Mkutano nchi za Afrika na NORDIC: Rais Magufuli awakaribisha wawekezaji kuwekeza nchini, kwa sababu kuna amani na ukuaji mzuri wa uchumi

Kwenye hotuba yake sijasikia akiwaambia kuwa ameamua kuwa Dictator ili kuimarisha uchumi, na kufuta mfumo wa vyama vingi ili aweze kununua ndege nyingi zaidi! mnampa sifa za kijinga ambazo hazistahili!
 
Viongozi wa nchi za Afrika tumetambua muafaka wetu uko miongoni mwetu, uhuru wa kisiasa hauwezi kuwa na tija kama hatuna ukombozi wa kiuchumi, lazima tubadilishe muelekeo na tushirikiane na nchi zenye nia ya kushirikiana kiuchumi.

Hakika wewe ni kiongozi mwenye upeo mkubwa sana unaoongozwa kwa uzalendo.

PIGA KAZI MZEE BABA STORY BAADAE.
 
Make Tanzania great Again

Hatuna wasiwasi chini ya Mzalendo Magufuli

Anaipaisha Tanzania

Waziri moja wa Norway ametokwa na machozi baada ya kuonana na kiongozi bora Magufuli

Amesema anatamani kuwa Mtanzania
Huyo labda anawalilia akina Azory tu ila wewe ni ujinga tu unakusumbua huwezi kuelewa. You will sink very low.
 
Kweli kabisa tangu tupate Uhuru hatujawahi kupata "matunda" ya mpasuko wa Taifa,kupigana risasi baada kushindwa kwa hoja Majukwaani,kuminywa Uhuru wa watu kujieleza,kuwa Dona Kantrii,ufisadi kwisha kabisa, kukiukwa Katiba wazi wazi,vitisho na kubambikiwa kesi uchwara wapinzani,nk.
Viongozi wa nchi za Afrika tumetambua muafaka wetu uko miongoni mwetu, uhuru wa kisiasa hauwezi kuwa na tija kama hatuna ukombozi wa kiuchumi, lazima tubadilishe muelekeo na tushirikiane na nchi zenye nia ya kushirikiana kiuchumi.

Soma jibu lako hapo juu.
 
Watanzania sasa wanafurahia matunda ya Rais wao kwa mara ya kwanza tangu tupate Uhuru
Matunda ya kukosa ajira kwa miaka 4 na matunda ya utekaji na mauaji !

2183704_IMG_1183.jpg
FB_IMG_1570952637609.jpg
 
Asichokijua Rais, hakuna mwekezaji mkubwa makini ambaye anaenda kuwekeza mahali kwa sababu eti mtaqala amewakaribisha kwenda kuwekeza. Multinational companies huwekeza baada ya nchi wanayotaka kwenda kuwekeza imefaulu vigezo.

Nimewahi mara kadhaa kushiriki kwenye kutengeneza vigezo na mara kadhaa pia nimewahi kufanya assessment ya kuangalia nchi kadhaa ili kuzipanga nchi ambazo makampuni hayo makubwa yanaweza kuwekeza.

Kwa ufupi, wawekezaji wanaenda kuwekeza kwenye nchi fulani kwa kuangalia mazingira ya uwekezaji yanavyolindwa na mifumo ya kiutawala, kisheria, kidemokrasia na uimara wa mifumo yote kwa ujumla.

Kwa sasa Tanzania haiwezi kuwa mahali pakuvutia kwa sababu mifumo inauawa, na nchi inakwenda kwa kufuata kauli za watawala.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom