Mkutano wa 50 wa mwaka wa Uwindaji wa Kitalii (Annual Hunting Convention)

Wazo Kuu

Senior Member
Oct 21, 2018
114
293
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro amewasili Jijini New York, Marekani leo tarehe 18 Januari 2022 kwa ajili ya kushiriki mkutano wa 50 wa mwaka wa Uwindaji wa Kitalii (Annual Hunting Convention) ulioandaliwa na Jumuiya ya Uwindaji ya Kimataifa

Mkutano huo unaotarajiwa kuanza kesho tarehe 19 Januari, 2022 katika Jiji la Las Vegas, Nevada nchini Marekani umelenga kuwakutanisha watunga sera na wafanya maamuzi katika ngazi za juu kutoka nchi mbalimbali duniani kuweza kujadili masuala ya kisera katika kuendeleza sekta ya uwindaji

Katika Mkutano huo, Dkt. Ndumbaro anatarajia kunadi fursa za uwekezaji za uwindaji wa kitalii zilizopo nchini Tanzania kwa lengo la kuwawezesha Matajiri wakubwa duniani kuchangamkia uwekezaji huo uliopo nchini Tanzania

Aidha katika mkutano huo Tanzania ni mshiriki muhimu ikizingatiwa kuwa Tanzania ni mojawapo ya nchi zinazoongoza duniani katika uhifadhi wa wanyamapori na uwindaji, Hivyo kupitia mkutano Tanzania itaweza kuongeza uelewa zaidi katika masuala ya kisera na maamuzi katika kuendeleza sekta ya uwindaji wa kitalii nchini

Katika hatua nyingine, Dkt. Ndumbaro atapata fursa ya kufanya mazungumzo na Wadau mbalimbali wa masuala ya utalii waliopo nchini ikiwa ni nafasi adimu ya kuwavutia kuja kuwekeza nchini humo

Katika mkutano huo, Waziri Ndumbaro ameambatana na Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Dkt. Maurus Msuha, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TAWA, Meja Jenerali, Hamis Semfuko, Kaimu Kamishna Uhifadhi wa TAWA, Mabula Misungwi,

Wengine ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa TAWA, Lulu Ng'wanakilala pamoja na Afisa Mhifadhi Mkuu wa Wanyamapori wa kutoka TAWA, Segolin Tarimo

Waziri Ndumbaro pamoja na ujumbe wake wamepokelewa na Mwenyeji wa Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Elsie Kanza

2 (1).jpg
 
Back
Top Bottom