Mkutano nchi za Afrika na NORDIC: Rais Magufuli awakaribisha wawekezaji kuwekeza nchini, kwa sababu kuna amani na ukuaji mzuri wa uchumi

Mwl.RCT

JF-Expert Member
Jul 23, 2013
13,564
18,589
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameshiriki Ufunguzi wa Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya nje wa Nchi za Afrika na NORDIC unaofanyika akatika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere JNICC Jijini Dar es salaam.

=====

HOTUBA YA RAIS MAGUFULI KWA UFUPI

Viongozi wa nchi za Afrika tumetambua muafaka wetu uko miongoni mwetu, uhuru wa kisiasa hauwezi kuwa na tija kama hatuna ukombozi wa kiuchumi, lazima tubadilishe muelekeo na tushirikiane na nchi zenye nia ya kushirikiana kiuchumi.

Ukilinganisha pato la nchi na Nordic na nchi Afrika ni tofauti sana, tofauti ni kubwa sana na sisi Waafrika lazima tijitafakari na tujifunze kwa nchi marafiki zetu wa Nordic.

Kwa miaka ya hivi karibuni nchi nyingi za Afrika zimepiga hatua kwenye uchumi, katika nchi zinazoongoza kwa ukuaji mzuri wa uchumi, tano zinatoka Afrika. Kuhusu amani, nchi nyingi Afrika zina amani licha ya kuwepo kwa changamoto kwa nchi chache.

Nchi yetu inashika nafasi ya pili kuwa na vivutio vingi vya utalii, tuna Mbuga za wanyama, Milima na miti mirefu Duniani iko kwetu.

Sisi pia tunapambana na rushwa, kwa sababu rushwa ni moja ya kansa ya uwekezaji barani Afrika.

Ili kuvutia biashara katika Bara letu la Afrika ni lazima tuweke mazingira mazuri na wezeshi kwa wafanyabiashara, lakini pia tuondoe urasimu.

Tunawakaribisha wawekezaji kuja kuwekeza Tanzania, kwa sababu tuna amani, ukuaji mzuri wa uchumi (uchumi unaokua kwa asilimia 7) lakini pia Tanzania ni mwanachama wa SADC.



Rais.PNG


Magufuli azifagilia nchi za Nordic kusaidia ukombozi Afrika

Rais Dk. John Magufuli amezipongeza nchi za Nordic kutokana na msaada wake mkubwa katika kusaidia harakati za ukombozi kwenye nchi mbalimbali hususani kusini mwa Afrika.

Rais Magufuli amesema hayo leo Ijumaa Novemba 8, katika ufunguzi wa mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje na nchi za Nordic ambapo Tanzania ndiyo mwenyeji wa mkutano huo uliozikutanisha nchi 34 zikiwamo za Nordic.

“Kama mnavyofahamu Tanzania ilikuwa mwenyekiti wa harakati za ukombozi ambapo kulikuwa na kambi nyingi za wakimbizi hivyo tunafahamu mchango mkubwa wa Nordic ikiwamo ujenzi wa Chuo cha Wapigania Uhuru wa Afrika Kusini cha Solomon Malangu Freedom College (Somapco), kilichojengwa mwaka 1975 mkoani Morogoro.

“Ikumbukwe kuwa nyakati hizo haikuwa rahisi kwa mataifa ya Ulaya kuja kuunga mkono jitihada za ukombozi kwa nchi za Afrika, lakini marafiki zetu wa nchi za Nordic walikuja, na huu ndiyo upekee wa nchi za Nordic ahsanteni sana,” amesema Rais Magufuli.

Amesema hata baada ya kusimamia harakati za kupigania uhuru nchi za Nordic zimeendelea kuwa washirika wa maendeleo wa nchi za Afrika, ambapo wameshirikiana katika nyanja nyingi ikiwamo afya, elimu, kilimo, sayansi, kilimo, amani na usalama.

Aidha, amesema nchi hizo hususani Tanzania, imenufaika na miradi mingi ya nchi za Nordic ikiwamo Kituo cha Elimu Kibaha (Kibaha Education Centre) na Kituo cha Utafiti cha Kilimo Uyole.

“Nchi za Nordic zilitusaidia kujenga vyuo vya ufundi na pia kwenye kampeni za kufuta ujinga (Illiteracy Campaign Programme), iliyotekelezwa miaka ya ‘70 na kuiwezesha Tanzania kufuta ujinga kwa ailimia 98 na hivyo kuwa nchi za kwanza Afrika kufikia kiwango hicho, sina hakika kama kiwango hicho kimeshafikiwa na nchi nyingine.

“Leo nataka niwashukuru kwa sababu na mimi ni product ya wanufaika wa nchi za Nordic kwa sababu digrii yangu ya kwanza kwa miaka yote mitatu nikifabnya thesis na research zilitolewa fedha na nchi ya Norway kwa kupiftia Shirika la Norad kwa hiyo na mimi nawashukuru.

“Kwa kuzingatia hayo yote napenda nitoe shukrani zangu za dhati kwa kuendelea kushirikiana na nchi za Afrika na tunawaomba mawaziri wetu wa mambo ya nje mfikishe salamu zetu kwa nchi zenu,” amesema.


Mtanzania
 
Hongera Magufuli kwa kujali Watanzania Endelea kuchapa kazi

Matunda ya kuwa mwenyekiti wa sadic yanaonekana sasa

Tanzania ni Nchi tajiri

Ni suala la kubadilisha raslimali kuwa utajiri

Tunabahati tumempata Rais Mzalendo mwenye nia ya dhati kuijenga Tanzania kiuchumi
 
Siku hizi Arusha kumesuswa?
Naona mikutano yote mikubwa ni Dar tu.
 
Asante Mh.Rais kuwakaribisha wawekezaji na miongoni mwa sababu ulizotaja utulivu wa kisiasa. Ni imani yangu kauli yako hiyo ikufikishe ubadidili mtazamo wako na wapambe wako wanaokupaka mafuta kwa mgongo wa chupa.

Leo hii hata Masiha mwana wa Mungu akigombea hawezi kupata 99% ya ushindi.

Jifunze kwake japo alikuwa na maamlaka, aliacha nature ichukue mkondo wake.
 
Watanzania sasa wanafurahia matunda ya Rais wao kwa mara ya kwanza tangu tupate Uhuru
Kweli kabisa tangu tupate Uhuru hatujawahi kupata "matunda" ya mpasuko wa Taifa,kupigana risasi baada kushindwa kwa hoja Majukwaani,kuminywa Uhuru wa watu kujieleza,kuwa Dona Kantrii,ufisadi kwisha kabisa, kukiukwa Katiba wazi wazi,vitisho na kubambikiwa kesi uchwara wapinzani,nk.
 
Mawaziri wa nchi tajiri zaidi Africa Wakutana wakiongozwa na nchi mwenyeji Tanzania. Mungu ibariki Africa Maendeleo hayana Chama....

Kuanzia sasa hatutaki tena misaada ya Mabeberu #MATAGA
IMG_20191108_131402.jpeg
 
Make Tanzania great Again

Hatuna wasiwasi chini ya Mzalendo Magufuli

Anaipaisha Tanzania

Waziri moja wa Norway ametokwa na machozi baada ya kuonana na kiongozi bora Magufuli

Amesema anatamani kuwa Mtanzania
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom