Tetesi: Mkutano mkuu CCM tarehe 7.7.2016; Mangula kuwa katibu mkuu, Bulembo naibu katibu mkuu

Status
Not open for further replies.

Pagan Amum

JF-Expert Member
Aug 28, 2015
1,932
4,400
Ukiwa ni mkakati wa kuisuka CCM, Comrade Mangula atapewa nafasi ya Katibu Mkuu wa chama hicho ili amsaidie Rais kukisuka chama. Pamoja na Mangula mwingine ni Abdallah Bulembo ambaye anategemewa kupewa nafasi ya naibu katibu Mkuu Bara.. Ikumbukwe Bulembo ni confident man wa Rais kwa sasa...

Pamoja na hilo, Mwenyekiti mpya, atatumia fursa hiyo kufumua kamati kuu yote kwa kuwaondoa wajumbe wake wote, na kuja na majina mapya ambao wengi sio wanasiasa bali ni wasomi wa nchi hii... Hii itaendana na mwenyekiti mpya kufumua sekretariate na kuunda mpya...

Kwa nafasi ya uenezi wa chama majina matatu yanatajwa tajwa... 1. Bashe 2. Lusinde 3. Ole Sendeka.

=======

Update:

Tetesi hizi si za kweli.
Taarifa sahihi za Mkutano huo ziko hapa: News Alert: - Mkutano mkuu wa CCM sasa rasmi tarehe 23 Julai 2016
 
Bashe hana nafasi ndani ya CCM. Mangula hawezi kuwa Katibu Mkuu wa CCM labda anaweza kubaki kwenye nafasi aliyonayo sasa. Bulembo anaweza kuwa na nafasi kubwa zaidi CCM. Ole Sendeka anaweza kuwa Mwenezi. Ila chama ndo kinaamua. Hizi ni hisia tu. CCM haifanyi mambo yake gizani. Kila kitu kitakuwa hadharani
 
ukisoma majina mpk unastuka!!bulembo?,kibajaji?.........
Bulembo ndo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi na ndiye aliyefanikisha mikakati ya ushindi wa CCM. Ndiye alikuwa msemaji wa Mgombea wetu wakati wa kampeni. Kibajaji ni Mbunge wa Mtera. Mnafahamu pia muziki wake anaowahenyesha pale Bungeni
 
Bashe hana nafasi ndani ya CCM. Mangula hawezi kuwa Katibu Mkuu wa CCM labda anaweza kubaki kwenye nafasi aliyonayo sasa. Bulembo anaweza kuwa na nafasi kubwa zaidi CCM. Ole Sendeka anaweza kuwa Mwenezi. Ila chama ndo kinaamua. Hizi ni hisia tu. CCM haifanyi mambo yake gizani. Kila kitu kitakuwa hadharani

Kwa ccm hata Lusinde anaweza kuwa makamu bara na yule Gudluck Mlinga Katibu mkuu au mwenezi. Sifa na vigezo kwa ccm wanavyo vya kutosha.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom