Mkutano mkuu wa Barrick gold mine wamzuia mwanaharakati kutoka Tanzania kuhudhuria | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkutano mkuu wa Barrick gold mine wamzuia mwanaharakati kutoka Tanzania kuhudhuria

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ngofilo, May 4, 2012.

 1. Ngofilo

  Ngofilo JF-Expert Member

  #1
  May 4, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 214
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  ​Mkutano wa mwaka huu wa Barrick Gold Mine uliofanyika Toronto Nchini Canada May 3, 2012, ulimzuia Mwanaharakati wa Haki za binadamu na mwanasheria wa masuala ya Maliasili Mr. Amani Mustafa Mhinda, ambaye pia ni Mkurugenzi wa asasi ya kijamii ya HAKIMADINI,inayoshughulika na haki za binadamu katika maeneo ya machimbo ya madini.

  Mhinda alikuwa amedhamiria kueleza wahudhuriaji wa Mkutano huo kuhusu umuhimu wa kujenga uwezo wa wachimbaji wadogo na jamii zinazoishi katika maeneo ya machimbo, ili ziweze kunufaika na rasilimali ya madini ya Tanzania, pamoja na kulinda na kutetea haki zao, ambayo pia ni agenda kuu ya HAKIMADINI yenye makao yake makuu mjini Arusha.

  Pamoja na kuwa na ajenda hiyo, Barrick Gold na uongozi wake walimzuia kuingia katika eneo la mkutano huo.

  Akinukuliwa na gazeti moja la kitaifa la Canada liitwalo The Canadian, Mhinda alieleza uhalali wake wa kuhudhuria mkutano huu huku akinukuu matukio ya uvunjwaji wa haki za binadamu yanayofanywa na makampuni ya uchimbaji.

  "Kama shirika lisilo la kiserikali la kitanzania na wananchi wa Tanzania, tunataka kuona mauaji na uvunjwaji wa haki za binadamu unaohusishwa na makampuni ya uchimbaji madini ya Canada yanamalizwa. Niko hapa kuwa wakilisha watanzania wengi ambao ni wahanga wa mgodi huu pamoja na Mama Otaigo, aliyefariki mwezi wa nne kwa kunywa maji yenye sumu yaliyopo karibu na Mgodi wa North Mara". Amani alisema

  Mwanaharakati huyo pamoja na wanaharakati wengine wa masuala ya haki za binadamu walinyimwa kuzungumza kuhusu matendo ya kinyanyasaji yanayofanyika kwenye maeneo ya machimbo ya madini nchini Tanzania katika mkutano Mkuu wa Mwaka wa Barrick Gold mine.

  Hatua hiyo ya kampuni ya Barrick Gold Mine kuwazuia wanaharakati wa Tanzania na kuwaruhusu wenzao wa nchi kama Papua New Guines na Chile kuliushangaza umati wa waalikwa kwenye mkutano huo.

  Mhinda alishutumu hatua iliyochukuliwa na Barick Gold ya kumzuia kuingia katika mkutano huo kama "juhudi za wazi za kuficha uvunjwaji wa haki za binadamu unaofanywa na makampuni ya uchimbaji na wawekezaji wengine kwa jamii za kitanzania".

  Pamoja na kufungiwa kuingia katika mkutano huo, Amani na wanaharakati wengine walipata nafasi ya kuelezea habari zao kwa maelfu ya watu waliokusanyika nje ya eneo la Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Barrick kwa ajili ya kupinga unyanyasaji unaofanywa na kampuni ya Barrick Gold ambayo ni kampuni kubwa zaidi ya uchimbaji dhahabu duniani, iliyoanzishwa na kusimamiwa na Peter Munk.

  Miongoni mwa wajumbe wa bodi ya kampuni hiyo ni pamoja na Waziri mkuu wa zamani wa Canada. Barick hupata fedha za serikali na misaada ya kidiplomasia. Makao makuu ya barrack yapo Toronto, Canada, wakati Africa Barrick, ni kampuni ya Uingereza ambayo humilikiwa kwa 70% na Barrick Gold
   
 2. Emil Mwangwa

  Emil Mwangwa Senior Member

  #2
  May 4, 2012
  Joined: May 9, 2011
  Messages: 132
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Znz hakuma madini yeyebalikwenda kufanya nini????
   
 3. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #3
  May 4, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Wanajua walichokfanya na wanachoendelea kukifanya apa Tz ndo maana wakamzuia as angetia kitumbua mchanga ila watu walokuwa nje ya jengo walipata msg.
  Ila watu wa Chile na Papua New Guinea waliluhusiwa ila Tz hatufai si dharau hii
   
 4. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #4
  May 5, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,223
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  Na wanaharakati wasisahau udokozi na kutoheshimu mipaka kwa watanzania kwenye maeneo ya wawekezaji
   
 5. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #5
  May 5, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,326
  Likes Received: 1,793
  Trophy Points: 280
  Sometimes we forget that Gama...Justice is a double edged sword. Kila mtu lazima atimize wajibu wake kadri inavyotakiwa.
   
Loading...