Mkutano maalum wa kidunia wa masuala ya Usalama waanza leo mjini Munich. Je,Tanzania imepeleka mwakilishi?

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
12,172
2,000
1550239938782.png

Mkutano umeanza leo na waendelea mjini Munich.

Kuna mikutano maalum wa masuala ua usalama unaoanza kufanyika mjini Munich nchini Ujerumani ambapo viongozi wapatao 35 kutoka nchi mbalimbali duniani wanatarajiwa kuhudhuria.

Makamu wa raisi wa Marekani Mike Pence na waziri wa mambo ya \nje wa Russia bwana Sergey Lavrov wanatarajiwa kuwa baadhi ya wazungumzaji.

Wahudhuriaji wengine ni pamoja na mabalozi na wanadiplomasia mbalimbali kutoka nchi mbalimbali pamoija na watengenezaji sera za kiusalama.

Mkutano huo wa 55 hufanyika kila mwaka mwezi February na unafanyika katika hoteli maarufu ya Bayerischer Hof iliyopo mjini Munich. Mkutano wa mwaka jana ulifanyika kati ya terehe 16 na 18 February mwaka jana.

Moja ya ajenda za mikutano huo ni msaada wa maendeleo kwa bara la Afrika ambapo huenda suala la ujenzi wa bwawa la Stiegler Gorge likazungumziwa kwa kuzingatia kuwa serikali ya ujerumani bado inaweka shaka lake kwenye mradi huo.

Masuala mengine ni pamoja na hali ya afya duniani na tishio la magonjwa ya kuambukiza ambapo Bill gates anaweza kupewa nafasi ya kuzungumzia hilo akitumia ugnjwa wa malaria.

Suala la ugaidi duniani pia halitapita bila kujadiliwa ambapo sehemu zenye maslahi ya nchi tajiri duniani kama nchini Kenya yataongelewa huku harakati za kijihadi pia zikiangakliwa baada ya vita hivyo kukaribia kuisha kabisa huko nchini Syria.

Majeshi ya Marekani na yale ya Russia na Syria yamewazunguka maeneo machache ya wanamgambo wa ISIS ambao wengi wameuawa na wengine kukimbilia kwenye makambi ya wakimbizi nchini Syria.

Haijulikani kama serikali ya Tanzania imealikwa kwenye mikutano huu muhimu au hata kama itawakilishwa na Dr Abdalah Possi ambae ni balozi wa Tanzania nchini Ujerumani.

Mikutano kama hi hujenga na kuimarisha wigo wa uelewa katika masuala mbalimbali khasa ya haya ya usalama ambapoi si tu kuzungumzia kuhusu usalama wa taifa kama nchi bali usalama wa kila kitu kuanzia Afya zetu, mipaka ya nchi yetu na usalama wa misaada tunayopewa na nchi zilizoendelea.
 
MALCOM LUMUMBA

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
16,965
2,000
Tanzania tuko vizuri sana kiusalama wala hatuna haja ya kwenda huko, hakuna changamoto ambayo kitengo hawawezi kutatua. Tena baada ya Raisi Magufuli kuingia madarakani Usalama wa nchi umekuwa imara sana kama kipindi cha Nyerere, yani kiufupi nchi iko pazuri mno.

Halafu kwanini tupoteze pesa nyingi kwenda huko Ulaya wakati tunatakiwa kuwatumikia watanzania hapa nchini na mahospitalini hakuna madawa! Watu wakienda huko wataende tu kupiga dili na kuzurura na mahawala wao. Pia unasahau kwamba hii mikutano ni mkusanyiko wa nchi za mabepari ambao wameiibia Tanzania kwa miaka mingi sana, twende huko kwao kufanya nini ?
Mlizoea safari za nje kama hizi zisizo na tija, sasa Hapa Kazi Tu. Mkuu Richard fanya kazi, Raisi kasema hakuna kwenda nje hovyo mpaka pale Tanzania inakuwa imenyooka.
 
Damaso

JF-Expert Member
Jul 18, 2018
909
1,000

Una uhakika na unachokiongea au unaleta masihala tu?
Unaelewa tunaposema neno "usalama"? Hapo hakuna tena usalama kwa wana ccm wala chadema hapa tunazungumzia usalama wa Taifa. Kama haukujua wanazungumza kuhusu nini kwenye huo mkutano kaa kimya uwaruhusu wadadisi ukweli na waelewa walete hoja za msingi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwahiyo wewe unataka kubishana na kauli za Raisi Dr Magufuli msomi wetu aliyetukuka eti ? AU Unataka kuniambia wewe unaijua sana nchi hii kuliko yeye mwenye nayo ?
 
Damaso

JF-Expert Member
Jul 18, 2018
909
1,000
Kwahiyo wewe unataka kubishana na kauli za Raisi Dr Magufuli msomi wetu aliyetukuka eti ? AU Unataka kuniambia wewe unaijua sana nchi hii kuliko yeye mwenye nayo ?
Aahh mbona unataka kutufanya watanzania kama wote wajinga kasoro Rais.
Nakupa mfano mzuri tu ndugu:
Nchi kama USA pamoja na Urusi bado mpaka leo zina changamoto ya madawa ya kulevya pamoja na ugaidi.
Acha hizo mambo pia usalama wa raia katika nchi hizo bado sio wa kuridhisha.
Unataka kusema kwamba Tz tumewazidi hawa jamaa kwa kurejea maneno ya mtukufu Rais wetu.
Elewa maswali haya kwanza ndugu:
1. Je Rais ndo anayo legality ya kufanya kila kitu on behalf of all pillars?
2. Kama hatuna hizo changamoto (kumaanisha kuwa tupo salama) je mauaji ya kibiti na zile maiti za rufiji zipo upande wa nchi gani?$

Halafu nakusahihisha ndugu acha kukariri mzee.
1. Rais sio mwenge nchi hii yeye ni kiongozi bhana.
2. Kuitwa mtukufu haimpi protection ya yeye kufanya anything to anyone tofauti na katiba.

Mimi naamini kila kauli ya Raisi Dr Magufuli kwasababu ni mzalendo kuliko maraisi wote waliopita. Tena anaijua hii nchi sana kwasababu amekaa madarakani miaka zaidi ya 20: Halafu changamoto za kiusalama ni Relative na siyo Universal, hivyo changamoto za mabepari siyo sawa na changamoto za kwetu.

Wewe umesahau tulivyompiga nduli Iddi Amin dada ?? Umesahau tulivyowapoga M23 kule Congo DRC ?? Umesahau ni jinsi gani kitengo kiliweza kuzuia mafisadi kama Lowassa wanaotumiwa na Mabepari kushika nchi ?? Umesahau tulivyowavua nguo mabepari kwenye ishu za makinikia ?? Au huoni ni jinsi gani tunaendelea kuwashughulikia wasalati na vibaraka wa mabepari ndani ya nchi yetu ??

Hivyo changamoto za kiusalama zipo sana lakini amini kwamba Tanzania iko salama. Yale ya kibiti umeona yanaendelea tena ??

Jakaya na Mkapa walienda sana huko lakini nchi haikupata faida yoyote ile. Mimi nashauri kwamba wasiende kabisa maana tuna mambo mengi ya kufanya hapa nchini kuliko kukaa tu kwenye huo mkutano wa mabepari, balozi Dr Possi anatosha.

Tena ikiwezekana tupunguze hata ofisi za ubalozi huko nje maana hazina manufaa yoyote yale, zaidi zaidi mabalozi huwa wanapeana kindugu na kwenda kupumzika tu huko. Tuwe na uzalendo na pesa za wananchi jamani, hivi mnavyoambiwa hii nchi imeibiwa sana huwa hamuelewi ?? Safari kama hizi ni moja ya chanzo cha sisi kuchelewa kupata maendeleo.

