Mkutano nchi za Afrika na NORDIC: Rais Magufuli awakaribisha wawekezaji kuwekeza nchini, kwa sababu kuna amani na ukuaji mzuri wa uchumi

Naona anajaribu kujivimbisha mbele ya wahisani lakini bila kujiamini. Anaposema kwamba ushirikiano wa kupeana misaada kwa sasa umepitwa na wakati eti kwavile huzuia uhuru wa kisiasa kwa nchi za Afrika kujiamulia mambo yao wenyewe kwani hajui kwamba kuomba au kupokea misaada ya wahisani ni hiyari ya nchi zenyewe? Hivi ni huru gani wa kisiasa anaoulilia Rais Magufuli? Anataka kusiwe na mfumo wa vyama vingi na uchaguzi wa kidemokrasia?

Hata hivyo sidhani kwamba anachokisema anamaanisha kweli. Nasema hamaanishi kwasababu hatujawahi kusikia/kuona serikali anayoiongoza ikikataa misaada ya mabeberu. Sana sana tunasikia serikali imenyimwa misaada kwa sababu hizi na zile. Bali serikali yenyewe inapotokea kupewa msaada huchukulia kuwa ni "mafanikio ya jitihada za serikali ya awamu ya tano" na hutangaza kwenye kila chombo cha habari.

Ingawa Rais Magufuli anatamani nchi yake ijitegemee kiuchumi, hadi sasa bado anaonesha ameshindwa kuwa na mikakati sahihi ya kuitoa nchi kwenye utegemezi. Anachojua yeye ni kuorodhesha rasilimali za nchi na kujisifia kubarikiwa lakini hajui ni jinsi gani azitumie hizo rasilimali kujikuza kiuchumi. Mkakati pekee alionao wa kukuza uchumi ni kujenga mazingira bora ili kuwavutia wawekezaji (mabeberu). Kiufupi Magufuli hana jipya katika kukuza uchumi wa nchi.
 
Anajimwambafai na kutoa maagizo na majigambo anafikiri hao wawekezaji ni wa kuteuliwa kama wakuu wa wilaya?

Wawekezaji hawahitaji kuitwa na kuhubiriwa upiuzi wenu wenu wa mataga wala kutishwa na vikauli uchwara.

Huyu dikteta hajiulizi kwanini Dubai au Singapore ni vituo vya uwekezaji kutokea popote duniani?

Uwekezaji wa dola bilioni 19 kujenga tu ka-bandari mnashindwa, eti mnaitisha mkutano muwavutie wawekezaji?

Ni nani kawadanganya kuwa mwekezaji anahitaji mkutano wa hadhara ndipo akawekeze? Kwani amekuwa nwanachama wa sisiemu?

Ni nani aliwaloga watanzania?

Binafsi sioni analofanya huyu mtu wenu zaidi ya kuitumbukiza nchi shimoni.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom