Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,499
- 9,279
Mkutano wa kati ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Jeshi la Polisi na wadau wa siasa nchini uliopangwa kufanyika Dodoma wiki hii. Sababu za kuahirishwa kwake inaelezwa ni ili kutoa nafasi zaidi kwa wadau wengi zaidi kushiriki kikamilifu.
Mkutano huo uliolenga kujadili maudhui ya utekelezaji wa sheria zinazoratibu shughuli zote za siasa Tanzania' ulikuwa uhudhuriwe pia na waziri mkuu, Kassim Majaliwa.
Msajili msaidizi wa vyama vya siasa nchini Tanzania, Sixty Nyahoza aliiambia BBC kwamba, mbali na waziri mkuu na baadhi ya mawaziri, mkutano huo ulipangwa kuhudhuriwa na pia wadau wote muhimu katika siasa vikiwemo vyama vya siasa, Azaki, waandishi wa habari na viongozi wa dini.
Kama ilivyonukuliwa na mtandao wa gazeti la Mwananchi, Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Tanzania, Juma Ali Khatib amesema mkutano huo hautakuwepo kama ulivyopangwa awali, lakini maandalizi yanaendelea kwa kuwa utafanyika mwezi Desemba, mwaka huu.
Hata hivyo tarehe ya kufanyika mkutano huo itatangazwa baadaye na utahusisha wadau tofauti wakiwamo wa vyama vya siasa vilivyotangaza kuususia kwa sababu tofauti.
Kabla ya kuahirishwa kwa mkutano huo, vyama vya Chadema na NCCR Mageuzi vilishatangaza kutoshiriki huku vikitoa masharti kwa Ofisi ya Msajili.
Alisema wadau wote wameshajulishwa kuhusu kuahirishwa kwa mkutano huo uliotarajiwa kuleta suluhu ya sintofahamu ya kisiasa nchini, hasa mvutano kati ya vyama vya siasa na Jeshi la Polisi.
Mkutano huo unakuja kufuatia kuwepo kwa mvutano wa muda mrefu kuhusu kuzuiwa kwa shughuli za kisiasa nchini humo, ambapo vyama vya upinzani vimekuwa vikilalamika kunyimwa fursa ya kufanya mikutano ya kisiasa kama sheria zinavyotaka.
BBC