Au mnasemaje ndugu JokaKuu na Nguruvi3
 
Nitajaribu kukujibu kuendana na uelewa wako. Tatizo letu tumemezeshwa mambo hatujaangalia kwa jicho undani. Twende pamoja ndugu.
1. Unajua sababu ya Iddi Amin kupigana na Tanzania?
1.1 Je unajua historia ya Kagera na mahusiano yake kwa Tanzania pamoja na Uganda?
2. Umewaita USA na Urusi kuwa mabepari!!! je unajua kuwa hawa ndo wanaochangia more than 40% ya bajeti ya Tz?
Kama na hilo haulijui basi chukua hii tena, hao mabepari ndo waanaongoza kwa kuleta non governmental organization kuleta misaada huku Afrika.
Chukua hii Hizo dream liner zenu mlizonunua wametengeneza kina mtukufuku Rais eehh.
Wahenga wanakuambia "Kamwe usimtusi baba kama hujui utakula wapi".
Fixation ya serikali hii zinaonekana ila mnajaribu kuzificha kwa few and unrelated comments ambazo mwisho wa siku zinawarudia wenyewe.
Nasubiri majibu ndugu lengo ni kuendeleza Tz moja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MALCOM LUMUMBA

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
16,965
2,000
Halafu nakusahihisha ndugu acha kukariri mzee.
1. Rais sio mwenge nchi hii yeye ni kiongozi bhana.
2. Kuitwa mtukufu haimpi protection ya yeye kufanya anything to anyone tofauti na katiba.

Sent using Jamii Forums mobile app
Raisi Magufuli ni mzalendo sana kumlinganisha na maraisi waliopita na ana nia njema sana na hii nchi. Naona ninyi meamua sasa kuwa makuwadi wa mafisadi na tarumbeta za mabepari mkihakikisha mnafanya kila juhudi kupinga maendeleo ya nchi hii.

Halafu uwe na heshima usitake kumfananisha Raisi Magufuli na mwenge, yule ni kama Baba yako mzazi. Lakini kubwa zaidi ni kwamba kukataza safari za nje Raisi hajavunja kabisa katiba ya nchi, kama kavunja nionyeshe Ibara gani hiyo.

Tatizo lenu ni kwamba mlizoea kupiga dili na sasa mirija yenu ya kula imekatwa mnalalama sana. Sijui ninyi CHADEMA mna matatizo gani aisee
 
MALCOM LUMUMBA

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
16,965
2,000
Nitajaribu kukujibu kuendana na uelewa wako. Tatizo letu tumemezeshwa mambo hatujaangalia kwa jicho undani. Twende pamoja ndugu.
1. Unajua sababu ya Iddi Amin kupigana na Tanzania?
1.1 Je unajua historia ya Kagera na mahusiano yake kwa Tanzania pamoja na Uganda?
2. Umewaita USA na Urusi kuwa mabepari!!! je unajua kuwa hawa ndo wanaochangia more than 40% ya bajeti ya Tz?
Kama na hilo haulijui basi chukua hii tena, hao mabepari ndo waanaongoza kwa kuleta non governmental organization kuleta misaada huku Afrika.
Chukua hii Hizo dream liner zenu mlizonunua wametengeneza kina mtukufuku Rais eehh.
Wahenga wanakuambia "Kamwe usimtusi baba kama hujui utakula wapi".
Fixation ya serikali hii zinaonekana ila mnajaribu kuzificha kwa few and unrelated comments ambazo mwisho wa siku zinawarudia wenyewe.
Nasubiri majibu ndugu lengo ni kuendeleza Tz moja

Sent using Jamii Forums mobile app

Naona ninyi wachagga wa CHADEMA meishiwa hoja na kuwa tarumbeta za mafisadi. Nduli Iddi Amini tulimpiga kwasababu alituvamia na alikuwa anaua sana watu wake, naambiwa alifikia hadi muda akawa anakula nyama za binadamu wenzake. Kagera ni sehemu ya Tanzania na haina uhusiano wowote ule na Uganda.

Urusi hachangii kwenye bajeti ya Tanzania, lakini hata hiyo asilimia 40% wanayotupa kama msaada ni peanuts kulinganisha na wanavyotuibia. Barrick/Accacia pekee tunawadai zaidi ya Trillioni 300 na hawajalipa mpaka leo, sasa hilo ni kampuni moja tu la kinyonyani hapa nchini. Tukiyakamata na mengine basi naamini tutafika mbali sana.

