Mkutano mkuu chama cha wanasheria Tanzania bara (TLS) kufanyika siku ya Jumamosi ukumbi wa AICC Arusha

Blaki Womani

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
11,221
2,000
TLS inapenda kuwajulsha kuwa siku ya jumamositarehe 15 Septemba 2018 kuanzia saa mbil asubuhi wanachama wachama hicho watakutana katika mkutano wao mkuu ambapo wanachama watajadili mambo mbalimbali yahusuyo chama hicho. Mgeni rasmi katika mkutano huo atakuwa ni Mr Ali Mfuruki.​

Mkutano huo utafuatiwa na chakula cha pamoja (fundraising dinner)wenye lengo la ukusanyaji pesa kwa ajili ya umaliziaji wa jengo la mawakili hao maarufu kama WAKILI HOUSE(LAAC). Hafla hiyo itaongozwa na MC mahiri bwana Ephrahim Kibonde huku mgeni rasmi akiwa ni huyohuyo Mr Ali Mfuruki.

Mkutano huo utarushwa live kupitia mitandao ya kijamii ya taasisi hiyo kupitia youtube account inayoendakwa jina la Tanganyika law society pia Facebook account yenye jina la Tanganyika Law Society.
KARIBUNI SANA
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom