Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 14,939
- 20,398
Mkutano umeanza leo na waendelea mjini Munich.
Kuna mikutano maalum wa masuala ua usalama unaoanza kufanyika mjini Munich nchini Ujerumani ambapo viongozi wapatao 35 kutoka nchi mbalimbali duniani wanatarajiwa kuhudhuria.
Makamu wa raisi wa Marekani Mike Pence na waziri wa mambo ya \nje wa Russia bwana Sergey Lavrov wanatarajiwa kuwa baadhi ya wazungumzaji.
Wahudhuriaji wengine ni pamoja na mabalozi na wanadiplomasia mbalimbali kutoka nchi mbalimbali pamoija na watengenezaji sera za kiusalama.
Mkutano huo wa 55 hufanyika kila mwaka mwezi February na unafanyika katika hoteli maarufu ya Bayerischer Hof iliyopo mjini Munich. Mkutano wa mwaka jana ulifanyika kati ya terehe 16 na 18 February mwaka jana.
Moja ya ajenda za mikutano huo ni msaada wa maendeleo kwa bara la Afrika ambapo huenda suala la ujenzi wa bwawa la Stiegler Gorge likazungumziwa kwa kuzingatia kuwa serikali ya ujerumani bado inaweka shaka lake kwenye mradi huo.
Masuala mengine ni pamoja na hali ya afya duniani na tishio la magonjwa ya kuambukiza ambapo Bill gates anaweza kupewa nafasi ya kuzungumzia hilo akitumia ugnjwa wa malaria.
Suala la ugaidi duniani pia halitapita bila kujadiliwa ambapo sehemu zenye maslahi ya nchi tajiri duniani kama nchini Kenya yataongelewa huku harakati za kijihadi pia zikiangakliwa baada ya vita hivyo kukaribia kuisha kabisa huko nchini Syria.
Majeshi ya Marekani na yale ya Russia na Syria yamewazunguka maeneo machache ya wanamgambo wa ISIS ambao wengi wameuawa na wengine kukimbilia kwenye makambi ya wakimbizi nchini Syria.
Haijulikani kama serikali ya Tanzania imealikwa kwenye mikutano huu muhimu au hata kama itawakilishwa na Dr Abdalah Possi ambae ni balozi wa Tanzania nchini Ujerumani.
Mikutano kama hi hujenga na kuimarisha wigo wa uelewa katika masuala mbalimbali khasa ya haya ya usalama ambapoi si tu kuzungumzia kuhusu usalama wa taifa kama nchi bali usalama wa kila kitu kuanzia Afya zetu, mipaka ya nchi yetu na usalama wa misaada tunayopewa na nchi zilizoendelea.