Tanzania ni nchi tajiri sana na tunaweza kujitegemea kwa kila kitu hadi kufikia kiwango cha kuwa Donour Country. Wewe huoni miradi mikubwa tunayoifanya mpaka sasa ? Tumehamishia makao mkuu kule Dodoma, n.k

Kuhusu ndege nadhani wewe una uelewa mdogo sana. Hayo madini wanayotengenezea wanayachukua hapahapa Afrika na Tanzania ikiwemo. Lakini pia msikashifu ununuzi wa ndege maana tuna ndege za kisasa ambazo nchi nyingine za Afrika hawana lakini pia tumetanua sekta ya utalii, na tukiruhusiwa kwenda nje ya nchi tutafika hadi Mumbai na Guangzhou.

Nashanga ninyi tu ndiyo mnapuuza juhudi za Raisi Magufuli, wakati World Bank wanaunga mkono na wamekubali kutoa mikopo zaidi kwasababu wanaona mabadiliko yanayofanyika hapa nchini. Tuna hali nzuri sana, deni la taifa limefika Trillioni 60 na bado tunakopesheka, na tutaendelea kukopa ili tujenge SGR, tununue ndege, tujenge Stiegler's gorge kufua umeme na mwishowe tuwe nchi ya viwanda kama tulivyoazimia hapo mwanzo.

Tuna majukumu haya yote, unataka twende huko Ujerumani kufanya nini ?? Tuwahurumie watanzania na tuwe wazalendo jamani

Eti baba swalehe sisi si tunaweza kuwa Dona Kantre ?
 
Vizuri asante kwa hoja zako zenye uhai.
1. Sijawahi kupuuza juhudi za Rais mtukufu kwanza kwa sababu najua kuwa anachokifanya sijawahi kupewa uwanja wa kuchangia, nahisi anapanga akiwa amepumzika kwake.
2. Ondoa kauli ya Wachaga wa Chadema bro. Kwani kila mtu aliye na uthubutu wa kuuliza kinachoendelea ni mpaka awe ndani ya chadema?
2.1 narejea kauli ya Rais mtukufu kuwa "maendeleo hayana chama" na pia Yohana sio Rais wa Ccm tu huyo ni Rais wa Jamhuri ya watu wa Tanzania.
3. Kuna baadhi ya vitu vinaleta dukuduku baina ya watanzania.
3.1 Kwann CAG anapuuzwa yeye pamoja na kazi yake?
3.2 Kuna mihimili mitatu, ila inaonekana dhahiri shairi kuwa kuna muhimili mmoja tu ambao unaendesha mihimili mingine.
3.3 Hakuna ulazima wa Rais kujibu kauli ambazo zinaweza kujibiwa na watendaji wake mfano: Polisi na Wakuu wa Mikoa.
Nawasilisha ndugu......

Mkuu mnakazana kusema madhaifu ya Raisi Magufuli, hivi mema yake hamyaoni ?? CAG mwenyewe alikiri mbele ya Raisi kwamba hakuna wizi wa Trilioni 1.5 sasa ninyi mnalazimisha! Kwani hamuoni kwamba ndiyo zimeenda kuleta maendeleo kule Chato ambako siku hizi kuna Uwanja ndege wa Kimataifa na hadi bandari ?

Elimu yetu imepanda sana watoto wanasoma bure hadi kidato cha nne, kule SUA panya wanafundishwa kutegua mabomu.

Kuhusu mhimili mmoja kusimama kuliko mingine ni sawa kabisa, maana huko kwenye mahakama na bunge kulikuwa na rushwa sana hivyo Raisi ananyoosha sasa. Tunapigana vita ya kiuchumi na mihimili kama mahakama na bunge imetumiwa sana na mafisadi kuvuruga kesi. Unakumbuka ile kesi ya Raisi ya Samaki kipindi kile ni waziri ilivyovurugwa na Mahakama hadi kuiletea nchi hasara ya mabilioni ya pesa ?? Unakumbuka ile kesi ya 2009 wakati ni waziri wa ujenzi mahakama iliiharibu na kuwatetea mabepari na kusababishia nchi yetu hasara kubwa sana hadi mwaka juzi ndege zetu za Bomberdier zilikamatwa huko CANADA ?

