Mkutano mkuu wa 20 wa CPC una umaalum gani kwa dunia?

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
VCG111406503875.jpg
Mkutano Mkuu wa 20 wa Wajumbe Wote wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) umefanyika hivi karibuni mjini Beijing. Matokeo makubwa ya kisiasa na kiitikadi yaliyopatikana kwenye mkutano huo si kama tu yataekeleza maendeleo ya China katika kipindi kichacho, bali pia yatanufaisha dunia nzima.

Mkutano huo umefafanua kuwa China itachagua njia maalum ya kichina katika kutimiza mambo ya kisasa, na kuleta hekima mpya kwa maendeleo ya dunia. Njia ya kichina katika kutimiza mambo ya kisasa ina sifa za kawaida, na pia ina sifa za Kichina ikilinganishwa na nchi nyingine duniani. Njia hiyo ya kiuvumbuzi itahimiza nchi nyingine kutafuta njia inayofaa hali zao katika kujiendeleza na kutimiza mambo ya kisasa. Katika historia, baadhi ya nchi zilizoendelea zilijiendeleza kwa njia ya kutumia nchi nyingine na kuchukua mali za nchi nyingine, lakini njia ya kichina ni ya amani na kulenga kuleta maendeleo ya pamoja.

Mkutano huo umesisitiza kuwa China itafungua mlango zaidi, na italeta fursa mpya za maendeleo duniani. Hivi sasa uchumi wa dunia unakabiliwa na changamoto mbalimbali, zikiwemo janga la UVIKO-19, mfumuko wa bei, vita, na vitendo vya kujilinda kibiashara. China itaendelea kufuata sera ya mageuzi na kufungua mlango, na kutoa fursa kubwa kwa dunia wakati inapojiendeleza. Mkutano huo kwa mara nyingine tena umetoa ahadi nzito ya kufungua mlango kwa dunia, ukionesha nia na hatua thabiti ya China ya kutoa mchango mpya kwa maendeleo ya dunia.

Mkutano huo umetetea kuzingatia amani na maendeleo ya dunia, na kuhimiza ujenzi wa jumuiya yenye hatma ya pamoja ya binadamu, na kutoa suluhisho la China kwa ajili ya kutatua changamoto za usimamizi wa mambo ya kimataifa. Hivi leo, dunia inakabiliwa na vitendo vya umwamba na siasa ya kinguvu, ambavyo vinadhuru maslahi za nchi mbalimbali haswa nchi zinazoendelea. Katika ripoti yake kwenye Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC, rais Xi Jinping wa China alisisitiza kuwa, China inashiriki katika mageuzi na uboreshaji wa mfumo wa usimamizi wa mambo ya kimataifa kwa hatua madhubuti, kutetea mfumo huo kuzingatia zaidi mazungumzo na kuleta mafanikio ya pamoja, kufuata utaratibu wa pande nyingi, na kuwa wa haki zaidi. China pia imependekeza Mpango wa Maendeleo ya Kimataifa na Mpango wa Usalama wa Kimataifa ili kuboresha mfumo wa usimamizi wa mambo ya kimataifa. Mkutano huo kwa mara nyingine tena umebainisha kuwa, China siku zote inafuata sera yake ya kidiplomasia ya kudumisha amani na kuhimiza maendeleo ya pamoja, na kuhimiza ujenzi wa jumuiya yenye hatma ya pamoja ya binadamu, na kuchangia busara ya kichina kwa amani na maendeleo duniani.
 
Back
Top Bottom