais, Prof Anna Mghwira kuwa mgombea

Chama cha Upinzani cha ACT-Wazalendo kupitia Prof. Kitila Mkumbo kimemtangaza Mwenyekiti wake Mama Anna Elisha Mghwira kuwa mgombea wa nafasi ya Urais kwa tiketi ya chama hicho katika mkutano mkuu unaoendelea jioni hii, huku mgombea mwenza akiwa ni Hamad Mussa Yusuph, mzawa wa Visiwani Zanzibar.

ACT-Wazalendo kinakuwa ni chama cha kwanza nchini Tanzania kusimamisha mgombea urais mwanamke katika historia ya siasa.

Anna Senkoro naye aligombea2005kwa PPT-MAENDELEO kwa SASA yupo ccm.wanawake wakimpigia kura woooooooote kuanzia madam speaker hadi Mdee,huyu Ana wa ACT atakuwa "RAIS"
 
hahahahahaaaaa kwangu kucheka maana nimenoa panga vizuri kuwakataa!!!!!!!!!!!!!!!!:mod:
 
Sasa wadhamini mikoa 10 Tz atafanikiwa kweli kwa masaa yaliyobaki manake kesho ndio Deadline
 
Mama ana yuko vizuri namkubali sana ingawa kitila mkumbo angetoa upinzani mkali kwa mgombea wa ccm na cdm, lakini sio mbaya tutampa kura za kutosha.
 
Mama ana yuko vizuri namkubali sana ingawa kitila mkumbo angetoa upinzani mkali kwa mgombea wa ccm na cdm, lakini sio mbaya tutampa kura za kutosha.
Kitila mwaka jana alisema atapambana na Mwigulu jimboni kokote atakakokuwa. Nausubiri mpambano huo kwa hamu kama kawli utakuwepo.
 
Kitila mwaka jana alisema atapambana na Mwigulu jimboni kokote atakakokuwa. Nausubiri mpambano huo kwa hamu kama kawli utakuwepo.

Kitila mukumbo ni moja kati ya wanasiasa waoga nadhani alivyoacha ubunge angegombea uraisi.angeibuka mwanasisa bora.
 
Back
Top Bottom