Kuhusu wakuu wa mikoa na wilaya, wale bado ni vijana damu bado inachemka, wana nia njema sana hivyo muwavumilie tu. Hata kama hamuwataki hamuwezi kuwatoa kwasababu Raisi wetu ni mwanaume wa kisukuma kutoka kanda ya ziwa, wanaume wa kanda za ziwa hasahasa wasukuma wanasifika sana kwa misimamo thabiti kuliko sehemu yoyote ile nchini, hivyo hamuwezi kumpangia nani anafaa na nani hafai.
 
1. Kuhusu ukabila wake tuache kwanza. Hiyo ni ishu nyingine kabsa.
2. Kweli zile pesa kama hazijapotea zimekwenda wapi?
2.1 hilo jibu mpaka leo halijajibiwa na bado tunaletewa kinki za kipuuzi kututoa kwenye mchezo.
2.2 Umeongea kuhusu Chato kujengwa uwanja wa ndege, swali ni kuwa huko Chato Kuna nini chenye manufaa kwa taifa. Kumbuka Geita ndo habari ya mjini kwenye pato la taifa ndugu. Nitafafanua kiasi, mwaka jana Geita ilichangia pato kubwa. Angalia hapa Ujenzi kiwanja cha Ndege kwa Rais Magufuli wazua mjadala – Millardayo.com kidogo kisha cheki hapa Zitto ang'ang'ania taarifa kuhusu uwanja wa ndege wa Chato | Azam | Habari | Swahili
3. Nipe maana ya kikatiba ya neno "Mamlaka" kisha Ukipata maana hiyo jaribu kuihusisha na anayoyafanya bwana Yohana.
Nawasilisha ndugu.

CAG aliulizwa kama kuna ufisadi umefanyika akajibu hapana. Wewe unataka kubishana na Raisi wetu ?

Kuhusu uwanja wa Chato kule ni nyumbani kwa kina Raisi Magufuli na huwa anaenda kupumzika, sasa ulitaka Raisi afikaje kwao ? Mbona Jakaya Kikwete alitaka kujenga bandari kule kwao Bagamoyo na hamkulalamika mnakuja kulalamika kwa Raisi Magufuli ? Halafu unajua kwamba Chato Airport utaitwa Geita Airrport, sasa unalalamika nini wakati uwanja utakuwa ni wa Geita ?

Mamlaka maana yake ni Authority or Power to act within certain jurisdiction or bounds of law. Lakini Raisi Magufuli hata akikosea ni udhaifu tu wa kibinadamu lakini jua kuwa ana nia njema sana na nchi hii, wakina Jakaya walilete kufuata Sheria lakini nchi haikufika popote pale. Kama unakumbuka alivyokuwa anamuapisha mama Anna Mghwira alisema " I give you power, and power is power, akikisumbua yoyote yule wewe mshughulikie tu kwa maslahi ya wananchi"

Mkuu demokrasia, utawala wa sheria na haki za binadamu havipo duniani, ni mbinu tu za kibepari kutaka kutukandamiza na kuiba rasilimali zetu kama walivyofanya kule Libya kwa Gaddafi na Kuwait kwa Saddam Hussein.

Mkuu Red Giant unakumbuka mabepari walichomfanyia Raisi wa Kuwait Saddam Hussein ?
 
Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
12,172
2,000
Tanzania tuko vizuri sana kiusalama wala hatuna haja ya kwenda huko, hakuna changamoto ambayo kitengo hawawezi kutatua. Tena baada ya Raisi Magufuli kuingia madarakani Usalama wa nchi umekuwa imara sana kama kipindi cha Nyerere, yani kiufupi nchi iko pazuri mno.

Halafu kwanini tupoteze pesa nyingi kwenda huko Ulaya wakati tunatakiwa kuwatumikia watanzania hapa nchini na mahospitalini hakuna madawa! Watu wakienda huko wataende tu kupiga dili na kuzurura na mahawala wao. Pia unasahau kwamba hii mikutano ni mkusanyiko wa nchi za mabepari ambao wameiibia Tanzania kwa miaka mingi sana, twende huko kwao kufanya nini ?
Mlizoea safari za nje kama hizi zisizo na tija, sasa Hapa Kazi Tu. Mkuu Richard fanya kazi, Raisi kasema hakuna kwenda nje hovyo mpaka pale Tanzania inakuwa imenyooka.

Mimi napiga kazi mkuu, usiwe na wasi.

:):)
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom